Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Ama kweli Matanga yana kazi! Gombesugu bado linachezwa kutafuta mchawi huku waliojipatia mali wanapeta wafiwa wakitoana ngeu!
 
1.
FMES

Ubishe usibishe Mkuu jina lako liko juu hapa uwanjani,

Mkuu wangu Isaya,

Mara nyingi sana ninakuambia kuwa ninakuheshimu sana, sasa ukianza kwenda this low utashusha heshima mkuu, mimi sibishi anything, isipokuwa ninasimamia hoja yangu ya msingi kuwa ninaamini 100% kuwa Balali amefariki na amezikwa tayari na sababu zote nimezitoa tayari, lakini katika kutafuta ukweli nimekwama kwa 20%, nayo ni habari ya Hospital alipokwenda kutibiwa au kuwa-confirmed kuwa amekufa na siku hasa aliyofariki, hilo ninasema hapa mbele ya umma kuwa sijaupata ukweli wake, lakini ninauaminia ukweli wa 80% niliokwisha upata, na ninamheshimu anyone ambaye haaamini na niko tayari ku-debate in a good faith kwa the good of the people at large na ili nielimishwe zaidi.

2.
tunatamani kusikia unasema nini, usisahau wewe ni msomi mzuri, msaada wako kwetu unahitajika, tuko tayari kulala chali ili mladi umesema, tuko tayari kwa lolote, na tuko tayari kuamini kile unachokisema Mkuu. Baba tunapopata mkanganiko wa kimawazo toka kwenu ninyi wakuu wetu hapa jamvini, hakika meli inaweza kuyumba,sasa sisi tushike wapi?

Mkuu my record is very clear on dataz hilo wala sina wasi wasi nalo, my life always relies on credibility, kwa sababu mradi ninaoufanyia kazi na wazungu, unanifanya niwe kwenye credibility trap kila siku ya Mungu, ndio maana sina wasi wasi kabisa kuwa Balali amefariki, machahce ambayo hayajathibitishwa kwangu ninayaona kuwa sio major katika ukweli mzima, ndani ya hii forum ni kweli kuna ambao tumekuwa mstari wa mbele kwenye kuhesabiwa, na ndio maana tumekuwa hatulali kutafuta ukweli wa ishu, leo ndio kwanza nimepata dataz nzito kuhusu documents zilizoachwa na marehemu na mahali zilipo, lakini bado sijazithibitisha lakini I am working on it na ninaamini it is only a matter of time kabla sijajibu kitendawili kilichoabki on this ishu!

3.
Invisible na wewe(FMES) ndiyo mlituaminisha kifo cha baba yetu, sasa mara mnarukaruka, kwa kuwa Invisible yeye kasafiri hayupo tutaendelea kumsubiri ili aje atujuze zaidi kuliko!!!

Mkuu ya Invisible sijui, lakini ya kwangu ninayajua na nimeyasema wazi, kwa sasa nipo ninajaribu kumalizia kitendawili, lakini niliyoyasema ninayaamini 100% kuwa amefariki, baada ya uchunguzi wangu nilifikia mahali nikakaa chini na ku-brain storm the whole mess, mimi ninawa-hold responsible familia nzima ya Muganda for this mess, kwa sababu ninaamini they knew better, au they should have handled this thing better than they did na pia niwaambie wazi kuwa wanayoyafanya sasa hivi hawajiletei mema na wananchi na ni haki ya wananchi kuwashambulia kwa sababu wanayoyafanya sasa hivi ni un-necessary kabisaa, lakini inawezekana pia wana sababu za msingi kwa kufanya wanayoyafanya kwenye hilo time will tell,

Nimejiuliza maswali machache kama bina-adam mcha Mungu, na mimi kama baharia huwa siku zote ninaamini sana my instinct kwa sababu mabaharia wengi huwa tuna instinct kama za Chui na huwa tunaziamini sana, kwa sababu zimetuokoa sana huko majuu kwenye shughuli zetu, lakini nimefikia mahali nimekubali kuwa amekufa na alifia nyumbani kwake, alikuwa akiishia karibu na Watergate Apartment au Watergate Hotel, katika eneo wanaloishi kina Condi Rice ninaamini kuwa pale ni DC unajua huwa ninchanganyikiwa sana betweeen DC, Maryland na Springfield,

Ninawaomba tunaochangia hii topic tuweke zaidi vitu maana the feedback kutoka kwa wananchi nzito sana kuwa tunaelimisha taifa hapa!

