Kiasi chake Lema yuko sahihi, niliishi USA miaka kumi niliporudi nchini niliamini Watanzania tuna laana

Kiasi chake Lema yuko sahihi, niliishi USA miaka kumi niliporudi nchini niliamini Watanzania tuna laana

Nchi kama Sweden, Finland, Norway,China,India.
Kutawaliwa sio kisingizio cha kuwa masikini, USA,China,India, Uingereza zimeshawahi tawaliwa.
Mikoa yote mikubwa imejengwa imepangiliwa na wao chek mji wa Arusha,Dar, MWANZA,Mbeya, Ruvuma, Dodoma nk sisi hata tu kupanga miji hatuwezi.
Miundombinu inafata watu leo ni tabu ukitaka kujenga barabara ni lazima ulipe fidia watu.
Kwanini miji hata huko maporini wasipeleke miundombinu then watu ndio wafate miundombinu.
Ukiangalia mimi sijabase sana kwenye point ya kutawaliwa maana najua hadi Uingereza imetawaliwa pia,Hoja yangu imebase hapo kwenye biashara ya utumwa ambayo kwa muda wa miaka zaidi ya 300 waafrica tuliharibiwa mfumo wetu wa maisha kwa kuwindwa kama digidgi katika jamii zetu..

Ni kweli Sweden,Finland na nyinginezo zimetawaliwa na pia USA,china,India zimetawaliwa pia lakini ukoloni wa maeneo hayo sio kama ule uliokuwa Africa,kumbuka tumetoka kwenye utumwa hatujakaa vizuri kujipanga tena watu wanakuja kututawala na kufuja rasilimali zetu wakati ambapo China,USA,India na nchi nyingine wananchi wao walikuwa wanafanya maendeleo katika nchi zao kutokana na kwamba nguvu kazi ya taifa iliendelea kubaki katika maeneo yao kujenga nchi..

Sasa sisi hata hatujaanza kujijenga anakuja mtu kukutawala na kucontrol kila kitu..
Wakati sisi tunataabika kwenye dhahama ya utumwa China walikuwa na empire kubwa sana zilizokuwa tayari zimejijenga na kufanya mapinduzi ya viwanda katika maeneo yao,India hivyohivyo,Ukoloni uliokuwepo USA pia ni tofaut na wa huku kwetu
Malaysia ,Singapore zilikuwa sawa tu na sisi,kilimo kimewatoa kwenye umasikini sisi tuna mabonde maji ya mito yanaishia baharini
Nilisema hapa suala kubwa ni uongozi mbovu tulionao tukiweza hapa tu basi tumepiga hatua
Kuwa dormant siwe kigezo kilicho tufanya tuwe nyuma,issue je china haikutawaliwa na Japan?,kumbe hapa tatizo ni kwamba Africa muda wake wa kujitawala ulikuwa Bado haujafika,hatuna vision katika mataifa yetu zaidi kila kitu tunatanguliza siasa na matumbo yetu katika issue kubwa za kitaifa,nakumbuka SA katika zama za makaburu ilifikia hatua ya kuanza kutengeneza siraha za nyuklia, assume baada ya muafrika kuchukua madaraka SA sio SA Ile ya mkabulu, Africa vinatutesa vitu vitatu;
1.Ubinafsi(HKM et al,2020)
2.Chuki(HKM et al,2022)
3.Unafiki(HKM et al,2019)
Afrika hasa chini ya jangwa la Sahara tukiondoa SA,ili tuweze kupiga hatua kubwa tunapaswa kuviondoa hivyo vitu hapo juu lakini Kwa nature yetu hiki kitu hakiwezekani ,muda wetu wa kujitawala ulikuwa Bado haujafika
Kuwa dormant kulikosababishw na external interference hasa karne ya 15 ni sababu ambayo hatutakiwi kuikwepa,point zako nyingne zote upo sahihi na nakubaliana nazo
Inakuwaje lakini sisi tulipata uhuru kipindi kimoja na nchi kama Malaysia lakini leo hii wenzetu wako mbali sana kiuchumu ukilinganisha na sisi.

Na wao walikuwa katika kiwango cha umasikini kama cha kwetu.
Suala kubwa ni nature ya uongozi tuliobahatika kuwa nao katika nchi zetu,viongozi wengi ni walafi sio visionary hawapo commited hawawrzi kujali shida tulizokuwa nazo km nchi hili ndilo tatzo kubwa
Unajua kua 1961 uchumi wa China ulikua sawa na wa Tanzania??
Sio kweli hizi ni sayings tu za kujifariji,china mapinduzi ya viwanda wamefanya karne ya 18 huko kipindi ambacho sisi bado hatujielewi kbs
 
Mkuu upo SAHIHI kabisaa kumbuka sisi waafrica ni uzao wa yule aliyemchungulia baba yake(mwanzo sura ya 9.)
 
