Kesi ya Uhaini ya Lissu: Heche kuendelea kutoa ushahidi Mahakamani Sept. 11. 2026

Kesi ya Uhaini ya Lissu: Heche kuendelea kutoa ushahidi Mahakamani Sept. 11. 2026

Lkn Lissu katukwamisha
leo
lengo lake Lissu tushajua ili Heche wakamwandae wenzie
kabla ya J3
lkn kazi anayo🫎✍️
 
MAHAKAMA INAHAIRISHWA MPAKA JUMATATU

Cross-Examination ya John Heche

Jaji Ndunguru: Shahidi, upo tayari kuendelea na maswali?

Heche: Nipo tayari.

Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, tuna maswali mengi kutokana na ushahidi mrefu alioutoa shahidi.

Nafikiri itakuwa vizuri tukaanza na shahidi fresh siku ya Jumatatu, kama itawapendeza.

Jaji Ndunguru: Shahidi wa Serikali atamaliza siku ya Jumatatu cross-examination?

Nassoro Katuga: Siwezi kusema nitamaliza siku ya Jumatatu; itategemea na cross-examination.

Jaji Ndunguru: Mjitahidi siku ya Jumatatu mmalize. Kama kitabaki, kiwe kidogo sana.

Nassoro Katuga: Tutajitahidi kuuliza yale ya muhimu.

Jaji Ndunguru: Shauri linahairishwa mpaka Jumatatu, saa 3:00 asubuhi.

MAJAJI WANATOKA.


TUKUTANE JUMATATU ASUBUHI.

WEKA EMOJI KAMA TUMEKUWA PAMOJA WIKI NZIMA.
Manyanza uwe na weekend njema kama ni Msabato, Sabato njema!
 
Unaweza Kuta,na Wewe unamwambia mwanao awe na Akili kama ulivyo na hizi Akili

Ndio umewai chap chap kabla sija Edit kwanini nawewe usini ignore
Mnadanganyana kuni ignore kumbe Macho 👀👀Kodo😆😆
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 15.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa mhusika yeyote kuwajibika vyovyote.

Heche: Waheshimiwa Majaji, sijawahi kusikia mtu yeyote akiwajibika kwa namna yoyote kwa mauaji makubwa ya namna hii siku ya uchaguzi.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, ufahamu wako iwapo kuna Kiongozi wa Serikali aliyewahi kuwajibika kwa mauaji hayo.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakuna Kiongozi yeyote wa Serikali aliyewajibika kwa namna yoyote.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo hotuba ya Jaji Chande imetoa jina la Kiongozi yeyote aliyetoa amri ya kutekeleza mauaji hayo.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakuna sehemu yoyote katika hotuba ya Jaji Chande iliyomtaja Kiongozi aliyetoa amri ya kutekeleza mauaji hayo.

Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, uwepo wa kesi ya mauaji dhidi ya mtu yeyote aliyehusika na mauaji makubwa hivi.

Heche: Waheshimiwa Majaji, sina ufahamu wa kesi yoyote ya mtu aliyekamatwa kwa kuhusika na mauaji makubwa hivi.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, walio uawa ni binadamu au wanyama pori waharibifu wa mazao?

Jaji Ndunguru: Rudia swali. Limekuwa multiple choice.

Lissu: Naomba kurudia swali.

Waeleze Waheshimiwa Majaji, Shahidi, kuhusu uhalali wa Serikali kuua watu wake.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakuna uhalali wa Serikali kuua watu wake, tena kwa idadi kubwa kiasi kile.

Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, hoja yetu ya kuahirisha uchaguzi ili tupate sheria nzuri za kusimamia uchaguzi ingekubaliwa, ingekuwaje?

Heche: Waheshimiwa Majaji, hoja zetu zingekubaliwa, pasingetokea maafa makubwa kiasi hicho.

Jaji Ndunguru: Hiyo ni fact au assumption?

Lissu: Shahidi amesema kwa ufahamu wake.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji, nini kilikuwa kisababishi cha kwanza alichotaja Jaji Chande cha maafa hayo?

Heche: Alisema ni madai ya muda mrefu ya Watanzania kutaka:

  • Katiba mpya;
  • Tume huru ya uchaguzi;
  • Kupambana na rushwa na ufisadi;
  • Ukosefu wa ajira;
  • Watu kutekwa nyara na kupotezwa;
  • Kutokushughulikiwa kwa masuala hayo.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
Duh! Hatari haya mashambulizi sio ya kawaida hata kidogo hii inaitwa unavyotaka mi ndivyo nataka
 
Mbona apo wanajidhalilisha tuh Hawa viongozi Huyo Heche Kila anachoongea waziwazi kinaonekana ni kweli na ni facts tupu ni Aibu kubwa kwa viongozi watu wamekufa jamani sio jambo la kawaida alafu bado wanataka kumsingizia Lissu sio poa kabisa aisee
Lissu alishajua mchezo ndio maana anawapeleka huko huko
 
Du! Hii babu kubwa, yaani East African community haikuona mauaji yaliyotokea badala yake waliona uchaguzi huru na wa hali. Wonders shall never end in east Africa
Mambo ya ajabu kabisa yaani hii kesi imefichua mambo mengi sana na kama ingekuwa live sijui ingekuaje
 
Haswa. HHongera zako.

Na hapo ulipokaa naamini leo umeshuhudia timu ya kipekee kabisa ya Mwenyekiti na Makamu wake mahakamani.

Nadiriki kusema haya waliyowasilisha mahakamani yatakaa kihistoria miaka mingi sana ndani ya taifa hili, bila kujali hukumu ya kesi itakwenda upande gani.
Hata hao majaji sio kwamba hawana akili watoe hukumu bila kuzingatia facts maana vyote vipo kwenye record na vitasomwa na ndio maana hata walivyoamua Samia, Majaliwa na Mpango hawana haja ya kuja mahakamani kama mashahidi walitoa na vifungu ambavyo vinawalinda
 
WATOTO wetu Wameuwawa
Wakati Watoto wao wamewaficha kabla ya zile Fujo Mo29

Lissu kaacha Mke Marekani na Watoto

Na Heche kaakisha kwanza Familia yake ipo salama
Ndio wakaja kukinukisha kuzuiya Uchaguzi nk
Na kupanga mipango ya
kuchoma Miundombinu yetu na ya watu Binafsi

Hakuna sababu ya kumuonea Uruma Lissu ❌️

Jiulize yeye kabla ya kukinukisha kawafikiria Watoto wetu
kwanza jibu ni Hakuna

Basi kama tumezika Watoto wetu kwanini upatwe Uruma kwake iyo Uruma yako ni Upumbavu 😡😡😡😡
Nani aliewaua watoto wetu??
 
Back
Top Bottom