Kesi ya Uhaini ya Lissu: Heche kuendelea kutoa ushahidi Mahakamani Sept. 11. 2026

TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 14.

Lissu: Sasa Shahidi, umeeleza jitihada za chama na mazungumzo na CCM, ukaeleza matatizo yaliyojitokeza mwaka 2024, ukaeleza ya “No Reforms, No Election”, ukaeleza ya mkutano wa tarehe 03 April.

Sasa nataka ueleze ya tarehe 29 October.

Sasa waeleze Waheshimiwa Majaji, wewe ulikuwa wapi na waeleze kama ulishiriki kupiga kura.

Heche: Waheshimiwa Majaji, mimi sikupiga kura katika uchaguzi wa tarehe 29 October 2025. Nilikuwa katika kituo cha Polisi Mtumba, Dodoma, baada ya kukamatwa hapa tarehe 22 October 2025.

Nassoro Katuga: Huu ushahidi kwamba nilikamatwa, Mahakama Kuu hapa nikapelekwa Mtumba, Dodoma, nikaletwa Oysterbay nikawakuta...

Ni ushahidi unaorudiwa.

Jaji Ndunguru: Tukiacha, tuone labda kuna sehemu anaelekea.

Lissu: Wala Waheshimiwa Majaji, sina nia ya kurudia ushahidi bali najengea msingi.

Lissu: Shahidi, sasa tueleze unafahamu nini kuhusu siku ya tarehe 29 October.

Heche: Waheshimiwa Majaji, nafahamu kwamba nilipotoka Polisi nilipata taarifa nyingi zinazohusiana na kile kilichotokea tarehe 29 October—watu kuuawa kwa wingi.

Kwa mujibu wa hotuba ya Jaji Chande, ni watu 518.

Waheshimiwa Majaji, kwa rekodi tu, Jaji Chande anasema haijulikani kabisa, lakini inaweza kuongezeka.

Mzee Joseph Sinde Warioba alisema ni wengi kuliko walio uawa katika Vita ya Kagera.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, tunaangalia hilo jibu la mwisho la Shahidi. Anasema kwamba Mzee Warioba alisema...

Tukio hilo liko hivyo, itakuwa tumepokea hearsay.

Huyu ni Shahidi wa fact kwa mujibu wa kifungu cha 167.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, kuna mambo mengi sana hapa yanaongelewa kama vile ni sheria, lakini si hivyo.

Ushahidi wa hearsay ni ushahidi unaohitaji corroboration—ushahidi ambao unahitaji kuthibitishwa tu na ushahidi mwingine.

Na tatu, ana nafasi kubwa ya kuja kufanya cross-examination.

Na mwisho, Mahakama ndiyo itaamua ni ushahidi gani una mashiko.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Lissu: Asante, Waheshimiwa.

Heche: Waheshimiwa, nilikuwa naeleza kwamba hiyo ni idadi kubwa ya watu kuuawa kwa pamoja tangu Vita vya Maji Maji, mwaka 1905 hadi 1907, na vyombo vya dola.

Lissu: Shahidi, naomba ufafanue hilo ulilosema kwamba haya ni mauaji makubwa kufanywa na Serikali toka kipindi cha Maji Maji.

Heche: Nimesema hivyo, Waheshimiwa Majaji, kwa sababu nafahamu historia ya nchi yetu.

Kwa sababu Dar es Salaam watu 130, Mwanza watu 90, na Mbeya na kwingineko.

Hakuna Serikali iliyowahi kuua watu wengi...

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 15.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa mhusika yeyote kuwajibika vyovyote.

Heche: Waheshimiwa Majaji, sijawahi kusikia mtu yeyote akiwajibika kwa namna yoyote kwa mauaji makubwa ya namna hii siku ya uchaguzi.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, ufahamu wako iwapo kuna Kiongozi wa Serikali aliyewahi kuwajibika kwa mauaji hayo.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakuna Kiongozi yeyote wa Serikali aliyewajibika kwa namna yoyote.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo hotuba ya Jaji Chande imetoa jina la Kiongozi yeyote aliyetoa amri ya kutekeleza mauaji hayo.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakuna sehemu yoyote katika hotuba ya Jaji Chande iliyomtaja Kiongozi aliyetoa amri ya kutekeleza mauaji hayo.

Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, uwepo wa kesi ya mauaji dhidi ya mtu yeyote aliyehusika na mauaji makubwa hivi.

Heche: Waheshimiwa Majaji, sina ufahamu wa kesi yoyote ya mtu aliyekamatwa kwa kuhusika na mauaji makubwa hivi.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, walio uawa ni binadamu au wanyama pori waharibifu wa mazao?

Jaji Ndunguru: Rudia swali. Limekuwa multiple choice.

Lissu: Naomba kurudia swali.

Waeleze Waheshimiwa Majaji, Shahidi, kuhusu uhalali wa Serikali kuua watu wake.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakuna uhalali wa Serikali kuua watu wake, tena kwa idadi kubwa kiasi kile.

Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, hoja yetu ya kuahirisha uchaguzi ili tupate sheria nzuri za kusimamia uchaguzi ingekubaliwa, ingekuwaje?

Heche: Waheshimiwa Majaji, hoja zetu zingekubaliwa, pasingetokea maafa makubwa kiasi hicho.

Jaji Ndunguru: Hiyo ni fact au assumption?

Lissu: Shahidi amesema kwa ufahamu wake.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji, nini kilikuwa kisababishi cha kwanza alichotaja Jaji Chande cha maafa hayo?

Heche: Alisema ni madai ya muda mrefu ya Watanzania kutaka:

  • Katiba mpya;
  • Tume huru ya uchaguzi;
  • Kupambana na rushwa na ufisadi;
  • Ukosefu wa ajira;
  • Watu kutekwa nyara na kupotezwa;
  • Kutokushughulikiwa kwa masuala hayo.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Hiyo lissu alikua gerezani hao chadema walifungiwa kufanya siasa sasa mambo si yaliishia apo hata siasa hawakufanya Tena mpaka vurugu zikaja kutokea siku ya uchaguzi huoni kama viongozi ndio wamewapa hasira wananchi wao wenyewe

..Lissu alikuwa gerezani.

..Mama alikuwa huku nje na kibunda chake cha BILLION 200 kwa ajili ya kampeni.

..halafu Mama pamoja na mapesa yote hayo analalamika eti watu walihongwa kufanya vurugu Oct 29.

..sijui mnanielewaa?!
 
Alisema wapi? Acha uongo
Kama hujui kauli hii ameongea Raisi basi inaonesha ujui unachoshabikia na sio tu Raisi pekee mpaka Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba na yeye ndio alikuwa wa Kwanza kuongea kwenye press yake ya Kwanza na waandishi habari
 
Nimekuuliza swali fupi sana. Haya maneno unahororoja ya nini? Weka ushahidi wa tuhuma yako hii
 
Hakuna mtu ana utulivu wa kujibu maswali kama Heche. Lissu anaweza kupanic lakini siyo Heche. Fuatilia mahojiano yote hasa aliyofanya na Manara. Manara alikuwa anajitahidi sana kumtoa kwenye mstari ila Heche akawa na utulivu sana. Ndio maana mpaka leo Manara anakazania kutaka mdahalo na Heche kwa kuwa kwenye redio yao aligaragazwa sana hasa alipoambiwa "check your facts" alipokuwa anataka kuaminisha watu bei ya mafuta Kenya ilikuwa kubwa kuliko ya Tanzania kwa kipindi kile.
Ile video ya mahojiano pale Wasafi kati ya Heche na Wasafi, Heche alikuwa mtulivu sana, Manara alijaribu kumkomoa jamaa ila jamaa akamtuliza na ikaonekana Manara kama fala tu.
 
Kesi ya Uhaini ya Lissu inaendelea huku John Heche akitarajiwa kuendelea kutoa ushahidi Mahakamani Sept. 11. 2026 ambapo jana Septemba 10 Mahakama Kuu ilikataa ombi la mshtakiwa Tundu Lissu la kuwaita baadhi ya mashahidi wa utetezi katika Kesi ya Uhaini Na. 19605/2025, ikieleza kuwa ushahidi wao hauna umuhimu kwani wajibu wa kuthibitisha kosa ni wa Jamhuri.

Aidha, Mahakama imeamuru kutolewa kwa wito (summons) kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF) Jenerali Jacob Mkunda, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camillus Wambura na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) Ramadhani Kingai ili wafike kutoa ushahidi upande wa utetezi. Kesi imeahirishwa hadi Septemba 11, 2026

Kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es salaam kwenye kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu na kuulizia kama salamu zake za rambirambi zimefika kwa Samia aliyefiwa na Mume wake.

Mahakama imeanza na leo tunaendelea na Sehemu ya 398

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ya Dar es Salaam, kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, inaendelea kwa shahidi wa tano wa utetezi kuendelea kutoa ushahidi wake. Shahidi huyo wa tano ni John Heche, ambaye kama kawaida alishawasili hapa mahakamani asubuhi na mapema sana, majira ya saa moja na nusu.

Mwenyekiti wetu Mhe. Tundu Lissu pia amewasili tayari ndani ya Ukumbi wa Mahakama.

Majaji pia wameingia, watu wote wakiwa wamesimama.

Mwenyekiti alikuwa kama na Dakika tatu za kusalimiana humu ndani kwa kuwaita wa watu kwa Majina kama kawaida yao.

Anasimama Wakili wa Serikali Ajuaye kutambulisha mawakili wa Serikali waliopo.

Anasema wao wapo tayari.

Mhe. Lissu kaulizwa kama yupo tayari, kajibu yupo tayari.

Shahidi anaambiwa apande Kizimbani so anaelekea kwenye kizimba cha kutolea ushahidi.

