Kibarua kimeota Nyasi: Waliozoea siasa za vita Mbowe, Lissu, Rais Samia waungana kujenga nchi. Funzo kwa...!

Kibarua kimeota Nyasi: Waliozoea siasa za vita Mbowe, Lissu, Rais Samia waungana kujenga nchi. Funzo kwa...!

Kama iliwezekana kufanya urafiki kati ya Seikali na Dr. Silaa (Padri ), urafiki kati ya Serikali na Mbowe (mchaga) ni rahisi zaidi!

Hizo siasa za udhaifu wa kikabila, kajadiliane na wanafunzi wenzio wa chuo cha uongozi cha CCM.
 
Samia hawezi siasa za ikulu na siasa za majukwaa ya nyomi na zomea zomea, na hata hivo ni Rais wa kipindi cha mpito 2021-2025 , hawezi na hataweza kuwa mgombea wa ccm hio 2025.

Mgombea mwenye hadhi hio na anaemudu viatu vya ikulu anafahamika na anaendelea vizuri na tuition ya Urais.

Pigeni mayowe vuvuzela ila Samia anaishia 2025, Marais wa Zali la mentali mwisho 2025.

HAHM ije mvua ije jua ije ukame ije mafuriko habari ndio hiyo.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Huu urafiki wa Mbowe na serikali baada ya kufutiwa kesi inabidi tuutazame kwa umakini mkubwa. Kwa sasa nasubiri muda nione muelekeo, lakini sio siri nina mashaka makubwa.
Mku ninaamini Mkutano Mkuu utawajia na majibu mazuri kwani mwelekeo ndo utatokea hapo
 
Sasa nu rasmi tunaelekea siasa za Ulaya na Marekani.

Siasa za maendeleo. Siasa za kistaarabu. Zile siasa za kitafutana kuuana, kutekana, kufungana na kufilisiana mali Mh Rais Samia ameona hazina tija kwa taifa.

Akiongea na Wasikilizaaji ktk Mtandao wa maongezi wa Club House Mh Makamu Mwenyekiti Chadema Tundu Antiphas Lissu ameungi mkono jambo zuri alilofanya Mh Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chama hicho kuwa ni jambo jema.

Ni jambo jema kwa kuwa Rais ameachana na siasa za mitulinga. Tumefikia hatua hii kwa jasho na damu, tumelipa gharama hapa tulipofika " alisema kiongozi huyo.

Aliongeza kuwa Mbinu na mikakati iliyotumika kuishi wakati za awamu ya tano haiwezi kuzaa matunda wakati wa awamu ya sita kwani wakati huo tuliamua kubadilika kwa ajili ya Individual survival.

Jambo hili limeungwa mkono na wadau mbali mbali wa siasa na watanzania woote wakidai kuwa sasa tunaelekea Tanzania Mpya.

Wito kwa vyombo vingine vya serikali viige mfano mwema wa Rais Samia.

Wikendi njema
Kwanini vijana wengi wa uvccm mnaonekana kuumizwa na kitendo cha mbowe kukutana na rais ikulu? Pia kwanini mnaonekana kuchukia pale ambapo viongozi wanaonyesha dalili za kuleta maridhiano katika Taifa?
 
Laana ya kushangilia kifo cha Magufuli itawatafuna milele Mbowe na Lisu.

Hata mwaka haujaisha saccos yao inakiona cha moto
Mke wake mwenyewe alishangilia sembuse hao ulio wataja! Ona mama ananawiri sio mchezo.
Tuache hayo, kinachofanywa sasa hivi kati ya Rais Samia na viongozi wa Chadema ndio kitu sahihi kwa taifa hili na mwanzo mzuri kuelekea maendeleo ya kweli na kuheshimu haki.
Muhimu tuu Samia asiwachekee wahafidhina walioko kwenye chama chake kwani wengi walishaingiwa na roho mchafu wa Magu.
 
The simple truth is; "siasa za kistaarabu" ndizo tunazoweza watanzania, kwani wangapi kati yetu wanaweza siasa za maandamano? wangapi wakiambiwa wajitokeze kuandamana wanaenda? wengi hubaki nyumbani wakidai waliogopa vitisho vya kina Mambosasa.

Kumbe hapa utaona hata kama wengi wanamtilia shaka Mbowe, lakini ikitokea Mbowe huyo huyo akawaambia waandamane hakuna kati yao atakayejitokeza, wote watajificha nyumbani kwao. Kabla ya kuanza kuwanyooshea kidole viongozi wa Chadema, kwanza tujitazame sisi.

