Kifo cha Asimwe Novath (Albino); Baba mzazi na Paroko msaidizi washikiliwa kwa tuhuma za mauaji

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Raia wema wanaochukia vitendo vya kinyama baada ya msako mkali kuanzia May 31, 2024 hadi usiku wa kuamkia leo June 19, 2024 wamefanikisha kukamatwa kwa Watu tisa wakiwa na viungo vinavyodhaniwa ni vya Mtoto Albino Asimwe Novart (aliyeuawa Wilayani Muleba Mkoani Kagera) wakiwa wamehifadhi katika vifungashio vya plastiki wakitafuta Mteja Mkoani Kagera.

Taarifa iliyotolewa leo na Msemaji wa Polisi, David Misime imesema Watuhumiwa waliokamatwa ambao wameeleza jinsi walivyoshiriki katika tukio hili ni pamoja Baba mzazi wa Mtoto huyo aitwaye Novart Venant, Desideli Evarist ambaye ni Mganga wa jadi Mkazi wa Nyakahama, Elipidius Rwegoshora Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bugandika ambaye anadaiwa kumfuata na kumshawishi Baba mzazi wa Mtoto ili wafanye biashara ya viungo vya binadamu na pia anatuhumiwa kuwa ndiye aliyemtafuta mganga wa jadi na kulipia gharama zote za uganga.

Watuhumiwa wengine ni Dastan Kaiza Mkazi wa Bushagara, Faswiru Athuman Mkazi wa Nyakahama, Gozibert Alkadi Mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Rwenyagira Burkadi Mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Ramadhani Selestine Mkazi wa Kamachumu na Nurduni Hamada Mkazi wa Kamachumu.

“Jeshi la Polisi linatoa kutoa onyo kali kwa Watu wanaoendekeza imani za kishirikina ikiwemo kupiga ramli chonganishi wakiaminishana kwamba wanaweza kupata utajiri kwa njia za kishirikina kuacha tabia hizo”
#MillardAyoUPDATES
 

Attachments

  • FB_IMG_1718807055553.jpg
    54.5 KB · Views: 2
Dah wagalatia kimeumana asee sijui tutajificha wapi? Tumekwisha asee.

Yesu tusaidie wakati huu mgumu tunapitia.

adriz Accumen Mo darcity hydroxo Webabu Adiosamigo Gavana mjingamimi Mlolongo ielewemitaa inamankusweke
 
Yani hata mteja hawakuwa naye! Huu ni wendawazimu wa aina gani!
 
Siyo kweli ni uwongo
 
Waliokata viungo vya mtoto walifuata agizo la huyo kiongozi wa dini, kwa kuwa wanaheshimu sana viongozi wa dini. Naomba huyo kiongozi wa dini abinywe ili azidi kutaja wateja wa hiyo biashara. Polisi msiangalie makunyanzi, mpeni adhabu ya mfano.
 
Nilisema kama mapadre wanaruhusiwa kwenda bar kunywa pombe, then haya siyashangai.

zamani padre alikuwa anakaa kwenye parish. hatoki pale mpaka kwa sababu maalum. Leo wako kwenye vilabu vya pombe wanakunywa na raia!

wameanza kujenga majumba mijini! ya nini na wewe ni padre maisha yako yako mikononi mwa Pope?
 
Baba Poroko? ukishtuka ulipo sipo jua lishazama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…