Lissu: Waeleze Majaji kwenye simu aliyokupigia Amani Golugwa alikuambia nini hasa.
Heche: Waheshimiwa Majaji Simu aliyonipigia Amani Golugwa alikuwa ananipa taarifa ya kuhudhuria Mkutano na watiania
Lissu: Waeleze Majaji Amani Golugwa alikuambia lengo la kukutana na watia nia ni nini?
Heche: Lengo la kukutana na watia nia ni kuendelea kufafanua kuhusu msimamo wa chama wa No Reforms No Election
Lissu: Waeleze majaji, Amani Golugwa alikuambia mkutano huo umeandaliwa na nani na utafanyika wapi?
Heche: Aliniambia Mkutano umeandaliwa na Sekretarieti ya Chama chini ya Katibu Mkuu na utafanyika Makao Makuu ya Chama Mikocheni Dar es Salaam.
Lissu: Sasa shahidi, tuhuma inayonikabili hapa Mahakamani inadai kwamba mimi ndio niliandaa huo mkutano, wewe unasemaje
Heche: Waheshimiwa Majaji hilo sio kweli, kwasababu Lissu hakuandaa mkutano mimi na yeye tulikuwa ziarani wala hakuhusika.
Lissu: Waeleze Majaji alikuambia nini juu ya waalikwa wengine nje ya watia nia.
Heche: Aliniambia kwamba Sekretarieti imeshaandaa mkutano na waalikwa wengine wote kupitia sekretarieti.

Lissu: Waeleze Majaji Amani alikuambia hao waalikwa wengine ni wakina nani
Heche: Hakufafanua kwa undani wageni wengine lakini aliniambia wapo waalikwa wengine.
Lissu: Tuhuma dhidi yangu zinasema kuwa mimi nilialika waandishi wa habari kwenye huo mkutano wewe unasemaje?

Heche: Hilo nalo sio kweli kwasababu maandalizi yote yalifanywa na Sekretarieti na sisi tulikuwa ziarani kwahiyo Lissu hakuhusika kabisa
Lissu: Waeleze Majaji hiyo tarehe 3/4/2025 wewe ulikuwa wapi.

Heche: Siku ya tarehe 3/4/2025 mimi pia nilikuwa miongoni mwa viongozi walioshiriki na nilipata nafasi pia ya kuzungumza kwenye huo mkutano uliofanyika makao makuu ya chama Mikocheni.

Lissu: Waeleze majaji viongozi wengine waliokuwepo kwenye huo mkutano

Heche: Alikuwepo Mwenyekiti Chadema Taifa Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Chadema Zanzibar, Nilikuwepo mimi, Katibu Mkuu John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Amani Golugwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Brenda Rupia Mkurugenzi wa Habari, Wakurugenzi wa chama, Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani Boniface Jacob pamoja na watia nia wenyewe waliotoka maeneo mbalimbali

Lissu: Waeleze Majaji nje ya viongozi na watia nia uliowataja, eleza uwepo wa watu wengine

Heche: Nakumbuka uwepo wa watu wengine nje ya hao niliowataja, kulikuwepo na waandishi wa habari, Mchungaji na Sheikh ambao waliomba ndio tukafungua kikao
Lissu: Waeleze majaji waandishi wa habari walikuwa wangapi
Heche: Waandishi wa habari walikuwa wengi kutoka vyombo mbalimbali idadi kamili sikumbuki na sikuwa na interest ya kuhesabu
Lissu: Waeleze Majaji hao waandishi wa habari walikuwa na nini
Heche: Walikuwa na camera, notebook, kalamu, vinasa sauti na vifaa vingine vya utendaji kazi vya waandishi wa habari

Lissu: Waeleze majaji idadi ya watu waliokuwepo kwenye huo ukumbi

Heche: Walikuwa watu wengi sina hakika ya idadi ya namba ila ni zaidi ya watu 200.

Sehemu ya 399

Makam Mwenyekiti John Heche anaendelea kutoa ushahidi wake.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji huo Mkutano ulifunguliwa na nani?

Heche: Ulifunguliwa na Sekretarieti kwa maana ya Katibu Mkuu, alianza kuzungumza na baadae kutukaribisha sisi viongozi kwa hierarchy.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji baada ya Katibu Mkuu kuzungumza alimkaribisha nani?

Heche: Alinikaribisha mimi nikazungumza kidogo na nikakukaribisha wewe Mwenyekiti

Mhe. Lissu: Mkutano ulichukua muda gani?

Heche: Masaa zaidi ya manne

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji mimi nilizungumza kwa muda gani

Heche: Waheshimiwa majaji mwenyekiti Tundu Lissu alizungumza zaidi ya masaa mawili.

Mhe. Lissu: Sasa shahidi maneno ninayoshtakiwa nayo yanasema hivi (Lissu anasoma maneno ya kwenye hati ya mashtaka), anauliza swali sasa, hayo maneno niliyoyasoma yamechukua muda gania?

Heche: Hayajamaliza hata dakika moja

Mhe. Lissu: Waeleze majaji katika hotuba yangu kama maneno niliyozungumza ni haya tu niliyoyasoma kwenye hati ya mashtaka

Heche: Waheshimiwa majaji hotuba ilikuwa na maneno mengi sio hayo tu uliyoyasoma kwenye hati ya mashtaka.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji maneno mengine niliyozungumza

Heche: Alizungumza kuhusu mfumo wetu wa uchaguzi jinsi ulivyo mbovu, hauku huru, umeharibiwa, namna ambavyo hauwezeshi wananchi kupata viongozi wanaowataka, namna ambavyo ni vigumu kwa mgombea wa upinzani hasa Chadema kufanikiwa kushinda uchaguzi hata kama anakubalika.

Aliezelea namna ambavyo mfumo unasababisha maafa na mauaji hasa wakati wa Uchaguzi, namna ambavyo mfumo huu unapendelea chama kimoja cha CCM kuanzia uchaguzi wa Rais mpaka madiwani na uchaguzi wa serikali za mitaa.

Alieleze namna ambavyo Polisi na Vyombo vya Dola na watumishi wa umma wanatumika kuharibu Uchaguzi, kwa ujumla alieleza namna mfumo usivyo huru na hautendi haki na unavyopaswa kubadilishwa kabla ya uchaguzi mwingine kuendelea.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilisema nini hasa kuhusu kinachopaswa kubadilishwa

Heche: Waheshimiwa Majaji, alizungumza kinachopaswa kubadilika ni mabadiliko ya Kikatiba na kisheria yanayosimamia chaguzi zetu. Mabadiliko ya namna ya kupata wawakilishi hasa Wabunge na mgawanyo wa majimbo.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilisema nini juu ya namna ya kuondoa maafa wakati wa uchaguzi?

Heche: Waheshimiwa Majaji, alisema namna ya kuondoa maafa ni kutengeneza mfumo wa uchaguzi ambao hauna upendeleo ambao ni huru na Haki unaotoa mazingira ya ushindani sawia bila kupendelea.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilisema nini juu ya mabadiliko yanayotakiwa kwenye Tume ya Uchaguzi.?

Heche: Alisema ni kutengeneza muundo mpya wa Tume ambao haumpi mamlaka Mwenyeti wa CCM kuunda na kutengeneza Tume kwahiyo kuwe na mfumo mpya kuanzia ngazi ya Taifa mpaka kwenye kata ili Tume iwe na watumishi wake wanaojitegemea isiwe inaazima watumishi wa Serikali ambao wote wanachukua maelekezo kutoka kwa waajili wao na hiyo Tume ndio iwe na mamlaka ya kugawa majimbo kulingana na vigezo vinavyofaa na sio upendeleo.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kwenye Hotuba yangu nilisemaje kuhusu kampeni za uchaguzi?

Heche: Tundu Lissu alitoa mifano namna ambavyo kampeni za Uchaguzi zinavyovurugwa na vyombo vya dola kama Polisi, Tume yenyewe ya Uchaguzi kupitia Kamati za Maadili na alitoa mfano wa namna yeye alivyosimamishwa kufanya kampeni za uchaguzi mkuu wa 2020 na wagombea wetu wengi namna wanavyopata matatizo wakati wa kampeni.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kuhusu wagombea wa vyama vya upinzani kuenguliwa hasa wa Chadema.

Sehemu ya 400

Heche: Lissu alieleza kwa kirefu kuhusu wagombea wa upinzani wanavyoenguliwa kwasababu zisizo za kisheria wala za kikatiba na akaeleza kwamba kwenye uchaguzi wa 2020 ndio ulivunja rekodi kwa wagombea wengi wa upinzani kuenguliwa na hivyo CCM kupita bila kupingwa.

Akatoa mifano kuwa hiyo engua engua inawanufaisha CCM kwasababu hata mgombea wa kitongoji wa CCM hajawahi kuenguliwa, akawa anatoa mfano wa Suzani Limbweni Kiwanga aliyekuwa mgombewa wa Jimbo la Mlimba namna alivyoenguliwa na alikuwa mbunge wa jimbo hilohilo mwaka 2015.

Alitoa ifano ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa wa 2024 kuwa ulivunja rekodi zote za engua engua na kwamba hata kama tutaenda kwenye Uchaguzi na tukaenguliwa wote sasa hapo tutakuwa tumeshiriki nini, hivyo haikuwa na maana ya sisi kushiriki halafu tukaenguliwa wote.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji nilisema nini kuhusu mawakala wa vyama na wagombea?

Heche: Lissu alieleza kuwa wakala anapaswa kuwa muwakilishi wa mgombea na Chama chake lakini sasa taratibu zimewekwa ngumu kuanzia namna ya kuwaapisha na kupewa utambulisho, wengi wanakuwa wanafungiwa nje wanazuiliwa kuingia kwenye vituo na wengine kukamatwa na polisi na hivyo wagombea na Chadema kukosa mawakala kwenye vituo.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilisema nini kuhusu yanayotokea siku ya uchaguzi?

Heche: Lissu alieleza namna ambavyo usumbufu unakuwepo siku ya uchaguzi, namna ya wapiga kura kupata majina yao, mara jina halionekani , mara limewekwa kituo kingine.

Alielezea pia namna ambavyo kura zisizo halali zinavoingizwa kwenye vituo vya kupigia kura, namna ambavyo mawakala wananyimwa fomu za matokeo na fomu za kujaza malalamiko wanayoyaona kwenye vituo vya kupigia kura lakini pia namna ambavyo majumuisho yanavyofanyika na kura kutangazwa ambazo sio halali.

Shahidi anakumbukumbu ni kama ile Hotuba yote ya Mhe. Lissu ipo kichwani.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilisema nini kuhusu kupinga mambo haya mahakamani???

Heche: Lissu alieleza namna ambayo ni ngumu na watu mbalimbali wamejaribu kupinga mambo haya kupitia njia za Kimahakama.

Lakini pia alieleza namna ambavyo hata ushahidi ni mgumu kuupata maana unakuwa umeharibiwa, ugumu wa fomu za matokeo maana zinakuwa zinaharibiwa na wasimamizi wa uchaguzi, alieleza pia gharama kubwa ambazo zinatakiwa kulipwa na wagombea au walalamikaji wanapotaka kufungua kesi ambavyo wanakuwa hawawezi.

