Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 61,459
- 100,799
hahahahaha mbwa hawa wanachezea kichapo kwa Lissu mbaya sana sana hawa walevi wakubwa hawa
ni sheria ipi inaruhusu aonane na mawakili wake gentleman?🐒Kwani mnafuata sheria gani huko au mnafuata matakwa yenu kumkomoa? Sema ni sheria gani inayokataza yeye asionane na mawakili wake? Usilete hisia zako za kiumalaya hapa.
Tuendelee kumlilia MunguI don't know man... Mi shabiki lialia tu.
CCM hawana mungu!Tuendelee kumlilia Mungu
Tuendelee kumlilia Mungu
Halafu hakimu ameona aibu anamwambia tuokoe mudaLissu anawafundisha sheria kwanza hapa, eegh anawapa somo kwanza jinsi ya kuripoti hahahahhaa
Yaani leo kaamua kujitetea mwenyeweHuyu jamaa ni level nyingine kabisa aiseee, LISSU hahahahahahaha mahakama inacheka f=ck
Watz wamechokaaaTuombe yale yanayoelekezwa Iran yaende pale Feri na chamwino.
kawapelekea moto vibaya sana sana sana, wamshukuru judge ni wa team yao, shenzi kabisa saa hizi wanaenda kunywa maji kwanzaYaani leo kaamua kujitetea mwenyewe
Hatari sanakawapelekea moto vibaya sana sana sana, wamshukuru judge ni wa team yao, shenzi kabisa saa hizi wanaenda kunywa maji kwanza
Siku hazikawii kufika, usikilizwaji kesi ya Lissu huo umewadia. Kama mnakumbuka wakayi uliopita upande wa mashtaka walisema wanahitaji muda zaidi kukamilisha upelelezi na wakaambiwa tarehe itakayopangwa kutakuwa hakuna nafasi ya hiki kisinngizio tena.
Je, nini kitatokea leo, upande wa mashtaka watatupa taulo na kuomba kutoendelea na kesi?
Wacha tusubiri kuona nini kitajiri.
====
Wananchi, wanachama na viongozi wa Chadema wakiendelea kuwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
View attachment 3371027
View attachment 3371033
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche akiingia katika chumba cha mahakama kwa ajili ya kufuatilia mashauri yanayomkabili mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu.
View attachment 3371065
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dkt. Wilbroad Slaa akiingia katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kufuatilia kesi zinazomhusu Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu
View attachment 3371019
Ulinzi umeimarishwa nje mahakama ya Kisutu.
View attachment 3370986
Gari za jeshi la Magereza na Polisi zikiingia katka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam ikiwa ni msafara wa peke yake unaoonekana kumbeba Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Tundu Lissu ili kuja kufuatilia mashauri yanayomkabili.
Tofauti na siku zingine leo Lissu aliingizwa kwa namna ya tofauti ambapo hata upatikanaji wa picha yake ulikua mgumu huku waandishi wakifanikiwa kuinasa t-shirt pekee(ya no reform no election) iliyozoeleka kuvaliwa na Lissu akiletwa mahakamani.
View attachment 3371024
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Wananchi tayari wameingia ndani ya ukumbi wa Mahakama. Anasubiriwa Tundu Lissu kupandishwa kizimbani. Hakimu pia aingie na kesi iendelee pale ilipoishia.
View attachment 3371102
Dada wa Tundu Lissu, Mchungaji Rose Lissu ameongoza maombi katika chumba ambacho inafanyikia kesi ya Lissu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam.
View attachment 3371112
Tayari Hakimu ameingia kwenye chumba cha mahakama kabla ya Lissu kuingia ambapo hajapata nafasi ya kuwasalimia waliohudhuria mahakamani hapo na kuishia kutikisa kichwa pekee.
