Kiasi chake Lema yuko sahihi, niliishi USA miaka kumi niliporudi nchini niliamini Watanzania tuna laana

Kiasi chake Lema yuko sahihi, niliishi USA miaka kumi niliporudi nchini niliamini Watanzania tuna laana

Mimi naona tupambane kwa uwezo wetu tu tusijilinganishe na mtu.

Kufikia karne ya 15 Marekani ilikuwa tayari imepiga hatua katika nyanja kadhaa kiuchumi,kijamii na kisiasa wakati huo mababu zetu wanavaa vibwaya na kuvuta kinyesi cha ng'ombe..

Kutoka karne ya 15 ambapo Marekani ilikuwa active mpk karne ya 21 ni miaka mia 6 hiyo na katika kipindi hicho mababu zetu wamepitia vipindi vigumu vya biashara za utumwa mara ghafla ukoloni huu hapa tunakuja kuachiwa huru mpaka sasa ni miaka 60 tu tangu tuanze kujitegemea..

Hivi mnaona ni sahihi kujilinganisha na watu ambao wameendelea tangu katne ya 15? Yaani wana miaka zaidi ya mia tano kwenye game!?...Hatuna laana balu mazingira yametuforce kuwa hivi
Hakuwa na marekani Karne ya 15 labda kuanzia ya 16(1770's)

Labda kama unataka kupigilia msumari hoja Yako lakini Ina chembe za fallacy.
 
Ukiangalia mimi sijabase sana kwenye point ya kutawaliwa maana najua hadi Uingereza imetawaliwa pia,Hoja yangu imebase hapo kwenye biashara ya utumwa ambayo kwa muda wa miaka zaidi ya 300 waafrica tuliharibiwa mfumo wetu wa maisha kwa kuwindwa kama digidgi katika jamii zetu..

Ni kweli Sweden,Finland na nyinginezo zimetawaliwa na pia USA,china,India zimetawaliwa pia lakini ukoloni wa maeneo hayo sio kama ule uliokuwa Africa,kumbuka tumetoka kwenye utumwa hatujakaa vizuri kujipanga tena watu wanakuja kututawala na kufuja rasilimali zetu wakati ambapo China,USA,India na nchi nyingine wananchi wao walikuwa wanafanya maendeleo katika nchi zao kutokana na kwamba nguvu kazi ya taifa iliendelea kubaki katika maeneo yao kujenga nchi..

Sasa sisi hata hatujaanza kujijenga anakuja mtu kukutawala na kucontrol kila kitu..
Wakati sisi tunataabika kwenye dhahama ya utumwa China walikuwa na empire kubwa sana zilizokuwa tayari zimejijenga na kufanya mapinduzi ya viwanda katika maeneo yao,India hivyohivyo,Ukoloni uliokuwepo USA pia ni tofaut na wa huku kwetu

Nilisema hapa suala kubwa ni uongozi mbovu tulionao tukiweza hapa tu basi tumepiga hatua

Kuwa dormant kulikosababishw na external interference hasa karne ya 15 ni sababu ambayo hatutakiwi kuikwepa,point zako nyingne zote upo sahihi na nakubaliana nazo

Suala kubwa ni nature ya uongozi tuliobahatika kuwa nao katika nchi zetu,viongozi wengi ni walafi sio visionary hawapo commited hawawrzi kujali shida tulizokuwa nazo km nchi hili ndilo tatzo kubwa

Sio kweli hizi ni sayings tu za kujifariji,china mapinduzi ya viwanda wamefanya karne ya 18 huko kipindi ambacho sisi bado hatujielewi kbs
Nakufuatilia comment zako na nakuelewa vizuri,napenda unavyochambua bila kuweka mambo ya vyama au nchi unajaribu kuongekea Africa as a whole,ni kweli Africa tuna matatizo yanayofanana
 
Ukweli wa kusema Lema Kawa mbunge wa Arusha kwa miaka 15, acha utoto dogo. Narudia tena, hizo barabara za Arusha zimejengwa wakati Lema akiwa mbunge, na wala hazijaletwa na mbunge, bali ni mikopo ambayo serikali imekopa. Kawatafute wajinga wenzio ndio uwaambie mbunge anaweza kujenga barabara, au Mradi wa maji wa 500b. Huo ujinga wa kusema mbunge amefanya kitu fulani wanaambiwa wasiojua miradi ya maendeleo inaendeshwaje.
Kwa hiyo kazi ya Lema ni ipi wewe Babu jinga? Kutukana watu maskini au?
 
Huwa najiuliza kwanini watu wengi walioenda Marekani huwa wanarudi nchini wakiwa hawana kitu huku akili zao kama haziko sawa... wewe mdukuzi na Lemutuz huwa ni mifano hai ya karibu. Nina ndugu yangu alikuwa akija likizo anafikia hoteli ya kitalii five star. Hadi siku anarudi bongo hakuwa na kitu. Alifariki katika umaskini wa kutisha. Lema nae kwenda tu Canada amerudi kawehuka..!! Inasikitisha sana. Matatizo ya Afrika hayawezi kutatuliwa kwa kutumia mbinu za mabeberu.

