PreGE2025 Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu upelelezi haujakamilika, yaahirishwa hadi Mei 19,2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu imeendelea tena leo, Jumanne Mei 06.2025 kwa ajili ya kutajwa

1746520158184.jpeg
Akizungumza mbele ya Mahakama katika kesi hiyo inayoendelea kwa njia ya mtandao Wakili wa Serikali Mwandamizi Tawabu Yahya amesema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo kuiomba Mahakama kuhairisha hadi tarehe nyingine

Hata hivyo, taarifa hiyo imeonekana kutopokelewa vyema na Mawakili wa utetezi wakiongozwa na Wakili Mpale Mpoki ambapo wameieleza Mahakama hiyo kuwa hawafurahishwi kwa namna upande wa Jamhuri unavyochelewesha upelelezi wa shauri hilo, hivyo kutumia hadhara hiyo kuomba kupatiwa maelezo ya kina ni kipi hasa kinakwamisha upelelezi wa shauri hilo ambalo tangu mwanzo ilielezwa kuwa ushahidi wake uko kwenye mtandao wa YouTube

Pia, Soma: Fuatilia LIVE Kesi dhidi ya Tundu Lissu. Inasikilizwa muda huu mahakamani

Upande wa Jamhuri kupitia kwa Wakili wa Serikali Mwandamizi Tawabu Yahya uliieleza Mahakama kuwa hakuna kifungu chochote cha sheria kinachowalazimisha kueleza nini kimesalia kwenye upelelezi, badala yake alitumia fursa hiyo kuieleza Mahakama kuwa pindi upelelezi wa shauri hilo utakapokamilika wataweka taarifa zake kwenye mfumo 'mtandao' sambamba na kuwapatia Mawakili wa utetezi

Hoja kubwa iliyowasilishwa na Mawakili wa utetezi Mahakamani leo kuhusiana na shauri hilo ni kwamba upelelezi ukamilike kwa wakati ili shauri hilo likasikilizwe Mahakama Kuu kama inavyotakiwa, kwani kuchelewesha kufanya hivyo ni kutomtendea haki mteja wao

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Hakimu Mkazi Mwandamizi Godfrey Mhini anayesikiliza shauri hili alitoa wito kwa upande wa Jamhuri kuhakikisha wanaharakisha upelelezi na kwamba tarehe inayofuata shauri hilo kutajwa wahakikishe waeleze hatua iliyofikiwa, baada ya kueleza hayo akaahirisha shauri hilo hadi Mei 19.2025 kwa ajili ya kutaja

Hata hivyo, mtuhumiwa wa kesi hiyo Tundu Lissu aliendelea kugoma kushiriki shauri hilo kwa njia ya mtandao, na badala yake Mkuu wa Gereza Ukonga Kamishna Msaidizi wa Magereza Juma Mwaibako alisema alipowasiliana na mshtakiwa amegoma kusikiliza shauri hilo kwa njia ya mtandao.

Chanzo: Jambo TV
 
Wenzetu walioendelea ukiona umekamatwa na kupelekwa mahakamani ujue A-Z zimefika asilimia 89 ila huku TZ unakamatwa kisha upelelezi ujakamilika.
Ndio maana kesi zimejaa magerezani watu kufungwa bila haki zao
 
Hao mawakili wa Chdema hawapo na Lissu kwa maana hawamtakii heli,inakuwaje kesi ndio kwanza imeanza tuseme hata kuanza bado ndio kwanza usikilizaji haujaisha, wanadai unacheleweshwa ?

Tatizo mlizoea Serikali ya kijeshijeshi ile ya babu Magufuri ...fungia ndani nyonga... Hamna Hii serikali ya Raisi SSH haina haraka inakwenda taratibu ,na mnajua Chelewa ufike ,ila kuna wachadema wanakihitaji kiti cha Lisu leo kabla ya kesho utawasikia wakiharakisha maamuzi.
 
Huku tunaishi kwa huruma ya Rais na siyo sheria na taratibu, mtu anaitwa DPP anapewa mamlaka makubwa mno bila sababu kulinda watawala madhalimu
 
Hao mawakili wa Chdema hawapo na Lissu kwa maana hawamtakii heli,inakuwaje kesi ndio kwanza imeanza tuseme hata kuanza bado ndio kwanza usikilizaji haujaisha, wanadai unacheleweshwa ?