Ahsante Mkuu
 
Mwanakijiji,
Unajua Utata tumeuzua sisi wenyewe hakuna chombo cha habari chochote kile ambacho kinaweza kuandika upupu kama huu wetu hapa.
1. Tumeambiwa Balali amefariki, tunataka ushihidi wakati sisi wenyewe hatuna ushahidi kuwa yu hai isipokuwa tunatafuta mchawi nje ya serikali inayohusika..hakuna mwingine isipokuwa Marehemu mwenyewe.
2. Katika picha zimetokelewakuna ile limo la kubeba maiti na wajuzi mnaweza kufahamu kwamba hilo gari hutoa maiti kule ilikohifanyiwa hadi kwenye mazishi na haiwezekani kabisa kuwepo na utaratibu huo kama hakuna kibali halali cha mfu, mahala gari hilo linapokwenda chukua maiti, kuishughulikia (make up) kwanza kabla ya kuilaza ktk jeneza na mengine mengi ambayo hayafanywi na familia ya marehemu iwe hata Mkewe. Hivi kweli serikali ya Marekani wanaweza kuingia kanyaboya kama hili!
3. Kuna ndugu za marehemu wamekuja hapa na hasira kubwa ya kuwaeleza mchawi nani leo mnakuja wakatisha tamaa kuwa wao ndiuo waongo!.. sababu ati hawakuionyesha maiti kwa wananchi wote wakati mtu kafia ugenini. Kwa desturi, kama hizi ndio maana waislaam hawaonyeshi maiti kwa sababu ya watu kama hawa hapa. Kinachowapeleka msibani ni UDAKU.. kujua maiti imeharibika kiasi gani, marehemu alikonda kiasi gani wengine watasema Duh, hata nywele zilimnyonyoka na kadhalika lakini yote haya yanamsaidia nini marehemu ama familia ya mfiwa!... ZERO..
4. Balozi wetu alikuwepo na wengine wengi ambao hakuna kati ya watu mnaowekea mashaka hamjajaribu kuonana nao na kuuliza maswala haya isipokuwa hapa kijiweni ambapo hakuna mtu aliyekwenda isipokuwa yule mmoja mnayemwekea mashaka pia. balozi hawezi ku report kwa rais wake false report huu ni ujinga mkubwa sisi kufikiria hivyo!
5. Familia ya wazazi wa Marehemu walikuwepo na hadi sasa hivi wapo ktk majonzi leo bado mnawawekea pia mashaka wao kama ilivyokuwa kifo cha Chifupa.
6. Na mwisho, amefia state gani haiwezi kuwa sababu kama marehemu kazikwa DC na walihudhuria watu mazishi hayo wengi wao wakiwa wageni nje ya viongozi wa serikali yetu. Ujumbe toka Ofisi mbali mbali za kimataifa ziliwakilishwa iwe kweli ulikuwa uongo hawa watu wakubali kuacha kazi zao kuhudhulia kanyaboya la Mama Muganda..basi huyu mama ana nguvu za ajabu sana.

Mkuu twendeni kwenye issue za muhimu, marehemu alikwisha hojiwa na hao TAKUKURU nushahidi wake sio lazima awepo yeye maanake inafahamika kuwa tayari kisha toa ushihidi wake. Kama kweli wangemtaka kisheria basi kesi nzima ingefunguliwa wakati akiwa nchini na ushahidi wake kusomwa lakini ni baada ya ushahidi wake aliiitwa Dodoma kuhusiana na ushahidi huo. From that day hakuwa salama kama alivyokuwa Amina Chifupa!..
Mkuu, kumbuka watu walifikiria mzaha ulipozungumzia hali yake, wachawi wakatafutwa... mara alikuwa na Ukimwi, wengine wakadai mwili wake wauone kuthibitisha kilichomuua. Tukaondoa kabisa dhana na machafu na dhulma ya serikali yetu..msiba huo ulipita kama ndoto, leo hatunaye na bado tumeshindwa kuwaweka wazi Mafisadi pamoja na kwamba list ipo mikononi mwa rais mwenyewe!..
How dump can we one be!... sisi kuendelea kutafuta wachawi nje ya circle inayohusiana na mabalaa yote haya!
Conclusion moja tu.. NDIVYO TULIVYO.
 
Kwa mawazo yangu nafiikiri hapa JF tumefungwa goli tena la offside na Mzee Mwanakijiji ndio aliliona hilo lakini washangiliaji walikuwa wamemzunguka kwa hiyo hata CCM walipofunga kwa kuotea yeye alikubali hilo goli kuweka mpira kati wakati Invisible alikuwa hata ameshindwa kuchukua mpira kutoka kwenye nyavu. Mkuu FMES alijaribu kumzuia referee lakini maji yalishamwagika sasa ni wakati wa kuwafuatilia wale ngedere waliokuwa wamekwenda London kuwakilisha their side of the story.

Bila kusahau SI's ambao wamelishwa peremende.
 
Mwanakijiji,
Unajua Utata tumeuzua sisi wenyewe hakuna chombo cha habari chochote kile ambacho kinaweza kuandika upupu kama huu wetu hapa.

