Kesi ya Uhaini ya Lissu: Heche kuendelea kutoa ushahidi Mahakamani Sept. 11. 2026

Kesi ya Uhaini ya Lissu: Heche kuendelea kutoa ushahidi Mahakamani Sept. 11. 2026

Du! Hii babu kubwa, yaani East African community haikuona mauaji yaliyotokea badala yake waliona uchaguzi huru na wa hali. Wonders shall never end in east Africa
We call it community, akili za watu wanaonunulika hata kwa masuala yaliyo wazi.
 
Multiple choice ni maswali ya form 4 failures!!
Nakusaidia kutoka Chatgpt:

1789135909729.png
 
Kwa wananchi wanachohitaji ni mahitaji, swala la vifungu ni technical na hilo lina wataalamu wake. Ukianza kuwauliza wananchi vifungu ujue huko ni kuishiwa hoja.
Katiba bila vifungu ni upumbavu. So funga domo lako hilo, wewe ni empty head
 
Kwani mtu akikwambia tunataka Katiba itakayompunguziarais madaraka au Katiba itakayomuondolea rais kunga, au katiba itakayotanua wigo wa uwajibikaji ni lazima akutajie kifungu? Mbona mnakuwa na mambo na maswali ya Kishenzishenzi ninyi watu?
Platinum member!
 
CHADEMA na Wafuasi wao wapo kufanya propaganda
Kwamba Mh Lissu kaonewa

Upande mwengine tupo kusema kweli ya kweli mbele ya Mungu

Ndiomana tukaweka mpaka Clip ili Wasomaji wapate faida ya
kuelewa kile kipo Mahakamani

Iyo Clip ya Lissu sauti zao na Heche

Leo Wafuasi wao wanajifanya kushangaa
Kwanini Lissu yupo Mahakamani au Lupango

Hawa ni Wanafiki mbele ya Mungu

MOTO 💥 ulichochewa na wao na tukapoteza Watoto wetu wakati watoto wamewaficha Sehemu Salama ❗️

Ushahidi mmesikia iyo Video
Kama bado ulikuwa ulidhani Lissu kaonewa futa Upumbavu kichwani mwako❌️

Lissu anavuna kile kile
kakipanda kupitia iyo video kupitia mipango
yao pamoja ✅️

CHADEMA na Wafuasi wao walitaka kudanganya watu kupitia media mbali mbali
Ili kujenga Uwongo kwamba Lissu kaonewa 🫎❌️

Sasa jiulize aya maneno kaongea nani
Sio mh LISSU
Na Shemeji yake HECHE ‼️‼️
 
Heche: Walitujibu kwa njia ya maandishi na kwenye majibu yao walisema kwamba wamekataa mambo yote tuliyokubaliana kwenye vikao hivyo vya Maridhano.
Sasa fikiria jambo la namna hii kufanyika na watu wanaolitakia taifa lao mema! Kweli!

Anayetaka kujuwa sababu ya Kinana kujiuzuru umakamu wa Mwenyekiti wa CCM ni hiii hapa.

Huwezi kuwa mtu na akili timamu ukaendelea kutumiwa kufanya uovu.
 
Acha kuharibu uzi kwa maswali yako ya la 7 B. Huwez kuniulizia kuhusu mahakama ni nini otherwise tukaulizane facebook! You can own people but you can't own a Judiciary, mahakama inatoa haki lakini binadamu anaweza kuipindisha kwa kujua au kutokujua.
Jipige kifua ujiite mpumbavu
 
Lengo lao kuuu kudanganya Wasomaji wa Jamii forum

Kueneza Uwongo kabla ya Ukumu
Ya Majaji

Team zetu za kusema kweli zipo macho
Kuakikisha mnapata kuelewa Ukweli
Kuongeza maarifa ya juu kesi ya Lissu ✍️
 
Katiba bila vifungu ni upumbavu. So funga domo lako hilo, wewe ni empty head
Wananchi hutoa madai yao, wataalam ndiyo huipanga kwa vifungu, elewa hilo.
Huwezi ukasimsma hapa na kudai nataka kifungu namba fulani na namba fulani. Hata huk bungeni kwenyewe wabunge huwasilisha mawazo halafu Kamati ndiyo hukaa kui shape katika vifungu
 
Hahaaa!! Endelea kutumia huu ushuzi ukunyime upeo wa kufikiri, mahakama ni watu?? Kwa hiyo wewe na mgane mkipewa mamlaka ya kisheria tayari ni mahakama? Hakuna mahakama bila vitabu vya sheria kama katiba n.k
Wewe ni Gen-Z halafu upo outdated, Dunia sasa ipo kwenye AI wewe bado unakomaa na analog thinking
 
