Kifo cha Asimwe Novath (Albino); Baba mzazi na Paroko msaidizi washikiliwa kwa tuhuma za mauaji

Baba paroko siyo padre,wamesema ni kijana alikua mlevi akachukuliwa na kanisa kulelewa ili aache pombe,siyo Kwamba na yeye ni paroko

ACHENI kulichafua kanisa, before hamjafanya utafiti

Tulia basi kwanza, lete hiyo taarifa kinzani. Kwa sasa taarifa ya geshi letu ra porisi ni baba paroko ndio muhusika.
 
Yani waziri katamba sana kana kwamba alizuia tukio ,asijipe umaarufu kupitia tukio ambalo limetuumiza sana mioyo yetu 😩
 
Acha kukashifu kanisa kanisa halijamtuma paroko ni yeye mwenyewe na uwendawazimu wake ata hivyo bado hajahukumiwa ni hadi mahakama itoe hukumu hapo ndio vizuri kumjudge sasa..
 
Hao wakabidhiwe wananchi wawaue taratibu kwa siku zaidi ya mia 600 wanapaswa wafe kwa uchungu mkali sana

Niliumia sana sana toka siku ya kwanza tu huyo mtoto alivyotoweka ,nilisali sn mtoto apatikane lkn haikuwa mapenzi ya Mungu ,nilipata taarifa jana nikiwa naelekea kazini ...kiukweli nilifika kazini na nikaondoka pasipo kumiaga yeyote yule kutokana na uchungu mzito mno niliokuwa nao

Niliwaza sana mtoto mdg kama yule anakutazama pasipo kujua nini kinatokea baada ya muda si mrefu
Unawezaje kuua mtoto kama yule yaani huna chembe yeyote ile ya huruma

Naomba kualikwa kutoa mateso makali sana kwa hao wendawazimu
 
Kwahiyo, mabaya yako uliyowahi kuyafanya hapa duniani, ukoo wako ndo ulaumiwe? Kanisa la RC siyo la mtu mmoja. Kama angekuwa ametumwa na kanisa kufanya hayo, sawa. Ila kama hajatumwa, kuwa kwake padre hakumaanishi kila anachokifanya katumwa na kanisa
 
Kwa spidi hii-bila kuwa na hata camera za barabarani , wanatakiwa kupongezwa sana.
 
Je vipi kama sio wao na wahusika wakuu hawajapatikana? Tuwahukumu ivo ivo kwa kutumia emotion zetu?
Sijawazungumzia hao waliokamatwa wala mtu yeyote specific ila nimezungumzia tukio kwa ujumla na uvumi unaosemwa kwamba matukio hayo husukumwa zaidi na imani za kishirikina ili mtu kujipatia utajiri au madaraka,hayo ndiyo masikitiko yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…