LISSU AOMBA KUZUNGUMZA
"Leo hii hapa tulipo ni siku ya 68 tangu nilipoletwa mbele ya mahakama yako tukufu na kusomewa mashtaka ya uhaini, siku 68 na toka siku niliposomewa mashtaka ya uhaini, Mh. uliagiza nipelekwe magereza nikawe mfungwa mahabusu na kwa siku 68 hizi nimekuwa mahabusu, kwa wiki moja gereza la Keko na tangu Ijumaa kuu nimekuwa gereza kuu la Ukonga siku 68.
Mawakili wangu hawa wamekuja kunitembelea gerezani ili tushauriane namna ya kukabiliana na mashtaka haya, hawajaacha kuja mahakamani, hawajaacha kuja magereza na muda wote ambao wamekuja katika siku hizi 68 hawajaruhusiwa kuniona na kuwasiliana na mimi. Hawajaruhusiwa kuonana na mimi na kuzungumza na mimi kwa faragha.
Kitu ambacho kimetokea Mh. ukiingia kwenye gereza kuu la ukonga unapopita reception kuna kachumba kulia, hako kachumba kamegawanywa mara mbili, na ukuta wa kioo, unapokuja wanasimama nyuma ya kioo upand wa reception na mimi nasimama upande mwingine wa kioo tunawasiliana kwa simu na mawakili, tunawasiliana kwa simu. Hakuna fursa ya kubadilishana nyaraka na mimi nina manyaraka mengi sana, hakuna fursa ya kuandika chochote kwa sababu hakuna meza hakuna kiti, mnazungumza kwa simu.
Kama mfungwa mwenye mawakili nina haki ya kuonana na mawakili in confidence ni haki, sio mapenzi ya bwana jela ni haki kama ambavyo nitafafanua hapa."
"In fact Mh. Hakimu kuna wakili mmoja alinitembelea hapa nikapiga sana kelele bwana jela akaniambia kama unaona simu haiwezekani akaniambia njoo ukae hapa reception palipojaa maafisa wa magereza, muongee yeye yupo upande wa pili wa lile lilango la green la chuma yupo upande wakili, mimi kipo upande wa gereza tunazungumza maafisa wote wa gereza kama walivyo hapa wananiangalia kila mtu ananisikiliza ninachozungumza.
Na kwenye simu Mh. hiyo simu anaisikiliza nani mwingine, nani anayejua kwamba kuna mtu mwingine huko anayesikiliza tunachozungumza. Nani anayejua kwamba kwenye 'control room' hakuna vinasa sauti. Sasa Mh. twende kwenye sheria. Mh. Nataka nikusomee kanuni ya 13 ya prisons (prison management regulations 1987, GN 60 of 1987 inasema hivi
'Every prisoner shall be given all reasonable opportunities of communication with his legal adviser or with such other person as the officer-in-charge may approve as representing the interests of the prisoner and a visit to a prisoner by the legal adviser or such other person shall take place within the sight but out of hearing of a prison officer.'1. A detained or imprisoned person shall be entitled to communicate and consult with his legal counsel.
Hii kanuni kuu kwamba wakili wanatakiwa wasisikilizwe maneno wanayoyazungumza na mtu mwingine yeyote, ni sehemu ya sheria kuu za kimtaifa Mh. Hakimu. Na nataka nisome The body of principles for the protection of all persons under any form of detention or imprisonment. Zinaitwa maarufu kama The Mandela principles, Kanuni za Mandela zilipitishwa na baraza kuu la umoja wa mataifa, zilipitishwa kwa resolution of the general assembly of united nations resolution number 43/173 of 9th December 1988. Kanuni kuu kuhusu ulinzi wa watu wote ambao wako mahabusu au wamefungwa. Kanuni ya 18 ya mandela's principles,
2. A detained or imprisoned person shall be allowed adequate time and facilities for consultations with his legal counsel.
3. The right of a detained or imprisoned person to be visited by and to consult and communicate, without delay or censorship and in full con-fidentiality, with his legal counsel may not be suspended or restricted save in exceptional circumstances, to be specified by law or lawful regula-tions, when it is considered indispensable by a judicial or other authority in order to maintain security and good order.
