Kisaikolojia, ni rahisi mtoto mdogo kujifunza lugha yoyote.
Watu wanazidharau hizi English medium za bei nafuu, lakini watoto wanafahamu Kiingereza cha Kitanzania ambacho kinawasaidia wakifika sekondari.
Kamwe, Kiingereza hakiwezi kufafana dunia nzima kwa sababu mbalimbali mojawapo ni kuathiriwa na lugha za wazawa ndio maana kuna East African English, lakini mimi nasema kuna Tanzanian English.
Pamoja na utofauti huu, lakini wanaozungumza Kiingereza kutoka nchi tofauti tofauti wataelewana hivyo hivyo kibishi tofauti na yule ambaye hajui kabisa.