Hakuna haja ya kuwaponda bodaboda au VICOBA kama vile ndo mbinu ya kutatua tatizo. Tulicho nacho mkononi ndo kitatuvusha na sio vinginevyo. Kama bodaboda imeonyesha matokeo mazuri basi tuboreshe badala ya kuropoka kwamba ni laana. VICOBA navyo viwekewe utaratibu mzuri kila kitu kitakuwa sawa.
Wewe ni mpuuzi unataka kila anekuja tz akuonyeshe asset anazomiliki,usijilinganishe na Lemutuz baba yake alishamwandalia maisha hapa Tz kitambo
 
Mwaka 1990 au 91 kama sikosei Nelson Mandela alifanya ziara nchini Tanzania, watu walijipanga kuanzia Pugu Road, Buguruni, Ilala, Kariakoo, Mnazi Mmoja, Posta mpaka Ikulu.

Kufika Ikulu naambiwa alimwaga machozi hatari maana wakati anafungwa jela alikokaa miaka zaidi ya 26 alipotoka alikuta maendeleo makubwa sana nchini kwake chini ya Makaburu. Akawa kama mshamba anashangaa shangaa tu maghorofa na mabarabara. Sasa akawaza kuwa kama Makaburu wameweza haya vipi Tanzania ambayo inajitawala chini ya Mwanajumuni wa Africa JK Nyerere.

Alichokikuta sasa, slums za Buguruni kwa Mnyamani, Malapa, Ilala, Posta ilikuwa ile aliyoiacha, ndio kisa cha kulia. Aliona Uhuru haujamkomboa Mtanzania.

Haya maneno sijayatunga, niliambiwa na mzee wangu aliyekuwa kiongozi mwandamizi kipindi hicho.

Sasa baada ya mimi kumaliza kidato cha sita nilienda USA nikatelekezwa New York na rafiki yangu wa high school. Nilikuja kuokolewa na Babu Sikare naarufu kama Albino Fulani (RIP)a mbaye pia nilisoma nae Dakawa High School na kukulia pamoja mitaa ya Oysterbay. Yeye akiishi Namanga flats za Tanesco na mimi nikiishi Chole.

Siku moja nikifanya mazoezi niliteguka mguu nikapiga simu ikaja ambulance mpaka hospital nikatibiwa nikapona hapo nilikuwa USA kumbuka. Baada ya kurudi nchini nilipitia msoto kwa miezi kadhaa, kuna siku niliumwa nikakosa hata Panadol, nikahitimisha kuwa tumerogwa au tuna laana.

Mnaompinga Lema mjitafakari, wenzetu wako mbali, mnapoendesha hizo crown zenu mnajiona maisha mmeyapatia.

Viongozi wetu bado wana kazi ya kututoa kwenye umasikini, tuko nyuma sana. Lema hakuyajua hayo maana alikuwa hajawahi kufika Duniani!

ni muda sahihi wa kupigania maendeleo ya vitu bila kutekana au kuuana.
Na hao wanaowapa hizo raha huko majuu waambieni waache kuwatumia vibaraka wao huku hadi.mkose panadol
 
Watu kama nyinyi mnashindwaje kutafakari zaidi? Mandela hatakuwa amelia kwa sababu ya serikali ya Tanzania kushindwa kuendeleza watu wake ili hali imejitawala! La! Alilia kuona hali aliyotuweka yeye, sisi waTanzania - yaani Tanzania kutumia rasilimali ndogo iliyo nayo, kusaidia kukomboa nchi nyingine, Mozambique, Namibia, Zimbabwe, Angola, etc. Alilizwa, kuona Tanzania inawekewa vikwazo na waingereza, wajerumani etc. Sababu ya kupigania uhuru wa watu wengine! Ndicho kilichomliza hasa!
Sasa mtu ambaye hajui maendeleo na mateso ya waafirica - Afrika Kusini, USA, UK etc. Atafikiri hawa wameendelea kwa sababu hawakulaaniwa. Waafrika wengi - mamilioni kwa mamilioni walikufa/waliuawa ili wazungu waweze kuleta ambulance dakika nne ajali inapotokea!
Halafu Mnamnanga Magufuli ambaye alianza kuwaletea maendeleo kidogo, watu wawili, wakafa au Wakapotea! Maana kwa America, Africa ya Kusini ambapo malaki na malaki ya waafrika waliuawa ili wapate maendeleo, mnaona hiyo sawa hawakulaaniwa.
Msione vyaelea vyaundwa. Watu wamekufa na kunyimwa haki zao huko mnakohusudu ulaya na marekani. Hapakuwepo na demokrasi mnayo imba kila siku.
Mpaka sasa UK hamna hata katiba mpya wala kuukuu!
Kusaidia ukombozi nchi za africa kumekusaidia nini wewe maskini wa tandale,Julia's alikuwa anapenda sifa aonekane shujaa
 
