Kiengereza kitumike shule za umma tokea msingi mpaka chuo

Kiengereza kitumike shule za umma tokea msingi mpaka chuo

Ego is the Enemy

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
8,201
Reaction score
16,246
Habari zenu.

Nimekaa hapa nimewaza Ni kwa Nini elimu yetu kingereza kisitumike kuanzia chekechea mpaka elimu ya juu.

Shida Ni Nini yaani Kuna watu wamekaa huko wakaona kuwa maarifa mengi yamevumbuliwa na waswahili ama Ni Nini.

Maarifa mengi mno yapo kwa lugha ya KIENGEREZA.

Mtoto akifika sekondari anaanza KIENGEREZA sio kumtesa hapa Ni Nini Mana anabakia kuumia kwa kukariri. Nawaza Hawa jamaa Wana shule zao hivyo wakiweka English watakosa watoto huko Ni mawazo yangu.

Yaani wakiwa huko kwa Sera na mipango ya elimu wao wanawaza Nini juu ya hili kuwa Kuna changamoto gani mtoto ataipata.

Wengine nadhani mtaongezea na kutoa maoni yenu.

Mie ninavyojua Kama mtoto anajua English anaweza anajifunza na kusoma kitu chochote mtandaoni akajifunza na akakimasta kabisa.

Afrika afrika afrika afrika Tanzania Tanzania Tanzania
 
Screenshot_20231106-105810.png
 
Mwalimu J.K. Nyerere:

^Wapo watu wasiosadiki kwamba jambo lolote la maana linaweza kuandikwa kwa Kiswahili. Lakini si kweli kusema kwamba Kiswahili hakiwezi kutumika katika uandishi wa vitabu mbalimbali vinavyohusu taaluma.^

^Ni wajibu wetu sote kujaribu kadiri tuwezavyo kuikuza lugha yetu katika kuandika, kusema na katika kuwaza.^

^Nchi za Afrika Mashariki zina lugha moja ya Kiswahili yenye nguvu ya kuiunganisha Afrika na kuunda Shirikisho la nchi za Afrika.^
 
Tatizo Bongo shule nyingi elimu kwa ujumla ni duni au substandard -- lugha ni changamoto mojawapo tu.

Kiingereza ni muhimu sana, lakini tatizo siyo tu la lugha. Hali ni mbaya kuliko inavyoonekana.

Congratulations to some government schools and most of the private schools, ingawa na zenyewe, nyingi, elimu bado ni duni sana.
 
Mataifa yasiyotumia kingereza kama lugha ya kufundishia na yamefanikiwa kielimu yamewezaje????

Kingereza sio suruhisho la elimu bora, ile ni lugha tu.

Kwetu hii lugha ni changamoto, yani tunajifunza kitu tusichokijua (physics) kwa lugha tusiyoijua ( Yani vyote viwili hatuvijui) unategemea tuwe na elimu bora.

Tutumie lugha tunayoijua tujifunze hayo tusiyoyajua.
 
Nchi ngapi za Afrika zinatumia kingereza lakini bado zipo hoi ?

Afu kule Asia nchi kibao hazitumii kingereza lakini zipo mbali, hata uko ulaya nchi nyingi tu hazitumii kingereza na bado zipo mbali.

Uko sahihi kabisa,hata mimi natamani tuchague lugha moja tu ya kufundishia kuanzia awali hadi chuo kikuu,kuliko huu mchanganyo wa sasa.
 
Habari zenu.

Nimekaa hapa nimewaza Ni kwa Nini elimu yetu kingereza kisitumike kuanzia chekechea mpaka elimu ya juu.

Shida Ni Nini yaani Kuna watu wamekaa huko wakaona kuwa maarifa mengi yamevumbuliwa na waswahili ama Ni Nini.

Maarifa mengi mno yapo kwa lugha ya KIENGEREZA.

Mtoto akifika sekondari anaanza KIENGEREZA sio kumtesa hapa Ni Nini Mana anabakia kuumia kwa kukariri. Nawaza Hawa jamaa Wana shule zao hivyo wakiweka English watakosa watoto huko Ni mawazo yangu.

Yaani wakiwa huko kwa Sera na mipango ya elimu wao wanawaza Nini juu ya hili kuwa Kuna changamoto gani mtoto ataipata.

Wengine nadhani mtaongezea na kutoa maoni yenu.

Mie ninavyojua Kama mtoto anajua English anaweza anajifunza na kusoma kitu chochote mtandaoni akajifunza na akakimasta kabisa.

Afrika afrika afrika afrika Tanzania Tanzania Tanzania
Ichaguliwe lugha moja tu ..
Ingawa kidunia English inafaa zaidi maana itasaidia watu wetu
 
Ukikijua kiingereza Ni rahisi mno kujifunza maarifa mengine Mana yanatolewa kwa English. Hatuna watalaamu wanaoweza ama waliofanya gunduzi wakaandika kwa lugha zetu. Hawa wanachokifanya Ni kubadilisha lugha Cha mwingine. Ukijua English uwanja Ni Moana mno wa Ajira ,kibarua popote unafanya kazi,hata waweza fungua geti la airport Amsterdam ingawa wanatumia Dutch language
 
Engine ya gari inavyofanya kazi wanaoelezea kitalaamu zaidi na wanaongea English,Sasa mtt akaishia la Saba ama la 11 anataka kujifunza ujuzi wa namna ya engine ya gari ulivyo anaweza akala lecture huko YouTube akapata ufahamu zaidi akichanganya aliyoelezewa aanakuwa very deep in know why/how
 
Hili naunga mkono 100% .

Cha kujiuluza, hao walimu wa kuwafundusha Kingereza masomo yote , wako wapi?

Labda ndiyi twebde hivyohuvyi bora lenders au na Walimu nao wainguzwe darasani kula wiki siju mija kufundishwa Kingereza jwa somo wanalo fundisha.

Mpangi mwengune nzuri ni u OK e aliokwisha uanzisha Kikwete, Mkonga utumije kufikisha mawasiliano shuke zote, wawe wanasomeshwa kwenye screen jutoka kwa Mwalim mmoja competent kwenye fani yake, walimu mashuleb I n j azu yai itakuwa ni supervision na facilitation.

...naunga mjono hoja
 
Back
Top Bottom