Kiswahili kimekuwa kigumu kiasi hiki?
Maslahi ya watu kwa sababu ya njaa za matumbo yao na familia zao. Vipi hayo yanaweza linganishwa na maslahi haya:
Mwananchi wa kawaida anayejielewa, anayekataa kuendelea kubambikiziwa kesi, kuendelea kudhulumiwa, kuendelea kubebeshwa mizigo ya kodi za wengine nk.
Au hata yule anayetaka mihimili ya utawala iliyo na uhuru kamili, anayetaka usawa, anayetaka uwajibikaji, anayetaka mawazo yake kusikilizwa nk.
Seriously, haikuingii akilini kuwa kwanini hapo pana tofauti?
Au ni ile mambo ya kujitia hamnazo?