TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI
Lissu: Shahidi, kwa ufahamu wako, kwa haya ambayo nimekuuliza na majibu yako: hakuna majina ya walio uawa, hakuna majina ya walioua, hakuna orodha. Tume ya Jaji Chande ilichunguza nini sasa, kwa ufahamu wako?
Heche: Waheshimiwa Majaji, nafikiri wao wenyewe watatoa maelezo vizuri. Mimi sipo katika position kwamba walichunguza nini na walichunguzaje.
Lissu: Sasa, shahidi, kuna ushahidi umetolewa Mahakamani kwamba kulikuwa na jitihada za chama kujadiliana na CCM juu ya mabadiliko ya Katiba na Tume ya Uchaguzi kabla ya hii “No Reform, No Election”.
Waeleze Waheshimiwa Majaji ufahamu wako.
Heche: Waheshimiwa Majaji, nina ufahamu na hili swala kwa sababu mimi binafsi nimeshiriki.
Nilikuwa kwenye timu ya CHADEMA iliyokutana na Rais aliyekuweko mwaka 2022 hadi 2025, Ikulu Chamwino, Dodoma.
Lissu: Hujamtaja huyo Rais, hana jina?
Heche: Rais Samia Hassan Suluhu.
Mimi binafsi nilikuwapo katika mazungumzo, tukajadili mambo mbalimbali.
Lissu: Mambo mbalimbali gani? Weka wazi.
Heche: Waheshimiwa Majaji, baada ya kuwepo kwa malalamiko ya uchaguzi wa mwaka 2019 na 2020, baadaye chama kikaanzisha kampeni ya madai ya Tume ya Uchaguzi.
Wakati huo chama kipo chini ya Freeman Mbowe.
Mwaka 2021 tulienda Mwanza kwenye kongamano la madai ya Katiba na mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi na ya Kikatiba kabla ya mwaka 2025, ambapo pangefanyika uchaguzi mwingine.
Hapo Mbowe na mimi tulikamatwa kama nilivyoeleza jana na baadaye akafunguliwa kesi ya ugaidi.
Baadaye tulipotoka, tukamuona Ikulu.
Baada ya kutueleza makubaliano yake, ndiyo tukaenda kumuona Rais Dodoma.
Katika kikao hicho, Waheshimiwa Majaji, kikao cha kwanza Ikulu Chamwino alikuwapo:
- Mwenyekiti Mbowe
- Saidi Issa, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama chetu Zanzibar
- Katibu Mkuu John Mnyika
Kwa upande wa Serikali alikuwapo:
- Rais Samia
- Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Feleshi
- Waziri George Simbachawene
- Mama Jenista Mhagama, Waziri
Upande wa CCM alikuwapo:
- Mzee Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti
- Na viongozi wengine siwakumbuki.
Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu wakaeleza matatizo ya uchaguzi, jinsi ambavyo tumeonewa na kunyanyaswa katika uchaguzi, mauaji katika uchaguzi, watu waliokimbia nchi na mambo yote ambayo yamekuwa yakilalamikiwa katika uchaguzi.
Kwenye kile kikao tukakubaliana kuunda timu ya watu watano kwa CHADEMA, CCM na Serikali, kwenda kupitia matatizo ya uchaguzi.
Upande wa CHADEMA iliundwa timu iliyokuwa chini ya:
- Mwenyekiti Mbowe
- Katibu Mkuu John Mnyika
- Wakili Jeremiah Mtobesya
- Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kutoka Zanzibar, Zeudi Mvamo
Jaji Ndunguru: Hana sababu ya kutaja majina. Mnyika ameshasema katika ushahidi wake.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, siyo kwa bahati mbaya ataje, ili kuweka uzito wa ushahidi wake kulingana na mashahidi wenzake.
Heche: Na mimi, Waheshimiwa Majaji, nilikuwapo.
Palikuwa na Sekretarieti ndogo ya Reginald Mjuni na mwanasheria, simkumbuki.
Na upande wa CCM palikuwa na watu watano.
Namkumbuka Makamu Mwenyekiti Abdulrahman Kinana, Andrew Chenge.
Wawili siwakumbuki majina yao, ila mmoja alikuwa ni Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Na palikuwa na Mawaziri. Sasa, mwanzoni alikuwa anaingia Jenista Mhagama na baadaye akawa anaingia George Simbachawene.
Waheshimiwa Majaji, hayo mazungumzo yalichukua mwaka mzima na sehemu.
1. Kukwamua mchakato wa Katiba.
2. Mapendekezo ya kukwamua mchakato wa Katiba.
3. Vyombo ambavyo vingeundwa katika kuandika na kuchakata mchakato wa Katiba.
4. Mapendekezo ya sheria ya uchaguzi.
5. Mapendekezo ya kuunda Tume ya Uchaguzi.
6. Kuhusu kesi mbalimbali za watu waliokuwa wamebambikiziwa na kufungwa kwa uongo.
7. Tulizungumza kuhusu watu waliokuwa wamekimbia nchi na viongozi waandamizi kama Mheshimiwa Tundu Lissu na Mjumbe wa Kamati Kuu Godbless Lema, Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini wakati ule, na Ezekiah Dobojo Wenje, Mjumbe wa Kamati Kuu.
8. Kuwaondoa maarufu “COVID-19”, wanawake walioenda Bungeni kinyume na utaratibu wa chama. Tulizungumza hilo.
9. Tulizungumza kuhusu kufungukia mikutano ya hadhara iliyokuwa imefungwa na Rais Magufuli kinyume na sheria.
10. Tulizungumza kuhusu kukomesha utekaji.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, naona tumefika saa 7 tayari, muda wa mapumziko. Tunaomba twende health break.
Tukirudi, kama nilivyosema, shahidi atarudi kwa ajili ya kuja kumalizia ushahidi wake.
Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka?
Nassoro Katuga: Upande wa Mashitaka hatuna pingamizi.
Jaji Ndunguru: Unaweza kutuambia kuwa ushahidi utaisha leo?
Lissu: Waheshimiwa Majaji, naweza kusema kwamba hii ngoma haitolala.
Jaji Ndunguru: La sivyo, nipunguze muda.
Lissu: Kupunguza muda wa health break ni kuniathiri, nikose muda wa consultation. But I can confirm, leo tutamaliza ushahidi wa DW5 ndani ya muda wa saa za Mahakama.
Jaji Ndunguru: Shahidi, unasemaje kuhusu mapumziko?
Heche: Mimi nikiwa hapa nitasema nini? Zaidi ya kuwasikiliza nyinyi.
Jaji Ndunguru: Sawa, tuonane saa 8 na nusu.
MAJAJI WANATOKA.
TUKUTANE SAA 8:30 MCHANA