Tatizo mlizoea Serikali ya kijeshijeshi ile ya babu Magufuri ...fungia ndani nyonga... Hamna Hii serikali ya Raisi SSH haina haraka inakwenda taratibu ,na mnajua Chelewa ufike ,ila kuna wachadema wanakihitaji kiti cha Lisu leo kabla ya kesho utawasikia wakiharakisha maamuzi.
Siku mumeo akisingiziwa kesi ya kijinga ndiyo akili ako itakaa sawa. Mjinga mkubwa wewe
 
Hao mawakili wa Chdema hawapo na Lissu kwa maana hawamtakii heli,inakuwaje kesi ndio kwanza imeanza tuseme hata kuanza bado ndio kwanza usikilizaji haujaisha, wanadai unacheleweshwa ?

Tatizo mlizoea Serikali ya kijeshijeshi ile ya babu Magufuri ...fungia ndani nyonga... Hamna Hii serikali ya Raisi SSH haina haraka inakwenda taratibu ,na mnajua Chelewa ufike ,ila kuna wachadema wanakihitaji kiti cha Lisu leo kabla ya kesho utawasikia wakiharakisha maamuzi.
Huu sasa ndo uwezo wa kuchanganua mambo wa mtu mwenye elimu ya ngumbalu, ndo maana kinjeketile wala hakupata shida na kizazi chenu enzi hizo! aliwaambia tu "SEMA MAJIII!" nasikia yalaaaah! nafwaa.
 
Kuna siku magufuli aliwauliza polisi mumemkamata mtu na kuku mnampeleka mahakamani mnada upelelezi haujakamilika ni upelelezi hupi wakati mumemkamata akiwa na kuku wa wizi.
 
Sasa mapambio kila sehemu anaupiga mwingi wakati anafanyia wenzie figisu, kwamba hajiamini...anajua fika ktk ushindani sawa uchaguzi mkuu kwake ni kimbembe...mnafki mkubwa!
 
Hao mawakili wa Chdema hawapo na Lissu kwa maana hawamtakii heli,inakuwaje kesi ndio kwanza imeanza tuseme hata kuanza bado ndio kwanza usikilizaji haujaisha, wanadai unacheleweshwa ?

Tatizo mlizoea Serikali ya kijeshijeshi ile ya babu Magufuri ...fungia ndani nyonga... Hamna Hii serikali ya Raisi SSH haina haraka inakwenda taratibu ,na mnajua Chelewa ufike ,ila kuna wachadema wanakihitaji kiti cha Lisu leo kabla ya kesho utawasikia wakiharakisha maamuzi.
Unajua ulicho andika? Kama wangekuwa hawako nae wasinge muwakilisha. Wanawasiliana nae sana, ni lissu ambae amegoma kufanya kwa mtandao
 
Upelelezi ukikamilika serikali itaweka mashahidi 60 na kwa mwaka watasikilizwa mashahidi wanne... tukifika shahidi wa 33 DPP atasema hana nia ya kuendelea na kesi na Lissu kuachiwa huru.. hadi hapo atakuwa katepeta na akili kumkaa sawa.
 
Hao mawakili wa Chdema hawapo na Lissu kwa maana hawamtakii heli,inakuwaje kesi ndio kwanza imeanza tuseme hata kuanza bado ndio kwanza usikilizaji haujaisha, wanadai unacheleweshwa ?

Tatizo mlizoea Serikali ya kijeshijeshi ile ya babu Magufuri ...fungia ndani nyonga... Hamna Hii serikali ya Raisi SSH haina haraka inakwenda taratibu ,na mnajua Chelewa ufike ,ila kuna wachadema wanakihitaji kiti cha Lisu leo kabla ya kesho utawasikia wakiharakisha maamuzi.
Wewe mwanamke, uko kwenye siku zako au? make unaongea ujinga
 
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu imeendelea tena leo, Jumanne Mei 06.2025 kwa ajili ya kutajwa

View attachment 3325993
Akizungumza mbele ya Mahakama katika kesi hiyo inayoendelea kwa njia ya mtandao Wakili wa Serikali Mwandamizi Tawabu Yahya amesema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo kuiomba Mahakama kuhairisha hadi tarehe nyingine

Hata hivyo, taarifa hiyo imeonekana kutopokelewa vyema na Mawakili wa utetezi wakiongozwa na Wakili Mpale Mpoki ambapo wameieleza Mahakama hiyo kuwa hawafurahishwi kwa namna upande wa Jamhuri unavyochelewesha upelelezi wa shauri hilo, hivyo kutumia hadhara hiyo kuomba kupatiwa maelezo ya kina ni kipi hasa kinakwamisha upelelezi wa shauri hilo ambalo tangu mwanzo ilielezwa kuwa ushahidi wake uko kwenye mtandao wa YouTube

Pia, Soma: Fuatilia LIVE Kesi dhidi ya Tundu Lissu. Inasikilizwa muda huu mahakamani

