Kibarua kimeota Nyasi: Waliozoea siasa za vita Mbowe, Lissu, Rais Samia waungana kujenga nchi. Funzo kwa...!

Kibarua kimeota Nyasi: Waliozoea siasa za vita Mbowe, Lissu, Rais Samia waungana kujenga nchi. Funzo kwa...!

Mwenye kuchagua mitulinga au ustaarabu ni Samia. Si Chadema wala si CCM.

Si CCM, kwani nani ana ubavu wa kauli au msimamo upi huko zaidi ya Samia?

Si Chadema kwani Samia akisisitiza haki zote zikiwemo za hao Chadema kuheshimiwa nani atakuwa na ugomvi na hilo?

Samia ajue akiminya haki za watu ni hakika kuwa atakayokuwa akiyapata ndiyo majibu yake.
Yeye ndiye anabeba dhamana ya Taifa. Lakini pia wadau wakubwa wenye heshima zao kama TL na FAM wakishirikiana matokeo ni makubwa
 
Magu hakuwa mwanasiasa bali mlevi wa madaraka. Hakuna mwanasiasa mstaarabu asiyetaka matusi anaweza kuwaambia wananchi wake wabaki na mavi yao nyumbani. Zungumzia mtu mwingine sio yule mshenzi.
Duuh
 
Kwani wewe chawa Lengo lako hasa maishani ni Lipi. Unadhani ulaya na marekani wanasiasa hawaviziani kuangushana. That’s normal. Sisi watu wa kawaida ndo wapumbavu tunakaa kutunga Hypotheses kuridhisha yaliyomo vichwani mwetu kama ushabiki wa Simba na Yanga. Weakness yenu kubwa Ni kufanya haya mawazo sehemu yako ya maisha katika furaha na huzuni. That’s why ukiona dalili ya kukaa pamoja tu kwako inakuwa kama mkeo kuenda Movie na x Wake na kulala huko.
Sema wewe mpumbavu usiite watu wa JF wapumbavu kama wewe.
 
Wale waliopata vyeo baada ya kutoka Chadema na kuanza kuitukana na kukashifu Kama Waitara, Mollel, Gekul, na mbunge wa Shinyanga mjini nk. wataanza na Nini tena?
Kule CCM Kuna Kibajaji,Musukuma, Mwigulu, nk Kuna policcm ya Zero na Kingai, Kuna watendaji Kama Msajili wa vyama na Kaijage wa Tume ya uchaguzi wote sifa yao ni vita dhidi ya Chadema hawata furahishwa na maridhiano yoyote
Hawa woote kazi hawana. Teuzi wataziona kwa macho tu kwenye Itv.
 
Sasa nu rasmi tunaelekea siasa za Ulaya na Marekani.

Siasa za maendeleo. Siasa za kistaarabu. Zile siasa za kitafutana kuuana, kutekana, kufungana na kufilisiana mali Mh Rais Samia ameona hazina tija kwa taifa.

Akiongea na Wasikilizaaji ktk Mtandao wa maongezi wa Club House Mh Makamu Mwenyekiti Chadema Tundu Antiphas Lissu ameungi mkono jambo zuri alilofanya Mh Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chama hicho kuwa ni jambo jema.

Ni jambo jema kwa kuwa Rais ameachana na siasa za mitulinga. Tumefikia hatua hii kwa jasho na damu, tumelipa gharama hapa tulipofika " alisema kiongozi huyo.

Aliongeza kuwa Mbinu na mikakati iliyotumika kuishi wakati za awamu ya tano haiwezi kuzaa matunda wakati wa awamu ya sita kwani wakati huo tuliamua kubadilika kwa ajili ya Individual survival.

Jambo hili limeungwa mkono na wadau mbali mbali wa siasa na watanzania woote wakidai kuwa sasa tunaelekea Tanzania Mpya.

Wito kwa vyombo vingine vya serikali viige mfano mwema wa Rais Samia.

Wikendi njema
Unakumbuka maadamano yenu ya wakati kwa bahati mbaya aliuawa Akwilina?
 
Wale waliopata vyeo baada ya kutoka Chadema na kuanza kuitukana na kukashifu Kama Waitara, Mollel, Gekul, na mbunge wa Shinyanga mjini nk. wataanza na Nini tena?
Kule CCM Kuna Kibajaji,Musukuma, Mwigulu, nk Kuna policcm ya Zero na Kingai, Kuna watendaji Kama Msajili wa vyama na Kaijage wa Tume ya uchaguzi wote sifa yao ni vita dhidi ya Chadema hawata furahishwa na maridhiano yoyote
Tumetoka mbali sana eti Kaijage naye ni jaji🤣🤣
 
Ngoja tuwe na subira. Usijekuta Mbowe anataka kutuuza. Siku zote nimekuwa siwaamini wanasiasa na viongozi wa dini. They are always selfish at some point and manipulators.

