Kiasi gani cha pesa uliwahi kuliwa kwenye DUBWI mpaka ukachanganyikiwa?

Kiasi gani cha pesa uliwahi kuliwa kwenye DUBWI mpaka ukachanganyikiwa?

Mtu na akili zako umeshika noti za elfu kumi unachenji mia mbili nyingi inamaana wew unapenda chelechelena sio noti
 
Like dude ni kipimo Cha akili na wengi wanaocheza Kuna kitu kinakua hakipo sawa kichwani. Imagine unatoa noti afu unapewa Mia mbili miambili such a stupid asshole๐Ÿ’”๐Ÿ’”๐Ÿ˜ฌ
 
Kuna watu wanaliwa kwenye dubwi mpaka wanachanganyikiwa.

Nishashushudia jamaa ameliwa laki 2 ya mtaji wa biashara ya mke wake kwenye dubwi.

Mkewe alimtuma akamnunulie vifaa vya kupikia vitafunwa kwa ajili ya biashara na ndo pesa pekee waliyokuwa nayo.

Jamaa kapita karibu na dubwi akapata tamaa acheze kidogo ale angalau elfu 50 sasa kwenye kucheza akajikuta kaangia hasara akawa anafosi arudishe angalau pesa aliyokuja nayo kilichomkuta pesa yote ikaliwa akaweka bondi smart phone yake kwa elfu 20 nayo ikaliwa.

kilichomponzaga alikuwa anawa dabo dabo wanyama anawaweka hata mara tano Tano ila return inakuja ndogo mwisho akarudi mweupe.

Mwingine katoka Moro kwenye kazi za ujenzi karudi na kwenye laki na ushee kabla hajafika kwake kaanzia kwenye dubwi mwisho wa siku kaliwa yote
Mimi nishacheza sana hili dubwana, nishaliwa sana na kula sana, ila mtaji wangu hua naanzia 100k nikiutafuta mkanda huku nikicheza na number za michezo zinazojizungusha kwenye kile kidude cha katikati kinachotoa maandishi mekundu na bonus. Naweza nikaliwa mpaka 70k na michezo 4-7 inaofuata mmoja ukanipa 180-200k naacha kucheza. Huwa sichezagi dubwi ya aina yote, ninalolijulia ni lile lenye mnyama mkubwa Tembo, alafu 20 Simba, Kichuya na Nyati.
Angalizo; Zipo baadhi ya siku lina lamba mtaji mzima na mara nyingi ikitokea hivi najua mchina ameshabadirisha settings, huwa naacha mpaka niizoee setting mpya.
For now nimeacha baada ya kugundua nilikuwa nacheza for fun huku nikiwa napiga gambe na mara nyingi mimi nakuwa loser, naweza nikalipuna lakini hela yote ikaishia kwenye pombe so furaha yangu imehamia sehemu nyingine๐Ÿ˜Š
 
Back
Top Bottom