Mkandara.. utata hatukuuzua sisi; wameuzua wao wenyewe. Kama Taarifa iliyopelekwa Ikulu na BoT inasema kuwa Ballali amefia Boston, halafu nyumba ya mazishi wanasema amefia DC, si haki kutalaumu sisi kwa utata huo.

1. Tumeambiwa Balali amefariki, tunataka ushihidi wakati sisi wenyewe hatuna ushahidi kuwa yu hai isipokuwa tunatafuta mchawi nje ya serikali inayohusika..hakuna mwingine isipokuwa Marehemu mwenyewe.
2. Katika picha zimetokelewakuna ile limo la kubeba maiti na wajuzi mnaweza kufahamu kwamba hilo gari hutoa maiti kule ilikohifanyiwa hadi kwenye mazishi na haiwezekani kabisa kuwepo na utaratibu huo kama hakuna kibali halali cha mfu, mahala gari hilo linapokwenda chukua maiti, kuishughulikia (make up) kwanza kabla ya kuilaza ktk jeneza na mengine mengi ambayo hayafanywi na familia ya marehemu iwe hata Mkewe.

Mzee mantiki yako hapo ni nzuri sana, the only thing you are missing ni motive gani inaweza kuwepo kwa mtu kufake kifo. Je mtu mwenye fedha nyingi akitaka kuigiza kifo anaweza, and to what extent atafanya hivyo? Has it been done before?

Hivi kweli serikali ya Marekani wanaweza kuingia kanyaboya kama hili!

Nafasi ya serikali ya Marekani kwenye misiba ni nini?

3. Kuna ndugu za marehemu wamekuja hapa na hasira kubwa ya kuwaeleza mchawi nani leo mnakuja wakatisha tamaa kuwa wao ndiuo waongo!.. sababu ati hawakuionyesha maiti kwa wananchi wote wakati mtu kafia ugenini. Kwa desturi, kama hizi ndio maana waislaam hawaonyeshi maiti kwa sababu ya watu kama hawa hapa. Kinachowapeleka msibani ni UDAKU.. kujua maiti imeharibika kiasi gani, marehemu alikonda kiasi gani wengine watasema Duh, hata nywele zilimnyonyoka na kadhalika lakini yote haya yanamsaidia nini marehemu ama familia ya mfiwa!... ZERO..

Point nzuri sana.. binafsi sioni kama hoja ya kuoneshwa mwili kwa public ni hoja yenye nguvu sana... lakini katika mazingira na wingu hili nadhani hoja ya an independent observer ambaye angesema ameona mwili wa Marehemu Ballali. Siku ya Jumanne familia ilipoenda kuview mwili pale DeVol funeral home nani ambaye hakuwa sehemu ya familia aliyepata nafasi ya kuona?

4. Balozi wetu alikuwepo na wengine wengi ambao hakuna kati ya watu mnaowekea mashaka hamjajaribu kuonana nao na kuuliza maswala haya isipokuwa hapa kijiweni ambapo hakuna mtu aliyekwenda isipokuwa yule mmoja mnayemwekea mashaka pia. balozi hawezi ku report kwa rais wake false report huu ni ujinga mkubwa sisi kufikiria hivyo
!

Mkandara, Ombeni Sefue kwa mara kadhaa huko nyuma na Ubalozi wake wameulizwa alipo Ballali na hawakujua; hata baada ya kifo uliza ni lini wao walipewa taarifa, na kama afisa yoyote wa Ubalozi alikuwepo siku ya Jumanne kwenye family viewing. Ombeni alitakiwa na serikali kwenda kwenye mazishi Ijumaa na familia walitoa mwaliko huo, lakini kama ni ushahidi basi ni shahidi wa Jeneza na ibada. Ombeni hajauona mwili wa Ballali.

5. Familia ya wazazi wa Marehemu walikuwepo na hadi sasa hivi wapo ktk majonzi leo bado mnawawekea pia mashaka wao kama ilivyokuwa kifo cha Chifupa.

Interested parties..
6. Na mwisho, amefia state gani haiwezi kuwa sababu kama marehemu kazikwa DC na walihudhuria watu mazishi hayo wengi wao wakiwa wageni nje ya viongozi wa serikali yetu. Ujumbe toka Ofisi mbali mbali za kimataifa ziliwakilishwa iwe kweli ulikuwa uongo hawa watu wakubali kuacha kazi zao kuhudhulia kanyaboya la Mama Muganda..basi huyu mama ana nguvu za ajabu sana.

Only if you knew what you actually said.