4. Interviews between a detained or imprisoned person and his legal counsel may be within sight, but not within the hearing, of a law enforce-ment official.
5. Communications between a detained or imprisoned person and his legal counsel mentioned in the present principle shall be inadmissible as evidence against the detained or imprisoned person unless they are connected with a continuing or contemplated crime.
Visits by ministers of religion
Mh. haki ya kwanza niliyonayo kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa magereza ni haki ya kuabudu Mungu, haki ya ibaada. Kanuni ya 14 ya hizi prison management regulations vilevile ipo kwenye Mandela's Principles. Na haki ya kuabudu kila Jumapili wakristo na mimi ni mkristo, wanafanyiwa ibaada gereza kuu la Ukonga. Na kwenye sikukuu za kikristo wafungwa wanafanyiwa ibaada gerezani mimi nilipelekwa Ukonga siku ya ijumaa kuu na nilipopokelekwa nilimuomba mkuu wa gereza nikasali sala ya ijumaa kuu akakataa, Jumapili ya pasaka akakataa, Jumatatu ya Pasaka Bw. Jela nataka niende kusali, akakataa na maekataa nimeomba na amekataa kila jumapili including ya jana. Wafungwa wengine wote wanakwenda kusali isipokuwa mimi.
Kanuni ya 14 inasema
(1) A minister of religion shall be admitted at proper and reasonable times to a prison to visit prisoners.
(2) A minister of religion shall be permitted to hold religious services at such hours and in such places as the officer-in-charge may permit and the officer-in-charge shall make such arrangements for the holding of religious services and for the religious instruction of prisoners shall not in any way interfere with the routine and administration of the prison.
Tunaruhusiwa kufundishwa dini, kama hujabatizwa ama, hujapata kipaimara au Komunyo utafundishwa hayo mambo ili ubatizwe au upate Kipaimara au uwe unapata mwili wa bwana na tatu inasema,
(3) The attendance of prisoners at religious services and religious instruction shall be voluntary.
Sio lazima hatulazimishwi kwenda kanisani, unaaenda ukitaka, mimi nimetaka nimekataliwa kwa siku 68. Kwa hiyo Haki yangu ya kuabudu imekiukwa vibaya sana.
si ili awaokoe hao jamaa, ila Lissu kawaweka kwenye 18 tena, next two weeks wanatakiwa kuja na majibu ya DPP. maana baada ya kukabwa wakasema upelelezi umekamilika na jalada liko kwa DPP, kakubali ila kawatega, hio terehe moja july siju watasemajeHalafu hakimu ameona aibu anamwambia yuokoe muda
Nimukuuliza usifanye ujuha wako ewe mtafiti uchwara. Unategemea kitu usichokuwa na ushahidi nacho. Jitahidi utapa uteuzi wa kuja kufyagia vyoo vyangu ili nikulipe kwa kila mwezi naona samia amekusahau.ni sheria ipi inaruhusu aonane na mawakili wake gentleman?🐒
Lissu anajua wapi pa kushika, amwaminya haswaa, hapo mawakili wa serikali wakajiwndae maana wiki ijayo watakomasi ili awaokoe hao jamaa, ila Lissu kawaweka kwenye 18 tena, next two weeks wanatakiwa kuja na majibu ya DPP. maana baada ya kukabwa wakasema upelelezi umekamilika na jalada liko kwa DPP, kakubali ila kawatega, hio terehe moja july siju watasemaje
huna haja ya kuropoka ikiwa huna uelewa wala ufahamu wa kutosha dhidi ya sheria na makosa ya uropokaji yanayomuandama huyo muungwana korokoroni.Nimukuuliza usifanye ujuha wako ewe mtafiti uchwara. Unategemea kitu usichokuwa na ushahidi nacho. Jitahidi utapa uteuzi wa kuja kufyagia vyoo vyangu ili nikulipe kwa kila mwezi naona samia amekusahau.