Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Jasusi;

Unaongea kwa mamlaka na kujiamani, lakini kama unajua lolote kuhusu agency za Serikali ya US na swala la privacy linavyo chukuliwa, basi usinge weza kusema mtu "awasiliane na idara za serikali ya DC" kutafuta info za mwenye Social Security Number. Hakuna idara ya Serikali inaweza kukupa info za mtu mwingine.

Pili, ili kuwa na social security profile na rekodi kuwepo idara ya Social Security, sio lazima uwe umefanya kazi Serikalini. Ingekuwa hivyo, basi Wamarekani wasiofanya kazi Serikalini wangekuwa hawapewi SSNumber.

Tatu, information za SSN za mtu zinaweza kupatikana mitandaoni informally, na ndio maana kuna tatizo la wizi wa identity Marekani, moja ya jinai inayoongezeka kuliko zote nyakati hizi za mapinduzi ya habari za elektronik.

Kwa hiyo mjomba, hili swala la upatikanaji wa social securiy information inaonekana hulijui jui vizuri, to say the least. Lete "dataz" kwenye eneo jingine, labda mambo ya "Nationa Insurance Number" za Uingereza , au "Social Insurance Number" za Canada na kwingineko ambapo unaweza "kutupeleka peleka" unavyo taka wale ambao hatujui lolote kuhusu viwanja hivyo. (And bear in mind, Google tunayo siku zote, kwa hiyo, chonde chonde hata huko kwenye "dataz" za viwanja vingine!)

Nadhani pia umejaribu kutugawa katika makundi ya "Wanaoamini kafa" na "Wasio amini kafa" wakati wengine tunatafuta tu habari bila kutetea tetea pande kishabiki. And, with such shattered credibility on your own info, labda bia umepoteza authority ya kutetea source za watu wengine as "95% correct!"

Mkuu KM,

Hii ndio faida ya JF, kila mtu kuna jambo analijua zaidi kuliko wengine na tukiunganisha dots, tunapata jawabu la tatizo sugu.

Endeleeni kutuelemisha hayo ya hapo USA, maana kusingelikuwa na Watanzania huko, hapa tulishafungwa magoli mengi na mchanga kibao machoni.
 
Waungwana hata mimi siamini kama Balali amekufa. mi naona hapa serikali inatupiga changa la macho. toka swala la EPA limeanza serikali imekuwa ikitoa taarifa tata kuhusu swala la balali na sababu zinajulikana.serikali ya awamu hii imekuwa ya ajabu kuliko zilizowahi kupita. swala la balali limekuwa na wasemaji wengi kuliko lile la ajira milioni moja, utafikiri wanahamasisha maendeleo. Alianza Rais kumtimua ugavana, Akaja Zakia,Ndulu, Salva, na sasa Membe na bado wataongezeka wote hawa wamekuwa wakiongolea swala la Balali na taarifa zao zote za utata hakuna kinachoeleweka. Kama Rais anataka serikali yake isibebeshwe lawama kuhusu kifo cha Balali basi hotuba yake ya mwisho wa mwezi huu ahutubie live na mbele ya waandishi wa habari kuhusu huu utata wa Kifo cha Balali tumuulize na maswali asipotoa majibu yatakayoridhisha jamii basi tusubiri 2010 tuiweke CCM pembeni hatuwezi kuendelea na usanii wa namna hii hatutafika. kama hamuamini subirini mtasikia mafisadi wanaanza kufa kimagumashi kama Balali. Tukaze buti safari ishaonekana ndefu kupitiliza.
 
Jasusi;

Unaongea kwa mamlaka na kujiamani, lakini kama unajua lolote kuhusu agency za Serikali ya US na swala la privacy linavyo chukuliwa, basi usinge weza kusema mtu "awasiliane na idara za serikali ya DC" kutafuta info za mwenye Social Security Number. Hakuna idara ya Serikali inaweza kukupa info za mtu mwingine.

Mkuu hapo tunasema lugha moja. Nilichojaribu kufanya ni kuonyesha kuwa yule aliyetuletea google ya social security na kuonyesha kuwa hawana data za marehemu ametu-mislead. Huwezi kupata data hizo unless wewe ni family member.