Mkuu twendeni kwenye issue za muhimu, marehemu alikwisha hojiwa na hao TAKUKURU nushahidi wake sio lazima awepo yeye maanake inafahamika kuwa tayari kisha toa ushihidi wake. Kama kweli wangemtaka kisheria basi kesi nzima ingefunguliwa wakati akiwa nchini na ushahidi wake kusomwa lakini ni baada ya ushahidi wake aliiitwa Dodoma kuhusiana na ushahidi huo. From that day hakuwa salama kama alivyokuwa Amina Chifupa!..

Una maana gani "from that day hakuwa salama"?

Mkuu, kumbuka watu walifikiria mzaha ulipozungumzia hali yake, wachawi wakatafutwa... mara alikuwa na Ukimwi, wengine wakadai mwili wake wauone kuthibitisha kilichomuua. Tukaondoa kabisa dhana na machafu na dhulma ya serikali yetu..msiba huo ulipita kama ndoto, leo hatunaye na bado tumeshindwa kuwaweka wazi Mafisadi pamoja na kwamba list ipo mikononi mwa rais mwenyewe!..

Mkandara hakuna watu wenye uwezo wa kufanya lolote, to go to unimaginable lenght to cover a crime. Wanadamu ndivyo walivyo. Na hakuna watu ambao wana hatari ya kufanya lolote kama walio madarakani au wenye nafasi nyeti ambazo zinatishiwa na ukweli. They are capable of wiping out whole communities if need be.

Kama Ballali is a victim of such people or if he perceived the gravity of the threat posed to him.. ana haki na sababu ya kufanya lolote lile kukwepa mikono ya watu hao. Na njia pekee ni ya kifo.

How dump can we one be!... sisi kuendelea kutafuta wachawi nje ya circle inayohusiana na mabalaa yote haya!
Conclusion moja tu.. NDIVYO TULIVYO.

Mzee kilichotokea BoT si jambo dogo, ni sisi tunaliona dogo lakini kama lingetoka Federal Reserve ya US, au Benki Kuu nyingine yoyote leo hii ingekuwa mshike mshike wa ajabu. Hivyo, Ballali siyo tu ni mtu muhimu lakini naffasi yake katika sakata zima imechanganyika mno kiasi kwamba siyo tu a player but also a victim. Na naamini at the end he discover he was more the later than the former.
 
Nilikuwa na maana hospital alikokuwa amelazwa, kisha tukaambiwa karudi nyumbani hali yake iliendelea vizuri na baadaye atarudi TZ kutoa ushahidi.. yote haya hamkuyawekea mashaka isipokuwa leo mliposikia amekufa!..
Yaani mnadai kujua zaidi kuhusu maiti kuliko alipokuwa hai as if kutabalisha kitu.. sasa kama hii sio NDIVYO TULIVYO nini hasa!

Mkandara,

Je hata hiyo hospitali aliyokuwa amelazwa ni hospitali ipi? Kama una taarifa tafadhali tujulishe. Wengine hatujui labda kama una taarifa ambayo sisi wengine hapa hatuna. Haijawahi kujulikana Ballali alilazwa hospitali gani toka alivyotoka TZ.
 