Akaeleza pia wingi wa kesi ambazo zingefunguliwa mfano wakati wa uchaguzi wa 2024 ambapo vijiji tu ni zaidi ya elfu kumi na saba ambavyo uchaguzi uliharibiwa kwahiyo isingekuwa rahisi kwa Chama kufungua kesi akamalizia kwamba kupitia kesi ya Mtikila Mahakama ilisema kwamba matatizo ya kisiasa yanapaswa kutatuliwa kisiasa sio lazima yaende Mahakamani.

Waheshimiwa majaji alisema pia kwamba kupitia kesi ya Dr. Amani Walid Kabourou ilisema kwamba uchaguzi ambao sio huru na haki sio Uchaguzi.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilisema nini kuhusu hoja ya kuahirisha uchaguzi wa mwaka jana??

Heche: Waheshimiwa majaji Lissu alisema kwamba sisi kama chama tuko tayari Uchaguzi usogezwe mbele yafanyike kwanza mabadiliko ya kikatiba na kisheria yatakayoruhusu Uchaguzi huru na wa haki ili kuepusha maafa kama mauaji, utekaji, watu kujeruhiwa na kwamba Uchaguzi ukisogezwa mbele wananchi watapata haki ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Sehemu ya 401

Mhe. Lissu: Waeleze majaji utofauti wa hotuba yangu ya tarehe 03/04/2025 na hotuba za mikutano ya hadhara na tulipokutana na wadau.

Heche: Hotuba ya tarehe 03/04/2025 ni iileile na hotuba na wadau na mikutano ya hadhara hakuna utofauti labda ni maneno tu lakini alizungumzia matatizo ya uchaguzi na namna ya kuyarekebisha.

Mhe. Lissu: Kuna ushahidi umeletwa hapa kuwa mkutano wa tarehe 03/04/2025 ulilushwa live?

Heche: Mimi nilikuwa ndani kwenye mkutano sina ufahamu kama ulikuwa live au haukuwa live lakini waandishi wa habari walikuwepo kwenye mkutano.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kuhusu recordings za mkutano huo wa Tarehe 03/04/2025 kama uliona kwenye Jambo Tv??

Heche: Niliona kwenye YouTube channel mbalimbali kama Mwanzo, the Chanzo na hata Jambo TV niliona.

Mhe.Lissu: Waeleze majaji hicho ulichoona katika YouTube ya Chanzo, Mwanzo na Jambo TV zina urefu wa muda gani?

Heche: Kwenye Jambo TV ipo kama takribani masaa mawili, Chanzo ipo video ya dakika 45, na Mwanzo Tv kama dakika 60 hivi au lisaa na kitu yaani ziko tofauti tofauti.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno haya (Lissu anasoma maneno ya kwenye hati ya mashtaka… wanasema msimamo huu unaashiria uasi … tutaenda kukinukisha sana sana),

Heche: Ni miongoni mwa maneno ambayo yapo niliyoyasikia

Mhe. Lissu: Waeleze majaji yale uliyoyazungumzia kwenye ushahidi wako kama yapo.

Heche: Yapo maneno hayo niliyoyasema kwenye ushahidi wangu kama vile kuepusha maafa, engua engua ya wagombea na mengine mengi maana ni hotuba ya masaa mengi.

Mhe. Lissu: Shahidi shtaka ambalo nashitakiwa nalo linaeleza kwamba mimi ndio nilichapisha hayo maneno Jambo Tv wewe unasemaje?

Heche: Waheshimiwa Majaji, sio kweli kwasababu Lissu sio mfanyakazi wa jambo TV na kuna Shahidi wa Jamhuri yule wa kwenye kiboksi humu alisema yeye ndio aliyechapisha, anaitwa P ni shahidi wa 17 wa Jamhuri.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji juu ya mimi kufanya chochote kwenye Mkutano huo zaidi ya kuzungumza???

Heche: Mwenyekiti wetu, Tundu Lissu hakugusa kitu chochote zaidi ya kuzungumza, hakugusa kamera wala radio.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa kosa la uasi kwenye Katiba ya Tanzania??

Heche: Sina ufahamu wa uwepo wa kosa lolote la uasi kwenye katiba.

Mhe.Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa kosa la kuhamasisha uasi kwenye Katiba ya Tanzania.

Heche: Sina ufahamu wowote wa kosa la kuhamasisha uasi kwenye Katiba.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamu wako uwepo wa kosa la kuvuruga uchaguzi kwenye Katiba.

Heche: Sina ufahamu wa uwepo wa kosa la kuvuruga uchaguzi kwenye katiba

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kuhusu uwepo wa kosa la kuzuia uchaguzi kwenye Katiba

Heche: Kwa ufahamu wangu hakuna uwepo wa kosa la kuzuia uchaguzi kwenye katiba.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamu wako uwepo wa kosa la kuhamasisha watu kuzuia uchaguzi?

Heche: Kwa ufahamu wangu hakuna uwepo wa kosa la kuhamasisha watu kuzuia uchaguzi kwenye Katiba.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji ufahamu wako kuhusu uwepo wa kosa la kukinukisha kwenye katiba hii?

Heche: Kwa ufahamu wangu hakuna uwepo wa kosa la kukinukisha kwenye Katiba

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwa ufahamu wako wako uwepo wa kosa linaloitwa kuzuia watu kwenda kupiga kura kwenye Katiba.

Heche: kwa ufahamu wangu hakuna kosa hilo kwenye katiba.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa kosa la uasi au rebellion kwenye Kanuni ya Adhabu.

Heche: Kwa ufahamu wangu sifahamu uwepo wa kosa la rebellion kwenye Sheria

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwa ufahamu wako uwepo wa kosa la kuhamasisha uasi kwenye Penal Code.

Heche: Sina ufahamu wa uwepo wa kosa la kuhamasisha uasi kwenye kwenye Kanuni ya Adhabu

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji ufahamu wako kuhusu uwepo wa kosa la kuvuruga uchaguzi kwenye Kanuni ya Adhabu

Heche: Sina ufahamu kuhusu uwepo wa kosa la kuvuruga Uchaguzi kwenye Kanuni ya Adhabu.

Sehemu ya 402

Makamu Mwenyekiti John Heche anaendelea kutoa ushahidi wake.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa kosa la kuzuia Uchaguzi kwenye Kanuni ya Adhabu?

Heche: Sina ufahamu wa uwepo wa kosa la kuzuia uchaguzi kwenye kanuni ya Adhabu

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwa ufahamu wako uwepo wa kosa la kukinukisha kwenye Kanuni ya Adhabu.

Heche: Sina ufahamu wa kosa la kukinukisha kwenye Kanuni ya Adhabu

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kuhusu uwepo wa kosa la kuvuruga uchaguzi kwenye Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2024??

Heche: Hakuna uwepo wa kosa la kuvuruga uchaguzi kwenye Sheria hiyo ya Uchaguzi.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kuhusu uwepo wa kosa la kuzuia uchaguzi kwenye Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2024???

Heche: Hakuna hilo kosa la kuzuia uchaguzi

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kuhusu uwepo wa kosa la kukinukisha kwenye Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2024

Heche: Hakuna uwepo wa kosa la kukinukisha kwenye Sheria ya Uchaguzi ya Mwaka 2024.

Mhe. Lissu: Shitaka linalonikabili linasema nilitengeza nia ya kuzuia uchaguzi wa 2025, waeleze majaji uwepo wa kosa la kutengeneza nia ya kuzuia uchaguzi kwenye Kanuni ya Adhabu???

Heche: Kwa ufahamu wangu hakuna uwepo wa kosa la kutengeneza nia ya kuzuia uchaguzi kwenye Kanuni ya Adhabu.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa kosa la kutengeneza nia ya kuzuia uchaguzi kwenye Katiba???

Heche: Hakuna kosa la kutengeneza nia ya kuzuia Uchaguzi kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno Serikali ya JMT kwenye hotuba yangu?

Heche: Hakuna mahali popote ambapo Mhe. Tundu Lissu alitaja Serikali ya JMT.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kuhusu uwepo wa maneno Rais wa JMT.

Heche: Hakuna maneno Rais wa JMT kwenye hotuba iliyotolewa na Tundu Lissu

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kuhusu uwepo wa maneno Makamu wa Rais wa JMT.

Heche: Hakuna uwepo wa maneno Makamu wa Rais wa JMT.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Waziri Mkuu wa JMT kwenye hotuba yangu ya tarehe 03/04/2025

Heche: Hakuna mahali ambapo alitajwa Waziri Mkuu wa JMT.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Baraza la Mawaziri wa JMT kwenye hotuba yangu?

Heche: Hakuna maneno Baraza la Mawaziri wa JMT kwenye hotuba ya Lissu.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Waziri, Naibu Waziri, Wakuu wa Mikoa au Wilaya?

Heche: Hakuna maneno Waziri, Naibu Waziri, wakuu wa mikoa au wilaya kwenye hotuba ya Tundu Lissu.

Mhe.Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Mkurugenzi wa Mashtaka?

Heche: Hakuna uwepo wa maneno Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya JMT au Mkurugenzi wa Mashtaka.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno halmshauri ya Mji, jiji, wilaya au Serikali ya mtaa?

Heche: Kwenye hotuba nzima hakuna maneno Halmashauri ya mji, jiji, wilaya, kitongoji , kijiji wala serikali ya mtaa.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno Wakurugenzi wa jiji, Manispaa, Halmashauri wala watendaji wa kata, vijiji?

Heche: Waheshimiwa Majaji kwenye hotuba yote Hakuna maneno wakurugenzi wa jiji, manispaa, halmashauri wala watendaji wa kata na vijiji.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno jeshi la polisi, jeshi la ulinzi, jeshi la akiba, mgambo wa jiji, jeshi la wananchi wa Tanzania na maneno ya aina hiyo???

Heche: Hakuna maneno Jeshi la Polisi, Jeshi la Ulinzi, Jeshi la akiba, mgambo wa jiji, Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye hotuba nzima ya Lissu.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji maneno yaliyopo kwenye hati ya mashtaka yanamtishia nani?

Heche: Waheshimiwa majaji, hayo maneno ni ya kawaida tu na wala hayajamtishia mtu yeyote.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji maneno niliyokusomea yana kosa gani?