Upande wa Jamhuri kupitia kwa Wakili wa Serikali Mwandamizi Tawabu Yahya uliieleza Mahakama kuwa hakuna kifungu chochote cha sheria kinachowalazimisha kueleza nini kimesalia kwenye upelelezi, badala yake alitumia fursa hiyo kuieleza Mahakama kuwa pindi upelelezi wa shauri hilo utakapokamilika wataweka taarifa zake kwenye mfumo 'mtandao' sambamba na kuwapatia Mawakili wa utetezi

Hoja kubwa iliyowasilishwa na Mawakili wa utetezi Mahakamani leo kuhusiana na shauri hilo ni kwamba upelelezi ukamilike kwa wakati ili shauri hilo likasikilizwe Mahakama Kuu kama inavyotakiwa, kwani kuchelewesha kufanya hivyo ni kutomtendea haki mteja wao

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Hakimu Mkazi Mwandamizi Godfrey Mhini anayesikiliza shauri hili alitoa wito kwa upande wa Jamhuri kuhakikisha wanaharakisha upelelezi na kwamba tarehe inayofuata shauri hilo kutajwa wahakikishe waeleze hatua iliyofikiwa, baada ya kueleza hayo akaahirisha shauri hilo hadi Mei 19.2025 kwa ajili ya kutaja

Hata hivyo, mtuhumiwa wa kesi hiyo Tundu Lissu aliendelea kugoma kushiriki shauri hilo kwa njia ya mtandao, na badala yake Mkuu wa Gereza Ukonga Kamishna Msaidizi wa Magereza Juma Mwaibako alisema alipowasiliana na mshtakiwa amegoma kusikiliza shauri hilo kwa njia ya mtandao.

Chanzo: Jambo TV
Dhuluma dhidi ya haki. Tundu Lissu aachiwe huru
 
Hao mawakili wa Chdema hawapo na Lissu kwa maana hawamtakii heli,inakuwaje kesi ndio kwanza imeanza tuseme hata kuanza bado ndio kwanza usikilizaji haujaisha, wanadai unacheleweshwa ?

Tatizo mlizoea Serikali ya kijeshijeshi ile ya babu Magufuri ...fungia ndani nyonga... Hamna Hii serikali ya Raisi SSH haina haraka inakwenda taratibu ,na mnajua Chelewa ufike ,ila kuna wachadema wanakihitaji kiti cha Lisu leo kabla ya kesho utawasikia wakiharakisha maamuzi.
Ndiyo sababu ulitolewa kwa scissor baada ya kuona unapenda kuchelewa!
 
Hamna kesi hapo, wanamtesa tuu Tundu Lissu. Kwa sheria zetu Prosecutors wanaweza kutesa tuu watu kisiasa, hata kama hamna kesi ya msingi. Badae wataleta Division Four wengi kutoa ushahidi.

Naona joto la No Reforms No Election limewagusa sana watawala. Huyu watamtoa Uchaguzi ukishaisha. Hii nchi inmuonea sana Lissu
 
Hao mawakili wa Chdema hawapo na Lissu kwa maana hawamtakii heli,inakuwaje kesi ndio kwanza imeanza tuseme hata kuanza bado ndio kwanza usikilizaji haujaisha, wanadai unacheleweshwa ?

Tatizo mlizoea Serikali ya kijeshijeshi ile ya babu Magufuri ...fungia ndani nyonga... Hamna Hii serikali ya Raisi SSH haina haraka inakwenda taratibu ,na mnajua Chelewa ufike ,ila kuna wachadema wanakihitaji kiti cha Lisu leo kabla ya kesho utawasikia wakiharakisha maamuzi.
Chupi ya bibi yako ww kwa hiyo unataka upelelezi ufanyike miaka saba na kama hatakutwa na hatia hiyo miaka saba aliyokaa mahabusu itafidiwa?
 
Hao mawakili wa Chdema hawapo na Lissu kwa maana hawamtakii heli,inakuwaje kesi ndio kwanza imeanza tuseme hata kuanza bado ndio kwanza usikilizaji haujaisha, wanadai unacheleweshwa ?

Tatizo mlizoea Serikali ya kijeshijeshi ile ya babu Magufuri ...fungia ndani nyonga... Hamna Hii serikali ya Raisi SSH haina haraka inakwenda taratibu ,na mnajua Chelewa ufike ,ila kuna wachadema wanakihitaji kiti cha Lisu leo kabla ya kesho utawasikia wakiharakisha maamuzi.
🌈
 
Hii nchi bado ina sheria za kizamani sana. How come umshitaki mtu huku ukiwa hujakamilisha upelelezi wa mashtaka uliyomshtaki?

Kama wakikuta hajafanya kosa watamfidia Lissu muda waliompotezea? We need a reshuffle kwakweli
 
Back
Top Bottom