Kibarua kimeota Nyasi: Waliozoea siasa za vita Mbowe, Lissu, Rais Samia waungana kujenga nchi. Funzo kwa...!

Kibarua kimeota Nyasi: Waliozoea siasa za vita Mbowe, Lissu, Rais Samia waungana kujenga nchi. Funzo kwa...!

Rasterman

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2015
Posts
33,894
Reaction score
44,117
Sasa ni rasmi tunaelekea siasa za Ulaya na Marekani.

Siasa za maendeleo. Siasa za kistaarabu. Zile siasa za kutafutana kuuana, kutekana, kufungana na kufilisiana mali Mh Rais Samia ameona hazina tija kwa taifa.

Akiongea na Wasikilizaaji ktk Mtandao wa maongezi wa Club House Mh Makamu Mwenyekiti Chadema Tundu Antiphas Lissu ameunga mkono jambo zuri alilofanya Mh Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chama hicho kuwa ni jambo jema.

Ni jambo jema kwa kuwa Rais ameachana na siasa za mitulinga. Tumefikia hatua hii kwa jasho na damu, tumelipa gharama hapa tulipofika " alisema kiongozi huyo.

Aliongeza kuwa Mbinu na mikakati iliyotumika kuishi wakati za awamu ya tano haiwezi kuzaa matunda wakati wa awamu ya sita kwani wakati huo tuliamua kubadilika kwa ajili ya Individual survival.

Jambo hili limeungwa mkono na wadau mbali mbali wa siasa na watanzania woote wakidai kuwa sasa tunaelekea Tanzania Mpya.

Wito kwa vyombo vingine vya serikali viige mfano mwema wa Rais Samia.

Wikendi njema
 
Kamwe huwezi kuwa na siasa za kistarabu kama za marekani na ulaya, kwenye nchi iliyojaa CHAWA!!ambao kwenye chama wanategemea upepo wa mwenyekiti wao(CCM) anasema nini na wao ndio huko huko, wenzetu huko unafiki ni mwiko, kila mwanachama, mtendaji serikal anasimamia sheria za nchi.

Hata kama mh.Rais ana weza kuwa na nia nzuri lakini yeye pekee hawezi kuifanya nchi ikawa hivyo!!mfano sakata la makonda linaloendelea sasa hivi na GSM, ni kama hakuna kitu viti, kila mtu hadi jeshi la polisi, linaogopa kusema chochote, kwani hawajui nini msimamo wa mheshimiwa, unaweza ukachangia chochote yakakukuta!!lakini subiria , mheshimiwa alizungumzie kidogo tu, labda achomekee, tu kuwa mbona vyombo vya dola, vimeshindwa kulitolea ufafanuzi, ndipo utawaona CHAWA, sasa, kuanzia ndani ya chama, na vyombo vyote vya ulinzi na usalama utavisikia vimeibuka, na kuanza kutoa matamko !!

Mfano ni kipindi kile cha jiwe, kuhusu makontena ya makonda.
Tatizo la Afrika siasa zake bila unafiki HUTOBOIIII
 
Uko sahihi,
Kamwe huwezi kuwa na siasa za kistarabu kama za marekani na ulaya, kwenye nchi iliyojaa CHAWA!!ambao kwenye chama wanategemea upepo wa mwenyekiti wao(CCM) anasema nini na wao ndio huko huko...
 
Huu ndio wakati wa wapinzani kuwasha moto, otherwise muitwe jina lingine na si wapinzani tens,,! Mmekula maharagwe ya wapi tena

Sisi tunaweza kubashiri mlichopatiwa kwenye hicho kinahoitwa maongezi na mkuu wa nchi,
 
Lissu anaonesha nia nzuri waliyonayo viongozi wa Chadema juu ya mustakabali wa amani, upendo na umoja wa taifa letu. Lengo ndio lilikuwa hili fungua ukurasa mpya wote waufuate na Chadema wameshaonesha njia.

Lakini pale aliposema siasa za awamu ya tano haziwezi kutumika awamu hii ya sita ningeshauri awe na subira. Huyu alishasema anaendeleza alipoishia mtangulizi wake, siasa hizo hazitatumika endapo mahitaji yatasikilizwa na kufanyiwa kazi.

Mfano mikutano ya vyama vya siasa, hii ni haki ya kikatiba, inapominywa makusudi na watawala hauwezi kuendelea kuwabembeleza kwa kwenda ikulu, lazima ipiganiwe, hapa ndipo naona siasa za awamu ya tano zinapoweza kujirudia.