Wananchi hutoa madai yao, wataalam ndiyo huipanga kwa vifungu, elewa hilo.
Huwezi ukasimsma hapa na kudai nataka kifungu namba fulani na namba fulani. Hata huk bungeni kwenyewe wabunge huwasilisha mawazo halafu Kamati ndiyo hukaa kui shape katika vifungu
Umeulizwa; katiba ya sasa vifungu vipi haviko sawa? Unatuletea mbwembwe za Ubeligiji
 
Heche: Madai ya muda mrefu ya watanzania kutaka Katiba Mpya, Tume huru ya Uchaguzi, Rushwa na ufisadi, Ukosefu wa Ajira na watu kutekwa nyara na kupotezwa.
OOooh!
Sasa Chande angeitwa mahakamani kutoa ushahidi wa utetezi, kumbe machafuko ynajulikana chanzo chake ni nini? Sasa kwa nini Tundu Lissu yupo mahakamani?

Huu ni utetezi mzuri kwa Tundu Lissu.
 
Jipige kifua ujiite mpumbavu
Siyo nikuite wewe hivyo kwa kuegemea matumiz ya CHATGPT eti mahakama ni watu. Mahakama ni chombo cha dola chenye kazi ya ... sasa watu ni chombo? Chombo hicho ndo huundwa na watu, katiba, jengo. Ukikomaa sana na akili unde unayoipa guided qns utatoka kapa
 
Siyo nikuite wewe hivyo kwa kuegemea matumiz ya CHATGPT eti mahakama ni watu. Mahakama ni chombo cha dola chenye kazi ya ... sasa watu ni chombo? Chombo hicho ndo huundwa na watu, katiba, jengo. Ukikomaa sana na akili unde unayoipa guided qns utatoka kapa
Chatgpt ni Modern Technology, watu wote wenye akili timamu wanatumia
 
TUNDU LISSU ANAMALIZA MASWALI YAKE KWA MH. JOHN HECHE.

SEHEMU YA 18

Taarifa ya Waangalizi wa Umoja wa Afrika (AU)

Lissu: Shahidi, twende katika taarifa ya watazamaji wa Umoja wa Afrika. Waliona nini?

Heche: Taarifa ya Waangalizi wa Umoja wa Afrika ilizungumzia uchaguzi kutokidhi vigezo vya uchaguzi katika nchi za Umoja wa Afrika.

Walieleza mapungufu makubwa yaliyokuwepo wakati wa upigaji wa kura na ujumuishaji wa kura.

Kwa ujumla, haukutimiza vigezo na viwango katika kuendesha uchaguzi wa kidemokrasia katika nchi ya kidemokrasia.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, waangalizi hawa wa Umoja wa Afrika waliona nini kuhusu mauaji?

Heche: Waheshimiwa Majaji, Waangalizi wa Umoja wa Afrika waliona mauaji yaliyojitokeza katika uchaguzi na siku iliyofuata.

Taasisi ya Thabo Mbeki

Lissu: Katika ushahidi wako unasema ulipata taarifa za taasisi za kikanda.

Heche: Taasisi ya Thabo Mbeki.

Lissu: Shahidi, kwa rekodi ya Mahakama, waeleze Waheshimiwa Majaji Thabo Mbeki ni nani?

Heche: Waheshimiwa Majaji, Thabo Mbeki ni Rais wa pili wa Afrika Kusini huru baada ya utawala wa Makaburu.

Na amekuwa kiongozi wa chama cha ANC, chama rafiki wa CCM. Mara nyingine wanabadilishana ujuzi.

Lissu: Taasisi ya wakfu wa Thabo Mbeki inasemaje?

Heche: Taasisi ya Thabo Mbeki inaeleza kuhusu taarifa za AU na SADC na mapungufu makubwa ya uchaguzi waliyoona Tanzania.

1. Tanzania inakosa serikali halali iliyochaguliwa na wananchi.
2. Serikali iliyopo madarakani imejiweka madarakani kwa udanganyifu na kwa mabavu.

Lissu: Kitu gani kingine Thabo Mbeki amesema?

Heche: Waheshimiwa Majaji, hayo ndiyo nayakumbuka.

Taarifa nyingine kuhusu uchaguzi

Lissu: Kuna taarifa gani nyingine kuhusu uchaguzi wa mwaka jana?

