PreGE2025 Kibango cha "No reforms No election" chatua Club ya Small Planet, wamiliki wakikana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wakuu

Naona No reforms inaendelea kuchanja mbuga hatimaye kiliwasili kwenye Club ya Small planet na baada ya video kusambaa wamiliki wamekiruka vibaya mno

===
Uongozi wa kampuni ya SMALL PLANET ENTERPRISES LIMITED ambayo ni miliki wa bar ya Small Planet - Sinza, umesikitishwa na unalaani vikali jambo ambalo limetokea katika usiku wa Jumamosi ya tarehe 07/06/2025 kuamkia Jumapili ya 08/06/2025 ambapo kumeonekana kuwa na Bango Mjongeo (Mobile Billboard) likiwa lina jumbe zenye viashiria vya kisiasa.

Kampuni ya SMALL PLANET ENTERPRISES LIMITED na Bar yake ya Small Planet - Sinza, inafanya shughuli zake chini ya sheria na hakuna namna yoyote inafungamana na upande wowote wa kisiasa hivyo jumbe iliyoonekana ikitembea katika mitandao ya kijamii ni njama tu za kikundi fulani kwa lengo la kuchafua taswira nzima ya Bar yetu kwenye upande wa ushindani wa kibiashara.

Kilichotokea ni kwamba, mmoja wa wahudumu wetu akiwa katika utendaji kazi wake alishinikizwa na moja ya mteja mwenye maslahi yake binafsi na kulazimisha kuandikwa kwa jumbe hiyo yenye viashiria vya siasa na kulazimisha itangazwe kwenye Bango Mjongeo la Bar yetu na kisha kurekodi na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Kampuni ya SMALL PLANET ENTERPRISES LIMITED na Bar yake ya Small Planet - Sinza, imeshaanza kuchukua hatua za kisheria kufuatilia ni nani aliyelazimisha jumbe hizo za kisiasa kuandikwa na kutangazwa katika bar yetu ili sheria iweze kufuata mkondo wake.
View attachment 3361711

View attachment 3361712
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Wanafatilia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya nani? Kwa kosa gani?
Wakimfukuza mhudumu tusimuache ateseke, anajitambua.
 
Wasije wakamfukuza tu alikuwa kwenye majukumu yake ya kila siku kama wengine wanavyoombaga kuwekewa maneno "Vibinti vya alfu mbili vitamu" nk
 
Shida iko wapi kama mteja wa ugimbi baadala ya kuandika jina lake yeye kaona hicho ndio muhimu Kwanza!
 
Jamaa wanaamua kujihami mapema...

Nchi ya waoga kuwahi kutokea duniani..
 
Wasije wakamfukuza tu alikuwa kwenye majukumu yake ya kila siku kama wengine wanavyoombaga kuwekewa maneno "Vibinti vya alfu mbili vitamu" nk
Na hapo ndipo ninapojiuliza, kosa lake lipo wapi? Hatua za kisheria dhidi ya nani?
 
Wakuu

Naona No reforms inaendelea kuchanja mbuga hatimaye kiliwasili kwenye Club ya Small planet na baada ya video kusambaa wamiliki wamekiruka vibaya mno

===
Uongozi wa kampuni ya SMALL PLANET ENTERPRISES LIMITED ambayo ni miliki wa bar ya Small Planet - Sinza, umesikitishwa na unalaani vikali jambo ambalo limetokea katika usiku wa Jumamosi ya tarehe 07/06/2025 kuamkia Jumapili ya 08/06/2025 ambapo kumeonekana kuwa na Bango Mjongeo (Mobile Billboard) likiwa lina jumbe zenye viashiria vya kisiasa.

Kampuni ya SMALL PLANET ENTERPRISES LIMITED na Bar yake ya Small Planet - Sinza, inafanya shughuli zake chini ya sheria na hakuna namna yoyote inafungamana na upande wowote wa kisiasa hivyo jumbe iliyoonekana ikitembea katika mitandao ya kijamii ni njama tu za kikundi fulani kwa lengo la kuchafua taswira nzima ya Bar yetu kwenye upande wa ushindani wa kibiashara.

Kilichotokea ni kwamba, mmoja wa wahudumu wetu akiwa katika utendaji kazi wake alishinikizwa na moja ya mteja mwenye maslahi yake binafsi na kulazimisha kuandikwa kwa jumbe hiyo yenye viashiria vya siasa na kulazimisha itangazwe kwenye Bango Mjongeo la Bar yetu na kisha kurekodi na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Kampuni ya SMALL PLANET ENTERPRISES LIMITED na Bar yake ya Small Planet - Sinza, imeshaanza kuchukua hatua za kisheria kufuatilia ni nani aliyelazimisha jumbe hizo za kisiasa kuandikwa na kutangazwa katika bar yetu ili sheria iweze kufuata mkondo wake.
View attachment 3361711

View attachment 3361712
Jitihada haijawai kuishinda Kudra.
 
Kila mtu afikiwe, mpaka kwenye derby ya simba na yanga mabango yawepo
 
hapo lingekuwa lile neno la ccm la " Oktoba tunatiki" wala wasingetoa hayo mabarua ya kukana.!
 
Back
Top Bottom