PreGE2025 Kibango cha "No reforms No election" chatua Club ya Small Planet, wamiliki wakikana

PreGE2025 Kibango cha "No reforms No election" chatua Club ya Small Planet, wamiliki wakikana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mnataka kuwaharibia wapika keki eeh?
0669a20e-3cfa-4dad-881f-353b3d38a58a.jpeg
 
Mimi ni CCM kuliko wewe na ukoo wako ila sipendi ukandamizaji na uonevu nataka Haki na utawala wa sheria.
Watu wote tungekuwa hivi, hii nchi ingepona. Watu tuna ndugu huko ccm, viongozi wakubwa wa Serikali. Ila tunasimamia haki, haijalishi unapata faida kiasi gani huko ila kaa upande wa haki.

Sasa hawa wengine wanaendeshwa na mambo ya chama au mtu fulani, kuwe na haki hakuna hawajali. Ila haya mambo hugeuka wanasema kulia kupokezana.
 
🤣🤣🤣🤣
Unatuma ujumbe then unakana, ila ujumbe unakuwa ushafika.
Malema: Nusu ya wabunge humu ndani ni wapumbavu

Wabunge wa ANC: Mheshimiwa Spika, Malema afute kauli.

Spika: Malema ongea lugha ya kistaarabu, futa kauli

Malema: Ninafuta kauli, nusu ya wabunge humu si wapumbavu

Wabunge wa ANC: Makofiii
 
🤣🤣🤣🤣🤣 Ila bunge la SA ni tamu sana.
 
Wakuu

Naona No reforms inaendelea kuchanja mbuga hatimaye kiliwasili kwenye Club ya Small planet na baada ya video kusambaa wamiliki wamekiruka vibaya mno

===
Uongozi wa kampuni ya SMALL PLANET ENTERPRISES LIMITED ambayo ni miliki wa bar ya Small Planet - Sinza, umesikitishwa na unalaani vikali jambo ambalo limetokea katika usiku wa Jumamosi ya tarehe 07/06/2025 kuamkia Jumapili ya 08/06/2025 ambapo kumeonekana kuwa na Bango Mjongeo (Mobile Billboard) likiwa lina jumbe zenye viashiria vya kisiasa.

Kampuni ya SMALL PLANET ENTERPRISES LIMITED na Bar yake ya Small Planet - Sinza, inafanya shughuli zake chini ya sheria na hakuna namna yoyote inafungamana na upande wowote wa kisiasa hivyo jumbe iliyoonekana ikitembea katika mitandao ya kijamii ni njama tu za kikundi fulani kwa lengo la kuchafua taswira nzima ya Bar yetu kwenye upande wa ushindani wa kibiashara.

Kilichotokea ni kwamba, mmoja wa wahudumu wetu akiwa katika utendaji kazi wake alishinikizwa na moja ya mteja mwenye maslahi yake binafsi na kulazimisha kuandikwa kwa jumbe hiyo yenye viashiria vya siasa na kulazimisha itangazwe kwenye Bango Mjongeo la Bar yetu na kisha kurekodi na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Kampuni ya SMALL PLANET ENTERPRISES LIMITED na Bar yake ya Small Planet - Sinza, imeshaanza kuchukua hatua za kisheria kufuatilia ni nani aliyelazimisha jumbe hizo za kisiasa kuandikwa na kutangazwa katika bar yetu ili sheria iweze kufuata mkondo wake.

1749446884880.png
 
Kilichotokea ni kwamba, mmoja wa wahudumu wetu akiwa katika utendaji kazi wake alishinikizwa na moja ya mteja mwenye maslahi yake binafsi na kulazimisha kuandikwa kwa jumbe hiyo yenye viashiria vya siasa na kulazimisha itangazwe kwenye Bango Mjongeo la Bar yetu na kisha kurekodi na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.
Mteja ameonesha ubunifu kwa hilo, mhudumu nae ameonesha ukomavu sana kwa kukubali kuning'iniza bango hewani na anaelewa nn anafanya!

Siku sio nyingi CCM wanaiga hii nawaju hawana ubunifu kazi kuiga iga tu!!
 
Back
Top Bottom