Kibabage amegoma kubadilika, mbadala wake huyu anatufaa sana aletwe..



Kibabage katika wachezaji karibu wote wa Yanga ndio hamna kitu kabisa, hana kabisa uwezo, pilika nyingi za bure na hana uwezo wa kufunga au kupiga shoot, alafu alivyo hana uwezo zaidi ya hapo alipofikia, Yanga ingeagana nae mapema kabisa
 
Jamani tutamlaumu kibabage bure, ila ukweli uko hapa, kikosi kinahitaji maboresho yafuatayo,beki wa kati mmoja wa kimataifa, left na right full backs wa ndani wenye uwezo, DM mmoja katiri wa ndani,ikishindikana kupatikana basi JONASI JERAD MKUDE,SURE BOY wapewe muda wacheze ili hata aucho hayupo basi awepo DM "Halisia" wa kuziba pengo hilo, forwadi mmoja wa kimataifa mwenye njaa,mfano fred michael coubran,christian lionel ateba mbida,mayele,nk. wachezaji wa kuwaweka pembeni kupisha usajili huo ni
1. jean othos baleke~aondoke jumla.
2. nickson clement kibabage ~mkopo
3.kibwana shomari~jumla
4. aziz andambwile mkopo
5. prince mpumelelo dube~jumla japo haiwezekani maana kumvunjia mkataba ndo changamoto.
 
Bryson nmemfuatilia, kuna haja ya kumrudisha!
 
Hukumshuhudia Oscar Joshua na Mwinyi Hajji
Acha utani mkuu,yaani amshuhudie Keneth Mkapa halafu awe hajawaona Haji Mwinyi na Oscer Joshua?Kifupi jamaa yupo sahihi,Yanga haina bahati ya kuwa na no 3 bora tangu aondoke Kenny Mkapa,ingawa walipita Alphonce Modest,Ramadhan Waso,Nurdin Bakari,Amir Maftah ambao walionesha ubora lakini hawakumfikia,pia wote hao nao walikuwa ni zao la Simba
 
Andambwile hana kiwango cha kucheza Yanga, tokea alivyokuwa Azam alikuwa injury prone na kiwango kibovu, wakamtema, sijui raisi aliona nini kwake!
 
Kweli huyo Mkapa sikumshudia
Nimezaliwa 1993
Umezaliwa katika miaka ya utawala wa Kenny Mkapa no 3 huku beki wa kulia akicheza Frederick Mwakalebela pale Yanga. Katika miaka 35 iliyopita ni Mohammed Hussein tu ndiye amecheza kwa kiwango bora na kwa muda mrefu kama Kenny Mkapa kwa mabeki wa kushoto hapa nchini.
 
Hivi Dube ana nini huyu jamaa. Mimi nilitilia mashaka sana rekodi yake ya ufungaji aliyotoka nayo Azam kwa misimu 3+.
 
Ken Mkapa alitanguliwa na mwarabu Ahmed Amasha, acha kabisa.
 

Huyu unayemuita Mzee mzima, anaanzaje na jina "Joyce"
 
Kibabage katika wachezaji karibu wote wa Yanga ndio hamna kitu kabisa, hana kabisa uwezo, pilika nyingi za bure na hana uwezo wa kufunga au kupiga shoot, alafu alivyo hana uwezo zaidi ya hapo alipofikia, Yanga ingeagana nae mapema kabisa
Watu wanaweza wakaona kama.tunamsagia kunguni sana ila kiukweli abadilike haraka sana
 
Sahihi,counterpart wake(Amasha Miafro) upande wa Simba alikuwa Mohammed Kajole,wa Mkapa kule Simba alikuwa Twaha Hamidu "Noriega"
Twaha alikuwa hamfikii hata kidogo Ken Mkapa maana Mkapa alikuwa kapanda balaa, nakumbuka aliwahi piga Kona mpaka ndani Simba 0-1 Yanga.
 
Kimsingi Joseph Guede alitakiwa kubaki ni basi tu siasa zetu hizi za soka jamaa angepewa muda kama wa dube angefunga zaidi imagine game zile sita tu magoli 9kama sikosei
 
Twaha alikuwa hamfikii hata kidogo Ken Mkapa maana Mkapa alikuwa kapanda balaa, nakumbuka aliwahi piga Kona mpaka ndani Simba 0-1 Yanga.
Sijasema kuwa alikuwa anamfikia,nimesema kuwa no 3 upande wa pili alikuwa Twaha Hamidu,pia nimesema hapo nyuma kwa zaidi ya miaka 35 iliyopita hakuna no 3 nchini, aliekuwa bora kama Mkapa,Shabalala angeweza kumfikia ingawa Mkapa alichomzidi ni kuwa Mkapa alikuwa na nguvu na ubabe pia alikuwa mfungaji mzuri wa mashuti ya mbali na free kick,nakumbuka mwaka 1992 alipomtungua Mwameja goli kwa shuti la mita nyingi,kisha wiki iliyofuata akawafunga Ismailia kwa umbali uleule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…