Jasusi;
Unaongea kwa mamlaka na kujiamani, lakini kama unajua lolote kuhusu agency za Serikali ya US na swala la privacy linavyo chukuliwa, basi usinge weza kusema mtu "awasiliane na idara za serikali ya DC" kutafuta info za mwenye Social Security Number. Hakuna idara ya Serikali inaweza kukupa info za mtu mwingine.
Pili, ili kuwa na social security profile na rekodi kuwepo idara ya Social Security, sio lazima uwe umefanya kazi Serikalini. Ingekuwa hivyo, basi Wamarekani wasiofanya kazi Serikalini wangekuwa hawapewi SSNumber.
Tatu, information za SSN za mtu zinaweza kupatikana mitandaoni informally, na ndio maana kuna tatizo la wizi wa identity Marekani, moja ya jinai inayoongezeka kuliko zote nyakati hizi za mapinduzi ya habari za elektronik.
Kwa hiyo mjomba, hili swala la upatikanaji wa social securiy information inaonekana hulijui jui vizuri, to say the least. Lete "dataz" kwenye eneo jingine, labda mambo ya "Nationa Insurance Number" za Uingereza , au "Social Insurance Number" za Canada na kwingineko ambapo unaweza "kutupeleka peleka" unavyo taka wale ambao hatujui lolote kuhusu viwanja hivyo. (And bear in mind, Google tunayo siku zote, kwa hiyo, chonde chonde hata huko kwenye "dataz" za viwanja vingine!)
Nadhani pia umejaribu kutugawa katika makundi ya "Wanaoamini kafa" na "Wasio amini kafa" wakati wengine tunatafuta tu habari bila kutetea tetea pande kishabiki. And, with such shattered credibility on your own info, labda bia umepoteza authority ya kutetea source za watu wengine as "95% correct!"
Mkuu KM,
Hii ndio faida ya JF, kila mtu kuna jambo analijua zaidi kuliko wengine na tukiunganisha dots, tunapata jawabu la tatizo sugu.
Endeleeni kutuelemisha hayo ya hapo USA, maana kusingelikuwa na Watanzania huko, hapa tulishafungwa magoli mengi na mchanga kibao machoni.