Siasa zetu zimejaa midomoni zaidi ya vitendo, huu ndio ukweli, tuna maneno mengi sana lakini vitendo ni sifuri, na tumejaa unafiki sana. Nashangaa Lissu leo anaesema anataka siasa za amani anaonekana tapeli na wale aliowaambia waandamane 2020 wakagoma!. Halafu hao hao wanagoma tena wasiende ikulu kwa mazungumzo wanataka wasuse!

Tatizo la watanzania ni vuvuzela sana, tatizo haliko kwa viongozi wa Chadema huu ndio ukweli. Kuna kundi kubwa la wajuaji wasiojielewa walioko "mstari wa mbele wa mapambano" wanaopotezea wengine muda tu, mitandaoni wanakwambia tuko wote, ukiwahitaji field huwaoni hata mmoja.

Siku zote kama hujui unapoenda, basi popote unapopelekwa we nenda tu, sio unagoma kupelekwa halafu ukiachwa peke yako unabaki umesimama hapo hapo miezi sita.
Ndo maana nakuambia kikubwa ni kuwa na subira
 
Marekani kuna Siasa za Kistaarabu ? Hili neno Gutter Politics sidhani kama lilikuwa coined Tanzania au Africa...

Current Politics and Politicians world over wamekuwa ..., well... Politicians....
 
Sasa nu rasmi tunaelekea siasa za Ulaya na Marekani.

Siasa za maendeleo. Siasa za kistaarabu. Zile siasa za kitafutana kuuana, kutekana, kufungana na kufilisiana mali Mh Rais Samia ameona hazina tija kwa taifa.

Akiongea na Wasikilizaaji ktk Mtandao wa maongezi wa Club House Mh Makamu Mwenyekiti Chadema Tundu Antiphas Lissu ameungi mkono jambo zuri alilofanya Mh Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chama hicho kuwa ni jambo jema.

Ni jambo jema kwa kuwa Rais ameachana na siasa za mitulinga. Tumefikia hatua hii kwa jasho na damu, tumelipa gharama hapa tulipofika " alisema kiongozi huyo.

Aliongeza kuwa Mbinu na mikakati iliyotumika kuishi wakati za awamu ya tano haiwezi kuzaa matunda wakati wa awamu ya sita kwani wakati huo tuliamua kubadilika kwa ajili ya Individual survival.

Jambo hili limeungwa mkono na wadau mbali mbali wa siasa na watanzania woote wakidai kuwa sasa tunaelekea Tanzania Mpya.

Wito kwa vyombo vingine vya serikali viige mfano mwema wa Rais Samia.

Wikendi njema
Una Mihemuko kama shivasi
 
Kamwe huwezi kuwa na siasa za kistarabu kama za marekani na ulaya, kwenye nchi iliyojaa CHAWA!!ambao kwenye chama wanategemea upepo wa mwenyekiti wao(CCM) anasema nini na wao ndio huko huko, wenzetu huko unafiki ni mwiko, kila mwanachama, mtendaji serikal anasimamia sheria za nchi.

Hata kama mh.Rais ana weza kuwa na nia nzuri lakini yeye pekee hawezi kuifanya nchi ikawa hivyo!!mfano sakata la makonda linaloendelea sasa hivi na GSM, ni kama hakuna kitu viti, kila mtu hadi jeshi la polisi, linaogopa kusema chochote, kwani hawajui nini msimamo wa mheshimiwa, unaweza ukachangia chochote yakakukuta!!lakini subiria , mheshimiwa alizungumzie kidogo tu, labda achomekee, tu kuwa mbona vyombo vya dola, vimeshindwa kulitolea ufafanuzi, ndipo utawaona CHAWA, sasa, kuanzia ndani ya chama, na vyombo vyote vya ulinzi na usalama utavisikia vimeibuka, na kuanza kutoa matamko !!

Mfano ni kipindi kile cha jiwe, kuhusu makontena ya makonda.
Tatizo la Afrika siasa zake bila unafiki HUTOBOIIII
Tuna hilo tatizo chief, kila kitu wanasubiri Rais aseme, ni wakati sasa wa kutoa hawa watu wenye mavitambi kwenye mamlaka, ni wapuuzi sana! Mimi ningekuwa hata OCD tu Makonda ningekuwa nimeshamnyoosha, ila hii mijinga inakaa eti inasubiri kauli ya Rais!!! samia ana shida sana na hawa wasaidizi wake vilaza wanaojali mitumbo yao
 
Hakuna urafiki wa Simba na Swala! Subiri uchaguzi wa 2025 harafu kitakachotokea hapo utatuambia.
Hakuna Urafiki wa CCM na Vyama vya Upinzani.
 