Pili, ili kuwa na social security profile na rekodi kuwepo idara ya Social Security, sio lazima uwe umefanya kazi Serikalini. Ingekuwa hivyo, basi Wamarekani wasiofanya kazi Serikalini wangekuwa hawapewi SSNumber.
Swadakta,
Hapo pia sijakuchanganya. SS hutolewa kwa wafanyikazi wowote wawe katika serikali au private industry. Hivi sasa anybody born in the US unapata ss automatically. Na wale wazamiaji akishapata tu residency na work permit anaruhusiwa kuwa na ss.

Tatu, information za SSN za mtu zinaweza kupatikana mitandaoni informally, na ndio maana kuna tatizo la wizi wa identity Marekani, moja ya jinai inayoongezeka kuliko zote nyakati hizi za mapinduzi ya habari za elektronik.

Lakini kwa kutafuta data za marehemu, especially just a few days after one's death itakuwa vigumu. That was my point.

Nadhani pia umejaribu kutugawa katika makundi ya "Wanaoamini kafa" na "Wasio amini kafa" wakati wengine tunatafuta tu habari bila kutetea tetea pande kishabiki. And, with such shattered credibility on your own info, labda bia umepoteza authority ya kutetea source za watu wengine as "95% correct!"
Siyo mimi niliyewagawa. Doubting Thomases ndio wameleta mgawanyiko huo. Ndio maana niliuliza kuwa sisi wana familia tungekuwa na faida gani kuficha kifo? Mimi najua amekufa. FMES amekuja hapa akisema he is 100% sure kuwa amekufa. Tatizo ni kwamba hapa wengi wanamwona marehemu kama mtuhumiwa. Au kama wengine walivyomuita "fisadi." Mimi kwangu marhemu alikuwa shahidi, na ndio maana nauliza kama kweli marhemu alichota mahela yale yote mbona tunatangaziwa kuwa wameanza kuyarudisha na majina ya wanayoyarudisha ni siri kuu ya TAKUKURU? Kwa nini RO alisema mwezi Desemba kuwa mgonjwa hatapona na ikiwa atapona itakuwa ni muujiza wa mwenyezi Mungu, na asirudi Bongo? Haya ndiyo maswali ambayo na sisi tungependa yajibiwe. Ndio maana naunga mkono kauli ya Mzee Slaa kuwa iundwe tume ya kuchunguza hicho kifo. Na hapa ningependa kuongezea kuwa kati ya mashahidi watakaoitwa kwenye hiyo tume awemo mama Mkapa kwani yeye mapema mwezi August, mbele ya dada mkubwa wa mke wa marehemu, alisema kuwa amepata habari mitaani kuwa gavana yuko kwenye life support katika hospitali ya Marekani. Tungetaka kujua hizo habari alizipata wapi---just a few weeks before Daudi took ill.
 
Waungwana hata mimi siamini kama Balali amekufa.kwanini mazishi yake yawe na mwaliko na kwa watu maalumu tu?? kwanini hakukuwa na upigaji picha??kwanini hajatokeza hata ndugu mmoja kuzungumzia hicho kifo wakati serikali haihusiki??? au hana ndugu?? na ule ulinzi waliouweka kule kwa mama yake wa nini au kuna mabaki ya EPA??? mi naona hapa serikali inatupiga changa la macho. toka swala la EPA limeanza serikali imekuwa ikitoa taarifa tata kuhusu swala la balali na sababu zinajulikana.serikali ya awamu hii imekuwa ya ajabu kuliko zilizowahi kupita. swala la balali limekuwa na wasemaji wengi kuliko lile la ajira milioni moja, utafikiri wanahamasisha maendeleo. Alianza Rais kumtimua ugavana, Akaja Zakia,Ndulu, Salva, na sasa Membe na bado wataongezeka wote hawa wamekuwa wakiongolea swala la Balali na taarifa zao zote za utata hakuna kinachoeleweka. Kama Rais anataka serikali yake isibebeshwe lawama kuhusu kifo cha Balali basi hotuba yake ya mwisho wa mwezi huu ahutubie live na mbele ya waandishi wa habari kuhusu huu utata wa Kifo cha Balali tumuulize na maswali asipotoa majibu yatakayoridhisha jamii basi tusubiri 2010 tuiweke CCM pembeni hatuwezi kuendelea na usanii wa namna hii hatutafika. kama hamuamini subirini mtasikia mafisadi wanaanza kufa kimagumashi kama Balali. Tukaze buti safari ishaonekana ndefu kupitiliza.
 
