Kibarua kimeota Nyasi: Waliozoea siasa za vita Mbowe, Lissu, Rais Samia waungana kujenga nchi. Funzo kwa...!

Kibarua kimeota Nyasi: Waliozoea siasa za vita Mbowe, Lissu, Rais Samia waungana kujenga nchi. Funzo kwa...!

Waanzilishi wa siasa za uadui hao hao wanaliliaji wa siasa za amani. Aiseee wanasiasa wanafiki
Hao wanaccm wa siasa za ugoko kwa ugoko wameamua kubadilika. Na sisi ndio kilio na shauku yetu ya toka zamani
 
Huu urafiki wa Mbowe na serikali baada ya kufutiwa kesi inabidi tuutazame kwa umakini mkubwa. Kwa sasa nasubiri muda nione muelekeo, lakini sio siri nina mashaka makubwa.
Tunajua chanzo cha wasi wasi wako ni kutonana na maumivu makubwa awamu ya tano ilisababisha.
 
Mbowe alitoa machozi pale kanisani, Jela sio mchezo. Ni bora wakatulia waachane na suala la katiba na maandamano, then 2025 watapewa viti 10 vya ubunge na mamilioni ya ruzuku kama ilivyokua 2010 hadi 2020.

Wanaozea jela alafu sisi makamanda uchwara hata kuandamana tunaogopa.
 
Kamwe huwezi kuwa na siasa za kistarabu kama za marekani na ulaya, kwenye nchi iliyojaa CHAWA!!ambao kwenye chama wanategemea upepo wa mwenyekiti wao(CCM) anasema nini na wao ndio huko huko, wenzetu huko unafiki ni mwiko, kila mwanachama, mtendaji serikal anasimamia sheria za nchi.Hata kama mh.Rais ana weza kuwa na nia nzuri lakini yeye pekee hawezi kuifanya nchi ikawa hivyo!!mfano sakata la makonda linaloendelea sasa hivi na GSM, ni kama hakuna kitu viti, kila mtu hadi jeshi la polisi, linaogopa kusema chochote, kwani hawajui nini msimamo wa mheshimiwa, unaweza ukachangia chochote yakakukuta!!lakini subiria , mheshimiwa alizungumzie kidogo tu, labda achomekee, tu kuwa mbona vyombo vya dola, vimeshindwa kulitolea ufafanuzi, ndipo utawaona CHAWA, sasa, kuanzia ndani ya chama, na vyombo vyote vya ulinzi na usalama utavisikia vimeibuka, na kuanza kutoa matamko !!
Mfano ni kipindi kile cha jiwe, kuhusu makontena ya makonda.
Tatizo la Afrika siasa zake bila unafiki HUTOBOIIII
CHAWA wapo kila chama kilichopewa usajili pale ofisi ya msajili. Waliokuwa wanaimba nyimbo za hamasa kila siku Mbowe alipokuwa akipelekwa mahakamani, akija kupata cheo kikubwa hawatakuwa CHAWA kweli!?.
 
CHAWA wapo kila chama kilichopewa usajili pale ofisi ya msajili. Waliokuwa wanaimba nyimbo za hamasa kila siku Mbowe alipokuwa akipelekwa mahakamani, akija kupata cheo kikubwa hawatakuwa CHAWA kweli!?.
Ule sio uchwawa. Ule ni upambanaji kwa ajili ya haki.

Chawa ni mlamba viatu kwa ajili ya kujipatia chochote.
 
Mbowe alitoa machozi pale kanisani, Jela sio mchezo. Ni bora wakatulia waachane na suala la katiba na maandamano, then 2025 watapewa viti 10 vya ubunge na mamilioni ya ruzuku kama ilivyokua 2010 hadi 2020.

Wanaozea jela alafu sisi makamanda uchwara hata kuandamana tunaogopa.
Mkuu kama ulizoea siasa za kutukana wapinzani tafuta kazi nyingine.