Heche: Waheshimiwa majaji hayo ni maneno ya kawaida kwenye siasa hivyo hayana kosa lolote

Sehemu ya 403

Mhe. Lissu: Waeleze majaji katika Mkutano wa 3/4/2025 uwepo wa maneno tutaenda kuchoma vituo vya kupigia kura moto?

Heche: Hakuna hayo maneno ya tutaenda kuchoma moto vituo vya kupigia kura kwenye hotuba wala kwenye video.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno tutaenda kuchoma vituo vya mwendokasi, ofisi za CCM na Serikali???

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakuna uwepo wa hayo maneno ya tutaenda kuchoma vituo vya mwendokasi, ofisi za CCM na Serikali hata kwenye video hayapo.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno tutakwenda kukata watu vidole?

Heche: Hakuna hayo maneno ya kusema tukakate watu vidole.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno watu wakaue Polisi au mtumishi wa Tume au mtu mwingine yeyote???

Heche: Waheshimiwa majaji, Tundu Lissu hakusema watu wakaue Polisi au mtumishi wa Tume au mtu mwingine yeyote.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji ufahamu wako kuhusu hotuba ya Jaji Othman Chande ya Matukio ya Oktoba 29???

Heche: Naifahamu

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama uliisikiliza yote?

Heche: Niliisikiliza yote.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo au kama Jaji Chande alisema vurugu za Oktoba 29 zilitokana na maneno ya Tundu Lissu???

Heche: Jaji Chande hakusema kuwa vurugu za Oktoba 29 zilitokana na maneno ya Tundu Lissu.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwenye hotuba wa Jaji Chande uwepo wa maneno juu ya aliyechochea au waliochochea??

Heche: Kwenye hotuba hiyo Jaji Chande hakutaja mtu yeyote aliyechochea, hakumtaja Lissu wala mtu yeyote.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa jina au majina ya chama cha siasa kilichochochea vurugu za Oktoba 29, 2025.

Heche: Kwenye hotuba hakuna jina au majina ya chama cha siasa kilichochochea vurugu za Oktoba 29, 2025

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa majina ya watu waliokata watu vidole au watu waliokatwa vidole?

Heche: Hanna uwepo wa majina ya watu waliokata au waliokatwa vidole.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwenye hotuba ya Chande uwepo wa majina ya askari polisi waliouwawa na watu waliowaua hao askari??

Heche: Hakuna majina ya askari waliouwawa au watu waliowaua.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji, majina ya watu waliouwawa au majina ya watu waliowaua???

Heche: Hakuna uwepo wa majina ya watu waliowawa na watu waliowaua.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji, kwenye hotuba ya Chande uwepo wa maeneo ambayo vituo vya mwendokasi , ofisi za CCM au za Serikali .

Heche: Sina kumbukumbu na hilo

Leo mshtakiwa na shahidi wake wanagonga nyundo sana, wanatema madini wote,

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa orodha ya magari ya watu binafsi au Serikali?

Heche: Hakuna mahala ambapo ilitolewa orodha ya magari, hakuna hata moja.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji, kuhusu wewe au viongozi wa chama kuitwa kwenda kueleza kuhusu chochote mbele ya Tume ya Jaji Chande.

Heche: Mimi binafsi sikuwahi kuitwa na sina ufahamu wa kiongozi yeyote wa chama chetu kwenda kutoa maelezo mbele ya Tume ya Jaji Chande.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kwa haya uliyoyatolea ushahidi, kwa ufahamu?

Heche: Siko kwenye nafasi nzuri ya kueleza wao walichunguza nini ila sisi hawakutusikiliza wala kutuita.

Sehemu ya 404

Lissu: Waeleze ufahamu wako juu ya jitihada za mazungumzo na Serikali kabla ya msimamo wa No reforms, No election?

Heche: Mimi binafsi nilishiriki, nilikuwa kwenye team ya CHADEMA iliyokutana na Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwepo mwaka 2022- 2025 Ikulu Dodoma.

Tulizungumza nae kutokana na malalamiko ya uchaguzi ya muda mrefu hasa uchaguzi wa 2019 na 2020 baadae Chama kilianzisha madai ya kampeni ya Katiba Mpya na mifumo ya uchaguzi wakati huo Mwenyekiti alikuwa ni Freeman Mbowe.

Tulienda Mwanza mwaka 2021 tulifanya Kongamano la kudai Katiba Mpya ili kuwezesha mabadiliko ya Uchaguzi, kama nilivyoeleza Mbowe alikamatwa na mimi nilikamatwa.

Baada ya Mbowe kutokea Ikulu ndio tukaenda kukutana na Rais Ikuku Chamwino Dodoma alikuwepo Mwenyekiti Mbowe, Said Issa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama chetu Zanzibar, Katibu Mkuu John Mnyika, na mimi mwenyewe.

Upande wa Serikali alikuwepo Rais Samia, Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati huo Jaji Eliezer Mbuki Feleshi, Waziri George Simbachawene, Jenister Mhagama sasa ni marehemu ila alikuwa Waziri,

Upande wa CCM alikuwepo Makamu Mwenyekiti wa CCM wa wakati huo mzee Abdullahiman Kinana na viongozi wengine wa CCM siwakumbuki vizuri.

Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu walieleza jinsi ambavyo tumenyanyaswa na kuonewa na uharibifu wa Uchaguzi,

Watu waliokimbia nchi na mambo mengine yaliyotokana na uchaguzi kwenye kile kikao ilikubaliwa kuwa iundwe Team ya watu watano, watano kutoka kila chama na upande wa Serikali.

Hizo team zingeenda kupitia kwa kina mifumo ya uchaguzi, matatizo ya kiuchaguzi na mapendekezo ya mabadiliko ya katiba na sheria za uchaguzi kabla ya 2025.

Upande wa Chadema iliundwa team iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Mbowe, Katibu Mkuu John Mnyika, Wakili Jeremia Mtobesya, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama kutoka Zanzibar Mhe. Zeudi Mvano, na mimi John Wegesa Heche nilikuwemo.

Upande wa CCM namkumbuka Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdullahiman Kinana, Andrew Chenge, wawakilishi wawili kutoka Zanzibar siwakumbuki majina yao na kulikuwa na Mawaziri, mwanzo aliingia Jenister Mhagama na baadae akaja Simbachawene.

Hayo mazungumzo yalichukua mwaka mzima na sehemu tuliandika na kupeleka mapendekezo yetu namna ya kukwamua mchakato wa Katiba namna ya kuukwamua, mapendekezo ya kisheria namna ya kuukwamua mchakato wa Katiba, Vyombo ambavyo vingeundwa katika kuhakikisha vinaandika katiba kuanzia mwanzo ikiwemo kuchakata maoni.

Tulipeleka pia mapendekezo ya sheria ya Uchaguzi, mapendekezo ya namna ya kuunda Tume Huru ya Uchaguzi, tulizungumza kuhusu kesi mbalimbali watu wetu walizokuwa wamebambikiziwa na wengine kufungwa kwa uongo, tulizungumza kuhusu viongozi waliokuwa wamekimbia nchi kwasababu ya usalama wao Makamu Mwenyekiti Mhe. Lissu, Godbless Lema, Ezekia Wenje Dibogo na wengine, madai ya kuwaondoa wabunge 19 (Covid-19) ambao walijipeleka Bungeni kinyume na taratibu za chama,

Tulizungumza kuhusu kufungulia mikutano ya hadhara iliyokuwa imefungwa kwa tamko la Rais Magufuli kinyume cha Sheria, namna ya kukomesha matukio ya utekaji watu.

Mhe. Lissu: Naomba tuahirishe baada ya lisaa na nusu turejee shahidi aje kuendelea na nina uhakika atamaliza leo

Jaji Ndunguru: Wakili wa Serikali

Katuga: hatuna pingamizi

Jaji Ndunguru: tujitahidi tumalizan
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 16.

Lissu: Jaji Mkuu Othuman Chande alisema nini juu ya utekaji nyara na upotezaji wa watu, kwa kumbukumbu zako?

Heche: Alisema watu wanatekwa, Waheshimiwa Majaji, kwa sababu za kimapenzi, ushirikina na sababu za kibiashara.

Lissu: Umetaja watu wa CHADEMA na CCM, akiwemo Humphrey Polepole na Kanguye wa CCM. Hili Jaji Mkuu Othuman Chande alisemaje juu ya hawa?

Heche: Hakusema lolote.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, uwezekano wa mtu kujiteka mwenyewe.

Nassoro Katuga: Sina sababu ya kuweka objection. Shahidi hatakiwi kutoa opinion na kupewa leading questions. Hili swali la mwisho kashajengewa uwezo, ndiyo anaulizwa.

Ni hayo, Waheshimiwa Majaji.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, swali langu liko very simple: Aeleze uwezekano wa mtu kujiteka.

Nassoro Katuga: Huyu siyo expert. Anachokitoa hapo ni opinion.

Lissu: Hilo naachana nalo, lisitupotezee muda.

Lissu: Shahidi, tueleze aina za utekaji alizoeleza Jaji Chande.

Heche: Hakueleza aina za utekaji. Utekaji ni mmoja tu.

Lissu: Kwenye ushahidi wako ulisema kwamba ulipotoka katika mahabusu ya polisi ulisoma taarifa nyingi za mauaji.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, hii siyo sahihi. Shahidi alisema alisikia, hakusema kwamba alisoma. Anamuuliza swali ili tukipinga, ndiyo shahidi aseme.

Lissu: Naomba nisomewe rekodi za Mahakama.

Jaji Ndunguru: (Anasoma rekodi) “Nilipata taarifa nyingi.”

Lissu: Asante, Wakili, kwa kunikumbusha. Kumbe nilipata, siyo nilisoma.

Haya shahidi, tutajie hizo taarifa ulizopata.

Heche: Nilipata taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari, kwa kusoma na kusikiliza. Nilipata ripoti kutoka kwa waangalizi wa kimataifa.

Lissu: Waangalizi wa nini?

Heche: Waangalizi wa uchaguzi.

Nilipata taarifa mbalimbali za jumuiya.

Nilipata taarifa za jumuiya za kikanda kama Afrika Mashariki.

Na taarifa za mashirika ya kidini.

Heche: Waheshimiwa Majaji, naweza kwenda short call?

