TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI.
SEHEMU YA 13.
MAHAKAMA IMEREJEA
Jaji Ndunguru: Tuendelee.
Nassoro Katuga: Kwa upande wa Serikali kuna mabadiliko kwenye kolamu.
Ametoka:
1. Ajuaye Zegeli
2. Job Mrema
Ameingia tena Tawabu Issa.
Kwa upande wa Mshtakiwa hakuna mabadiliko.
Shauri limekuja kwa ajili ya utetezi. Upande wa Jamhuri tupo tayari kuendelea kumsikiliza Shahidi wa Utetezi.
Jaji Ndunguru: Mshtakiwa unasemaje?
Lissu: Nipo tayari, Mheshimiwa.
Jaji Ndunguru: Shahidi unakumbushwa kuwa bado upo chini ya kiapo. Naomba tuendelee.
Lissu: Mheshimiwa Jaji, naomba nikumbushwe maswali mawili ya mwisho.
Jaji wa Kushoto: Shahidi aliongelea kuhusu wale wabunge wanawake kutolewa Bungeni, na pili kuhusu kibali cha mikutano.
Heche: Waheshimiwa Majaji, ni kufunguliwa kwa mikutano, siyo kibali.
Majaji: Sawa.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo kuna jambo jingine mlilozungumzia katika huo mkutano.
Heche: Waheshimiwa Majaji, tulizungumzia pia kukomesha vitendo vya utekaji nyara, ubambikaji wa kesi za uongo kwa watu, na kwa ujumla kupitia mfumo wote wa haki jinai kuurekebisha na kurudisha demokrasia.
Lissu: Shahidi, katika ushahidi wako ulisema mazungumzo hayo yalichukua takribani mwaka mzima. Sasa waeleze Waheshimiwa Majaji, mazungumzo hayo yaliishaje?
Heche: Waheshimiwa Majaji, wakati wote wa mazungumzo sisi tulikuwa tunapeleka malalamiko yetu kwa maandishi.
Wakati wote huo wajumbe wa CCM walikuwa wanatusikiliza na kusema wanayabeba na kwenda kumweleza Rais tuliyokuwa tunazungumza ili tuwe katika picha moja.
Waheshimiwa Majaji, kuna wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa chama chetu na Makamu Mwenyekiti walienda kwa pamoja kumuona Rais kumweleza tulichokuwa tumezungumza.
Miongoni mwa mapendekezo yalikuwa ni kufanya Press Conference moja kwa pamoja ya Mbowe na Kinana kueleza makubaliano ambayo tumeyafikia.
Mazungumzo yaliisha pale tulipodai tujibiwe kwa maandishi, kama ambavyo sisi tumekuwa tunawaandikia kwa maandishi.
Hapo ndiyo tulipoishia. Mpaka leo hakuna kikao cha maridhiano ambacho kimefanyika.
Waheshimiwa Majaji, majibu ambayo walituletea walikataa mapendekezo yetu yote.
Lissu: Ukisema majibu yao, una maana gani?
Heche: Upande wa Chama cha Mapinduzi walitujibu sisi CHADEMA kuwa wamekataa mapendekezo yote.
Lissu: Waliwajibu kwa njia gani?
Heche: Walitujibu kwa njia ya maandishi na kukataa mapendekezo yetu yote.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.