mzee aliweza vipi kulazwa kwa jina bandia katika hospitali za Marekani? Najua kwenye hoteli kuna sera za kuwaficha celebrities under assumed names.. lakini kwenye matibabu ni ngumu kidogo. Lakini kwa vile Marehemu keshatutoka sidhani kama kuna ubaya wa hata kutoa jina alilotumia kwani hakuna mtu yeyote anayeweza kumfanya lolote sasa.
Mzee Mwkjj,
All you need is the collusion of your personal doctor. Mambo kwisha.
As for name I did not ask so honestly I do not know.
 
Mzee Mwkjj,
All you need is the collusion of your personal doctor. Mambo kwisha.
As for name I did not ask so honestly I do not know.

Kwi kwi kwi!!!! ukimtembelea ulikuwa unamwita nani? Kwanini mtu aingie kwenye yote haya ya kudanganya mpaka majina wakati yuko nje ya nchi?

Kambona na kuandamwa kote na Nyerere wala hata hakuhangaika kubadili jina.

Kama ni kweli basi Ballali alikuwa hata anakimbia kivuli chake. Hata baada ya kufa bado alikuwa naogopa hata baadhi ya watu kuuangalia mwili wake. Huu ni uwoga uliokithiri kiwango.
 
Siyo mimi niliyewagawa. Doubting Thomases ndio wameleta mgawanyiko huo. Ndio maana niliuliza kuwa sisi wana familia tungekuwa na faida gani kuficha kifo? Mimi najua amekufa. FMES amekuja hapa akisema he is 100% sure kuwa amekufa. Tatizo ni kwamba hapa wengi wanamwona marehemu kama mtuhumiwa. Au kama wengine walivyomuita "fisadi." Mimi kwangu marhemu alikuwa shahidi, na ndio maana nauliza kama kweli marhemu alichota mahela yale yote mbona tunatangaziwa kuwa wameanza kuyarudisha na majina ya wanayoyarudisha ni siri kuu ya TAKUKURU? Kwa nini RO alisema mwezi Desemba kuwa mgonjwa hatapona na ikiwa atapona itakuwa ni muujiza wa mwenyezi Mungu, na asirudi Bongo? Haya ndiyo maswali ambayo na sisi tungependa yajibiwe. Ndio maana naunga mkono kauli ya Mzee Slaa kuwa iundwe tume ya kuchunguza hicho kifo. Na hapa ningependa kuongezea kuwa kati ya mashahidi watakaoitwa kwenye hiyo tume awemo mama Mkapa kwani yeye mapema mwezi August, mbele ya dada mkubwa wa mke wa marehemu, alisema kuwa amepata habari mitaani kuwa gavana yuko kwenye life support katika hospitali ya Marekani. Tungetaka kujua hizo habari alizipata wapi---just a few weeks before Daudi took ill.

Mkuu Jasusi,

Kwanza sio kweli kuwa habari za kifo cha Ballali haziaminiwi kwa vile kuna watu wanamuona yeye kama fisadi au mtuhumiwa. Mimi muda wote nimekuwa namuona Ballali kama mtuhumiwa na fisadi lakini nilikubali habari za kifo chake na kuzitetea hapa kwa karibu wiki nzima.

Mabilioni ya pesa za watanzania yameibwa BoT wakati Ballali akiwa gavana wake. Katika hili hakuna maswali. Kama hakuhusika au kama alilazimishwa na kina Kikwete na Mkapa basi hicho ndicho kitu ambacho muda wote amekuwa anapewa nafasi kuelezea ukweli ili huo ukweli umweke huru.

