Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Wananchi wengi wanawashangaa sana hawa wanaolilia katiba mpya, wakiwa mimacho yamewatoka, mapovu yakiwatoka, mishipa ya shingo imetuna, wameva nguo nyekundu kuashiria kumwaga damu za watu hadi waipate hiyo katiba wanayoitaka. Dhumuni lao nini hasa mpaka wanataka kumwaga damu.
Mbona hii katiba iliyopo tumekuwa nayo miaka mingi tu na nchi ilikuwa imetulia hadi kuwa kinara cha amani Afrika. Mbona katiba hii tuliyo nayo tumekuwa tukiifanyia updates na upgrades ili kwenda na wakati. Mbona katiba hii tuliyonayo tuliifanyia upgrade kubwa mwaka 1984 hadi kuingiza haki zote za binadamu zilizoazimiwa na Umoja wa Mataifa (UN).
Update moja wapo ni ya mwaka 1992 ambayo ilianzisha vyama vingi vya siasa, kitu kilichowezesha hadi chadema ikazaliwa na akina Mbowe kupatikana. Mbona mataifa makubwa duniani kama USA na Germany katiba zao ni zile zile za tangia ujima ila huzifanyia updates na upgrades tu ili kwenda na wakati kama ambavyo sisi tunavyofanya. Haijatokea mataifa haya eti yakadai katiba mpya na kufuta iliyokuwapo.
Ni kitu gani hasa kimetokea hii miaka ya karibuni kilicholifanya kundi hili la wanasiasa hadi kufikia kutaka kumwaga damu za Watanzania? Kwa mtu ye yote mwenye akili timamu jibu lake liko wazi. Wana masilahi binafsi ya kushika Dola. Kwa katiba hii hii tuliyonayo tangia kuanzisha vyama vingi vya siasa, vyama vya upinzani vimekuwa vikiimarika kwa kasi ya kuridhisha na kutoa tumaini ya kuweza kushika dola jinsi miaka ilivyokuwa ikienda.
Uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, Lyatonga Mrema wa upinzani alimtoa kamasi Benjamini Mkapa wa chama tawala. Ilibidi Nyerere atoke ustafuni na kuzunguka nchi nzima kuokoa jahazi. Kama Nyerere hangalifanya hivyo, Mrema alikuwa anachukua Dola kwa katiba hii hii tuliyonayo. Hivyo hivyo uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 Dr Willbrad Silaa wa upinzani alimtoa jasho Jakaya wa chama tawala na hatasahau. Mwaka 2015 ilikuwa balaa zaidi. JPM wa chama tawala alipita kwa taabu dhidi ya Edward wa upinani.
Tatizo chama kilichokuwa kikuu cha upinzani kati ya mwaka 2015 hadi 2020 kikajivuruga chenyewe kwa sababu ya ubinafsi wa mwenyekiti wake. Watu muhimu kwenye chama hicho wakakikimbia hadi ilipofika uchaguzi mkuu wa 2020 kikafa kifo cha mende. Kinasingizia Tume ya Uchaguzi kwamba muundo wake hauko vizuri. Hili ni jambo dogo sana halihitaji katiba mpya. Sheria husika ya NEC inaweza kurekebishwa. Returning Officers huko wilayani badala ya kuwa wakurugenzi wa halimashauri wanaweza wakawa District Magistrates kama ilivyo huko India. Ni kubadilisha sheria tu.