Mwanakijiji,
Labda nami nitumie mtindo wenu pamoja na kwamba umechagua pale unapotaka kuongeza swali badala ya kujibu hoja zangu..
Well nianze hili:-
Mkandara.. utata hatukuuzua sisi; wameuzua wao wenyewe. Kama Taarifa iliyopelekwa Ikulu na BoT inasema kuwa Ballali amefia Boston, halafu nyumba ya mazishi wanasema amefia DC, si haki kutalaumu sisi kwa utata huo
Utata wenu ni wapi Balai amefia au ni Balali kafa kweli? maanake sioni report mbili hizo zilizotolewa zikisema amekufa na nyingine ikisema hakufa..Kama report imeenda Ikulu na kusema amefia Boston kwani huyo aliyeipeleka hawezi kufanya makosa na Familia ikarekebisha hilo. Swala ni Balali amekufa au hakufa au sio, mengine yote ni uzushi unaotokana na dhana yenu.
Mzee mantiki yako hapo ni nzuri sana, the only thing you are missing ni motive gani inaweza kuwepo kwa mtu kufake kifo. Je mtu mwenye fedha nyingi akitaka kuigiza kifo anaweza, and to what extent atafanya hivyo? Has it been done before?
.. bado wewe hujanipa motive katika maelezo yako. Mtu mwenye fedha nyingi sana yuko salama zaidi Marekani labda iwe anatafutwa na serikali ama vyombo vya kimataifa.. Balali hakuwa mmoja wa hao watu Kisha kama ni kukimbia Mafia bado ushihidi upo ktk mashirika ya usafiri, airport na pengine passport yake kutumika.
Kama serikali yetu inamhitaji basi ni wao wanaotakiwa kuweka mashaka ya kifo hiki kwa sababu kinawaweka ktk hali mbaya zaidi. Ushahidi wa Balali Upo TAKUKURU na kule Dodoma alikokwenda kujieleza.. sasa Balali wa nini kama aliweza kuondoka salama sehemu zote mbili. Mwenye fedha hakimbii starehe hata siku moja na kama imewahi kutokea basi ni kwa wale waliopewa maficho na serikali za majuu..
Nafasi ya serikali ya Marekani kwenye misiba ni nini?
Nafasi ya serikali ya Marekani nakuomba soma maelezo yangu hapo juu kuhusiana na kibao cha kifo ambacho ni lazima kiwepo kabla hujakubaliwa mazishi..Hii ikiwa ni pamoja na clearance toka hospital kuhusiana na kifo cha huyo mtu.
Point nzuri sana.. binafsi sioni kama hoja ya kuoneshwa mwili kwa public ni hoja yenye nguvu sana... lakini katika mazingira na wingu hili nadhani hoja ya an independent observer ambaye angesema ameona mwili wa Marehemu Ballali. Siku ya Jumanne familia ilipoenda kuview mwili pale DeVol funeral home nani ambaye hakuwa sehemu ya familia aliyepata nafasi ya kuona?
Wewe ulitaka nani awepo ambaye ungemwamini zaidi!... member wa JF wote sio wakazi wa DC na pengine hawana uhusiano na marehemu. Hata kama wangealika watu hasa toka JF mtu kama mimi nisingeenda bado mngeuliza mbona Mkandara hakwenda....kuna kitu hapa. Kama ni wewe wangezua jingine kuwa umelipwa fedha nyingi sana na Mama Muganda.
Mkandara, Ombeni Sefue kwa mara kadhaa huko nyuma na Ubalozi wake wameulizwa alipo Ballali na hawakujua; hata baada ya kifo uliza ni lini wao walipewa taarifa, na kama afisa yoyote wa Ubalozi alikuwepo siku ya Jumanne kwenye family viewing. Ombeni alitakiwa na serikali kwenda kwenye mazishi Ijumaa na familia walitoa mwaliko huo, lakini kama ni ushahidi basi ni shahidi wa Jeneza na ibada. Ombeni hajauona mwili wa Ballali.
Mkuu mbona unazungusha hapa! linmi ubalozi wamepewa taarifa haiwezi kabisa kuingiliana na mashaka ya kifo. Mara ngapi watu wamekufa na Ubalozi wamepewa habari mwisho mwisho, na kuna wengine hata Ubalozi hawakufahamishwa...Ni lini Balozi alitakiwa kuuona mwili ili kuhakikisha kifo kimetokea. Je, unataka kusema kuwa hata Sefue ameingizwa mjini?.. mbona yeye ndiye mwenye ukaribu sana na familia ya inayokisiwa? au ndio Sefue pia yupo kundi moja na Balali, Mkapa na wengineo kukimbia upepo. Maanake sielewi wanamkimbiza mafichoni kwa kitu gani haswa ikiwa Mkpa mwenyewe tumesha ambiwa tumwache mzee wa watu. My point ni kwamba ku view maiti sio big deal at all na binafsi nimewahi kufanya hivyo sii zaidi ya mara tatu maisha yangu yote..haipunguzi imani ama ukweli wa kifo. Basi nadhani hata Ditopile yawezekana yuu hai ulipata kuuona mwili wake.
Only if you knew what you actually said.
Mkuu waliohudhulia mazishi yale sii Wabongo tu huyu mama hawezi kuwafunga kamba watu wote kwa fedha gani?... Nguvu gani aliyokuwa nayo kuweza kuwapanga watu hadi makaburini ili kuficha ukweli wa kifo cha mmewe.. come now mkuu vipi hata familia ya wazazi wa marehemu wanunuliwe kwa kitu gani hasa!..
Ebu nambie wewe unafikiri Balali kajichimbia akikimbia kitu gani hasa!..hao wachunguzi waliokwenda Marekani? kuna uhakika gani kama hawa walikuwa wametumwa na serikali licha ya hapo sio mara ya kwanza wao kwenda US.
Una maana gani "from that day hakuwa salama"?
Mkuu wanaojua habari za Balali wanafahamu aliumwa toka alipotoka Dodoma na swala la sumu lilijuilikana mapema sana isipokuwa halikuzungumzwa kama vile Amina Chifupa..
Mkandara hakuna watu wenye uwezo wa kufanya lolote, to go to unimaginable lenght to cover a crime. Wanadamu ndivyo walivyo. Na hakuna watu ambao wana hatari ya kufanya lolote kama walio madarakani au wenye nafasi nyeti ambazo zinatishiwa na ukweli. They are capable of wiping out whole communities if need be.
Kama Ballali is a victim of such people or if he perceived the gravity of the threat posed to him.. ana haki na sababu ya kufanya lolote lile kukwepa mikono ya watu hao. Na njia pekee ni ya kifo.
Sijakuelewa hapo! Binadamu wenye akili timamu hutafuta criminal baada ya crime kutokea, sasa kama kifo cha Balali ni crime as it is hapo mnaweza kwenda kokote. Hao viongozi unaowasema pamoja na kutishiwa bado nyie macho yenu yapo kwa Balali sio viongozi yaani focus yote mnajaribu kuiondoa toka kwa viongozi the real suspects na kuipeleka kwa maiti.. Ushahidi upo Takukuru, viongozi waliokuwepo Dodoma na baadhi ya watu ambao wameomba muda kuhakikisha haki inapata nafasi yake. Kote huko kuna ushahidi tosha ambao umekaliwa kuficha ukweli. Msiyaone yote haya ila mnatafuta mchawi hapa kuficha ubaya wa serikali yetu. Awe amekufa ama hakufa, hili swala bado liko wazi kabisaaa! Balali sio evidence anaweza kuwa shahidi kama tutaweza fungua mashtaka.. hadi leo nani kafungua?... hakuna wakati report tunazo mikononi.
Mzee kilichotokea BoT si jambo dogo, ni sisi tunaliona dogo lakini kama lingetoka Federal Reserve ya US, au Benki Kuu nyingine yoyote leo hii ingekuwa mshike mshike wa ajabu. Hivyo, Ballali siyo tu ni mtu muhimu lakini naffasi yake katika sakata zima imechanganyika mno kiasi kwamba siyo tu a player but also a victim. Na naamini at the end he discover he was more the later than the former.

