Mwaka 1990 au 91 kama sikosei Nelson Mandela alifanya ziara nchini Tanzania, watu walijipanga kuanzia Pugu Road, Buguruni, Ilala, Kariakoo, Mnazi Mmoja, Posta mpaka Ikulu.
Kufika Ikulu naambiwa alimwaga machozi hatari maana wakati anafungwa jela alikokaa miaka zaidi ya 26 alipotoka alikuta maendeleo makubwa sana nchini kwake chini ya Makaburu. Akawa kama mshamba anashangaa shangaa tu maghorofa na mabarabara. Sasa akawaza kuwa kama Makaburu wameweza haya vipi Tanzania ambayo inajitawala chini ya Mwanajumuni wa Africa JK Nyerere.
Alichokikuta sasa, slums za Buguruni kwa Mnyamani, Malapa, Ilala, Posta ilikuwa ile aliyoiacha, ndio kisa cha kulia. Aliona Uhuru haujamkomboa Mtanzania.
Haya maneno sijayatunga, niliambiwa na mzee wangu aliyekuwa kiongozi mwandamizi kipindi hicho.
Sasa baada ya mimi kumaliza kidato cha sita nilienda USA nikatelekezwa New York na rafiki yangu wa high school. Nilikuja kuokolewa na Babu Sikare naarufu kama Albino Fulani (RIP)a mbaye pia nilisoma nae Dakawa High School na kukulia pamoja mitaa ya Oysterbay. Yeye akiishi Namanga flats za Tanesco na mimi nikiishi Chole.
Siku moja nikifanya mazoezi niliteguka mguu nikapiga simu ikaja ambulance mpaka hospital nikatibiwa nikapona hapo nilikuwa USA kumbuka. Baada ya kurudi nchini nilipitia msoto kwa miezi kadhaa, kuna siku niliumwa nikakosa hata Panadol, nikahitimisha kuwa tumerogwa au tuna laana.
Mnaompinga Lema mjitafakari, wenzetu wako mbali, mnapoendesha hizo crown zenu mnajiona maisha mmeyapatia.
Viongozi wetu bado wana kazi ya kututoa kwenye umasikini, tuko nyuma sana. Lema hakuyajua hayo maana alikuwa hajawahi kufika Duniani!
Tumetoka kwenye ukoloni wa mwendazake sasa ni muda sahihi wa kupigania maendeleo ya vitu bila kutekana au kuuana.