Iam Sorry to say that lakini ndio mwelekeo wa Mama Samia
 
Katiba mpya ni pigo kwa ccm hawako tayari kwa hilo kwa gharama yoyote

Suala msumari kwa chadema kwa sasa ni katiba mpya sasa ukiangalia hapo usalama na amani vitatoka wapi
 
The simple truth is; "siasa za kistaarabu" ndizo tunazoweza watanzania, kwani wangapi kati yetu wanaweza siasa za maandamano? wangapi wakiambiwa wajitokeze kuandamana wanaenda? wengi hubaki nyumbani wakidai waliogopa vitisho vya kina Mambosasa.

Kumbe hapa utaona hata kama wengi wanamtilia shaka Mbowe, lakini ikitokea Mbowe huyo huyo akawaambia waandamane hakuna kati yao atakayejitokeza, wote watajificha nyumbani kwao. Kabla ya kuanza kuwanyooshea kidole viongozi wa Chadema, kwanza tujitazame sisi.

Siasa zetu zimejaa midomoni zaidi ya vitendo, huu ndio ukweli, tuna maneno mengi sana lakini vitendo ni sifuri, na tumejaa unafiki sana. Nashangaa Lissu leo anaesema anataka siasa za amani anaonekana tapeli na wale aliowaambia waandamane 2020 wakagoma!.

Tatizo la watanzania ni vuvuzela sana, tatizo haliko kwa viongozi wa Chadema huu ndio ukweli. Kuna kundi kubwa la wajuaji wasiojielewa walioko "mstari wa mbele wa mapambano" wanaopotezea wengine muda tu, mitandaoni wanakwambia tuko wote, ukiwahitaji field huwaoni hata mmoja.
Hakina mbowe ndio matapeli wa siasa za nchi hii,nakumbuka kipindi cha dkt Slaa wananchi tulikuwa tunajitokeza kufanya chochote tulichokuwa tukielezwa na viongozi wa Chadema,kila siku tulikuwa tukitoka kwenda kwenye maandamano na mikutano yao, iwe mvua au jua tulikuwa tuko nao, mpaka akina Mbowe wakaota kiburi,Moto wa Chadema ulikuja kuzimwa na Mbowe na Lissu kwa tamaa zao za kipumbavu,eti wanakwenda ikuru kugawana vyeo,wakamleta mtu ambaye walipatia mtaji wa kisiasa kwa kumwita fisadi,gafra huyo aliyeitwa fisadi eti hakapewa nafasi ya kugombea urais,wakamwacha aliyekuwa njenzi wa chama,tangu hapo wenye akili zao tuliliona anguko la Chadema tukatukanwa, Sasahivi Chadema inakwenda kuwa kama tlp ya mrema,eti mnakwenda kufanya siasa za usitarabu 🤣🤣Sema Mbowe ameshindwa siasa, Sasahivi inabidi hawapigie magoti CCM waweze kumfikilia kumpatia angarau viti kama viwili vya ubunge ili maisha yaendelee,kama alivyokuwa akifanya mrema, CCM hauwezi kufanya siasa za usitarabu ukawaweza.Niko tayari kwa matusi
 
kwamba tunaweza siasa za kistaarabu lakini za Maandamano hatuwezi.
Kama hatujitokezi kwenye maandamano maana yake nini ipi kama sio hatuziwezi? na ajabu zaidi, hata hizo unazoita za kistaarabu nazo wapo wasiozitaka.

Kiongozi akifanya hata hizo anatiliwa shaka, sijui kuna aina gani nyingine ya siasa iliyobaki itakayowafaa watu wa sampuli hii.
 
Mkuu kama ulizoea siasa za kutukana wapinzani tafuta kazi nyingine.

Iam Sorry to say that lakini ndio mwelekeo wa Mama Samia
Haha kuna upinzani nchi hii? Acha mzaha mkuu. Sasa agenda ya upinzani ni nini? Katiba mpya? Uhuru wa maoni? Tume huru Au nini?
Sasa mbowe atahubiri nini? Kilichobaki watakua wamamtukana marehemu ili kumfurahisha mama, kujikomba ili kidogo wafikiriwe ruzuku.
 