Mkuu kwa mtaji huu swala la BoT linaonekana dogo sana isipokuwa Balali ndiye swala..siku zote crime hutazamwa kilichotokea act na sio mtu aliyetenda kwanza hilo ni swala la baadaye mahakamani.. Up to this moment hakuna mashtaka yoyote hivyo wapuuza ni sisi wenyewe. Yaonyesha wazi kuwa fedha zile ziliondoka benki kuu kihalali isipokuwa walishindwa kurudisha mikopo hiyo!... nani aliyekuwa akiidhinisha mikopo hatujui nini hatua za kwanza kupata mikopo iole hajtujui..leo hii Balali ni mkisiwa baada ya kufa tena basi sio mhusika mkuu isipokuwa shahidi na wapo wengi pale BoT wanaweza kutoa ushahidi kama wa Balali nani kawatafuta!
 
Ndugu zangu bado tunaufuatilia huu mjadala kwa karibu sana.

Ila naona sasa mjadala huu unaelekea kusikotakikana.
Ni maoni yangu tu.

Nilishatabiri jf kugawanyika kuhusu something which was about to come in regard to corruption scandals.
Naona kabisa kuwa ni wazi kuna wanao engineer hii movie.

Ma main producers na ma actors wako kazini.
Sitaki kusema mengi sana ila naomba nikumbushe jambo moja....

Ninashangazwa sana kuona watanzania wengi bado ni mambumbu wa kisiasa!
Huu mjadala ni wazi umeanza kugawanyika alongside party lines...As in CCM vs Upinzani na pia kuna uwezekano wa inflictions kwenye kambi hizo pinzani za chama tawala na vile vyama mbadala.

Taratibu na kwa masikitiko makubwa...Mjadala huu pia umeanza kuwa kama vile ni kituko flani hivi!
Kuna watu ambao wanadhani kuwa Ballali alikuwa kama raia wengine tu wa kawaida na kwa hiyo kama ni wanandugu pekee wameuona mwili hiyo inatosha kwasababu hata mazishi ya watanzania wengine hufanyika hivyo na hakuna anayelaumu! Hizi sasa ni siasa!

Issue ya Ballali kwa niaba ya wale tunaoona eye to eye..Isitugawanye kwenye misingi ya kivyama,kujuana na ama ushabiki na urafiki!

Hii ni issue ambayo kila Mtanzania yuko entitled to know about!Matter of fact..In details as they see fit!
Nawapa pongezi kina MWK na MKJJ kwa kubadili mawazo.

Field Marshall nasikia wewe ni CCM na hivyo ndio maana naona pia unashindwa kujua ni upande upi ni sahihi..Licha ya kwamba unaelekea kubase kwenye kauli zako za 100% belief on Ballali's death.

At the same time unaonekana kussuport kwa kiasi fulani uwezekano wa Ballali kuwa hai.

Hapo nashindwa sana kuelewa...Halafu ni mara nyingi mijadala imegeuka na kuwa personal kiasi cha kuanza kuwachosha wananchi wengi wasomaji wanaofuatilia hii issue kwa ukaribu kiasi kwama wameingiwa na wasiwasi mkubwa na mara nyingi wamejaribu kukwambia kwa kuanza kutanguliza heshima zao based on how the know you ever since they've joined JF.