Kama kweli serikali ya Samia inataka siasa za kistaarabu muda ni huu, ifanye kazi kwa vitendo, haki iwepo kwa wote bila kujali itikadi zao, kinyume na hapo, ni wao ndio watakaokuwa wanaleta siasa za vurugu wala sio upinzani.
 
Samia hawezi siasa za ikulu na siasa za majukwaa ya nyomi na zomea zomea, na hata hivo ni Rais wa kipindi cha mpito 2021-2025 , hawezi na hataweza kuwa mgombea wa ccm hio 2025.

Mgombea mwenye hadhi hio na anaemudu viatu vya ikulu anafahamika na anaendelea vizuri na tuition ya Urais.

Pigeni mayowe vuvuzela ila Samia anaishia 2025, Marais wa Zali la mentali mwisho 2025.

HAHM ije mvua ije jua ije ukame ije mafuriko habari ndio hiyo.
 
Ngoja tuwe na subira. Usijekuta Mbowe anataka kutuuza. Siku zote nimekuwa siwaamini wanasiasa na viongozi wa dini. They are always selfish at some point and manipulators.

Lakin kama nia kweli ni siasa za kistaarabu kama wanazofanya wenzetu wa south Africa na Kenya it's okay. Mradi tu Mbowe asiwasaliti watu. Atapata laana mbaya sana. Na itakuwa down fall yake kubwa no matter what he have been doing. Watu wana akili zao, sio mapunda
 
Hakuna we subiri uone...umpige risasi aungane nawe? Umweke jela aungane nawe? Binadamu huyuhuyu ninaemfahamu au?
 
Kamwe huwezi kuwa na siasa za kistarabu kama za marekani na ulaya, kwenye nchi iliyojaa CHAWA!!ambao kwenye chama wanategemea upepo wa mwenyekiti wao(CCM) anasema nini na wao ndio huko huko...
Nani kakuambia Marekani na ulaya kuna siasa za kistaarabu?? Hivi umesahau au umeamua kujitoa ufahamu kuhusu songombingo zilizotokea marekani wakati wa uchaguzi uliopita uliomhusisha Trump na Biden na vurugu zake zote?

Siasa za kistaarabu ziko mbinguni peke yake yake, ambapo imekubalika kuwa kuna Mungu Mwenyezi mmoja tu aliyeumba mbingu na nchi na vyote vinavyoonekana na visivyoonekana na visivyoweza kuonekana, utukufu una yeye milele na milele AMINA.
 
Kamanda haongelei tena katiba mpya. Kaiweka mfukoni! CDM ni CCM C
IMG_20220312_080249.jpg
 
Ngoja tuwe na subira. Usijekuta Mbowe anataka kutuuza. Siku zote nimekuwa siwaamini wanasiasa na viongozi wa dini. They are always selfish at some point and manipulators. Lakin kama nia kweli ni siasa za kistaarabu kama wanazofanya wenzetu wa south Africa na Kenya it's okay. Mradi tu Mbowe asiwasaliti watu. Atapata laana mbaya sana. Na itakuwa down fall yake kubwa no matter what he have been doing. Watu wana akili zao, sio mapunda
The simple truth is; "siasa za kistaarabu" ndizo tunazoweza watanzania, kwani wangapi kati yetu wanaweza siasa za maandamano? wangapi wakiambiwa wajitokeze kuandamana wanaenda? wengi hubaki nyumbani wakidai waliogopa vitisho vya kina Mambosasa.

Kumbe hapa utaona hata kama wengi wanamtilia shaka Mbowe, lakini ikitokea Mbowe huyo huyo akawaambia waandamane hakuna kati yao atakayejitokeza, wote watajificha nyumbani kwao. Kabla ya kuanza kuwanyooshea kidole viongozi wa Chadema, kwanza tujitazame sisi.

Siasa zetu zimejaa midomoni zaidi ya vitendo, huu ndio ukweli, tuna maneno mengi sana lakini vitendo ni sifuri, na tumejaa unafiki sana. Nashangaa Lissu leo anaesema anataka siasa za amani anaonekana tapeli na wale aliowaambia waandamane 2020 wakagoma!. Halafu hao hao wanagoma tena wasiende ikulu kwa mazungumzo wanataka wasuse!

Tatizo la watanzania ni vuvuzela sana, tatizo haliko kwa viongozi wa Chadema huu ndio ukweli. Kuna kundi kubwa la wajuaji wasiojielewa walioko "mstari wa mbele wa mapambano" wanaopotezea wengine muda tu, mitandaoni wanakwambia tuko wote, ukiwahitaji field huwaoni hata mmoja.

