Kesi ya Uhaini ya Lissu inaendelea Mahakamani, DCI Kingai kutoa ushahidi wake Septemba 18, 2026

Kesi ya Uhaini ya Lissu inaendelea Mahakamani, DCI Kingai kutoa ushahidi wake Septemba 18, 2026

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
KESI ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu itaendelea tena mchana leo, Ijumaa Septemba 18.2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam

KESI hiyo inayosikilizwa mfululizo mbele ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru inakuja Mahakamani hapo leo kwaajili ya upande wa utetezi kuendelea kutoa ushahidi wake, ambapo shahidi wa SITA (6), Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) CP Ramadhan Kingai ataanza kutoa ushahidi wake kuanza saa 08:00,

Juzi, Septemba 16.2026, KESI hiyo ilipotajwa mara ya mwisho Mahakamani hapo, mshtakiwa Tundu Lissu ambaye anajitetetea mwenyewe aliieleza Mahakama kuwa atatumia muda wa asubuhi leo kukutana (kuteta) na shahidi huyo, ili kwa pamoja wajiandae kabla ya Mahakama kuanza, ambapo kikao cha mapema cha wawili (2) hao kitafanyika kwenye viunga vya Mahakama.

Ikumbukwe kuwa, licha ya kuwa shahidi wa SITA wa utetezi lakini DCI Kingai ni shahidi wa KWANZA (1) kati ya mashahidi watatu (3) ambao ni vigogo wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini wanaotarajiwa kufika Mahakamani hapo kutoa ushahidi kwa upande wa utetezi,

Wengine ni, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF) Jenerali Jacob John Nkunda, na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camilius Wambura ambao kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mshtakiwa Mahakamani mara ya mwisho aloyoipata kutoka kwa Msajili wa Mahakama ni kwamba wote wamesafiri kikazi wako

Updates za Mahakamani

Mjumbe wa kamati Kuu CHADEMA, Godbless Lema akiwasili Mahakamani

Viongozi na wana CHADEMA wamewasili kwenye ukumbi wa Mahakama ambapo kesi ya Lissu itaendelea.


Tundu Lissu aingia mahakamani kumdodosa DCI Kingai kesi ya uhaini

Last time tuliishia part 431 so leo tunaendelea na -;

Part 432.

Mhe. Tundu Lissu ameingia Mahakamani watu wana vibe sana wanaimba Mwamba Mwamba huku wakipiga makofi mengi sana.

Majaji wote watatu wameingia na kuketi kwenye viti vyao.

Wakili wa Serikali Ajuaye amesimama na kutambulisha jopo lake na kuwa wako tayari kuendelea.

Mhe. Lissu na yeye anasema niko tayari kuendelea.

Mhe. Lissu amesimama na kusema kwamba nimekutana na Kamishna wa Polisi Ramadhani Kingai ambaye nilikuwa nimependekeza awe shahidi wangu wa leo, nimekutana nae Mahakamani kwenye chumba hiki hiki waheshimiwa majaji, naweza kuthibitisha kwamba ameheshimu wito wa Mahakama amekuja na nimezungumza nae kuhusu yeye kuwa shahidi wa upande wa utetezi na nimezungumza nae kiasi cha kutosha, baada ya kumueleza maeneo ambayo ningependa ayatolee ushahidi ameniambia kwamba yeye hawezi na hayuko tayari kutoa ushahidi kwa upande wangu kwa maneno yake mwenyewe amesema

“Yeye yuko upande wa wale wanaoomba na watakaoshangilia nikipatikana na hatia”

Kwahiyo amesema hayupo tayari kuja kutoa ushahidi kwa niaba yangu.

Nimemuelewa Waheshimiwa Majaji kama hayuko tayari siwezi kumlazimisha kutoa ushahidi ambao hataki kuutoa.

Waheshimiwa Majaji Kingai ameniambia kitu kingine kuhusiana na mashahidi wengine wawili IGP Camillius Wambura na CDF Jacob Mkunda, amesema vilevile hata wao watakaporejea nchini na kupata wito wa Mahakama msimamo wao utakuwa ni huo huo kwamba na wao hawatakuwa tayari kutoa ushahidi kwa upande wa utetezi kwasababu ile ile kuwa wako upande wa wale wanaoombea na watakaoshangilia nikipatikana na hatia.

Katika Mazingira haya waheshimiwa majaji maana yake ni kwamba sina mashahidi zaidi kwahiyo naomba kufunga ushahidi kwa upande wa utetezi.

Ni hayo tu waheshimiwa majaji.
 
KESI ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu itaendelea tena mchana leo, Ijumaa Septemba 18.2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam

KESI hiyo inayosikilizwa mfululizo mbele ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru inakuja Mahakamani hapo leo kwaajili ya upande wa utetezi kuendelea kutoa ushahidi wake, ambapo shahidi wa SITA (6), Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) CP Ramadhan Kingai ataanza kutoa ushahidi wake kuanza saa 08:00,

Juzi, Septemba 16.2026, KESI hiyo ilipotajwa mara ya mwisho Mahakamani hapo, mshtakiwa Tundu Lissu ambaye anajitetetea mwenyewe aliieleza Mahakama kuwa atatumia muda wa asubuhi leo kukutana (kuteta) na shahidi huyo, ili kwa pamoja wajiandae kabla ya Mahakama kuanza, ambapo kikao cha mapema cha wawili (2) hao kitafanyika kwenye viunga vya Mahakama.

Ikumbukwe kuwa, licha ya kuwa shahidi wa SITA wa utetezi lakini DCI Kingai ni shahidi wa KWANZA (1) kati ya mashahidi watatu (3) ambao ni vigogo wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini wanaotarajiwa kufika Mahakamani hapo kutoa ushahidi kwa upande wa utetezi,

Wengine ni, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF) Jenerali Jacob John Nkunda, na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camilius Wambura ambao kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mshtakiwa Mahakamani mara ya mwisho aloyoipata kutoka kwa Msajili wa Mahakama ni kwamba wote wamesafiri kikazi wako
ok.🐒
 
Anaenda
Kukaangwa Mshitakiwa na Shahidi wake🫎‼️

Mh Lissu anapenda Sifa sifa wkt yeye yupo Lupango❗️

akikaangwa niyeye ndiyo ataenda mazima uko Lupango❗️

Wale yeye kaamua kuwachekesha wanaenda makwao kusimulia upumbavu wa Mshtakiwa 🫎🫎
muda ndio Mwalimu✍️
 
R. Kingai
Kazi yake ndogo tu kuthibitisha tuhuma za Mshitakiwa🫎🫎

Kama mh Lissu ajafunga Mashahidi wake leo leo
Muda ndio Mwalimu 🦘🦘🦘
 
Back
Top Bottom