Kiasi gani cha pesa uliwahi kuliwa kwenye DUBWI mpaka ukachanganyikiwa?

Kiasi gani cha pesa uliwahi kuliwa kwenye DUBWI mpaka ukachanganyikiwa?

Kuna siku kama nilikuona na baba levo jirani, yule anaonekanaga na wakamaria tu 😂
Baba Levo nasikia kadundwa na Harmo kisa walikuwa wanagombaniana pesa za tajiri kwenye cassino 😂😂😂😂
Nilivyoisikia hii story madogo wanasimuliana nilicheka..
 
Baba Levo nasikia kadundwa na Harmo kisa walikuwa wanagombaniana pesa za tajiri kwenye cassino 😂😂😂😂
Nilivyoisikia hii story madogo wanasimuliana nilicheka..
😂 nimesikia pia kapigwa mpaka pua imekuwa ndogo.
 
Kuna watu wanaliwa kwenye dubwi mpaka wanachanganyikiwa.

Nishashushudia jamaa ameliwa laki 2 ya mtaji wa biashara ya mke wake kwenye dubwi.

Mkewe alimtuma akamnunulie vifaa vya kupikia vitafunwa kwa ajili ya biashara na ndo pesa pekee waliyokuwa nayo.

Jamaa kapita karibu na dubwi akapata tamaa acheze kidogo ale angalau elfu 50 sasa kwenye kucheza akajikuta kaangia hasara akawa anafosi arudishe angalau pesa aliyokuja nayo kilichomkuta pesa yote ikaliwa akaweka bondi smart phone yake kwa elfu 20 nayo ikaliwa.

kilichomponzaga alikuwa anawa dabo dabo wanyama anawaweka hata mara tano Tano ila return inakuja ndogo mwisho akarudi mweupe.

Mwingine katoka Moro kwenye kazi za ujenzi karudi na kwenye laki na ushee kabla hajafika kwake kaanzia kwenye dubwi mwisho wa siku kaliwa yote
Hawa ndiyo mambo ya jamii forum.ajabu lijitu liutuzima linacheza dubwi?
 
Kuna mwamba namjua, kwanza kabisa yeye anaamini chochote kilichotengenezwa na binadamu kinamapungufu .

Hivyo yeye alijikita sana katika kuyachunguza hayo madude ya mchina (bonanza ), akayajua udhaifu wake ulipo , ili likupe pesa akagundua lile bonanza linakitu kama pini ambayo pindi utakapo ingiza coin ya sh 200 , hii coin ikiigusa tu hiyo pini ndiyo hilo bonanza hukupatia pesa, na ili bonanza litoa pesa akagundua pia lazima liwe limeshaingiza kiasi kilichopangwa katika mfumo wake kwanza na baada ya hapo huanza kukubali kutoa pesa .nje na hapo kila coin utakayoiweka haigusi ile pin na mchezaji hujikuta kaliwa .

Jamaa akakaa chini na kutafakari kwa kina sana namna ya kufanya ili aweze kumpiga mchina vizuri kwa kupitia hayo mabonanza aliyoyatapaza ovyo huko mtaani . Na kuja na njia ifuatayo

- alichukua coin ya sh mia mbili na kuitoboa pale katikati hali iliyopelekea upande mmoja wa coin asa ule upande msumari uliotokezea kuwa na mvimbo au muinuko , akachukua msasa na kupunguza muinuko ule ili coin ile isiweze kugoma pindi atakapoingiza kwenye mlango wa bonanza wa kuingizia pesa .

- lakini pia , ili mbidi awe mvumilivu kidogo , kwani alitakiwa kuwahi asubuhi na mapema sehemu lilipo bonanza husika ambalo alikuwa ameliweka kwenye target ya kulimanga pesa siku hiyo . Hivyo angesubilia hapo kwa muda labda tuseme toka asubuhi mbaka jioni huku akilifuatilia ni mara ngapi limetoa au kutokutoa kabisa , bonanza ambalo lilikuwa halijatoa sana ni wazi lilikuwa na kiasi kikubwa sana cha pesa ukilinganisha na lile linalotoa toa hovyo . Hivyo yeye alilitaka hili ambalo halitoi hovyo maana hili ndilo lilikuwa lenye pesa nzuri ndani yake .

- yeye alikuwa akifika anaweka ile coin yake kwa kuhakikisha hakuna anaye mfuatilia na baada ya coin kuingia ule mvimbo au muinuko wa coin pindi ulipogusa tu ile pin , bonanza bila ubishi lilikuwa linacheua ( kutoa ) pesa ya kutosha . Na baada ya hapo angeondoka haraka sana tayari kwa mkakati mpya wa kulipiga bonanza jingine .

Note :coin alimbidi kuzitengeneza nyingi maana ikishaingia kule kuitoa isingewezekana hivyo ilimbidi kuzitengeneza coin za mtindo huu mara kwa mara itakapo kufanya huu uhuni .

Hali hii iliwasumbua sana wachina kwani pindi walipofungua mfumo wa bonanza na kuona uhuni huu uliwauma sana walipeana taarufa juu ya swala hili na kuamua kubadilisha mfumo wa kuingizia coin .

Lakin mbaka wanafanikiwa jamaa tayari naye alikuwa kasha waliza sana mbaka kuweza kununua bodaboda yake na kwasasa achezi tena madude hayo kajikita safii katika kazi yake ya bodabod .
 
Unataka uniulizie wapi jirani, hapa au Piiiiiii em au kwa hapa dirishani linalotazama gorofa lako?
😂😂😂 Koh koh koh
Ghorofa lipi tena?? Hivi bonyokwa siku hizi kuna maghorofa??
Halafu kweli niko serious kuna kitu nataka kukuuliza sema nasahau..!!
 
😂😂😂 Koh koh koh
Ghorofa lipi tena?? Hivi bonyokwa siku hizi kuna maghorofa??
Halafu kweli niko serious kuna kitu nataka kukuuliza sema nasahau..!!
Si lilibebwa na maji umesahau tupo wapi? 😂

Kwahiyo hata sasa umesahau?
 
Back
Top Bottom