Hakuwa na marekani Karne ya 15 labda kuanzia ya 16(1770's)

Labda kama unataka kupigilia msumari hoja Yako lakini Ina chembe za fallacy.
Marekani ipo tangu karne ya kwanza lakini Foreigners walianza kuingia karne ya 15..Before karne ya 16 Marekani tayari kulishakuwa na empires kubwa kama Aztecs na Incas na walikuwa tayari wameendelea kidogo kwenye masuala kadhaa hususani kilimo cha mahindi cha mashamba makubwa na maritime technology pia..hiyo Marekani ya kuanzia karne ya 16 ilikuja kuendelezwa na wazungu lakini maendeleo yalikuwepo before ambayo yaliizid baadhi ya empire za Africa pia
 
Kwa hiyo kazi ya Lema ni ipi wewe Babu jinga? Kutukana watu maskini au?

Ndio nakuambia katafute wajinga wenzio ndio uwaambie kuwa mbunge kafanya jambo fulani la maendeleo. Na kwa kusaidia ni kuwa kuwa kazi za mbunge ni tatu nazo ni :
  1. Mwakilishi wa wananchi wake bungeni.
  2. Kutunga sheria akiwa bungeni.
  3. Kuisimamia na kuishauri serikali.
Hizo hapo juu ndio kazi za mbunge, na zote hizo Lema kazifanya. Ni wapi inaonyesha mbunge analeta maendeleo? Au ni wapi inaonyesha mbunge anakusanya kodi kwa ajili ya kuleta maendeleo? Wajinga wa aina yako ndio huwa wanadanganywa kuwe mbunge analeta maendeleo. Hivyo mradi wowote ukifanyika kwenye eneo hilo, wanasiasa matapeli husema mbunge ndio kaleta.
 
Marekani ipo tangu karne ya kwanza lakini Foreigners walianza kuingia karne ya 15..Before karne ya 16 Marekani tayari kulishakuwa na empires kubwa kama Aztecs na Incas na walikuwa tayari wameendelea kidogo kwenye masuala kadhaa hususani kilimo cha mahindi cha mashamba makubwa na maritime technology pia..hiyo Marekani ya kuanzia karne ya 16 ilikuja kuendelezwa na wazungu lakini maendeleo yalikuwepo before ambayo yaliizid baadhi ya empire za Africa pia
Sisi karne ya 21 mahindi yanatushinda kulima
 
Ndio nakuambia katafute wajinga wenzio ndio uwaambie kuwa mbunge kafanya jambo fulani la maendeleo. Na kwa kusaidia ni kuwa kuwa kazi za mbunge ni tatu nazo ni :
  1. Mwakilishi wa wananchi wake bungeni.
  2. Kutunga sheria akiwa bungeni.
  3. Kuisimamia na kuishauri serikali.
Hizo hapo juu ndio kazi za mbunge, na zote hizo Lema kazifanya. Ni wapi inaonyesha mbunge analeta maendeleo? Au ni wapi inaonyesha mbunge anakusanya kodi kwa ajili ya kuleta maendeleo? Wajinga wa aina yako ndio huwa wanadanganywa kuwe mbunge analeta maendeleo. Hivyo mradi wowote ukifanyika kwenye eneo hilo, wanasiasa matapeli husema mbunge ndio kaleta.
Labda kama ni mwakiloshi wa nyie mataahira
 
Na wewe pia hukujua kuchagua maneno ungesema “baadhi ya Watanzania wana laana”
Sasa na mimi nakurudishia mwenyewe hiyo laana maana unayo wewe na wanao na ndugu zako wote mpaka kizazi cha nne walahi[emoji35]
You hollow pathetic mind walahi[emoji35]
 
Labda kama ni mwakiloshi wa nyie mataahira

Ndio maana nakuambia ww ni wale wajinga mnaodanganywa kuwa maendeleo yanaletwa na mbunge na mnaamini. Leo nadhani umepata elimu ya kazi za mbunge, ndio maana umeishia kujibu huu utoto maana ulikuwa hujui lolote. Kama uko hapa jukwaani umeishia kubeba upotoshaji kuwa Lema Kawa mbunge kwa miaka 15, utakuwa unajua lolote sasa.
 
Ndio maana nakuambia ww ni wale wajinga mnaodanganywa kuwa maendeleo yanaletwa na mbunge na mnaamini. Leo nadhani umepata elimu ya kazi za mbunge, ndio maana umeishia kujibu huu utoto maana ulikuwa hujui lolote. Kama uko hapa jukwaani umeishia kubeba upotoshaji kuwa Lema Kawa mbunge kwa miaka 15, utakuwa unajua lolote sasa.
Tangu lini Chadema mkawa na akili? Mnachoweza nyie ni ulalamishi,kutukana,kulaumu,kuorodhesha shida za Watzn na mkijitahidi mtasema ooh Marekani,sijui canada mara Malaysia kukosa vile na hivi ila you have no solution.

Wapuuzi nyie ndio maana mnaangukia pua miaka na mikaka.
 
Back
Top Bottom