Mkuu unadhani nina tatizo kama siasa hizo zitakuwa za win win situation, tatizo langu ni pale hizo siasa za maridhiano zitakapokuwa kaburi letu. Wakati Lowassa anakuja cdm maelezo yalikuwa ni mengi mazuri, lakini nilibaki na msimamo wangu kuwa yule mzee sio. Leo hii Lowassa yuko wapi? Nina mashaka makubwa na haya makubaliano ya sasa, na hili lazima nifuate dhamira yangu kuliko anachoongea kiongozi yoyote. Natoa muda lakini mashaka yangu ni dhahiri.
Amini mkuu at least hii miaka ya mama angalau tunaweza kufanya siasa za kistaarabu kwakuwa tupo chini ya uangalizi wa wenye fedha .

Haikuwa rahisi kwa mh Mbowe kufutiwa haya mashitaka.

Lazima kuna msukumo fulani nyuma ya pazia na kwa kuzingatia hilo amini kwa miaka atakayokuwepo madarakani kutakuwa na siasa za kistaarabu hata kama ni kwa kuviziana.
 
Kwisha Lissu, Ameuza chama ili apate kurudi kuishi tanzania, ili mbowe atoke jela miezi 8 ilitosha ku-sarender, sioni tofauti ya Chadema na TLP, Tanzania tunahitaji chama kipya cha upinzani kitakachokuwa na mtazamo wa upinzani lakini matumaini kwa wananchi
Kahangaikeni na cuf yenu iliyo mezwa na Zitto
 
Sina tatizo na maelezo yako mazuri, shaka langu ni utekelezaji wa haya maelezo yako mazuri kwa suala la win win situation. Ni dhahiri nina mashaka na hiki kinachoendelea sasa, kutokana na uzoefu wangu wa makubaliano ya aina hii. Kwakuwa wameshakutana na rais na wanatuaminisha kuna nia njema, ngoja nisubiri matokeo. Lakini shaka yangu ni bayana kwani naona kuna kuingizana mjini, kwenye hili niko tayari kubaki mwenyewe.
Kwa ufupi mazingira tunayo enda kuyaishi ni sawa na jirani zetu wa Kenya.
 
Ebu tuwe wakweli kidogo......

Mbona ile
"Join the Chain"
imeondolewa mitandaoni ghafla baada ya ujio wa mwenyekiti Mbowe?
 
Thubutu!! Kunyea debe ni habari nyingine!! katoka huko kajisalimisha kwa chifu Hangaya huku mkia ukiwa umefyata!!! Lisu naye huko aliko honey moon ilishaisha kitambo!!! Sasa hivi mabeberu wameachana na wakimbizi uchwara kama kina LISU bali wanahudumia wakimbizi wa kizungu toka Ukraine!!! Kwa beberu hapendwi mtu bali maslahi!! na beberu hanaga rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu! Ndiyo maana sasa hivi Rais Maduro wa Venezuela ni hot cake na anapigiwa magoti!!!
Umelenga "Bull" mkuu!
 
Sasa nu rasmi tunaelekea siasa za Ulaya na Marekani.

Siasa za maendeleo. Siasa za kistaarabu. Zile siasa za kitafutana kuuana, kutekana, kufungana na kufilisiana mali Mh Rais Samia ameona hazina tija kwa taifa.

Akiongea na Wasikilizaaji ktk Mtandao wa maongezi wa Club House Mh Makamu Mwenyekiti Chadema Tundu Antiphas Lissu ameungi mkono jambo zuri alilofanya Mh Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chama hicho kuwa ni jambo jema.

Ni jambo jema kwa kuwa Rais ameachana na siasa za mitulinga. Tumefikia hatua hii kwa jasho na damu, tumelipa gharama hapa tulipofika " alisema kiongozi huyo.

Aliongeza kuwa Mbinu na mikakati iliyotumika kuishi wakati za awamu ya tano haiwezi kuzaa matunda wakati wa awamu ya sita kwani wakati huo tuliamua kubadilika kwa ajili ya Individual survival.

Jambo hili limeungwa mkono na wadau mbali mbali wa siasa na watanzania woote wakidai kuwa sasa tunaelekea Tanzania Mpya.

Wito kwa vyombo vingine vya serikali viige mfano mwema wa Rais Samia.

Wikendi njema

Mwenye kuchagua mitulinga au ustaarabu ni Samia. Si Chadema wala si CCM.

Si CCM, kwani nani ana ubavu wa kauli au msimamo upi huko zaidi ya Samia?

Si Chadema kwani Samia akisisitiza haki zote zikiwemo za hao Chadema kuheshimiwa nani atakuwa na ugomvi na hilo?

Samia ajue akiminya haki za watu ni hakika kuwa atakayokuwa akiyapata ndiyo majibu yake.
 
Back
Top Bottom