Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuhitimisha ushahidi Mkuu leo, Agosti 26, 2026 Mahakamani

Mh moto unaumwanga Mtoto wa Mungu lissu , nachelea kusema kusanya wabunge wote , baraza la mawaziri kama lipo ni sawa na Lissu Mmoja,

Ila najifunza kitu Simba huzaa Simba, yule Mwanae wa kiume amekaa kikachero sana , familia ikibarikiwa ina barikiwa ,inaweza ikawa Lissu asiwe Rais ila mwanae akaja fanya makubwa kwenye Taifa kuliko yeye.

Note
Lissu na Heche kwa sasa ndo wanasiasa maharufu Afrika , ndo ukweli

Wawakili ya Serikali hata hayaoni haya , , mpo kadhaa , uyu yupo Mahabusu mnajadili kila atua na bado anawatoa kamasi , vipi kama angekua na mda wa kushaurina na mawakili wake, jiandaeni futi 7 , hakuna jiwe litavaki bila kusagwa asema Bwana
 
🤣
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA MAHAKAMANI

Waheshimiwa Majaji, niliwaonyesha mashahidi hawa watatu, PW1, PW2 na PW16, kifungu cha 52(2) cha Sheria ya Habari, kinachosema siyo uchochezi kusema ubovu wa Katiba na ubovu wa sheria kwa lengo la kubadilisha hayo, na wakasema ndiyo, wanafahamu.

Nikawauliza, mlizingatiaje vifungu hivi wakati wa upelelezi wenu? Na hawakuwa na cha kusema.

Waheshimiwa Majaji, niliwaonyesha mashahidi watatu, PW1, PW2 na PW16, PGO 1, kuwa nguzo kuu wakati wa upelelezi wa makosa ya jinai ni kwamba watuhumiwa hawana hatia.

Na nilipowaonyesha, walisema ndiyo, ni hii.

Na katika PGO hiyo hiyo, niliwaonyesha kifungu kingine kinachosema polisi wasipofuata presumption of innocence, kwamba mtuhumiwa hana hatia, wakasema ni kweli.

Ushahidi wa PW1 na PW2 unasema waliona ile video tarehe 04 April 2025.

Mkutano unaodaiwa makosa yamefanyika ni kesho yake, tarehe 03 April, akamuonyesha vipande vipande.

Baada ya kuangalia video ile siku hiyo hiyo, PW2 akaamuru lifunguliwe faili la uhaini, wala hakutaka kushauriana na wanasheria.

Kwa hiyo, siku hiyo wakaona Tundu Lissu afunguliwe kesi ya uhaini.

Amini Mahamba kwenye ushahidi wake anasema siku hiyo hiyo alipoteuliwa kuwa kiongozi wa timu, na wakaandaa kesi ya uhaini siku hiyo hiyo.

Kwa hiyo, walikuwa na majibu tayari: mimi ni Muhaini. Hawakwenda kwa wanasheria wala IGP wao.

Na kwa vile walikuwa na majibu, Waheshimiwa Majaji, ndiyo maana waliulizwa: Mliwatafuta viongozi wa CHADEMA muwaulize? Wakasema hapana.

Waliulizwa walinitafuta mimi kuniuliza maana yake ni nini? Wakajibu hawakuniuliza.

Hata walipoletewa ushahidi wa PW17 siku tatu baadaye, maelezo ya PW17 yanaeleza yeye ndiye aliyechapisha na akasema hapakuwa na uhaini. Ila kwa sababu wao walikuwa na majibu kwamba mimi ni Muhaini, hata hawakusoma hayo maelezo.

Nilimuuliza Amini: Ulisoma maelezo ya nani aliyachapisha na kusambaza? Akasema ndiyo, alisoma.

Kwanini mnanihoji wakati maelezo ya shahidi wenu yanaeleza yeye ndiye aliyechapisha? Hakuwa na majibu.

Utaratibu mwingine wa upelelezi wa mashahidi PW1, PW2 na PW16 kuhusu PGO 1, paragraph ya jinai, ni kwamba jinai ni makosa tu kama inakuwa imetajwa na sheria kama kosa.

Nikawauliza waangalie kama kuna kifungu cha kuzuia au kuvuruga uchaguzi. Wakasema hakuna.

Nikawaonyesha Ibara ya 151(1) ya Katiba juu ya Serikali, na kwamba Serikali ni nini, juu ya tafsiri ya neno Serikali.

Je, katika maneno mnayosema nimesema, kuna neno nimesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Wakasema hakuna.

Nikawauliza, kuna neno Serikali ya Mapinduzi Zanzibar? Wakasema hakuna.

Nikawauliza, kuna neno Mkuu wa Mkoa fulani? Wakasema hakuna.

Kuna jina la Rais au Makamu wa Rais? Wakasema hakuna.

Nikawauliza, kuna jina au neno linalohusisha kiongozi wa Serikali Kuu au Serikali za Mitaa? Wakasema hakuna.

Nikawauliza, sasa hiyo Serikali mnayosema nimetengeneza nia ya kutishia ni Serikali ipi, kama siyo hizo zinazotambuliwa na Katiba ya nchi yetu? Hawakuwa na chochote cha maana cha kueleza.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, ushahidi huo wa kutishia Serikali, hicho kifungu cha 39(2)(d) hakitekelezeki kwa mazingira yoyote yale.