Mimi ni kati ya wale wanaoamini kuwa Ballali ametumika tu hapa na wezi wako bongo au kokote waliko wakila na kutumbua mapesa ya nchi. Nimemwita Ballali kama kipisi cha mkuyu. Kuna nafasi kubwa sana ya kusafisha jina la Ballali (kama hana hatia) lakini so far yanayofanyika sio sehemu kabisa ya hayo. Kama ni kweli kuwa Ballali amempatia Mkono (fisadi mwingine anayetakiwa kuwa jela kwa wizi wa mali ya watanzania) ushahidi wa kesi yake, basi ukweli ni kuwa Ballali hakuwa na hana nia safi ya kusafisha jina lake.

Mimi nimeamua kutoamini habari za kifo cha Ballali kutokana na mchanganyiko katika mambo matatu:

1. Ballali alikuwa akitibiwa wapi mpaka mauti yalipomkuta?
2. Ballali alikufa lini na wapi - so far zimetajwa siku tatu tofauti?
3. Kwa nini hakuna report za kifo cha Ballali kwenye record za serikali hapa US?

Kwa imani niliyojenga kwa watu kama wewe ambao kwa muda mrefu sana hapa JF tumekuwa pamoja katika mapambano haya, ndiyo maana nimeacha hiyo asilimia tano kwenye doubts zangu. Otherwise ningekataa hizi habari kwa asilimia mia moja.
 
Mkuu KM,

Hii ndio faida ya JF, kila mtu kuna jambo analijua zaidi kuliko wengine na tukiunganisha dots, tunapata jawabu la tatizo sugu.

Endeleeni kutuelemisha hayo ya hapo USA, maana kusingelikuwa na Watanzania huko, hapa tulishafungwa magoli mengi na mchanga kibao machoni.

Mtanzania,

Kwa bahati mbaya kwa wengine hapa, hii habari ya kifo cha Ballali imefanya tutumie siku zetu za likizo kabla na baada ya memorial day kufuatilia hii habari kwa makini zaidi. Ukianza kuona habari kuwa inawezekana Ballali alitumia jina tofauti na la kwake (kwa sababu za kiusalama) basi ujue kuwa tumenusa kwa kiwango kikubwa na kulikuwa hakuelekei kupata taarifa kwa jina la Ballali (na hili lina-justify my doubts kwa kiwango kikubwa).

Katika issue ya death certificate, bado narudia nilichosema kwenye thread ya Mushi (hivi amepotelea wapi huyu) kuwa sio lazima hii itolewe mapema. Kule DC wana office ya CME (Chief of Medical Examiner) ambayo inahusika kabisa na mazingira ya kifo kama cha Ballali. So far, hakuna records zozote nilizopata za kuonyesha kuwa Ballali amekufa. Jumatano jioni niliwatumia official request na sababu za kwa nini nataka kujua kama Ballali amekufa na kwa nini. So far nasubiria official response.

Jibu la juu juu nililopata ni kuwa, hakuna record hiyo by wednesday night. Kwa leo tumeambiwa hapa kuwa Ballali alitumia jina la bandia kwenye tiba (kitu ambacho kinawezekana kabisa na ni rahisi kufanyika), inaita kuona kama labda itasemwa hapa kuwa Ballali aliandikisha pia kifo chake kwa jina la bandia.

Inatia uchungu kuwa ninaingilia sana maisha binafsi ya watu (hasa familia ya Ballali) ambao kwa kweli najua kuwa hii issue inawaumiza sana na wao sio tu kuwa hawausiki na kilichotokea bali pia ni unfair kuhusishwa na haya yote.

Hata hivyo inafikia hatua kutafuta haya mambo ili kuwa kwenye nafasi nzuri ya kukomboa nchi yetu kama kweli hilo ndilo lengo letu hapa JF.

Asante.
 
