Unazifuatilia kwa ukaribu comments zangu. Hongera
Mashambulizi ni mazuri sana!!TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI
SEHEMU YA 2.
Lissu: Shahidi, kwa unavyokumbuka, mkutano wote hadi mwisho, kuanzia ufunguzi wa Katibu Mkuu hadi mwisho, unaweza kuwa ni muda gani?
Heche: Kulikuwa na mambo mengi, kuanzia maombi na kila kitu.
Jumla inaweza kuwa masaa manne na kidogo.
Lissu: Katika hayo masaa manne na kidogo, mimi nilizungumza kwa muda gani?
Heche: Waheshimiwa Majaji, Mwenyekiti Tundu Lissu alizungumza kwa zaidi ya masaa 4.
Lissu: Sasa, shahidi, nashitakiwa kwa maneno yafuatayo:
"Wanasema kitu kimoja sahihi hapa. Wanasema hivi..., tutahamasisha uasi, ni kweli...
Huu uchaguzi tutauvuruga, kwa sababu tunaenda kukinukisha vibaya sana..."
Haya maneno kuyasoma yamechukua dakika ngapi?
Heche: Hayamalizi hata dakika moja.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, katika masaa mawili na kidogo, maneno niliyoyazungumza ni haya tu?
Heche: Siyo kweli, Waheshimiwa Majaji, kwamba hayo ni maneno pekee.
Alizungumza kwa kirefu mambo ya uchaguzi.
Lissu: Hayo mazungumzo marefu yalikuwa ya jambo gani?
Heche: Mazungumzo hayo marefu yalihusu uchaguzi.
Namna ambavyo mfumo mzima wa uchaguzi umeharibika, umeharibiwa, ni mbovu, haupo huru na ambavyo hauwezeshi wananchi kupata wanachotaka.
Namna ambavyo ni vigumu kwa mgombea wa upinzani, hasa CHADEMA, kufanikiwa kushinda uchaguzi hata kama anakubalika.
Namna ambavyo mfumo huu unasababisha mauaji na maafa wakati wa uchaguzi.
Namna ambavyo mfumo huu unaruhusu upendeleo wa wazi kwa Rais, Wabunge na Madiwani.
Namna ambavyo vyombo vya dola vinatumika kuharibu uchaguzi/watumishi wa umma.
Kwa ujumla, alieleza namna ambavyo mfumo huu siyo huru na hautendi haki na unavyopaswa kubadilishwa kabla ya uchaguzi.
---
Lissu: Shahidi, kuhusu hilo la mwisho ulilosema, namna unavyopaswa kubadilishwa, waeleze Waheshimiwa Majaji nini kinachopaswa kubadilishwa.
Heche: Waheshimiwa Majaji, alizungumza kuwa kinachopaswa kubadilika ni Katiba na mabadiliko ya sheria zinazosimamia chaguzi zetu.
Mabadiliko ya namna ya kupata wawakilishi, hasa Wabunge, na mgawanyo wa majimbo.
---
Lissu: Shahidi, umesema katika mazungumzo yangu nilisema namna chaguzi zinavyosababisha maafa.
Waeleze Waheshimiwa Majaji nilisema nini kuhusu namna ya kuondoa maafa.
Heche: Waheshimiwa Majaji, alisema namna ya kuondoa maafa katika uchaguzi ni kutengeneza uchaguzi ambao ni huru na wa haki (sawia).
Unaotoa ushindani wa haki ambao hautengenezi upendeleo na unaotoa usawa kwa watu wote.
---
Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji kuhusu Tume ya Uchaguzi. Nilisema nini kuhusu mabadiliko yanayotakiwa?
Heche: Waheshimiwa Majaji, alisema mabadiliko yanayotakiwa katika Tume ni kutengeneza muundo mpya wa Tume.
Ambao haumpi mamlaka Mwenyekiti wa CCM na Kiongozi wa CCM wa kuunda Tume.
Pawe na muundo mpya wa Tume kuanzia Taifa mpaka kwenye Kata.
Iwe na watumishi wake wanaojitegemea, siyo wa Serikali ambao wote wanachukua maelekezo kutoka kwa mwajiri wao.
Na hiyo Tume ndiyo iwe na mamlaka ya kugawa majimbo kulingana na vigezo vinavyofaa na siyo upendeleo.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
Tupo pamoja ManyanzaTUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI
SEHEMU YA 4.
Lissu: Sasa, shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji nilivyosema kuhusu kupinga mambo yote haya Mahakamani.
Heche: Waheshimiwa Majaji, alieleza namna ambavyo ni ngumu kupinga mambo haya Mahakamani.
Akaeleza namna njia mbalimbali zilivyotumika kupinga mfumo wa uchaguzi.
Akaeleza namna ambavyo hata ule ushahidi ambao ungetumika Mahakamani unavyokuwa umeharibiwa tangu mwanzo.
Kwa hiyo alieleza haya, zile fomu ambazo mlalamikaji angetumia Mahakamani zinavyokuwa zimeharibiwa tangu mwanzo.
Akaeleza zile gharama kubwa ambazo wagombea wanatakiwa kulipa ili kufungua kesi.
Akaeleza pia wingi wa kesi ambazo zingefunguliwa.
Akaeleza mfano wa uchaguzi wa Vijiji zaidi ya 17,000 ulivyoharibiwa; kesi 17,000 zingesikilizwaje?
Na akamalizia kwa kusema Mahakama yenyewe ilisema kupitia kesi ya Mtikila kwamba matatizo ya kisiasa yanaweza kutatuliwa kisiasa.
Siyo kila jambo la kwenda Mahakamani.