Siku zote kama hujui unapoenda, basi popote unapopelekwa we nenda tu, sio unagoma kupelekwa halafu ukiachwa peke yako unabaki umesimama hapo hapo miezi sita.
 
Kamwe huwezi kuwa na siasa za kistarabu kama za marekani na ulaya, kwenye nchi iliyojaa CHAWA!!ambao kwenye chama wanategemea upepo wa mwenyekiti wao(CCM) anasema nini na wao ndio huko huko, wenzetu huko unafiki ni mwiko, kila mwanachama, mtendaji serikal anasimamia sheria za nchi.Hata kama mh.Rais ana weza kuwa na nia nzuri lakini yeye pekee hawezi kuifanya nchi ikawa hivyo!!mfano sakata la makonda linaloendelea sasa hivi na GSM, ni kama hakuna kitu viti, kila mtu hadi jeshi la polisi, linaogopa kusema chochote, kwani hawajui nini msimamo wa mheshimiwa, unaweza ukachangia chochote yakakukuta!!lakini subiria , mheshimiwa alizungumzie kidogo tu, labda achomekee, tu kuwa mbona vyombo vya dola, vimeshindwa kulitolea ufafanuzi, ndipo utawaona CHAWA, sasa, kuanzia ndani ya chama, na vyombo vyote vya ulinzi na usalama utavisikia vimeibuka, na kuanza kutoa matamko !!
Mfano ni kipindi kile cha jiwe, kuhusu makontena ya makonda.
Tatizo la Afrika siasa zake bila unafiki HUTOBOIIII
Ni mwanzo mzuri sasa tunakoelekea siasa za utu.
 
Lisu na Mbowe waingia vitani baada ya join the chain kufutwa
Thubutu!! Kunyea debe ni habari nyingine!! katoka huko kajisalimisha kwa chifu Hangaya huku mkia ukiwa umefyata!!! Lisu naye huko aliko honey moon ilishaisha kitambo!!! Sasa hivi mabeberu wameachana na wakimbizi uchwara kama kina LISU bali wanahudumia wakimbizi wa kizungu toka Ukraine!!! Kwa beberu hapendwi mtu bali maslahi!! na beberu hanaga rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu! Ndiyo maana sasa hivi Rais Maduro wa Venezuela ni hot cake na anapigiwa magoti!!!
 
Waanzilishi wa siasa za uadui hao hao wanaliliaji wa siasa za amani. Aiseee wanasiasa wanafiki
 
Waanzilishi wa siasa za uadui hao hao wanaliliaji wa siasa za amani. Aiseee wanasiasa wanafiki
 
Huu urafiki wa Mbowe na serikali baada ya kufutiwa kesi inabidi tuutazame kwa umakini mkubwa. Kwa sasa nasubiri muda nione muelekeo, lakini sio siri nina mashaka makubwa.
Kama iliwezekana kufanya urafiki kati ya Seikali na Dr. Silaa (Padri ), urafiki kati ya Serikali na Mbowe (mchaga) ni rahisi zaidi!
 
The simple truth is; "siasa za kistaarabu" ndizo tunazoweza watanzania, kwani wangapi kati yetu wanaweza siasa za maandamano? wangapi wakiambiwa wajitokeze kuandamana wanaenda? wengi hubaki nyumbani wakidai waliogopa vitisho vya kina Mambosasa.

Kumbe hapa utaona hata kama wengi wanamtilia shaka Mbowe, lakini ikitokea Mbowe huyo huyo akawaambia waandamane hakuna kati yao atakayejitokeza, wote watajificha nyumbani kwao. Kabla ya kuanza kuwanyooshea kidole viongozi wa Chadema, kwanza tujitazame sisi.

Siasa zetu zimejaa midomoni zaidi ya vitendo, huu ndio ukweli, tuna maneno mengi sana lakini vitendo ni sifuri, na tumejaa unafiki sana. Nashangaa Lissu leo anaesema anataka siasa za amani anaonekana tapeli na wale aliowaambia waandamane 2020 wakagoma!.

Tatizo la watanzania ni vuvuzela sana, tatizo haliko kwa viongozi wa Chadema huu ndio ukweli. Kuna kundi kubwa la wajuaji wasiojielewa walioko "mstari wa mbele wa mapambano" wanaopotezea wengine muda tu, mitandaoni wanakwambia tuko wote, ukiwahitaji field huwaoni hata mmoja.
Siasa za maandamano sio za kistaarabu?? Mkuu unaelewa maana halisi ya bustaarabu?
 
Back
Top Bottom