Mkuu Jasusi,

Mimi ni kati ya wale wanaoamini kuwa Ballali ametumika tu hapa na wezi wako bongo au kokote waliko wakila na kutumbua mapesa ya nchi. Nimemwita Ballali kama kipisi cha mkuyu. Kuna nafasi kubwa sana ya kusafisha jina la Ballali (kama hana hatia) lakini so far yanayofanyika sio sehemu kabisa ya hayo. Kama ni kweli kuwa Ballali amempatia Mkono (fisadi mwingine anayetakiwa kuwa jela kwa wizi wa mali ya watanzania) ushahidi wa kesi yake, basi ukweli ni kuwa Ballali hakuwa na hana nia safi ya kusafisha jina lake.

MWK,
Na mimi pia naamini kabisa kuwa hatimaye ukweli utajulikana na jina la marehemu kusafishika. Ungemwona mgonjwa na hali aliyokuwa nayo baada ya kulazwa hospitali hili la kusafisha jina lake ungeliona secondary. Kupona kwake was our priority. Having said that, sina hakika na siamini kuwa Mkono amepewa ushahidi wowote na marehemu kama ilivyodaiwa elsewhere. Lakini ninaamini kuna watu wema tu nchini Tanzania ambao watatupa ushirikiano wao katika kufanikisha hilo.
 
Nimeingia hii site kutafuta death record na nikaambulia patupu:

http://www.public-records-now.com/Search/death/default.aspx?from=hys0300400105&piid=46

"Marehemu" kwa kuwa aliwahi kuishi US, lazima atakuwa either ali-apply for credit, or has created records that are public by law. Kama alikufa, hai-make any sense kutokuwemo death records zake huko US.

Contacts za jamaa wanaoripoti hizo death records ni 1-800-610-2703. Working hours ni Monday-Friday 7 am - 5 pm PST. Give me some time hadi nitoke hapa ulinzini PPF Tower ili baadaye nifanye utomaso zaidi kwenye hili suala, ama kama kuna mtu anaweza kuwa-call hao jamaa kuulizia hizi details afanye hivyo na atupe details.
 
Kuna wako mstari wa mbele kumuunga mkono Mbowe na kauli yake kuwa Balali ameuliwa na serikali, lakini cha kushangaza ni kwamba watu haohao wanakataa kuwa Balali amekufa, this is getting a little confusing!
 
MWK,
Na mimi pia naamini kabisa kuwa hatimaye ukweli utajulikana na jina la marehemu kusafishika. Ungemwona mgonjwa na hali aliyokuwa nayo baada ya kulazwa hospitali hili la kusafisha jina lake ungeliona secondary. Kupona kwake was our priority. Having said that, sina hakika na siamini kuwa Mkono amepewa ushahidi wowote na marehemu kama ilivyodaiwa elsewhere. Lakini ninaamini kuna watu wema tu nchini Tanzania ambao watatupa ushirikiano wao katika kufanikisha hilo.

Jasusi,

Hata mimi sina doubt kuwa hizi habari zitatoka karibuni. Nina hakika kuwa hata asipozitoa Ballali au ndugu zake Ballali, kuna wengine wengi tu watazitoa na ukweli wote utajulikana.

Nimefurahi pia kujua kuwa fisadi Mkono hakupewa hizi habari. Nakuhakikishia kuwa kati ya watu wengi wema wanaoweza kutumika kusafisha jina la Ballali ni mimi. Ninachotaka kujua ni ukweli na nothing but ukweli. So far sijaona ukweli mkamilifu katika hii habari yote ya Ballali.

Ninaelewa kuwa tiba ilikuwa muhimu sana kabla ya mengine yote. Kama hili ni case hapa, basi natumaini kuwa muda si mrefu hicho kinachosubiriwa itabidi kitoke haraka sana iwezekanavyo. Unajua muda mwingine timing ni kitu muhimu sana kwenye siasa. Wewe uko US na unaona kinachompata Scott sasa hivi. Ametoa habari za Bush lakini timing iko wrong so habari yake inakosa umuhimu mkubwa zaidi kama ingetoka mapema zaidi.

Zaidi sana naomba nikukumbushe kuwa nothing here is personal. Nakuhakikishia kuwa ningeshika the same bango kwa Ballali hata kama angekuwa ni baba yangu. Familia yetu tumeapa kuwa tutatosana iwapo mmoja wetu atajihusisha na ufisadi wa kudhulumu masikini ambao hawana hatia yoyote kama watanzania.
 
