Kiengereza kitumike shule za umma tokea msingi mpaka chuo

Suluhu ni moja tu,kitumike kiswahili mpaka elimu za juu
 
Nchi ngapi za Afrika zinatumia kingereza lakini bado zipo hoi ?

Afu kule Asia nchi kibao hazitumii kingereza lakini zipo mbali, hata uko ulaya nchi nyingi tu hazitumii kingereza na bado zipo mbali.
Ungekua karibu ungekunywa bia nyingi
 
Mbona waundaji wa hizo engine wanaandika na kutoa maarifa kijapan,yameendaje kwenye kiingereza
Usizungimze bila kufikiri
Kiswahili kinaweza kutumika katika elimu kuanzia awali mpaka juu kabisa na kikawa na matokeo chanya sana.
Haitokuwa na maana kama tuna lugha ya Taifa kiswahili na kinatumiwa na sehemu kubwa ya east and central africa halafu hakitumiki kwenye elimu,ni jambo la ajabu
Narudia tena ni jambo la ajabu sana
 
Mjomba wenye wizara yao hawataruhusu hili kutokea, maana haohao ndo wenye shule za private zinazofanya biashara kwa mtaji wa kutumia Lugha ya kizungu😜😜
 
Basi tuue kabisa shule zote hata private watumie kiswahili Mana Ni Cha maana mno. Sijakataa ,unajua wachina wanavyohangaika na English ama hao wajapani. Usipojua English kimapana Ni kuwa umejifungia kwa set A but kwa English Ni universal language
 
NYERERE mfumo wake ulifeeli ilitakiwa tuwe Kama China russiia ama Malaysia Ila huku Sera yake ilifeli,pia NYERERE sio Mungu elewa. Ni binadamu wa kawaida tu
 
Nyie huko kingereza cha nini?

Miziki ya zuchu mboso inawatosha

Nyie huko endeleeni kukata mauno na kuzagamuana tu

Ova
 
Basi tuue kabisa shule zote hata private watumie kiswahili Mana Ni Cha maana mno. Sijakataa ,unajua wachina wanavyohangaika na English ama hao wajapani. Usipojua English kimapana Ni kuwa umejifungia kwa set A but kwa English Ni universal language
Wachina hawahangaiki kujifunza kiingereza tu, mchina anajifunza lugha ya sehemu anayotarget kwenda kama ni ujeruman atajifunza lugha yao kama ni Italy au ufaransa ni hivyo hivyo

Kwa nchi yetu tunahitaji sana kuwa na ujuzi wa lugha zote mbili
 

TAFAKARI
Lugha sio Kusoma Kuandika na Kuongea peke yake.

Wasomi na Wanataaluma wa Lugha wanasema

"Language is the expression of Ideas by means of speech-sounds combined into word. Words are combine into sentences, this combination answering to that of Ideas into thoughts"

Kazi za Lugha ni pamoja na mawasiliano,utambulisho wa Jamii, watu na tamaduni zao, mawazo au fikra na hisia.

Watanzania, wanatokea Jamii ya Mwafrika. Jamii hii ina Utambulisho, (expresses its Identity) wa kipekee.

Hivyo basi, Lugha ni mfumo changamano unaojumuisha aina mbalimbali za mawasiliano zaidi ya kusoma, kuandika na kuzungumza.

Tafakari :Jaribu kutafsiri kifungu hicho juu(in bold and italics) kwa kiswahili au lugha nyingine yeyote na urudi kwa Kiingereza. If you get lost in translation, then you're lost in expression and therefore, your identity!
 
Uko sahihi. Tulikosea sana tulipoamua kutumia kiswahili. Kwa Tanzania kiingereza siyo lugha tu, ila ni factor inayoweza kutumika kupima usomi na utaalam wa mtu. Nakuapia kama bunge letu lingekuwa linaendesha kila kitu kwa kiingereza basi watu wa hovyo kama kina Musukuma au Kibajaji wasingekuwepo. Pia kama ume-note Tanzania sasa hivi kila sekta ina watu wanaojigamba kuwa ni wataalam kumbe ni vilaza. Hebu fikiria kitu kama uchambuzi wa mambo nyeti unakuta unakuwa rahisi kufanya kwa sababu lugha inayotumiaka ni kiswahili na mtu yeyote anaweza kujifanya kuelezea. Watu kima kina Makonda wangepotea kabisa kwenye uteuzi kwa sababu porojo wanazopiga kwa kiswahili wasingeweza kuzisema kwa kiingereza.
 
Moja ya sababu inayofanya nchi za Afrika ziwe wasindikizaji duniani huku zimejaa wasomi mbumbumbu ni watu wake kujifunza kwa lugha wasizozielewa vyema.
 
NYERERE mfumo wake ulifeeli ilitakiwa tuwe Kama China russiia ama Malaysia Ila huku Sera yake ilifeli,pia NYERERE sio Mungu elewa. Ni binadamu wa kawaida tu
Kufeli kwa mfumo wa Mwalimu Nyerere haina maana kwamba Kiswahili kiwekwe pembeni wala Inglishi iachwe. Hapana.

Mfumo wetu wa lugha mbili ni mzuri sana. Tatizo kuna wanasiasa wanaoongoza fani za kitaaluma wasikojua zinakopaswa kuelekea.

Tatizo siyo Kiswahili wala Inglishi; shida iko kwenye taaluma yenyewe -- ni duni. Elimu ya Bongo ni duni, ni duni, ni duni sana!

Afrika bado tuna safari ndefu ya kupiga kielimu; kwa Tanzania, inavyoonekana hiyo safari ya elimu ni kana hata hatujaianza bado.

Si ajabu wasomi wachache wanaobahatika kufaulu na kubobea vizuri wanaishia kwenye nchi za wengine, hasa Ulaya, Marekani, China, nk. What a shame!

Taifa linaendeshwa na wanataaluma na wasomi makapi, baada ya cream kuhamia mamitoni. If that isn't neo-colonialism, I really don't know what is!

Intellectual slavery is alive & well throughout Africa! Wake up guys!
 
Kiswahili ni lugha finyu sana. Lugha ya kitumwa na inafifisha akili za watu.
Lugha ni mfereji tu wa kupitishia maarifa. Hakuna maarifa yaliyopo sasa yasiyoweza kueleweka 100% kwa lugha adhimu na azizi ya Kiswahili.

Moja ya sababu inayofanya nchi za Afrika ziwe wasindikizaji duniani huku zimejaa wasomi mbumbumbu ni watu wake kujifunza kwa lugha wasizozielewa vyema.
Hii inaaplai kwa lugha zote mbili -- Kiswahili & Inglishi. Lugha hizi mbili zingetiliwa mkazo unaotakiwa mashuleni, tangu awali, zikatumika kufundishia vyema taaluma-fani za sanaa, ufundi, sayansi, na biashara, elimu yetu ingekuwa ya kiwango cha Mlima Kilimanjaro.
 
Kiingereza hakiwezi kutumika vyema kama lugha ya kufundishia kama kiswahili. Sababu ni kuwa siyo lugha ya kila siku ya mtanzania.
 
Utumwa na ukoloni haujakutoka kichwani, ujerumani wanatumia kiingereza!?..hawana maarifa!?.. kiingereza kiwe somo Kama masomo mengine,boresha walimu wa English,mtu asome mpaka form four,kwisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…