TANZIA Kibaha Vijijini: Diwani Mteule wa CCM Kata ya Kikongo afariki pamoja na wajukuu zake wawili baada ya nyumba yao kuchomwa moto

TANZIA Kibaha Vijijini: Diwani Mteule wa CCM Kata ya Kikongo afariki pamoja na wajukuu zake wawili baada ya nyumba yao kuchomwa moto

Hapo ndo mnapokosea, matendo kama haya yakiwakuta Wapinzani likes CHADEMA, ACT huwa mnakaa kimya.
Thatswhy yakiwakuta ninyi hakuna anaewaonea huruma, hii italeta matokeo mabaya sana kwa taifa letu, Vijana ambao ni kizazi cha kesho wanacheka huku wanalia, ipo siku aijuaye Allah mtaliingiza taifa mahala pabaya sana.
agwe..

Amnesty International na ujeremani wanatuonea huruma
 
Kinacho sikitisha ni pale madhila Kama haya yanaoneka yakitokea kwa baadhi ya watu kana kwamba ndio pekee wanaostahili kuishi kuliko wengine ambao huonekana kwamba wao kuuawa au kupotezwa ni haki yao!
 
Nimeona kwenye taarifa watu wamefikishwa mahakamani huko kusini kuhusu masuala ya uchaguzi kwa kukutwa na vitu hatarishi, ajabu wengi wao wamevunjwa miguu na mikono! Alipoombwa hakimu watu hao watibiwe, mwanasheria wa serikali akaweka pingamizi kwamba sio kazi ya mahakama kuangalia afya za washtakiwa!

Wakazuiwa kupewa dhamana na ikaamuriwa ibaki busara ya magereza kama watibiwe au la! Nimesikitika sana!

Kweli kwa hayo mnataka niungane nanyi majanga yanapowakuta, Mungu anisamehe ila moyo umekataa kabisaa!
 
Wakati wa kuiba kura na kufanya uharamia CCM mnajisahau kwamba kuna maisha baada ya uchaguzi?
Uchaguzi ukishamalizika sio busara kuweka vyama mbele,ungesema diwani mteule ingetosha.

Mungu amlaani/awalaani walio ondoa uhai wa wenzao.
 
MWENYEZI MUNGU, awafanyie wepesi Wapumzike kwa amani, kifo cha moto ni cha mateso Sana, pole kwa wanafamilia wote, jamaa na majirani, R. I. P fatma na wajukuu
Ni kweli ingawa mara nyingi kinachoua ni moshi na sio moto. Kwa vyovyote vile, kifo ni kifo na marehemu wanastahili kuombewa ili Mwenyezi Mungu awaweke mahali pema peponi.
 
Tungekuwa tumeanzia kwenye kulaani mauji ya wapinzani pia (hasa pemba), vipigo vya polisi, wizi wa kura, uporwaji wa haki kwenye chaguzi zetu, bambikizi za makesi, vitisho vinavyopelekea wapendwa wetu kukimbia nchi, nk wala tusingefika huku.
 
Back
Top Bottom