Jaji Ndunguru: Sawa, tunakuruhusu.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Hakuna mtu ana utulivu wa kujibu maswali kama Heche. Lissu anaweza kupanic lakini siyo Heche. Fuatilia mahojiano yote hasa aliyofanya na Manara. Manara alikuwa anajitahidi sana kumtoa kwenye mstari ila Heche akawa na utulivu sana. Ndio maana mpaka leo Manara anakazania kutaka mdahalo na Heche kwa kuwa kwenye redio yao aligaragazwa sana hasa alipoambiwa "check your facts" alipokuwa anataka kuaminisha watu bei ya mafuta Kenya ilikuwa kubwa kuliko ya Tanzania kwa kipindi kile.
Inaonekana unafuatalia mambo, safi sana.
 
Hiyo lissu alikua gerezani hao chadema walifungiwa kufanya siasa sasa mambo si yaliishia apo hata siasa hawakufanya Tena mpaka vurugu zikaja kutokea siku ya uchaguzi huoni kama viongozi ndio wamewapa hasira wananchi wao wenyewe
[
/QUOTE]

Majibu ni ayo ndugu
Kawasha Moja kisha kaenda Lupango
Lkn MOTO 💥uliendelea kuwaka kufikia
Miundombinu ya Serikali 👈
na watu Binafsi !
Lkn ukiweza kujipa moyo kuwa bado kaonewa iyo ni shida zako
Mahakamani watatenda HAKI tu✍️
 
Attachments

  • 6381504-457b5131fdfe1ba30241f5952f4311e0.mp4
    1.5 MB
  • IMG-20260827-WA0012.jpg
    IMG-20260827-WA0012.jpg
    22.3 KB · Views: 13
Kesi ya Uhaini ya Lissu inaendelea huku John Heche akitarajiwa kuendelea kutoa ushahidi Mahakamani Sept. 11. 2026 ambapo jana Septemba 10 Mahakama Kuu ilikataa ombi la mshtakiwa Tundu Lissu la kuwaita baadhi ya mashahidi wa utetezi katika Kesi ya Uhaini Na. 19605/2025, ikieleza kuwa ushahidi wao hauna umuhimu kwani wajibu wa kuthibitisha kosa ni wa Jamhuri.

Aidha, Mahakama imeamuru kutolewa kwa wito (summons) kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF) Jenerali Jacob Mkunda, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camillus Wambura na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) Ramadhani Kingai ili wafike kutoa ushahidi upande wa utetezi. Kesi imeahirishwa hadi Septemba 11, 2026

Kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es salaam kwenye kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu na kuulizia kama salamu zake za rambirambi zimefika kwa Samia aliyefiwa na Mume wake.

Mahakama imeanza na leo tunaendelea na Sehemu ya 398

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ya Dar es Salaam, kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, inaendelea kwa shahidi wa tano wa utetezi kuendelea kutoa ushahidi wake. Shahidi huyo wa tano ni John Heche, ambaye kama kawaida alishawasili hapa mahakamani asubuhi na mapema sana, majira ya saa moja na nusu.

Mwenyekiti wetu Mhe. Tundu Lissu pia amewasili tayari ndani ya Ukumbi wa Mahakama.

Majaji pia wameingia, watu wote wakiwa wamesimama.

Mwenyekiti alikuwa kama na Dakika tatu za kusalimiana humu ndani kwa kuwaita wa watu kwa Majina kama kawaida yao.

Anasimama Wakili wa Serikali Ajuaye kutambulisha mawakili wa Serikali waliopo.

Anasema wao wapo tayari.

Mhe. Lissu kaulizwa kama yupo tayari, kajibu yupo tayari.

Shahidi anaambiwa apande Kizimbani so anaelekea kwenye kizimba cha kutolea ushahidi.

Lissu: Waeleze Majaji kwenye simu aliyokupigia Amani Golugwa alikuambia nini hasa.
Heche: Waheshimiwa Majaji Simu aliyonipigia Amani Golugwa alikuwa ananipa taarifa ya kuhudhuria Mkutano na watiania
Lissu: Waeleze Majaji Amani Golugwa alikuambia lengo la kukutana na watia nia ni nini?
Heche: Lengo la kukutana na watia nia ni kuendelea kufafanua kuhusu msimamo wa chama wa No Reforms No Election
Lissu: Waeleze majaji, Amani Golugwa alikuambia mkutano huo umeandaliwa na nani na utafanyika wapi?
Heche: Aliniambia Mkutano umeandaliwa na Sekretarieti ya Chama chini ya Katibu Mkuu na utafanyika Makao Makuu ya Chama Mikocheni Dar es Salaam.
Lissu: Sasa shahidi, tuhuma inayonikabili hapa Mahakamani inadai kwamba mimi ndio niliandaa huo mkutano, wewe unasemaje
Heche: Waheshimiwa Majaji hilo sio kweli, kwasababu Lissu hakuandaa mkutano mimi na yeye tulikuwa ziarani wala hakuhusika.
Lissu: Waeleze Majaji alikuambia nini juu ya waalikwa wengine nje ya watia nia.
Heche: Aliniambia kwamba Sekretarieti imeshaandaa mkutano na waalikwa wengine wote kupitia sekretarieti.

Lissu: Waeleze Majaji Amani alikuambia hao waalikwa wengine ni wakina nani
Heche: Hakufafanua kwa undani wageni wengine lakini aliniambia wapo waalikwa wengine.
Lissu: Tuhuma dhidi yangu zinasema kuwa mimi nilialika waandishi wa habari kwenye huo mkutano wewe unasemaje?

Heche: Hilo nalo sio kweli kwasababu maandalizi yote yalifanywa na Sekretarieti na sisi tulikuwa ziarani kwahiyo Lissu hakuhusika kabisa
Lissu: Waeleze Majaji hiyo tarehe 3/4/2025 wewe ulikuwa wapi.

Heche: Siku ya tarehe 3/4/2025 mimi pia nilikuwa miongoni mwa viongozi walioshiriki na nilipata nafasi pia ya kuzungumza kwenye huo mkutano uliofanyika makao makuu ya chama Mikocheni.

Lissu: Waeleze majaji viongozi wengine waliokuwepo kwenye huo mkutano

Heche: Alikuwepo Mwenyekiti Chadema Taifa Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Chadema Zanzibar, Nilikuwepo mimi, Katibu Mkuu John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Amani Golugwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Brenda Rupia Mkurugenzi wa Habari, Wakurugenzi wa chama, Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani Boniface Jacob pamoja na watia nia wenyewe waliotoka maeneo mbalimbali

Lissu: Waeleze Majaji nje ya viongozi na watia nia uliowataja, eleza uwepo wa watu wengine

Heche: Nakumbuka uwepo wa watu wengine nje ya hao niliowataja, kulikuwepo na waandishi wa habari, Mchungaji na Sheikh ambao waliomba ndio tukafungua kikao
Lissu: Waeleze majaji waandishi wa habari walikuwa wangapi
Heche: Waandishi wa habari walikuwa wengi kutoka vyombo mbalimbali idadi kamili sikumbuki na sikuwa na interest ya kuhesabu
Lissu: Waeleze Majaji hao waandishi wa habari walikuwa na nini
Heche: Walikuwa na camera, notebook, kalamu, vinasa sauti na vifaa vingine vya utendaji kazi vya waandishi wa habari

Lissu: Waeleze majaji idadi ya watu waliokuwepo kwenye huo ukumbi

Heche: Walikuwa watu wengi sina hakika ya idadi ya namba ila ni zaidi ya watu 200.

Sehemu ya 399

Makam Mwenyekiti John Heche anaendelea kutoa ushahidi wake.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji huo Mkutano ulifunguliwa na nani?

Heche: Ulifunguliwa na Sekretarieti kwa maana ya Katibu Mkuu, alianza kuzungumza na baadae kutukaribisha sisi viongozi kwa hierarchy.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji baada ya Katibu Mkuu kuzungumza alimkaribisha nani?

Heche: Alinikaribisha mimi nikazungumza kidogo na nikakukaribisha wewe Mwenyekiti

Mhe. Lissu: Mkutano ulichukua muda gani?

Heche: Masaa zaidi ya manne

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji mimi nilizungumza kwa muda gani

Heche: Waheshimiwa majaji mwenyekiti Tundu Lissu alizungumza zaidi ya masaa mawili.

Mhe. Lissu: Sasa shahidi maneno ninayoshtakiwa nayo yanasema hivi (Lissu anasoma maneno ya kwenye hati ya mashtaka), anauliza swali sasa, hayo maneno niliyoyasoma yamechukua muda gania?

Heche: Hayajamaliza hata dakika moja

Mhe. Lissu: Waeleze majaji katika hotuba yangu kama maneno niliyozungumza ni haya tu niliyoyasoma kwenye hati ya mashtaka

Heche: Waheshimiwa majaji hotuba ilikuwa na maneno mengi sio hayo tu uliyoyasoma kwenye hati ya mashtaka.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji maneno mengine niliyozungumza

Heche: Alizungumza kuhusu mfumo wetu wa uchaguzi jinsi ulivyo mbovu, hauku huru, umeharibiwa, namna ambavyo hauwezeshi wananchi kupata viongozi wanaowataka, namna ambavyo ni vigumu kwa mgombea wa upinzani hasa Chadema kufanikiwa kushinda uchaguzi hata kama anakubalika.

Aliezelea namna ambavyo mfumo unasababisha maafa na mauaji hasa wakati wa Uchaguzi, namna ambavyo mfumo huu unapendelea chama kimoja cha CCM kuanzia uchaguzi wa Rais mpaka madiwani na uchaguzi wa serikali za mitaa.

Alieleze namna ambavyo Polisi na Vyombo vya Dola na watumishi wa umma wanatumika kuharibu Uchaguzi, kwa ujumla alieleza namna mfumo usivyo huru na hautendi haki na unavyopaswa kubadilishwa kabla ya uchaguzi mwingine kuendelea.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilisema nini hasa kuhusu kinachopaswa kubadilishwa

Heche: Waheshimiwa Majaji, alizungumza kinachopaswa kubadilika ni mabadiliko ya Kikatiba na kisheria yanayosimamia chaguzi zetu. Mabadiliko ya namna ya kupata wawakilishi hasa Wabunge na mgawanyo wa majimbo.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilisema nini juu ya namna ya kuondoa maafa wakati wa uchaguzi?

Heche: Waheshimiwa Majaji, alisema namna ya kuondoa maafa ni kutengeneza mfumo wa uchaguzi ambao hauna upendeleo ambao ni huru na Haki unaotoa mazingira ya ushindani sawia bila kupendelea.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilisema nini juu ya mabadiliko yanayotakiwa kwenye Tume ya Uchaguzi.?

