Tetesi: Kibarua cha CAG kuota nyasi

Humu kuna watu huwa wana tabia ya kuandika jambo fulani bila kuwa na ufahamu nalo. Inashangaza kumsikia au kuona watu wakiandika CAG anaweza kutumbuliwa au mwingine anatamka afukuzwe,,,,,!. Acheni ushabiki huyo magufuri hata ubavu wa kumtumbua huyu jamaa hana maana analindwa na sheria ngojeni astaafu au afariki
 
kwa sisi wanafunzi wa Mussa J Assad, hatujastushwa na hili, tunamfahamu hababaishi katika kazi zake.

nikizikumbuka zile 'get five or get zero' ha haa

viva Assad
 
Sidhani kama unajua CAG,Judge & Gavana,.sio watu wa kutumbuliwa kindenzi kama wengine
...anyway_angeshatumbuliwa kitambo sana,..only that Jiwe hana ubavu huo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
uko sahihi
 
Mlivyoambiwa ELIMU ELIMU ELIMU sijui kama mlielewa

Unaujua utaratibu wa kumfuta kazi CAG?

Umeonyesha ujinga wa hali ya juu sana, hivi unaujua utaratibu na sheria za vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano? havikufutwa? je ni taratibu na sheria ngapi za nchi ikiwemo katiba ambavyo vinanavunjwa kila siku? you should think before you defile me
 

Kutokujua ni sawa sawa na kiza kinene, CAG hawezi kutolewa kwa kauli za kisiasa bali for professional misconduct au yeye mwenyewe aamue kuachia ngazi.
 
Spika Job Ndugai alipaswa kutumia busara kwa kuifanyia kazi kauli ya CAG, lakini ikitokea kwasababu zozote sakata hili likamtoa CAG kwenye kiti chake itakuwa bahati mbaya sana maana nchi itakuwa imepoteza mtu mwenye heshima, anayeijua kazi kazi. Habari jema ni kwamba ataondoka (kama ataondoka) akiwa sifa ya CAG aliye mkweli anayesema ukweli bila kumumunya maneo.
 
dah dah !
naliona jiwe linavyobadilikabadilika rangi
jinsi dili lake la 1.5 tr linavyokomaliwa na Asad hadi bunge linaonekana urojo !
LIVE LONG CAG ASAD MPAKA KIELEWEKE !
kkk !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutokujua ni sawa sawa na kiza kinene, CAG hawezi kutolewa kwa kauli za kisiasa bali for professional misconduct au yeye mwenyewe aamue kuachia ngazi.


Hivi unaota au umeshaamka? Tanzania ya sasa hakuna sheria inayoheshimiwa isipokuwa kauli za kisiasa na ndio zinazofanya kazi.
 
Hawez kushika nafasi yoyote serikalin baada ya kuachia nafasi yake ya CAG

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…