Naomba pia niwashukuru wale wote walioko upande wa wazalendo!

Kuna watu kadhaa ambao wanauliza maswali kiasi cha kwamba na mimi naonelea niwe tu mwangaliaji ama msomaji kama wananchi wengine!

Maswali amabo yanatuwakilisha wananchi wazalendo...Watu kama kina Mtanzania, Kuhani Mkuu,Mchelea Mwana, Gaijin, Bubu, Isaya Mwita, Mwalimu Moshi,Kitila Mkumbo, Chakaza, Field88, Mama Paroko....Hawa ni baadhi tu lakini kuna wengineo wengi ambao ninaamini kuwa wakisimamia upande wa wazalendo kama wanavofanya hivi sasa basi tutaupata ukweli hapa hata iweje!

Halafu kuna wale ambao wanakaa pembeni na kuchagua magrupu na kusubiri muda wa kujibu posting na kuanza kuwakatisha wengine tamaa!

Kuna ndugu yangu alinilaumu kwa kusema eti natumia sijui serch engine gani!?

Sasa mimi nina tofauti gani na mwananchi wa kawaida?
Mimi sina mikonnection ya kuweza kuzipata hizo nyeti za Ballali..Mimi ni kama watanzania wenzangu ambao nao pia walizipata habari hizi kupitia hapa jf.

Na kutokea mwanzo nilipingana hapa vikali na MKJJ na MWK..Na kutokea mzozo kiasi cha mimi kufikiria kuwa ni rupia imepenyezwa na mafisadi!

Baada ya kugeuza kwao mawazo...Na mimi kama binadamu nikaonelea ni muhimu kuwapa binadamu wenzangu the benefit of doubt!

Sasa kama Mungu ataendelea kutupa uzima...Then ni wazi kuwa wazalendo will emerge victourious!
 
kwa nini tunaishi kwenye speculations tu? kuna mwana JF ambaye amesema anajua watu waliomuua Balali(which means anajua kuwa Balali amekufa, otherwise asingezungumia watu waliomuua), kwa nini jitihada zisiwe kwenye kumuomba mwenzetu huyu athibitishe kwa manufaa ya wana JF walio na shaka na kifo hicho?
Au tunapenda maisha ya kwenye speculations?
 
Kwani tatizo ni kwamba amekufa au hajafa? Kwangu mimi hoja kuwa amekufa haina mashaka sana.. na hoja kuwa yawezekana hajafa haina msingi zaidi. Lakini zote mbili zina implication yake na kwangu ndio hasa kiini cha mjadala huu.

Jmushi... mimi sijabadili mawazo yangu kuhusu lolote kwani sikuwahi kutoa mawazo yangu kuhusu jambo hili.
 
MKJJ mawazo yako yanajulikana toka mwanzo kuwa Ballali apewe kinga..Na msimamo wako wewe mwenyewe baada ya wewe mwenyewe kutangaza kifo chake ni kuwa Ballali alitakiwa kupewa kinga.

Naomba tusiingize siasa na tuwe honest...Maana hizo kauli zako hapo juu zinapingana na nyingine ulizopost previously...Ambazo umeonekana uki question baadhi ya legitimacy ya issue zinazodai kuwa Ballali kafa.

Angalia MWK alivyopata support kubwa ya wana jf baada a kuweka wazi kuwa yuko upande wa wananchi..Upande uliogubikwa na mashaka kutokana na mazingira halisi ya kifo hicho pamoja na kesi nzima ya EPA!

Kitendo chako cha kusema hujabadilisha mawazo kimenishtua kidogo.
 
MKJJ mawazo yako yanajulikana toka mwanzo kuwa Ballali apewe kinga..Na msimamo wako wewe mwenyewe baada ya wewe mwenyewe kutangaza kifo chake ni kuwa Ballali alitakiwa kupewa kinga.

Once again.. huchukui muda kufuatilia kitu. Kwanini nilipendekeza Ballali apewe kinga? Of course you don't why unless you take a wild guess.

Naomba tusiingize siasa na tuwe honest...Maana hizo kauli zako hapo juu zinapingana na nyingine ulizopost previously...Ambazo umeonekana uki question baadhi ya legitimacy ya issue zinazodai kuwa Ballali kafa.

No sir, I have not.

Angalia MWK alivyopata support kubwa ya wana jf baada a kuweka wazi kuwa yuko upande wa wananchi..Upande uliogubikwa na mashaka kutokana na mazingira halisi ya kifo hicho pamoja na kesi nzima ya EPA!

mmh.. usilolijua ni kama usiku wa kiza.

Kitendo chako cha kusema hujabadilisha mawazo kimenishtua kidogo.