Waheshimiwa Majaji, maneno ya kifungu hicho cha adhabu ni maneno ya Kiingereza: “The Executive of United Republic.”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Kazi yako ni njema
 
Kumpa kesi ya uhaini wamefail sana kesi ilitakiwa kuwa ni "Uchochezi", Wange win kwa mujibu wa kauli zake hizi.
Akili zao zinawaza kukomoa tu kama unakumbuka hata makesi yao ya ugaidi waliyoyajumua, Heche aliwasitua kidogo tu kuwa watatoa taarifa duniani kote na hata FIFA na CUF wafahamishwe juu ya ugaidi huu. Walistuka wakaona wameingia chaka ghafla yule waziri wa mambo ya CCM akairekebisha kidogo eti ooooh " kuna viashiria na sio ugaidi wenyewe"
 
Huyo Waziri mwenyewe sasa
 
😆
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA MAHAKAMANI

Ni ushahidi wangu kwamba The Executive inaweza kuwa Rais kwa sababu Rais ni Chief Executive. Inaweza kuwa Vice President au Prime Minister, wote hao ni Executive.

Inaweza kuwa ni Ministers au Deputy Ministers, wote hao ni Executive.

Inaweza kuwa Regional au District Commissioners, wote hao ni Executive.

Waheshimiwa Majaji, Wakurugenzi wa Halmashauri wanaitwa Executive Directors. Kwa hiyo wanaweza kuwa wa Manispaa, wa Majiji; wao wote ni Executive.

Waheshimiwa Majaji, Executive wanaweza kuwa ni Watendaji wa Kata, wanaitwa Ward Executive Officers.

Executive wanaweza kuwa Village Executive Officers au Watendaji wa Mitaa, ambao wanaitwa Mtaa Executive Officers.

Na wanaweza kuwa ni Watendaji au Watumishi wowote wa Serikali ambao si Watendaji wa Mahakama au wa Bunge.

Kwa hiyo, kifungu cha 39(2)(d) kinachosema hivyo, ni ushahidi wangu kwamba kipo too broad.

Ukikosana na Mtendaji wa Kijiji upewe uhaini, hakuna atakayeponea. Kipo too broad.

Ndiyo maana hii kesi hawawezi kuthibitisha na wameshindwa kuthibitisha.

Umemtisha nani, Rais au mtendaji? Hakuna.

Ni ushahidi wangu kwamba kifungu hicho kilichotungwa specifically baada ya Makungu Matata, wakati wa chama kimoja, hakifai tena kuwepo katika sheria zetu. Ndiyo ushahidi wangu.

Waheshimiwa Majaji, kwenye ushahidi wa upande wa Mashitaka, hakuna shahidi hata mmoja aliyetoa ushahidi kwamba hiyo nia yangu ya kuitishia Serikali ilitekelezeka au la.

Hakuna aliyesema Serikali waliogopa sana. Ilikuwa hapakukalika siku hiyo.

Waheshimiwa Majaji, kukosekana kwa ushahidi huo kuna maana kubwa sana.

Ni ushahidi wangu kwamba kwenye kosa kama hili la uhaini, ambapo ni intention ya kosa, upande wa Mashitaka ulitakiwa waeleze matokeo ya hiyo intention.

Upelelezi wa kesi hii ulifanyika kienyeji enyeji sana, bila kuzingatia sheria.

Waheshimiwa Majaji, nilikamatwaje?

Wakati wa ukamataji, Waheshimiwa Majaji, Jeshi la Polisi liliendelea kufanya mambo kienyeji enyeji kwa kutokuzingatia sheria.

Waheshimiwa Majaji, nilikamatwa mji wa Mbinga, Mkoa wa Ruvuma, siku ya tarehe 09 April mwaka jana, majira ya saa 12 jioni.

Mimi ndiyo nilikuwa nahutubia mkutano huo wa hadhara.

Mikutano yetu inaisha saa 12. Kabla ya kumalizia mkutano, nilifuatwa na Polisi jukwaani. Simkumbuki jina, ila alijitambulisha kuwa ni OCD wa Mbinga.

Akaniambia kwamba, “Nakutaka kituoni sasa hivi,” jukwaani.

Nikamuuliza, “Unanitakia nini na nimefanya kosa gani?”

Akaniambia, “Wewe twende, utajua hayo mbele ya safari.”

Nikawambia, “Afande, hiyo siyo utaratibu wa kisheria wa nchi hii. Huna mamlaka ya kunipeleka kituoni kama huniambii kosa langu, na usiponiambia siendi.” Hivyo ndivyo nilivyomwambia.

Huyo Bwana OCD alishuka kwenye jukwaa, nikaendelea kuwaaga wananchi.

Nikasikia kishindo cha mabomu ya machozi.

Wakapiga watu kwa mabomu ya machozi mengi sana na wakapiga watu kwa virungu.

Na mimi sijui nilikamatwa vipi, ila nikajikuta katika gari ya Polisi, nimewekwa chini sakafuni na nimekanyagwa kwenye shingo.

Sikuwa peke yangu. Tulikuwa na wenzangu watatu. Tulipofika Polisi, walinipeleka kwenye Ofisi ya OC CID. Hawakunipeleka mahabusu. Sitatoa ushahidi wa uongo.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…