Mtanzania,

Kwa bahati mbaya kwa wengine hapa, hii habari ya kifo cha Ballali imefanya tutumie siku zetu za likizo kabla na baada ya memorial day kufuatilia hii habari kwa makini zaidi. Ukianza kuona habari kuwa inawezekana Ballali alitumia jina tofauti na la kwake (kwa sababu za kiusalama) basi ujue kuwa tumenusa kwa kiwango kikubwa na kulikuwa hakuelekei kupata taarifa kwa jina la Ballali (na hili lina-justify my doubts kwa kiwango kikubwa).

Katika issue ya death certificate, bado narudia nilichosema kwenye thread ya Mushi (hivi amepotelea wapi huyu) kuwa sio lazima hii itolewe mapema. Kule DC wana office ya CME (Chief of Medical Examiner) ambayo inahusika kabisa na mazingira ya kifo kama cha Ballali. So far, hakuna records zozote nilizopata za kuonyesha kuwa Ballali amekufa. Jumatano jioni niliwatumia official request na sababu za kwa nini nataka kujua kama Ballali amekufa na kwa nini. So far nasubiria official response.

Jibu la juu juu nililopata ni kuwa, hakuna record hiyo by wednesday night. Kwa leo tumeambiwa hapa kuwa Ballali alitumia jina la bandia kwenye tiba (kitu ambacho kinawezekana kabisa na ni rahisi kufanyika), inaita kuona kama labda itasemwa hapa kuwa Ballali aliandikisha pia kifo chake kwa jina la bandia.

Inatia uchungu kuwa ninaingilia sana maisha binafsi ya watu (hasa familia ya Ballali) ambao kwa kweli najua kuwa hii issue inawaumiza sana na wao sio tu kuwa hawausiki na kilichotokea bali pia ni unfair kuhusishwa na haya yote.

Hata hivyo inafikia hatua kutafuta haya mambo ili kuwa kwenye nafasi nzuri ya kukomboa nchi yetu kama kweli hilo ndilo lengo letu hapa JF.

Asante.

Mwafrika wa Kike,

Kwenye hili jua kila unachofanya unamsaidia mama Tanzania. Tanzania ni kubwa kuliko Ballali au familia ya Ballali.

Tukipata jibu sahihi kwenye hili tutakuwa tumetengeneza maadili mema kwa viongozi wa baadaye.

Hatutakiwi kuwaonea huruma mafisadi, watoto wanaokufa kwa kukosa dawa, nao wana familia zao, hawana kosa lolote kwa mungu lakini imebidi wafe kwasababu ya nchi kukosa madawa na huduma zingine.

Ballali alikuwa na choice na akaamua kuwatumikia mafisadi. Mimi simwonei huruma kabisa ingawaje naionea huruma familia yake. Husomeshi mtoto mpaka kuwa Dr. ili awe jambazi.

Kwenye hili lazima tuwe tayari hata kuwachangia wale wachache ambao wana uwezo wa kututafutia ukweli juu ya hili jambo.

Kazi nzuri MWK.
 
Kuna wako mstari wa mbele kumuunga mkono Mbowe na kauli yake kuwa Balali ameuliwa na serikali, lakini cha kushangaza ni kwamba watu haohao wanakataa kuwa Balali amekufa, this is getting a little confusing!

kumbuka kuwa hakuna mtu aliyelazimisha yeyote kuamini tofauti hapa. Mbowe ametokea kuamini kifo cha Ballali na ameiamini familia ya Ballali na serikali ya Tanzania kuwa Ballali amekufa. Ukitaka kujadili statement ya Mbowe unaacha feeling zako binafsi otherwise utakuwa biased.

Mimi binafsi niliamini kuwa Ballali amekufa lakini uchunguzi wangu umepelekea kuamini tofauti. Kwa vile mimi sikulazimisha watu kuamini kifo cha Ballali, kwa sasa pia sitalazimisha watu kutokuamini kifo hicho (in this case hata Mbowe na yule mropokaji Membe aliyekimbia kueleza kuwa serikali haiusiki na kifo cha Ballali bila hata kuulizwa na yeyote yule).
 