Heche: Alisema ni kutengeneza muundo mpya wa Tume ambao haumpi mamlaka Mwenyeti wa CCM kuunda na kutengeneza Tume kwahiyo kuwe na mfumo mpya kuanzia ngazi ya Taifa mpaka kwenye kata ili Tume iwe na watumishi wake wanaojitegemea isiwe inaazima watumishi wa Serikali ambao wote wanachukua maelekezo kutoka kwa waajili wao na hiyo Tume ndio iwe na mamlaka ya kugawa majimbo kulingana na vigezo vinavyofaa na sio upendeleo.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kwenye Hotuba yangu nilisemaje kuhusu kampeni za uchaguzi?

Heche: Tundu Lissu alitoa mifano namna ambavyo kampeni za Uchaguzi zinavyovurugwa na vyombo vya dola kama Polisi, Tume yenyewe ya Uchaguzi kupitia Kamati za Maadili na alitoa mfano wa namna yeye alivyosimamishwa kufanya kampeni za uchaguzi mkuu wa 2020 na wagombea wetu wengi namna wanavyopata matatizo wakati wa kampeni.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kuhusu wagombea wa vyama vya upinzani kuenguliwa hasa wa Chadema.

Sehemu ya 400

Makam Mwenyekiti John Heche anaendelea kutoa ushahidi wake.

Heche: Lissu alieleza kwa kirefu kuhusu wagombea wa upinzani wanavyoenguliwa kwasababu zisizo za kisheria wala za kikatiba na akaeleza kwamba kwenye uchaguzi wa 2020 ndio ulivunja rekodi kwa wagombea wengi wa upinzani kuenguliwa na hivyo CCM kupita bila kupingwa.

Akatoa mifano kuwa hiyo engua engua inawanufaisha CCM kwasababu hata mgombea wa kitongoji wa CCM hajawahi kuenguliwa, akawa anatoa mfano wa Suzani Limbweni Kiwanga aliyekuwa mgombewa wa Jimbo la Mlimba namna alivyoenguliwa na alikuwa mbunge wa jimbo hilohilo mwaka 2015.

Alitoa ifano ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa wa 2024 kuwa ulivunja rekodi zote za engua engua na kwamba hata kama tutaenda kwenye Uchaguzi na tukaenguliwa wote sasa hapo tutakuwa tumeshiriki nini, hivyo haikuwa na maana ya sisi kushiriki halafu tukaenguliwa wote.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji nilisema nini kuhusu mawakala wa vyama na wagombea?

Heche: Lissu alieleza kuwa wakala anapaswa kuwa muwakilishi wa mgombea na Chama chake lakini sasa taratibu zimewekwa ngumu kuanzia namna ya kuwaapisha na kupewa utambulisho, wengi wanakuwa wanafungiwa nje wanazuiliwa kuingia kwenye vituo na wengine kukamatwa na polisi na hivyo wagombea na Chadema kukosa mawakala kwenye vituo.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilisema nini kuhusu yanayotokea siku ya uchaguzi?

Heche: Lissu alieleza namna ambavyo usumbufu unakuwepo siku ya uchaguzi, namna ya wapiga kura kupata majina yao, mara jina halionekani , mara limewekwa kituo kingine.

Alielezea pia namna ambavyo kura zisizo halali zinavoingizwa kwenye vituo vya kupigia kura, namna ambavyo mawakala wananyimwa fomu za matokeo na fomu za kujaza malalamiko wanayoyaona kwenye vituo vya kupigia kura lakini pia namna ambavyo majumuisho yanavyofanyika na kura kutangazwa ambazo sio halali.

Shahidi anakumbukumbu ni kama ile Hotuba yote ya Mhe. Lissu ipo kichwani.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilisema nini kuhusu kupinga mambo haya mahakamani???

Heche: Lissu alieleza namna ambayo ni ngumu na watu mbalimbali wamejaribu kupinga mambo haya kupitia njia za Kimahakama.

Lakini pia alieleza namna ambavyo hata ushahidi ni mgumu kuupata maana unakuwa umeharibiwa, ugumu wa fomu za matokeo maana zinakuwa zinaharibiwa na wasimamizi wa uchaguzi, alieleza pia gharama kubwa ambazo zinatakiwa kulipwa na wagombea au walalamikaji wanapotaka kufungua kesi ambavyo wanakuwa hawawezi.

Akaeleza pia wingi wa kesi ambazo zingefunguliwa mfano wakati wa uchaguzi wa 2024 ambapo vijiji tu ni zaidi ya elfu kumi na saba ambavyo uchaguzi uliharibiwa kwahiyo isingekuwa rahisi kwa Chama kufungua kesi akamalizia kwamba kupitia kesi ya Mtikila Mahakama ilisema kwamba matatizo ya kisiasa yanapaswa kutatuliwa kisiasa sio lazima yaende Mahakamani.

Waheshimiwa majaji alisema pia kwamba kupitia kesi ya Dr. Amani Walid Kabourou ilisema kwamba uchaguzi ambao sio huru na haki sio Uchaguzi.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilisema nini kuhusu hoja ya kuahirisha uchaguzi wa mwaka jana??

Heche: Waheshimiwa majaji Lissu alisema kwamba sisi kama chama tuko tayari Uchaguzi usogezwe mbele yafanyike kwanza mabadiliko ya kikatiba na kisheria yatakayoruhusu Uchaguzi huru na wa haki ili kuepusha maafa kama mauaji, utekaji, watu kujeruhiwa na kwamba Uchaguzi ukisogezwa mbele wananchi watapata haki ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Sehemu ya 401

Makam Mwenyekiti John Heche anaendelea kutoa ushahidi wake.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji utofauti wa hotuba yangu ya tarehe 03/04/2025 na hotuba za mikutano ya hadhara na tulipokutana na wadau.

Heche: Hotuba ya tarehe 03/04/2025 ni iileile na hotuba na wadau na mikutano ya hadhara hakuna utofauti labda ni maneno tu lakini alizungumzia matatizo ya uchaguzi na namna ya kuyarekebisha.

Mhe. Lissu: Kuna ushahidi umeletwa hapa kuwa mkutano wa tarehe 03/04/2025 ulilushwa live?

Heche: Mimi nilikuwa ndani kwenye mkutano sina ufahamu kama ulikuwa live au haukuwa live lakini waandishi wa habari walikuwepo kwenye mkutano.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kuhusu recordings za mkutano huo wa Tarehe 03/04/2025 kama uliona kwenye Jambo Tv??

Heche: Niliona kwenye YouTube channel mbalimbali kama Mwanzo, the Chanzo na hata Jambo TV niliona.

Mhe.Lissu: Waeleze majaji hicho ulichoona katika YouTube ya Chanzo, Mwanzo na Jambo TV zina urefu wa muda gani?

Heche: Kwenye Jambo TV ipo kama takribani masaa mawili, Chanzo ipo video ya dakika 45, na Mwanzo Tv kama dakika 60 hivi au lisaa na kitu yaani ziko tofauti tofauti.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno haya (Lissu anasoma maneno ya kwenye hati ya mashtaka… wanasema msimamo huu unaashiria uasi … tutaenda kukinukisha sana sana),

Heche: Ni miongoni mwa maneno ambayo yapo niliyoyasikia

Mhe. Lissu: Waeleze majaji yale uliyoyazungumzia kwenye ushahidi wako kama yapo.

Heche: Yapo maneno hayo niliyoyasema kwenye ushahidi wangu kama vile kuepusha maafa, engua engua ya wagombea na mengine mengi maana ni hotuba ya masaa mengi.

Mhe. Lissu: Shahidi shtaka ambalo nashitakiwa nalo linaeleza kwamba mimi ndio nilichapisha hayo maneno Jambo Tv wewe unasemaje?

Heche: Waheshimiwa Majaji, sio kweli kwasababu Lissu sio mfanyakazi wa jambo TV na kuna Shahidi wa Jamhuri yule wa kwenye kiboksi humu alisema yeye ndio aliyechapisha, anaitwa P ni shahidi wa 17 wa Jamhuri.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji juu ya mimi kufanya chochote kwenye Mkutano huo zaidi ya kuzungumza???

Heche: Mwenyekiti wetu, Tundu Lissu hakugusa kitu chochote zaidi ya kuzungumza, hakugusa kamera wala radio.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa kosa la uasi kwenye Katiba ya Tanzania??

Heche: Sina ufahamu wa uwepo wa kosa lolote la uasi kwenye katiba.

Mhe.Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa kosa la kuhamasisha uasi kwenye Katiba ya Tanzania.

Heche: Sina ufahamu wowote wa kosa la kuhamasisha uasi kwenye Katiba.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamu wako uwepo wa kosa la kuvuruga uchaguzi kwenye Katiba.

Heche: Sina ufahamu wa uwepo wa kosa la kuvuruga uchaguzi kwenye katiba

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kuhusu uwepo wa kosa la kuzuia uchaguzi kwenye Katiba

Heche: Kwa ufahamu wangu hakuna uwepo wa kosa la kuzuia uchaguzi kwenye katiba.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamu wako uwepo wa kosa la kuhamasisha watu kuzuia uchaguzi?

Heche: Kwa ufahamu wangu hakuna uwepo wa kosa la kuhamasisha watu kuzuia uchaguzi kwenye Katiba.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji ufahamu wako kuhusu uwepo wa kosa la kukinukisha kwenye katiba hii?

Heche: Kwa ufahamu wangu hakuna uwepo wa kosa la kukinukisha kwenye Katiba

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwa ufahamu wako wako uwepo wa kosa linaloitwa kuzuia watu kwenda kupiga kura kwenye Katiba.

Heche: kwa ufahamu wangu hakuna kosa hilo kwenye katiba.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa kosa la uasi au rebellion kwenye Kanuni ya Adhabu.

Heche: Kwa ufahamu wangu sifahamu uwepo wa kosa la rebellion kwenye Sheria

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwa ufahamu wako uwepo wa kosa la kuhamasisha uasi kwenye Penal Code.

Heche: Sina ufahamu wa uwepo wa kosa la kuhamasisha uasi kwenye kwenye Kanuni ya Adhabu

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji ufahamu wako kuhusu uwepo wa kosa la kuvuruga uchaguzi kwenye Kanuni ya Adhabu

Heche: Sina ufahamu kuhusu uwepo wa kosa la kuvuruga Uchaguzi kwenye Kanuni ya Adhabu.

