Kiasi chake Lema yuko sahihi, niliishi USA miaka kumi niliporudi nchini niliamini Watanzania tuna laana

Ahaa mimi sikurudi na kitu ila nilirudi na knowledge na exposure kubwa tu ambao ni mtaji mkubwa sana kwangu
 
Isitoshe zaidi Tanzania ina vyanzo vingi mnoo ambavyo tukiamua kufanya maendeleo ya nchi yetu, Itawezekana vema kabisa.

Nadhani Utawala mbovu ndio sababu ya haya yote toka hapo mwanzo.
 
Nchi kama Sweden, Finland, Norway,China,India.
Kutawaliwa sio kisingizio cha kuwa masikini, USA,China,India, Uingereza zimeshawahi tawaliwa.
Mikoa yote mikubwa imejengwa imepangiliwa na wao chek mji wa Arusha,Dar, MWANZA,Mbeya, Ruvuma, Dodoma nk sisi hata tu kupanga miji hatuwezi.
Miundombinu inafata watu leo ni tabu ukitaka kujenga barabara ni lazima ulipe fidia watu.
Kwanini miji hata huko maporini wasipeleke miundombinu then watu ndio wafate miundombinu.
 
Malaysia ,Singapore zilikuwa sawa tu na sisi,kilimo kimewatoa kwenye umasikini sisi tuna mabonde maji ya mito yanaishia baharini
 
Tuna tatizo kubwa
 
Uzembe + wizi wa kodi zetu + kuishi maisha ya kwenye tv (ubishoo) + mwanaume anatembea na leso eti hataki kuchafuka, atafanya kazi ya aina gani kweli mwanaume dizaini hiyo? Atazalisha mali kweli huyo!

Uimara wa uchumi wetu ujengwe na kuchapa kazi kwa kila mmoja, uzalendo kwa nchi, kutokufuja mapato ya nchi na asiwepo mwizi na mzembe popote pale

Ndani ya miaka 10 tu, yatosha kufikia malengo na kuondokana naumasikini

Mwenye boda boda naye apige kazi! Siungi mkono hata kidogo Tamko la Lema
 
Yaani wazurulaji wawili mmekutana mnasapotiana upuuzi vile!
 
Watu kama nyinyi mnashindwaje kutafakari zaidi? Mandela hatakuwa amelia kwa sababu ya serikali ya Tanzania kushindwa kuendeleza watu wake ili hali imejitawala! La! Alilia kuona hali aliyotuweka yeye, sisi waTanzania - yaani Tanzania kutumia rasilimali ndogo iliyo nayo, kusaidia kukomboa nchi nyingine, Mozambique, Namibia, Zimbabwe, Angola, etc. Alilizwa, kuona Tanzania inawekewa vikwazo na waingereza, wajerumani etc. Sababu ya kupigania uhuru wa watu wengine! Ndicho kilichomliza hasa!
Sasa mtu ambaye hajui maendeleo na mateso ya waafirica - Afrika Kusini, USA, UK etc. Atafikiri hawa wameendelea kwa sababu hawakulaaniwa. Waafrika wengi - mamilioni kwa mamilioni walikufa/waliuawa ili wazungu waweze kuleta ambulance dakika nne ajali inapotokea!
Halafu Mnamnanga Magufuli ambaye alianza kuwaletea maendeleo kidogo, watu wawili, wakafa au Wakapotea! Maana kwa America, Africa ya Kusini ambapo malaki na malaki ya waafrika waliuawa ili wapate maendeleo, mnaona hiyo sawa hawakulaaniwa.
Msione vyaelea vyaundwa. Watu wamekufa na kunyimwa haki zao huko mnakohusudu ulaya na marekani. Hapakuwepo na demokrasi mnayo imba kila siku.
Mpaka sasa UK hamna hata katiba mpya wala kuukuu!
 
Vijana wetu wamekulia katika jamii yenye mafisadi na wao wanataka wajikwamue. Wafanye nini? Hata kupata hiyo pikipiki ni kazi!! Lema yupo sawa kiuchumi ndio maana kasema vile. Labda tujiulize hizo pesa zake ni za uhalali? Angepitia njia kama ya bodaboda hangesema hivyo. Naomba huyu bwana achunguzewe. Hiyo biashara ya magari ilikuwa na uhalali? Narudia tena "bodaboda ni kazi sawa na nyingine". Kwa kijana mwenye nidhamu ya pesa atakupigia mahesa kwa mwezi anaingiza ngapi.
 
Ila hata ungekuwa wewe unawapinga makaburu unafungwa miaka 26 unakuta nchi inawaka,ina maendelei makubwa,ukaenda nchi inayojitawala mji umejaa slums ungejisikiaje,Africa tuna tatizo kubwa tukubali tu
 
Kuwa dormant siwe kigezo kilicho tufanya tuwe nyuma,issue je china haikutawaliwa na Japan?,kumbe hapa tatizo ni kwamba Africa muda wake wa kujitawala ulikuwa Bado haujafika,hatuna vision katika mataifa yetu zaidi kila kitu tunatanguliza siasa na matumbo yetu katika issue kubwa za kitaifa,nakumbuka SA katika zama za makaburu ilifikia hatua ya kuanza kutengeneza siraha za nyuklia, assume baada ya muafrika kuchukua madaraka SA sio SA Ile ya mkabulu, Africa vinatutesa vitu vitatu;
1.Ubinafsi(HKM et al,2020)
2.Chuki(HKM et al,2022)
3.Unafiki(HKM et al,2019)
Afrika hasa chini ya jangwa la Sahara tukiondoa SA,ili tuweze kupiga hatua kubwa tunapaswa kuviondoa hivyo vitu hapo juu lakini Kwa nature yetu hiki kitu hakiwezekani ,muda wetu wa kujitawala ulikuwa Bado haujafika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…