Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
..hizo fomu zinatolewa KIENYEJI sana.
..msimamizi alitakiwa achukue na nakala ya KITAMBULISHO, pamoja na anuani ya kila anayechukua fomu.
..kwa kilichotokea inatakiwa MAMLAKA za juu za Tume ya Uchaguzi, baada ya kujiridhisha kuhusu mgombea halali wa CDM, zitoe maelekezo chama hicho kipewe fomu nyingine kwa ajili ya mgombea wao.
Nakubaliana na wewe. Chadema wanatakiwa kuzibana Mamlaka ya juu ya Tume ili ichukue hatua kali kukomesha tabia kama hizi kabla hazijaota mizizi.
Anachonishangaza Msimamizi ni kukataa kata kata kuchukua hatua yeyote ya kujiridhisha kuwa watu wenye nia ovu hawajamtumia kama daraja kufanikisha ajenda yao. Anashindwa nini kuwasiliana na uongozi wa chama husika kinachodaiwa kuandika barua ya uthibitisho ili wathibitishe uhalali wa barua hiyo?
Katibu Mkuu wa Chadema anatakiwa kutoa tamko kuhusu suala hili na kuitaka Tume ifute jina la aliyechukua na wamuadhibu. Mambo haya yalianza kwa Meya Boniface na sasa tunayaona yanafanyika Kimamba na Kilombero.
Ukimya wa Chadema unaonyesha kuwa hawako serious kama chama.
Amandla...