Waheshimiwa Majaji, alisema pia kwamba Mahakama kupitia kesi ya Walid Kaborou ilisema kwamba uchaguzi ambao siyo huru siyo uchaguzi.
Lissu: Shahidi, nilisema nini kuhusu hoja ya kuahirisha uchaguzi wa mwaka jana?
Heche: Waheshimiwa Majaji, alisema sisi kama chama tulikuwa tayari uchaguzi usogezwe mbele, mabadiliko yafanyike.
Mazingira yatakayoruhusu uchaguzi huru na wa haki kuepusha maafa.
Na kwamba chaguzi zilizopita zilikuwa zinasababisha maafa.
Waheshimiwa Majaji, naomba break dakika 5.
Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji tofauti ya hotuba yangu ya tarehe 03 na wadau na kwenye mikutano ya hadhara.
Heche: Hotuba aliyozungumza Mwenyekiti kuhusu mifumo ya uchaguzi na matatizo ya mifumo ya uchaguzi, na namna ya kurekebisha na kusogea mbele ili mifumo irekebishwe, ni hotuba ileile kwa ujumla.
SHARE SHARE SHARE
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI
SEHEMU YA 3
Lissu: Sasa, shahidi, katika mazungumzo uliyosema moja ya mambo ambayo tumezungumza kwa wadau ni kampeni za uchaguzi.
Waeleze Waheshimiwa Majaji, katika hotuba yangu hili nililisemaje?
Heche: Waheshimiwa Majaji, Mwenyekiti Tundu Lissu alieleza kwa kutoa mifano jinsi katika kampeni mikutano inavyovurugwa na vyombo vya dola, aidha Polisi au Tume yenyewe.
Akawa anatoa mfano wa namna yeye alivyokuwa akisimamishwa kufanya kampeni zake mwaka 2020 wakati wa kampeni, namna ambavyo watu wetu wanazuiwa kufanya kampeni.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, nilisema nini kuhusu kuenguliwa kwa wagombea wa upinzani, hasa CHADEMA?
Heche: Waheshimiwa Majaji, alieleza kwa kirefu namna ambavyo wagombea wa CHADEMA na vyama vingine wanavyoenguliwa kwa sababu ambazo siyo za Kikatiba wala Kisheria.
Na akaeleza kwamba uchaguzi wa 2020 ulivyovunja rekodi kwa wagombea wengi wa upinzani kuenguliwa na CCM wakapita bila kupingwa.
Akaeleza kwamba Tume inavyoinufaisha CCM kwa jinsi ambavyo wagombea wa CCM hawajawahi kuenguliwa, iwe Vitongoji, Vijiji au Majimbo.
Akatolea mfano mgombea wetu wa CHADEMA, Susan Kiwanga, aliyeenguliwa akiwa ni Mbunge wa 2015 hadi 2020 katika Jimbo la Mlimba.
Na akawa anatoa mifano katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Kwamba 2024 ulivunja rekodi za engua-engua.
Kwa vipi tukashiriki uchaguzi ambao tunajua tunaenda kuenguliwa?
---
Lissu: Shahidi, eleza Waheshimiwa Majaji, nilisema nini kuhusu masuala yanayohusu mawakala wa vyama na mawakala wa wagombea?
Heche: Waheshimiwa Majaji, alieleza jinsi wakala anavyotakiwa kulinda interest ya wagombea na vyama vyao.
Taratibu na mazingira zimewekwa ngumu kiasi kwamba kupewa utambulisho na kiapo ni vigumu.
Mawakala wamekuwa wakikamatwa wanapojaribu kuingia katika vituo.
Wengi wanakuwa wanafungiwa nje.
Wanazuiliwa kuingia katika vituo.
Na hivyo mgombea na chama cha CHADEMA kinakosa mawakala.
---
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, nilisema nini juu ya yanayotokea siku ya uchaguzi?
Heche: Waheshimiwa Majaji, alieleza namna ambavyo usumbufu unakuwapo siku ya uchaguzi.
Namna ya wapiga kura kupata majina yao.
Mara jina halionekani, unaambiwa jina lipo kituo kingine.
Namna ambavyo kura ambazo siyo halali zinaingizwa katika vituo.
Namna ambavyo mawakala na wagombea wanavyonyimwa fomu za matokeo.
Namna ambavyo mawakala wananyimwa zile fomu za kujaza irregularities (malalamiko) wanayoona yametokea ndani ya vituo.
Namna ambavyo majumuisho yanavyofanyika na kura kutangazwa ambazo siyo halali.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
Mimi Nina wasiwasi na Heche anaweza kuchemka hasa akibanwa na akina KatugaTwende sasa, kumeshawaka mahakamani, halafu naomba kuuliza mashahidi wengine wameshafika hapo au bado? Nataka kujua mapema kabisaa.
Amefumua mengi sana, ingekuwa ni hatari kwake angeshaambiwa na LissuMimi Nina wasiwasi na Heche anaweza kuchemka hasa akibanwa na akina Katuga
Komenti za popoma utazijua tu.Na Lissu mbona kama hanatuchelewesha makusudi sisi kuongea na Shemeji yake
MJaji watoe neno maswali yawe na ukomo kwa Lissu ❗️
Ijumaa hii mapema tu tukabidhiwe uyu atwambie Tone tone kaweka wapi
Kachukuwa wapi na wapi ❗️
Zamu yetu kunogewe nae Heche ❗️
Mh Lissu pengine leo atayajua hasioyajua kumusu Heche
Kapokea pesa kwa MACCM❗️
leo Lissu ajiandae kupigwa na Butwaa
Yumkin mengi kafichwa leo
ndio leo