Heche: Waheshimiwa Majaji, kuna taarifa ya Umoja wa Ulaya (EU), taarifa ya Umoja wa Mataifa (UN), taarifa ya Commonwealth (Jumuiya ya Madola), na taarifa ya Mabaraza ya Makanisa Duniani.

Taarifa ya Umoja wa Ulaya (EU)

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, taarifa ya Umoja wa Ulaya ilisemaje kuhusu uchaguzi wa Tanzania?

Heche: Kwanza, Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wangu—

Jaji Ndunguru: Sema taarifa inasema nini.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, taarifa ya Umoja wa Ulaya ilisemaje kuhusu uchaguzi wa Tanzania?

Heche: Taarifa za EU zilisikitishwa na taarifa za kutekwa watu wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Wameeleza pia kwamba uchaguzi haukufanyika kwa vigezo vinavyotakiwa, uchaguzi huru na wa haki (credible).

Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji, EU walisemaje kuhusu mauaji?

Heche: Taarifa ya EU ililaani matukio ya mauaji na kuitaka Serikali ifanye uchunguzi huru, na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria.

Baraza la Makanisa Duniani

Lissu: Baraza la Makanisa Duniani lilisema nini kuhusu uchaguzi Tanzania?

Heche: Waheshimiwa Majaji, Baraza la Makanisa Duniani lililaani.

Kwanza, walilaani mauaji na kusema kwamba uhai ni kitu kinachotolewa na Mwenyezi Mungu mwenyewe.

Kwa hiyo, hiyo haki ya kuishi inapaswa kulindwa vizuri na kwa nguvu zote.

Walizungumzia uchaguzi wa Tanzania kwamba haukufuata vigezo na kanuni za kidemokrasia za uchaguzi kuwa huru na wa haki.

Pia walizungumzia kukosekana kwa mizania ambayo ingewezesha uchaguzi kufanyika kwa haki na usawa.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa (UN)

Lissu: Shahidi, unasema ulipata taarifa ya Umoja wa Mataifa. Waeleze Waheshimiwa Majaji, taarifa ya Umoja wa Mataifa ilisema nini kuhusu Tanzania?

Heche: Waheshimiwa Majaji, ilizungumzia pia uchaguzi wetu ambao haukuwa huru na wa haki na umeukiuka misingi ya kidemokrasia ya wananchi kuchagua viongozi wanaowataka.

Walizungumza pia kuhusu kukamatwa kwa viongozi na kubambikiwa kesi, kupewa kesi za uongo.

Walitaka watu wote walioambikiwa kesi za uongo waachiwe.

Mahusiano ya Tanzania na taasisi na nchi zilizotoa taarifa

Lissu: Sasa shahidi, baada ya yote haya ambayo umeyatolea ushahidi, naomba uwaeleze Waheshimiwa Majaji, hizi taasisi za kikanda za majirani zetu wa Afrika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa—kwa ufahamu wako, elezea mahusiano ya Tanzania na nchi hizo zilizoandika ripoti hizo.

Heche: Uhusiano wetu ni mzuri na nchi hizo.

Tanzania ni mwanachama mwanzilishi wa Umoja wa Afrika.

Vilevile, katika Jumuiya ya Afrika Mashariki hakuna nchi yoyote ambayo tuna ugomvi nayo.

Uhusiano wetu ni mzuri na nchi za SADC. Tulisaidia kupigania uhuru wa Afrika Kusini na Namibia.

Lissu: Jumuiya ya Ulaya?

Heche: Jumuiya ya Ulaya ni rafiki wa Tanzania na wadau wa maendeleo.

Nimekuwa Bungeni, wanachangia maendeleo kwenye bajeti zetu.

Lissu: Umoja wa Mataifa?

Heche: Uhusiano wetu ni mzuri. Sijui kama tuna tatizo nao.

Swali la mwisho

Lissu: Swali langu la mwisho.

Nimeshitakiwa kwa uhaini, nipo ndani inaelekea mwaka na nusu sasa. Kwa ufahamu wako, hii kesi ikoje?

Heche: Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wangu, hii ni kesi ya uongo yenye lengo la kukandamiza demokrasia.

Kurudisha nyuma harakati zetu CHADEMA kudai mabadiliko.

Ni kama kesi nyingi za kisiasa, za watu ambao hawawezi kushindana. Wanatumia mfumo wetu wa haki jinai na vyombo vya dola kukandamiza wapinzani wao.

Ni kesi ambayo inatumika kupoteza rasilimali za nchi na malengo yake ni kuumiza chama chetu CHADEMA.

Lissu: Umemaliza?

Heche: Nimemaliza.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, sina swali na shahidi huyu.

NIMEMALIZA

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Back
Top Bottom