Lakin kama nia kweli ni siasa za kistaarabu kama wanazofanya wenzetu wa south Africa na Kenya it's okay. Mradi tu Mbowe asiwasaliti watu. Atapata laana mbaya sana. Na itakuwa down fall yake kubwa no matter what he have been doing. Watu wana akili zao, sio mapunda
Yaani Mbowe kusota kote ndani na unyanyasaji wote aliofanyiwa,aje kywauza watu wake sasahivi???
Mbona ushindi upo karibu!
Sidhani kama hata anafikiria hilo.
 
Huu urafiki wa Mbowe na serikali baada ya kufutiwa kesi inabidi tuutazame kwa umakini mkubwa. Kwa sasa nasubiri muda nione muelekeo, lakini sio siri nina mashaka makubwa.
Mbowe hajawa rafiki wa serikali na wala hawezi kuwa rafiki wa serikali.
 
Unakumbuka maadamano yenu ya wakati wa Akwilina?
Baada ya watu wa vita kuzuia mawakala wa chama chetu kuapa na kupeww barua za utambulisho. DED kajukumuguru nadhani walishamtumbua awamu hii.
 
Yaani Mbowe kusota kote ndani na unyanyasaji wote aliofanyiwa,aje kywauza watu wake sasahivi???
Mbona ushindi upo karibu!
Sidhani kama hata anafikiria hilo.
Wale mnaoungulia rohoni poleni. Sisi wanachadema halisi tunasonga mbele. Mbowe tunamuunga mkono 100%
 
Baada ya watu wa vita kuzuia mawakala wa chama chetu kuapa na kupeww barua za utambulisho. DED kajukumuguru nadhani walishamtumbua awamu hii.
safari hii, jiepushe maana mtiti huo hutachomoka
 
Nimekuelewa sana ndugu yangu lkn kwa politics ground tuliyo nayo kwa sasa naamini nivizuri tukaanza na hapa tulipo anzia.

Kumbuka hata mbuyu ulianza kama mchicha brother.

Siasa za kufulisiana,
Siasa za kufunguliana kesi za ugaidi,
Siasa za chuki na kuwaumiza viongozi wa cdm nadhani sasa tuziepuke .

Kumbuka hata viongozi wetu nao ni binadamu kama mimi na wewe wanahisi machungu wanayo tendewa.
Mwanzo ni mzuri. Tuhukumu kwa mengine
 
Nimeoina vizuri, ila cdm inapaswa kuangalia kwenye matokeo ya muda mrefu. Ndio maana nimefanya rejea kwenye ujio wa Lowassa ambapo faida ilikuwa ni ya muda mfupi. Cdm ni taasisi kubwa inapaswa kuwa na vision ya 💯 yrs toka sasa, na sio muda mfupi ambao huyu mama atakaa madarakani kaka yangu.
Vision inakuwa divided kwenye misions
 
Jidanganye, unaambiwa "once a whore always a whore", unadhani anaongoza nchi peke yake?
Urais ni Taasisi na Taasis imeshaamua.

Mkuu tafuta kazi nyingine ile ya kutukana wapinzani hakuna tena
 
Mkuu mazingira ya Kenya yaliletwa na Wakenya walio upande wa Raila, kwani Uhuru aliogopa shari toka kwa wafuasi wake. Kinachofanyika sasa ni makubaliano yasiyo wazi ya mama Samia na viongozi kadhaa wa cdm. Na sio makubaliano ya ccm na cdm. Ifahamike ccm bara ndio wenye nguvu, huyo mama hana ushawishi bali analindwa na cheo cha urais alichokipata kwa bahati mbaya. Hivyo anachofanya ni kuwahadaa wapinzani ili atawale bila kelele, kisha makubaliano hayo yatumike kama udhaifu wa cdm. Rejea ule utapeli wa Magufuli muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu, kati yake na Mbatia na Lipumba na alichokifanya kwenye uchaguzi.

Naona wazi cdm wakiingizwa mkenge kwa mtazamo wa Mbowe kutokana na alichoongea na mama Samia, lakini hapo kuna mazingira ya Mbowe kufaidika binafsi, na kidogo sana cdm kama taasisi. Bado nina kumbukumbu mbaya ya ujio wa Lowassa ndani ya cdm, na alichokuwa anaoongea Mbowe kwenye utetezi wake wa kumpokea Lowassa. Matokeo ya kumpokea Lowassa ni kuharibu haiba ya cdm,na kibaya zaidi aliishia kupandikiza siasa za kikondoo. Leo hii Lowassa hayupo karudi ccm, na cdm imebaki na siasa za uwoga. Mnao amini siasa za maridhiano ya maneno matupu sitaki kuwazuia, lakini ukweli ccm hawawezi kukubali maridhiano ya mezani bila mivutano. Muda utasema kwenye hii shaka yangu.
All precautions considered.

Tindo unadhani wewe u a maumivu kuliko Freeman?
 
Back
Top Bottom