Sehemu ya 402

Makamu Mwenyekiti John Heche anaendelea kutoa ushahidi wake.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa kosa la kuzuia Uchaguzi kwenye Kanuni ya Adhabu?

Heche: Sina ufahamu wa uwepo wa kosa la kuzuia uchaguzi kwenye kanuni ya Adhabu

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwa ufahamu wako uwepo wa kosa la kukinukisha kwenye Kanuni ya Adhabu.

Heche: Sina ufahamu wa kosa la kukinukisha kwenye Kanuni ya Adhabu

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kuhusu uwepo wa kosa la kuvuruga uchaguzi kwenye Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2024??

Heche: Hakuna uwepo wa kosa la kuvuruga uchaguzi kwenye Sheria hiyo ya Uchaguzi.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kuhusu uwepo wa kosa la kuzuia uchaguzi kwenye Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2024???

Heche: Hakuna hilo kosa la kuzuia uchaguzi

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kuhusu uwepo wa kosa la kukinukisha kwenye Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2024

Heche: Hakuna uwepo wa kosa la kukinukisha kwenye Sheria ya Uchaguzi ya Mwaka 2024.

Mhe. Lissu: Shitaka linalonikabili linasema nilitengeza nia ya kuzuia uchaguzi wa 2025, waeleze majaji uwepo wa kosa la kutengeneza nia ya kuzuia uchaguzi kwenye Kanuni ya Adhabu???

Heche: Kwa ufahamu wangu hakuna uwepo wa kosa la kutengeneza nia ya kuzuia uchaguzi kwenye Kanuni ya Adhabu.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa kosa la kutengeneza nia ya kuzuia uchaguzi kwenye Katiba???

Heche: Hakuna kosa la kutengeneza nia ya kuzuia Uchaguzi kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno Serikali ya JMT kwenye hotuba yangu?

Heche: Hakuna mahali popote ambapo Mhe. Tundu Lissu alitaja Serikali ya JMT.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kuhusu uwepo wa maneno Rais wa JMT.

Heche: Hakuna maneno Rais wa JMT kwenye hotuba iliyotolewa na Tundu Lissu

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kuhusu uwepo wa maneno Makamu wa Rais wa JMT.

Heche: Hakuna uwepo wa maneno Makamu wa Rais wa JMT.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Waziri Mkuu wa JMT kwenye hotuba yangu ya tarehe 03/04/2025

Heche: Hakuna mahali ambapo alitajwa Waziri Mkuu wa JMT.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Baraza la Mawaziri wa JMT kwenye hotuba yangu?

Heche: Hakuna maneno Baraza la Mawaziri wa JMT kwenye hotuba ya Lissu.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Waziri, Naibu Waziri, Wakuu wa Mikoa au Wilaya?

Heche: Hakuna maneno Waziri, Naibu Waziri, wakuu wa mikoa au wilaya kwenye hotuba ya Tundu Lissu.

Mhe.Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Mkurugenzi wa Mashtaka?

Heche: Hakuna uwepo wa maneno Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya JMT au Mkurugenzi wa Mashtaka.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno halmshauri ya Mji, jiji, wilaya au Serikali ya mtaa?

Heche: Kwenye hotuba nzima hakuna maneno Halmashauri ya mji, jiji, wilaya, kitongoji , kijiji wala serikali ya mtaa.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno Wakurugenzi wa jiji, Manispaa, Halmashauri wala watendaji wa kata, vijiji?

Heche: Waheshimiwa Majaji kwenye hotuba yote Hakuna maneno wakurugenzi wa jiji, manispaa, halmashauri wala watendaji wa kata na vijiji.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno jeshi la polisi, jeshi la ulinzi, jeshi la akiba, mgambo wa jiji, jeshi la wananchi wa Tanzania na maneno ya aina hiyo???

Heche: Hakuna maneno Jeshi la Polisi, Jeshi la Ulinzi, Jeshi la akiba, mgambo wa jiji, Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye hotuba nzima ya Lissu.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji maneno yaliyopo kwenye hati ya mashtaka yanamtishia nani?

Heche: Waheshimiwa majaji, hayo maneno ni ya kawaida tu na wala hayajamtishia mtu yeyote.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji maneno niliyokusomea yana kosa gani?

Heche: Waheshimiwa majaji hayo ni maneno ya kawaida kwenye siasa hivyo hayana kosa lolote

Sehemu ya 403

Makamu Mwenyekiti John Heche anaendelea kutoa ushahidi wake.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji katika Mkutano wa 3/4/2025 uwepo wa maneno tutaenda kuchoma vituo vya kupigia kura moto?

Heche: Hakuna hayo maneno ya tutaenda kuchoma moto vituo vya kupigia kura kwenye hotuba wala kwenye video.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno tutaenda kuchoma vituo vya mwendokasi, ofisi za CCM na Serikali???

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakuna uwepo wa hayo maneno ya tutaenda kuchoma vituo vya mwendokasi, ofisi za CCM na Serikali hata kwenye video hayapo.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno tutakwenda kukata watu vidole?

Heche: Hakuna hayo maneno ya kusema tukakate watu vidole.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno watu wakaue Polisi au mtumishi wa Tume au mtu mwingine yeyote???

Heche: Waheshimiwa majaji, Tundu Lissu hakusema watu wakaue Polisi au mtumishi wa Tume au mtu mwingine yeyote.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji ufahamu wako kuhusu hotuba ya Jaji Othman Chande ya Matukio ya Oktoba 29???

Heche: Naifahamu

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama uliisikiliza yote?

Heche: Niliisikiliza yote.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo au kama Jaji Chande alisema vurugu za Oktoba 29 zilitokana na maneno ya Tundu Lissu???

Heche: Jaji Chande hakusema kuwa vurugu za Oktoba 29 zilitokana na maneno ya Tundu Lissu.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwenye hotuba wa Jaji Chande uwepo wa maneno juu ya aliyechochea au waliochochea??

Heche: Kwenye hotuba hiyo Jaji Chande hakutaja mtu yeyote aliyechochea, hakumtaja Lissu wala mtu yeyote.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa jina au majina ya chama cha siasa kilichochochea vurugu za Oktoba 29, 2025.

Heche: Kwenye hotuba hakuna jina au majina ya chama cha siasa kilichochochea vurugu za Oktoba 29, 2025

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa majina ya watu waliokata watu vidole au watu waliokatwa vidole?

Heche: Hanna uwepo wa majina ya watu waliokata au waliokatwa vidole.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwenye hotuba ya Chande uwepo wa majina ya askari polisi waliouwawa na watu waliowaua hao askari??

Heche: Hakuna majina ya askari waliouwawa au watu waliowaua.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji, majina ya watu waliouwawa au majina ya watu waliowaua???

Heche: Hakuna uwepo wa majina ya watu waliowawa na watu waliowaua.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji, kwenye hotuba ya Chande uwepo wa maeneo ambayo vituo vya mwendokasi , ofisi za CCM au za Serikali .

Heche: Sina kumbukumbu na hilo

Leo mshtakiwa na shahidi wake wanagonga nyundo sana, wanatema madini wote,

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa orodha ya magari ya watu binafsi au Serikali?

Heche: Hakuna mahala ambapo ilitolewa orodha ya magari, hakuna hata moja.

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji, kuhusu wewe au viongozi wa chama kuitwa kwenda kueleza kuhusu chochote mbele ya Tume ya Jaji Chande.

Heche: Mimi binafsi sikuwahi kuitwa na sina ufahamu wa kiongozi yeyote wa chama chetu kwenda kutoa maelezo mbele ya Tume ya Jaji Chande.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kwa haya uliyoyatolea ushahidi, kwa ufahamu?

Heche: Siko kwenye nafasi nzuri ya kueleza wao walichunguza nini ila sisi hawakutusikiliza wala kutuita.

Sehemu ya 404

Lissu: Waeleze ufahamu wako juu ya jitihada za mazungumzo na Serikali kabla ya msimamo wa No reforms, No election?

Heche: Mimi binafsi nilishiriki, nilikuwa kwenye team ya CHADEMA iliyokutana na Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwepo mwaka 2022- 2025 Ikulu Dodoma.

Tulizungumza nae kutokana na malalamiko ya uchaguzi ya muda mrefu hasa uchaguzi wa 2019 na 2020 baadae Chama kilianzisha madai ya kampeni ya Katiba Mpya na mifumo ya uchaguzi wakati huo Mwenyekiti alikuwa ni Freeman Mbowe.

Tulienda Mwanza mwaka 2021 tulifanya Kongamano la kudai Katiba Mpya ili kuwezesha mabadiliko ya Uchaguzi, kama nilivyoeleza Mbowe alikamatwa na mimi nilikamatwa.

Baada ya Mbowe kutokea Ikulu ndio tukaenda kukutana na Rais Ikuku Chamwino Dodoma alikuwepo Mwenyekiti Mbowe, Said Issa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama chetu Zanzibar, Katibu Mkuu John Mnyika, na mimi mwenyewe.

Upande wa Serikali alikuwepo Rais Samia, Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati huo Jaji Eliezer Mbuki Feleshi, Waziri George Simbachawene, Jenister Mhagama sasa ni marehemu ila alikuwa Waziri,

Upande wa CCM alikuwepo Makamu Mwenyekiti wa CCM wa wakati huo mzee Abdullahiman Kinana na viongozi wengine wa CCM siwakumbuki vizuri.

Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu walieleza jinsi ambavyo tumenyanyaswa na kuonewa na uharibifu wa Uchaguzi,

Watu waliokimbia nchi na mambo mengine yaliyotokana na uchaguzi kwenye kile kikao ilikubaliwa kuwa iundwe Team ya watu watano, watano kutoka kila chama na upande wa Serikali.

Hizo team zingeenda kupitia kwa kina mifumo ya uchaguzi, matatizo ya kiuchaguzi na mapendekezo ya mabadiliko ya katiba na sheria za uchaguzi kabla ya 2025.

Upande wa Chadema iliundwa team iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Mbowe, Katibu Mkuu John Mnyika, Wakili Jeremia Mtobesya, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama kutoka Zanzibar Mhe. Zeudi Mvano, na mimi John Wegesa Heche nilikuwemo.

Upande wa CCM namkumbuka Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdullahiman Kinana, Andrew Chenge, wawakilishi wawili kutoka Zanzibar siwakumbuki majina yao na kulikuwa na Mawaziri, mwanzo aliingia Jenister Mhagama na baadae akaja Simbachawene.