Hakina mbowe ndio matapeli wa siasa za nchi hii,nakumbuka kipindi cha dkt Slaa wananchi tulikuwa tunajitokeza kufanya chochote tulichokuwa tukielezwa na viongozi wa Chadema,kila siku tulikuwa tukitoka kwenda kwenye maandamano na mikutano yao, iwe mvua au jua tulikuwa tuko nao, mpaka akina Mbowe wakaota kiburi,Moto wa Chadema ulikuja kuzimwa na Mbowe na Lissu kwa tamaa zao za kipumbavu,eti wanakwenda ikuru kugawana vyeo,wakamleta mtu ambaye walipatia mtaji wa kisiasa kwa kumwita fisadi,gafra huyo aliyeitwa fisadi eti hakapewa nafasi ya kugombea urais,wakamwacha aliyekuwa njenzi wa chama,tangu hapo wenye akili zao tuliliona anguko la Chadema tukatukanwa, Sasahivi Chadema inakwenda kuwa kama tlp ya mrema,eti mnakwenda kufanya siasa za usitarabu [emoji1787][emoji1787]Sema Mbowe ameshindwa siasa, Sasahivi inabidi hawapigie magoti CCM waweze kumfikilia kumpatia angarau viti kama viwili vya ubunge ili maisha yaendelee,kama alivyokuwa akifanya mrema, CCM hauwezi kufanya siasa za usitarabu ukawaweza.Niko tayari kwa matusi
Wakati wa Dr. Slaa nakumbuka maandamano pekee yaliyofanyika yalikuwa Arusha ndipo Josephine mke wa Slaa alipoumizwa na polisi.

Nipe mfano wa mikoa mingine iliyowahi kufanya maandamano ya Chadema hapa Tanzania kama unavyodai yalikuwa yakifanyika kila siku.

Mwisho unapodai Lissu na Mbowe waliiuza Chadema licha ya madhila yote waliyopitia wakati wa awamu ya tano (Lissu kupigwa risasi, Mbowe kufungwa na kuharibiwa assets zake) nipe ushahidi wa kuuzwa huko.
 
Laana ya kushangilia kifo cha Magufuli itawatafuna milele Mbowe na Lisu.

Hata mwaka haujaisha saccos yao inakiona cha moto
Na wala hakauna laaana watakayoipata yá kushangilia kifo chá magufuli.

Aliyepata laana ni yeye magufuli aliyekufuru kwa kusema aende akachaguliwe ili aongoze malaika hii ni laana tosha iliyomkumba.
 
Ngoja tuwe na subira. Usijekuta Mbowe anataka kutuuza. Siku zote nimekuwa siwaamini wanasiasa na viongozi wa dini. They are always selfish at some point and manipulators. Lakin kama nia kweli ni siasa za kistaarabu kama wanazofanya wenzetu wa south Africa na Kenya it's okay. Mradi tu Mbowe asiwasaliti watu. Atapata laana mbaya sana. Na itakuwa down fall yake kubwa no matter what he have been doing. Watu wana akili zao, sio mapunda
Kwanini usichukue wewe nafasi ya Mbowe? Uwe kiongozi wa upinzani!!
 
Wakati wa Dr. Slaa nakumbuka maandamano pekee yaliyofanyika yalikuwa Arusha ndipo Josephine mke wa Slaa alipoumizwa na polisi.

Nipe mfano wa mikoa mingine iliyowahi kufanya maandamano ya Chadema hapa Tanzania kama unavyodai yalikuwa yakifanyika kila siku.

Mwisho unapodai Lissu na Mbowe waliiuza Chadema licha ya madhila yote waliyopitia wakati wa awamu ya tano (Lissu kupigwa risasi, Mbowe kufungwa na kuharibiwa assets zake) nipe ushahidi wa kuuzwa huko.
Wakati wa Slaa Chadema walifanya oppression nyingi na zikafaniwa na kuwa na mwitikio wa nyomi la watu, mpaka Chadema ikawa tishio kwa watawala ccm,akina Slaa walikuwa wakito tamko linajadiwa nchi mzima.
 
Back
Top Bottom