Mtanzania,

Kwa bahati mbaya kwa wengine hapa, hii habari ya kifo cha Ballali imefanya tutumie siku zetu za likizo kabla na baada ya memorial day kufuatilia hii habari kwa makini zaidi. Ukianza kuona habari kuwa inawezekana Ballali alitumia jina tofauti na la kwake (kwa sababu za kiusalama) basi ujue kuwa tumenusa kwa kiwango kikubwa na kulikuwa hakuelekei kupata taarifa kwa jina la Ballali (na hili linajustfy my doubts kwa kiwango kikubwa).

Katika issue ya death certificate, bado narudia nilichosema kwenye thread ya Mushi (hivi amepotelea wapi huyu) kuwa sio lazima hii itolewe mapema. Kule DC wana office ya CME (Chief of Medical Examiner) ambayo inahusika kabisa na mazingira ya kifo kama cha Ballali. So far, hakuna records zozote nilizopata za kuonyesha kuwa Ballali amekufa. Jumatano jioni niliwatumia official request na sababu za kwa nini nataka kujua kama Ballali amekufa na kwa nini. So far nasubiria official response.

Jibu la juu juu nililopata ni kuwa, hakuna record hiyo by wednesday night. Kwa leo tumeambiwa hapa kuwa Ballali alitumia jina la bandia kwenye tiba (kitu ambacho kinawezekana kabisa na ni rahisi kufanyika), inaita kuona kama labda itasemwa hapa kuwa Ballali aliandikisha pia kifo chake kwa jina la bandia.

Inatia uchungu kuwa ninaingilia sana maisha binafsi ya watu (hasa familia ya Ballali) ambao kwa kweli najua kuwa hii issue inawaumiza sana na wao sio tu kuwa hawausiki na kilichotokea bali pia ni unfair kuhusishwa na haya yote.

Hata hivyo inafikia hatua kutafuta haya mambo ili kuwa kwenye nafasi nzuri ya kukomboa nchi yetu kama kweli hilo ndilo lengo letu hapa JF.

Asante.

Kama ni hivyo hii inaashiria mambo makuu yafuatayo:

1. Serikali kupitia Mkono (akiwa mwanasheria) na (kwa nafasi yake ya ubunge)
inafahamu taarifa zote kuhusu Balali.

2. Inaonekana Balali alikuwa ana uraia wa nchi mbili na alipokwenda USA alitumia pasi ya USA hivyo kumuonesha kwamba tarehe ya mwisho kuingia Tanzania alitumia moja ya pasi alizo nazo ikiwemo ile ya diplomatic.

3.Serikali ya marekani inatambua hayo kupitia wilaya yake ya Washington na imekuwa ikishirikiana na ubalozi, familia ya Balali na sehemu zote ambazo amepitia iwe hospitali au wherever.

4. Kama makachero wa Tanzania walikwenda US basi wanajua pia situation ya Balali na pengine walipoingia wakapigwa mkwara mzito na wakarejea Tanzania.

5.Kama nilivyowahi kusema katika posts zangu zinazomhusu Balali, ni kwamba huyu bwana ni mtu muhimu na yumo katika lists ya distinguished leaders wa Tanzania.

Hivo kwa mtizamo wangu ni kwamba yatatokea mambo ambayo yatakuja kuwa ni surprice kubwa kwa sisi wote katika fore·see·able future.
 
Wakuu,

Contradiction nyingine ni kwamba kulingana na jasusi, RO alionana na Ballali na kushangaa
kuona alikuwa mzima na alimshauri akipona asirudi TZ.

Wakati huo huo eti Makachero saba walitumwa kumtafuta Ballali USA, ikabidi mpaka Dr. wetu atumie jina bandia hospitali.

Kama boss wa Makachero (RO) alikuwa anajua aliko Ballali na alishaonana naye, kweli kulikuwa na sababu zipi za kuwatuma Makachero wengine saba kumtafuta?

Moja ya hizi habari mbili kwa vyovyote sio sahii.
 