Hayo mazungumzo yalichukua mwaka mzima na sehemu tuliandika na kupeleka mapendekezo yetu namna ya kukwamua mchakato wa Katiba namna ya kuukwamua, mapendekezo ya kisheria namna ya kuukwamua mchakato wa Katiba, Vyombo ambavyo vingeundwa katika kuhakikisha vinaandika katiba kuanzia mwanzo ikiwemo kuchakata maoni.

Tulipeleka pia mapendekezo ya sheria ya Uchaguzi, mapendekezo ya namna ya kuunda Tume Huru ya Uchaguzi, tulizungumza kuhusu kesi mbalimbali watu wetu walizokuwa wamebambikiziwa na wengine kufungwa kwa uongo, tulizungumza kuhusu viongozi waliokuwa wamekimbia nchi kwasababu ya usalama wao Makamu Mwenyekiti Mhe. Lissu, Godbless Lema, Ezekia Wenje Dibogo na wengine, madai ya kuwaondoa wabunge 19 (Covid-19) ambao walijipeleka Bungeni kinyume na taratibu za chama,

Tulizungumza kuhusu kufungulia mikutano ya hadhara iliyokuwa imefungwa kwa tamko la Rais Magufuli kinyume cha Sheria, namna ya kukomesha matukio ya utekaji watu.

Mhe. Lissu: Naomba tuahirishe baada ya lisaa na nusu turejee shahidi aje kuendelea na nina uhakika atamaliza leo

Jaji Ndunguru: Wakili wa Serikali

Katuga: hatuna pingamizi

Jaji Ndunguru: tujitahidi tumalizane na huyu shahidi

Kesi inaahirishwa hadi saa nane na nusu

===========

Mahakama imerejea majira Saa Tisa kasoro Alasiri.

Sehemu ya 405

Majaji walishaingia, Mhe. Lissu yupo na Upande wa Jamhuri wapo.

Anasimama Nassoro Katuga anasema mchana huu hayupo Ajuaye na Job Mrema na sisi tuko tayari kuendelea.

Mshitakiwa Mheshima Tundu Lissu anasema yupo tayari kuendelea pia.

Shahidi no. 5, John Heche tayari amepanda kizimbani

Jaji Ndunguru anamwambia Shahidi nakukumbusha kwamba upo chini ya kiapo.

Mhe. Lissu anasema nikumbushwe nilipoishia ili tuendelee.

Anakumbushwa.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa jambo lingine mlilozungumzia kwenye hivyo vikao?

Heche: Kukomeshwa vitendo vya utekaji nyara, ubambikaji wa kesi za uongo kwa watu kwa ujumla ni kuupitia mfumo wote wa Haki jinai na kurudisha Demokrasia ya kweli.

Mhe. Lissu: Kuhusu ratiba ya mambo hayo mliyokuwa mnayazungumzia?

Heche: Katika mapendekezo yetu tulikuwa na roadmap ya namna ya kukwamua mchakato wa Katiba mpya na ratiba nzima ambayo ilisema mambo yote yangekamilika kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za mwaka 2024.

Mhe. Lissu: Mazungumzo hayo yaliishaje?

Heche: Wakati wote tulipokuwa tunazungumza tulipeleka kwa maandishi ratiba na mapendekezo yetu.

Wajumbe wa CCM walikuwa wanatusikiliza na wanabeba kwamba wanaenda kufanya consultation na Rais ambae aliteua hiyo timu kumueleza hayo tunayozungumza ili tuwe kwenye picha moja.

Kuna wakati Mh. MBOWE NA KINANA wameenda kumuona Rais kwa Pamoja kupeleka mazungumzo tuliyokuwa tumefanya kwenye kikao.

Makubaliano ilikuwa Mbowe na Kinana wafanye Press conference ya pamoja kuelezea walichokubaliana, mazungumzo yaliisha pale tuliposema tujibiwe kwa maandishi kuwa tuandikieni na nyie upande wa CCM na Serikali kuwa kati ya mapendekezo yetu yote yapi tumekubaliana.

Mhe. Lissu: Waliwajibu kwa njia gani?

Heche: Walitujibu kwa njia ya maandishi na kwenye majibu yao walisema kwamba wamekataa mambo yote tuliyokubaliana kwenye vikao hivyo vya Maridhano.

Mhe.Lissu: Hayo majibu waliyaleta lini?

Heche: Siwezi kukumbuka exactly tarehe lakini ilikuwa mwaka 2023 na sisi tuliendelea na ziara zetu kwenda kwa wananchi so mazungumzo yetu na CCM yakaishia hapo.

Mhe. Lissu: Siku ya Tarehe 29/10/2025 wewe ulikuwa wapi na kama ukishiriki kwenye kupiga kura?

Heche: Hiyo Tarehe 29/10 nilikuwa kituo cha Polisi Mtumba Dodoma ambapo nilikamatwa tangu tarehe 22/10 huo huo.

Nilipotoka Polisi nilipata taarifa nyingi kuhusiana na kilichotokea, watu kuuwawa kwa zaidi ya watu 518 na Mzee Joseph Warioba anasema watu waliouwawa ni wengi kuliko waliokufa kwenye vita ya Kagera.

Anasimama Katuga anasema sio kwamba napinga lakini hiyo habari ya Mzee Warioba ni Hearsay Evidence haipaswi kuchukuliwa.

Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji kama hapingi amesimama kufanya nini? Pia kuna mambo yanasemwa kama ni sheria vile lakini sio sheria kabisa.

Hearsay Evidence inahitaji kuwa Corroborated na ushahidi mwingine, mimi nimebaki na mashahidi wengine watatu kwahiyo atulie tu na mwisho yeye ana nafasi ya kuja kufanya Cross Examination sasa si asubiri aje kumuuliza maswali shahidi.

Jaji Ndunguru: Haya tuendeleee.

Mhe. Lissu: Ahsante. Haya ulisemaje hapo?

Heche: Nilitaka kumalizia kwa kusema hakuna Serikali imewahi kuua watu wengi toka vita vya majimaji hadi leo, hii ndo Serikali imeua watu wengi sana.

Sehemu ya 406 itaendelea....
Asante mkuu naomba uendelee kumwaga nondo za updates.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 17.

Lissu: Watajie taarifa za taasisi za kidini ulizopata.

Heche: Nilipata taarifa za Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC).

Lissu: Taarifa gani nyingine ya kidini?

Heche: Shura ya Maimamu.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa kumbukumbu zako, tarehe hizi taarifa za Baraza la Maaskofu Katoliki na Shura ya Maimamu zilitolewa lini?

Heche: Ilikuwa ni mwezi Novemba mwaka jana.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, ripoti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ilisema nini?

Heche: Ilizungumzia mauaji ya Oktoba 29.

Pia ilipendekeza ufanyike uchunguzi huru ili kuwabaini waliohusika na hatua zichukuliwe dhidi ya waliobainika kuhusika.

Ila ililaani matumizi ya nguvu yaliyopitiliza dhidi ya wananchi au waandamanaji.

Ilizungumzia hali ya kidemokrasia, kuhusu wananchi kunyimwa haki ya kupata viongozi wanaowataka, na ilitoa mfano kwamba hali hiyo imekuwepo tangu mwaka 2016.

Kumekuwa na manung’uniko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi kuhusu madai yao.

Ilizungumzia pia kuhusu hali ya usalama, kwamba wananchi wanaishi kwa hofu na kwamba kumekuwa na matukio ya utekaji nyara.

Lissu: Sasa shahidi, ulisema ulipata taarifa ya Shura ya Maimamu. Ilisemaje?

Heche: Shura ya Maimamu ililaani matukio ya mauaji.

Wakaeleza namna ambavyo uchaguzi ulikosa sifa ya kuitwa uchaguzi.

Ilikemea namna ambavyo vyombo vya dola vilitumia nguvu iliyopitiliza.

Lissu: Ulisema umepata taarifa za waangalizi wa uchaguzi.

Heche: Nilipata taarifa ya uchaguzi ya AU (African Union).

Taarifa ya waangalizi wa uchaguzi ya SADC.

Taarifa ya uchaguzi ya Afrika Mashariki (East African Community).

Lissu: Taarifa zote zilitolewa tarehe gani?

Heche: Zote ni za mwezi Novemba mwaka jana.

Ripoti ya East African Community

Lissu: Tuanze na taarifa ya waangalizi wa Afrika Mashariki (East African Community).

Heche: Taarifa ya Afrika Mashariki inasema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na hakuna lolote lililojitokeza.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama taarifa hiyo ya Afrika Mashariki iliona mauaji makubwa yanayolalamikiwa kutokea.

Heche: Haijasema lolote kuhusu kuwepo kwa mauaji.

Lissu: Vipi suala la kuchoma miundombinu kwenye hiyo ripoti?

Heche: Hawajasema lolote kuhusu kuchomwa kwa miundombinu.

Lissu: Wakumbushe Waheshimiwa Majaji ni nchi gani zinaunda Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Heche: Tanzania, Kenya, Rwanda, Burundi, Congo na Sudan Kusini.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, katika hizo nchi—Kenya, Rwanda, Burundi, Congo na Sudan Kusini—hali ya demokrasia ikoje?

Heche: Kwa nchi zote hizo, ukitoa Kenya, hali ya demokrasia katika hizi nyingine ni mbaya.

Uganda ipo chini ya Rais Museveni, ana miaka 30 na zaidi.

Lissu: Rwanda je?

Heche: Huko nako Rais alipata kura asilimia 98, zaidi ya asilimia 97.6 ya Samia.

MAHAKAMA: Kicheko.

Ripoti ya SADC

Lissu: Twende kwenye ripoti ya SADC.

Heche: Wanasema uchaguzi haukufikia viwango vya kidemokrasia kwa nchi za SADC.

Wamezungumza pia matatizo waliyokutana nayo siku hiyo ya uchaguzi, kwa sababu palikuwa na vizuizi vilivyotokana na zuio lililotangazwa mapema saa 5 asubuhi siku ya uchaguzi.

Lissu: Wamesema nini juu ya matukio ya mauaji?

Heche: Waheshimiwa Majaji, waliongelea na kusikitishwa na matumizi makubwa ya nguvu.

Walizungumzia taarifa za mauaji katika uchaguzi na siku yenyewe ya uchaguzi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE.
 
Back
Top Bottom