Huna lolote ujualo kuhusu Arusha zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani. Nenda kawaulize wakazi wa Arusha barabara za mitaa zenye lami ziliwekwa lini, Mradi mkubwa wa maji umesainiwa kabla ya 2015 na utekelezaji wake haukutegemea msukumo wowote wa diwani, mbunge awe wa CCM au CDM.

Usitake kuleta upotoshaji wa kijinga hapa. Kama unasubiri taarifa za maendeleo ya Arusha kupitia kwa Gambo basi umefeli pakubwa.
Unaleta domo bila facts 😆😆😆😆

Nimekupa ukweli hapo au huna bando ? Unataka ukweli gani mwingine?
 
Tuliza akili soma tena utaelewa nilichomaanisha
Hata nikituliza akili naona bado unaamini unastahili kuwa nyuma kimaendeleo. Soma development phases za China, Singapore na Malaysia utabidili mtazamo wako.
 
Sawa, wanasaidiwaje? Mimi nimesema ardhi nzuri na mvua za kuaminika kama factors muhimu katika maendeleo ya kilimo. Hizo fursa hazitumiwi vilivyo ila zikitumika vilivyo mkulima atainuka.
Mfano huko nilikosema mtu analima heka 5 anavuna gunia 25 badala yab100. Ndio kilimo kina changamoto lakini ukikabiliana nazo unatoka.
Nilienda mahali bagamoyo nikakuta mtu amejenga karibu bwawa ambalo halikauki lakini alikuwa anatafuta mboga nikaenda kumnunulia mbegu za bamia, maboga na biringanya nikamuelekeza nikamtafutia na samadi kutoka maboma ya wamang'ati baada alinishukuru.
Kwa hiyo usikatishe watu tamaa kama alizeti hazina bei mnaotawala mna mpango gani au mnazidi tu kuagiza korie
Kwani wewe huoni mipango ya serikali kwenye Kilimo na kutafuta masoko? Wewe na Chadema unadhani mtafanya lipi jipya ikiwa hamna hata mawazo Wala strategy zaidi ya kulalamika?
 
Mandela alifanya ziara nchini Tanzania, watu walijipanga kuanzia Pugu Road, Buguruni, Ilala, Kariakoo, Mnazi Mmoja, Posta mpaka Ikulu.

Kufika Ikulu naambiwa alimwaga machozi hatari maana wakati anafungwa jela alikokaa miaka zaidi ya 26 alipotoka alikuta maendeleo makubwa sana nchini kwake chini ya Makaburu. Akawa kama mshamba anashangaa shangaa tu maghorofa na mabarabara. Sasa akawaza kuwa kama Makaburu wameweza haya vipi Tanzania ambayo inajitawala chini ya Mwanajumuni wa Africa JK Nyerere.
Wakiambiwa wana lanaa wanaona kama wametukanwa😅😅😅
 
Kwani wewe huoni mipango ya serikali kwenye Kilimo na kutafuta masoko? Wewe na Chadema unadhani mtafanya lipi jipya ikiwa hamna hata mawazo Wala strategy zaidi ya kulalamika?
Chini ya Ccm Tanzani aina laana. Ukitaka kutoamini acha tu.
 
Ingekuwa kulima ni rahisi hivyo ungekuta wakulima wote ni matajiri

Mdomo Kila mtu anao,Leo hii Singida wanalalamika alizeti hazinunuliki
Hata kulima tuta la mchicha na lenyewe ni kazi
 
Unaleta domo bila facts 😆😆😆😆

Nimekupa ukweli hapo au huna bando ? Unataka ukweli gani mwingine?

Ukweli wa kusema Lema Kawa mbunge wa Arusha kwa miaka 15, acha utoto dogo. Narudia tena, hizo barabara za Arusha zimejengwa wakati Lema akiwa mbunge, na wala hazijaletwa na mbunge, bali ni mikopo ambayo serikali imekopa. Kawatafute wajinga wenzio ndio uwaambie mbunge anaweza kujenga barabara, au Mradi wa maji wa 500b. Huo ujinga wa kusema mbunge amefanya kitu fulani wanaambiwa wasiojua miradi ya maendeleo inaendeshwaje.
 
Back
Top Bottom