TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI
SEHEMU YA 2.
Lissu: Shahidi, kwa unavyokumbuka, mkutano wote hadi mwisho, kuanzia ufunguzi wa Katibu Mkuu hadi mwisho, unaweza kuwa ni muda gani?
Heche: Kulikuwa na mambo mengi, kuanzia maombi na kila kitu.
Jumla inaweza kuwa masaa manne na kidogo.
Lissu: Katika hayo masaa manne na kidogo, mimi nilizungumza kwa muda gani?
Heche: Waheshimiwa Majaji, Mwenyekiti Tundu Lissu alizungumza kwa zaidi ya masaa 4.
Lissu: Sasa, shahidi, nashitakiwa kwa maneno yafuatayo:
"Wanasema kitu kimoja sahihi hapa. Wanasema hivi..., tutahamasisha uasi, ni kweli...
Huu uchaguzi tutauvuruga, kwa sababu tunaenda kukinukisha vibaya sana..."
Haya maneno kuyasoma yamechukua dakika ngapi?
Heche: Hayamalizi hata dakika moja.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, katika masaa mawili na kidogo, maneno niliyoyazungumza ni haya tu?
Heche: Siyo kweli, Waheshimiwa Majaji, kwamba hayo ni maneno pekee.
Alizungumza kwa kirefu mambo ya uchaguzi.
Lissu: Hayo mazungumzo marefu yalikuwa ya jambo gani?
Heche: Mazungumzo hayo marefu yalihusu uchaguzi.
Namna ambavyo mfumo mzima wa uchaguzi umeharibika, umeharibiwa, ni mbovu, haupo huru na ambavyo hauwezeshi wananchi kupata wanachotaka.
Namna ambavyo ni vigumu kwa mgombea wa upinzani, hasa CHADEMA, kufanikiwa kushinda uchaguzi hata kama anakubalika.
Namna ambavyo mfumo huu unasababisha mauaji na maafa wakati wa uchaguzi.
Namna ambavyo mfumo huu unaruhusu upendeleo wa wazi kwa Rais, Wabunge na Madiwani.
Namna ambavyo vyombo vya dola vinatumika kuharibu uchaguzi/watumishi wa umma.
Kwa ujumla, alieleza namna ambavyo mfumo huu siyo huru na hautendi haki na unavyopaswa kubadilishwa kabla ya uchaguzi.
---
Lissu: Shahidi, kuhusu hilo la mwisho ulilosema, namna unavyopaswa kubadilishwa, waeleze Waheshimiwa Majaji nini kinachopaswa kubadilishwa.
Heche: Waheshimiwa Majaji, alizungumza kuwa kinachopaswa kubadilika ni Katiba na mabadiliko ya sheria zinazosimamia chaguzi zetu.
Mabadiliko ya namna ya kupata wawakilishi, hasa Wabunge, na mgawanyo wa majimbo.
---
Lissu: Shahidi, umesema katika mazungumzo yangu nilisema namna chaguzi zinavyosababisha maafa.
Waeleze Waheshimiwa Majaji nilisema nini kuhusu namna ya kuondoa maafa.
Heche: Waheshimiwa Majaji, alisema namna ya kuondoa maafa katika uchaguzi ni kutengeneza uchaguzi ambao ni huru na wa haki (sawia).
Unaotoa ushindani wa haki ambao hautengenezi upendeleo na unaotoa usawa kwa watu wote.
---
Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji kuhusu Tume ya Uchaguzi. Nilisema nini kuhusu mabadiliko yanayotakiwa?
Heche: Waheshimiwa Majaji, alisema mabadiliko yanayotakiwa katika Tume ni kutengeneza muundo mpya wa Tume.
Ambao haumpi mamlaka Mwenyekiti wa CCM na Kiongozi wa CCM wa kuunda Tume.
Pawe na muundo mpya wa Tume kuanzia Taifa mpaka kwenye Kata.
Iwe na watumishi wake wanaojitegemea, siyo wa Serikali ambao wote wanachukua maelekezo kutoka kwa mwajiri wao.
Na hiyo Tume ndiyo iwe na mamlaka ya kugawa majimbo kulingana na vigezo vinavyofaa na siyo upendeleo.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.