Kiengereza kitumike shule za umma tokea msingi mpaka chuo

Korea Lugha yao wameanza nayo 1444, japan wana lugha yao toka zamani sanaaa, China vivyo hivyo,
Sisi kiswahili kimeingia mwaka 1950+
Huko ndani ndani hadi leo watu hawajui kiswahili vizuri, 😂 huyo mtu bado unampa kazi ya kujifunza English then Physics iliyo katika English, utakuta tu mtu hajui
Uko sahihi kabisa,hata mimi natamani tuchague lugha moja tu ya kufundishia kuanzia awali hadi chuo kikuu,kuliko huu mchanganyo wa sasa.
 
Ongezea pia kwamba walimu wengi wanaofundisha nao hawajui wanachofundisha.

Shule nyingi za serikali, failures ndio walimu wa wanafunzi. Sasa hapo tutegemee nini?

Hapo pia tusiwasahau waongoza wizara, maafisa elimu, waratibu, nk. Hali ni tete kwa kweli.

Elimu ni muhimu sana, lakini serikali inaweka kipaumbele (tena nacho kidogo tu) kwenye majengo, wanasahau kuboresha nyenzo, hali na taaluma ya walimu na wadau wengine wa elimu.
 
 
Kumbe sio shida lugha, shida mnashindwa kupakia videos ambazo hazipo kwenye lugha yenu, ndio muone mlivyo wazito sasa, mbona kwenye lugha zingine wanazipata.

Kama shida ni lugha hao waliosoma English medium mbona wapo mtaani humu, kama taifa wamelisaidia nini ?

Nchi ngapi hapa Africa wanatumia English kama official language na wamefikia wapi ? [emoji849]
 
Watuambie Malawi hawa hapo tu.
 
Kiswahili tu tujitenge na dunia,
English tu tuue lugha yetu,
Kiswahili then English (kama ilivyo sasa)cha moto tunakiona.
 
Hapana haiwezekani, nchi inahitaji wapagazi kwenye bandari zao, sasa wote tukifunga tai na suti nani atajulikana kuwa si mtoto wa waziri, shukuru na ujivunie lugha yako.
 
Napendekeza lugha hii ndiyo itumike nchini kote na huyu apate nishani kwa kubuni lugha hii.
 
Wazo zuri, ila je walimu hao wa kufundisha kimombo tangu shule ya msingi wapo ?! Walimu wenyewe wa msingi ze... ze... ok... nyingi wazo lako litatimia ?
 
Mbona zipo shule za kiingereza za Serikali nyingi tu ? Mfano kwa Ilala pekeyake kuna shule 9 za kiingereza
 
Nchi ngapi za Afrika zinatumia kingereza lakini bado zipo hoi ?

Afu kule Asia nchi kibao hazitumii kingereza lakini zipo mbali, hata uko ulaya nchi nyingi tu hazitumii kingereza na bado zipo mbali.
Wajuaji Kama nyinyi ndo mmeifikisha hii nchi hapa

Wachina wahindi mpaka leo wanajitahid wakijue kiingereza pamoja na kwamba wameendelea kiiteknolojia,sembuse tz kajamba nani hatuña teknolojia yeyote eti tunajifanya kiingereza sio lazima
 
Nchi ngapi za Afrika zinatumia kingereza lakini bado zipo hoi ?

Afu kule Asia nchi kibao hazitumii kingereza lakini zipo mbali, hata uko ulaya nchi nyingi tu hazitumii kingereza na bado zipo mbali.
Nchi Gani Asia haitumiki kiingereza

Sent from my Pixel 5 using JamiiForums mobile app
 
Wajuaji Kama nyinyi ndo mmeifikisha hii nchi hapa

Wachina wahindi mpaka leo wanajitahid wakijue kiingereza pamoja na kwamba wameendelea kiiteknolojia,sembuse tz kajamba nani hatuña teknolojia yeyote eti tunajifanya kiingereza sio lazima
Mimi nimesema wapi tusijue kingereza ?

Mimi point yangu ni kwenye masomo yawe ya kiswahili na English libakie kama somo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…