Habari ya RO kuonana na Ballali bado ninaiamini na Jasusi ameisema hapa. Hiyo ya makachero saba bado sijaiamini kabisa na ilivyotoka mara ya kwanza ilitoka kiudakuudaku sana.

Taratibu tu tutafikia kwenye uvungu wa kila kitu... tuliyopata leo ni revelation ya nguvu sana kwenye hii case..... Na nampongeza sana Jasusi kwa kushiriki kwenye huu mjadala. Ni wachache sana wangeweza kufanya hivyo.
 
Mkuu Jasusi,

Mimi ni kati ya wale wanaoamini kuwa Ballali ametumika tu hapa na wezi wako bongo au kokote waliko wakila na kutumbua mapesa ya nchi.Nimemwita Ballali kama kipisi cha mkuyu. Kuna nafasi kubwa sana ya kusafisha jina la Ballali (kama hana hatia) lakini so far yanayofanyika sio sehemu kabisa ya hayo. Kama ni kweli kuwa Ballali amempatia Mkono (fisadi mwingine anayetakiwa kuwa jela kwa wizi wa mali ya watanzania) ushahidi wa kesi yake, basi ukweli ni kuwa Ballali hakuwa na hana nia safi ya kusafisha jina lake.

MWK,
Na mimi pia naamini kabisa kuwa hatimaye ukweli utajulikana na jina la marehemu kusafishika. Ungemwona mgonjwa na hali aliyokuwa nayo baada ya kulazwa hospitali hili la kusafisha jina lake ungeliona secondary. Kupona kwake was our priority. Having said that, sina hakika na siamini kuwa Mkono amepewa ushahidi wowote na marehemu kama ilivyodaiwa elsewhere. Lakini ninaamini kuna watu wema tu nchini Tanzania ambao watatupa ushirikiano wao katika kufanikisha hilo.

Nakubaliana kiasi fulani na wewe ila tatizo liko hapo kwenye higlight.

Sidhani kama taarifa za nini haswa kilichofanyika kwenye issue ya EPA zilitakiwa zisubiri mpaka alazwe hospitali.

Kwa hiyo maana yangu ni kwamba...Ballali alikuwa na muda mwingi tu wa kuweka ukweli wote bayana.

Kuna taarifa kuwa alikuwa fine tu mwezi januari mwaka huu.
Toka aumwe...Na yeye kuwa na wasiwasi kuwa ni sumu aliwekewa..Then kwanini hakuzitumia nafasi zote alizopata wakati akiwa mzima?

Swala la yeye kutembelewa hospitali akiwa hoi bin taaban na kudhoofu kiasi cha kutia huruma lingepewa kipa umbele zaidi kama angekuwa tayari keshaweka mambo ya ufisadi wazi.

Kama wengine ambavyo wamedai hapa jf ni hili....Inaeleweka labda Ballali hakutaka ajulikane mahali alipokuwa akitibiwa kwasababu za usalama wake.
Sasa kama ni marehemu ni kivipi usalama wake utakuwa kwenye hati hati?

Hili linakuwa possble kivipi wakati serikali ilishasema inajua mahali alipo? Na pia yeye kulipiwa either na BOT ama serikali yenyewe?

Unataka kusema Ndulu atamgomea Rais habari za Ballali either mahali alipo, ama alipolazwa?

Haya sasa unasema keshakufa..Serikali itaufanyia nini huo mwili wake uliokufa kama ungeonekana?
Marehemu ni toka lini akawa mwoga?
 
Contradiction nyingine ni kwamba kulingana na jasusi, RO alionana na Ballali na kushangaa kuona alikuwa mzima na alimshauri akipona asirudi TZ.

Wakati huo huo eti Makachero saba walitumwa kumtafuta Ballali USA, ikabidi mpaka Dr. wetu atumie jina bandia hospitali.

Kama boss wa Makachero (RO) alikuwa anajua aliko Ballali na alishaonana naye, kweli kulikuwa na sababu zipi za kuwatuma Makachero wengine saba kumtafuta?

Moja ya hizi habari mbili kwa vyovyote sio sahii.

Inawezekana zote mbili sio sahihi.

Unaonaje?
 
Back
Top Bottom