Kifaduro na kisonono cha wakataa ndoa, zimwi la kuogopwa sana kwenye jamii

Kifaduro na kisonono cha wakataa ndoa, zimwi la kuogopwa sana kwenye jamii

Ninavyompelekeaga nyuzi za watu wa JF halafu tunawacheka wote. Yani ni raha sana kwa kweli.
Siye tunaingia Ig tunacheka na reels kisha X , tunamalizia JF tunajadili comment moja baada ya nyingine huku tukifikia hatua ya kujadili Ids za huku na kujaribu kumchora mmiliki wake atakuwaje kisha nashangaa kaishia usingizini katikati ya maongezi anakuja kushituka ni morning groly....

kuna msimu mnajikuta mpo kwa Iddy Makengo mnasoma visa vya wapenzi wanavyotendana kimoyo moyo unawaza siku tusije kuwa sie tu...

Ndoa tamu sana
 
Kila nikitaka kuoa hii kitu inanijia Mshana Jr

KATAA NDOA ,NDOA NI UTAPELI TUNZA AFYA YAKO YA AKILI NA MALI ZAKO.
 
Attachments

  • 20250226_191524.jpg
    20250226_191524.jpg
    157.4 KB · Views: 1
Siye tunaingia Ig tunacheka na reels kisha X , tunamalizia JF tunajadili comment moja baada ya nyingine huku tukifikia hatua ya kujadili Ids za huku na kujaribu kumchora mmiliki wake atakuwaje kisha nashangaa kaishia usingizini katikati ya maongezi anakuja kushituka ni morning groly....

kuna msimu mnajikuta mpo kwa Iddy Makengo mnasoma visa vya wapenzi wanavyotendana kimoyo moyo unawaza siku tusije kuwa sie tu...

Ndoa tamu sana
Ndoa tamu sana! hasa unapokumbuka hakuna kulala na nanihii. .😀
 
Za kuambiwa changanya na zako. Mwenzio yuko na mkewe /mumewe anakwambia wewe kataa ndoa! Mbona yeye hatoki? Kalaga baho
 
Ndoa ni haramu iliyohalalishwa. Ni mwanaume mjinga pekee atakubali kuwa kwenye ndoa.
 
Ndoa hufanyoka mbinguni. Hii ina maana kwamba ndoa zimepangwa kabla au hutokea kulingana na mapenzi ya Mungu. Taasisi ya ndoa ina nafasi takatifu na yenye neema kubwa kiasili.

ZamaniWazazi walianza kutafuta mwenzi anayefaa kwa watoto wao punde tu wanapofikisha umri wa kuoa. Lakini ushawishi wa utamaduni wa Kimagharibi na kupenda mali umeleta mabadiliko kwa vijana ambao wamejikita zaidi katika taaluma na hivyo kuchelewesha ndoa hadi wawe wametulia vizuri. Wakati mwingine kutafuta mwenzi mkamilifu pia ni sababu ya kuchelewa kwa ndoa. Baadhi ya watu wamechelewa kwa sababu za hovyo kabisa huku wengine wakikataa kabisa ndoa. Kwasababu za kimaumbie
Yesu anasema walio jaliwa ndiyo wanaokataa ndoa kati ya watakatifu kwa ajili ya mapenzi ya mungu ...tena anasema akiwaambia wafuasi wake kuwa kama wataweza kuishi bila ya ndoa na wafanye hivyo maana walio jaliwa ndiyo wana weza kufanya hivyo.
 
Kristo alikuwa kanyooka Sana na kamwe hakuzuia watu wasioane bali alifafanua ili watu wawe na uchaguzi
 
Kristo alikuwa kanyooka Sana na kamwe hakuzuia watu wasioane bali alifafanua ili watu wawe na uchaguzi
Nani kasema alizuia watu wasioane ?! Yesu alicho eleza hapo ni fafanuzi ya best advice decision...na hiyo best advice decision yake ni kutokuoa wala kuolewa.
 
Ndoa haikwepeki kwa mwanaume aliyekamilika kisawa sawa akilini na maungoni!

Ukiona mtu anasema hawezi kuwa mmoja wa waliooa jua kimoja kati ya hivyo kimekufa either kichwa cha juu au cha chini au vyote kwa ujumla
📌📌
 
Back
Top Bottom