Kuna mambo mawili naamini CDM watayafanya
1. Kutoa taarifa polisi, pamoja na hili kupeleka malalamiko yao tume ya uchaguzi kwa kilichotokea
2. Waonyeshe jinsi msimamizi wa uchaguzi anavyo lifanya jambo hili kuwa hawezi kuchukua hatua hadi pale atakaporudishiwa fomu iliyochukuliwa. Nimemsikiliza kiongozi wa CDM akieleza kuwa fomu ilichukuliwa kabla CDM hawajachagua mgombea wao. Katika yote hili ndio rahisi kujiridhisha kama ni kweli na kama ni hivyo basi ile formu ni batili moja kwa moja. Pia kuna list ya CDM je ni nani alichaguliwa?
Sasa mama kushinikiza CDM wamleteee ile fomu anategemea wao watampata wapi huyo "mhalifu"? Cha ajabu kabisa inasemekana hawana namba za simu za wagombea wala anuani za makazi yao. Hivi ni vitu ambavyo havina mjadala vinatakiwa viwepo vinginevyo NEC hawako serious. Mama anashikilia barua aliyoletewa ni halali-anajuaje kuwa ni halali wakati wahusika wana mwambia si halali. Uhalali si signature tu bali na contents za barua. Anasema sio swala la busara ni swala la sheria. Kama sheria ina mapungufu unafanya je.
Matokeo kama haya yanathibitisha bado tuna elements za ushenzi. Badala ya kudhibiti washenzi, tunajaribu kuwakingia kifua kwa manufaa ya kisiasa.