I have noticed.. unashtushwa na vitu visivyoshtusha kwa sababu havifit kwenye chupa ya mawazo uliyowaweka watu fulani. Hautakuwa wa kwanza..
 
jmushi1,
Hao upande wa wananchi unaozungumzia hapa ni upi maanake sijaona watanzania kwa wingi wakitaka kujua kama Balali amekufa ama yuu hai!..
Mkuu hiki ni kijiwe na mara nyingi watu huanzisha mada kutokana na jinsi wanavyojisikia wao. Haiwakilishi mtu yeyote isipokuwa inaweza kujenga imani yoyote ile iwe positive ama negative. lakini pamoja na yote hayo ni ujinga kwetu kuanza kukubali jambo kwa sababu tu hakuna ushahidi.. Hii ndio janja ya viongozi wetu kila siku kuwaondoa watu kwa sababu ushahidi wa kiafirka ni mtu..NMdio tunawaona hao kina Mama Simba wakija kwa jeuri kutaka mtu asimame kuonyesha ushahidi hali akifahamu fika kwamba hakuna mtu mwenye ushahidi huo isipokuwa serikali yenyewe..

Mimi siku base maelezo yangu ktk dhana yoyote inayohusiana na kifo cha Balali isipokuwa nakubali kilichosemwa kisha naangalia mbele..nataka kuiona hiyo report ya EPA kama imekwisha kamilika pia report ya madini inachukua sura gani mpya..Kikubwa kushinda yote ni kuhakikisha CCM wanaondoka coming 2010.. sina sababu ya kuwatetea tena.
Nachojaribu kufanya hapa ni kuweka fikra zetu ktk maswala muhimu yanayohusiana na Balali awe kafa ama mzima kwangu haibadilishi kitu kwani MAFISADI bado wapo na wanatesa kishenzi. Ushahidi tunao wakutosha na ndio maana hata swala lka Richmond hatukumhitaji yule mhindi kuwepo nchini kutoa ushahidi kufikia Lowassa kujiuzuru.
Uzalendo wetu utazidi kukomaa na kujenga UMOJA ikiwa tutahitaji zaidi kuwajibishwa kwa viongozi walioweka mkataba wa Richmond badala yake tunarushiwa changa la macho na kusahau yaliyoko mbele yetu. Balali is gone, he is history, now ni kitu gani tulichabakia nacho ambacho kitatupeleka kule tunakohitaji kwenda!..
Nitarudia kusema I don't care who Balali was! wamesha pita kina Rutihinda kwa story kama hizi yaani naona kama history inajirudia (Dejavu) na haikufanyika kitu. sasa hivi ni mageuzi kuondoka kwa gavana wa benki haiwezi kuwa sababu ya kuturudisha nyuma iwe kajificha sijui ama yuko Kaburini... paperwork hazikuzikwa zipo kuweza kusimamisha kesi, unless unataka kunambia hatuwezi kushinda vita hii bila Balali ambaye wewe mwenyewe hufahamu yupo kundi gani...
Akiwa upande wa mafisadi ndio kabisa hawezi kutusaidia akiwa hai kwa sababu he is among the sangara. Akiwa upande wa serikali na shahidi tunayemhitaji then nambie ni lini serikali hiyo imemtaka kutoa ushahidi?..
Hapa mkuu tunafukuza kivuli... nasema hivi wamekufa wengi wenye nguvu kuliko Balali na hamkutaka kuuliza kitu! Siku JK ameondoa heshima ya visa yake Marekani kama kiongozi ndio uheshimiwa ulitoka siku hiyo hiyo, hivyo Balali amekufa kama sisi wengine isipokuwa alikuwa shahidi muhimu sana kwetu wananchi.
 
Field Marshall nasikia wewe ni CCM na hivyo ndio maana naona pia unashindwa kujua ni upande upi ni sahihi..Licha ya kwamba unaelekea kubase kwenye kauli zako za 100% belief on Ballali's death.

Eti ninashindwa kujua upande upi ni sahihi, lakini nimesema wazi kuwa ninaamini kuwa Balali amefariki kwa 100%? Halafu kwa nini mimi ndio ishu wakati wewe mwenyewe husemi unachoamini na sababu zake? Kama umeamua kuamini maneno ya MMJ na MWK then kwa nini usiseme unachoamini kuliko kujaribu kurukia jina langu bila sababu ya msingi?

Hivi jamani hiki ninachosema sio kiswahili lugha ya taifa letu kuwa ninaamini 100% kuwa Balali amefariki na amezikwa tayari! Mushi vipi mkuu unasema maneno kurasa nzima unachosema hakieleweki vipi bro? Mbona ulipooongea kwenye Radio na MMJ uilionekana una akili sana mkuu kuliko unapoandika?

Mnachotaka kwangu ni nini hasa? Msimamo wangu nimeusema wazi kuwa ninaamini kwa 100% kuwa Balali amefariki na amezikwa tayari, sasa exactly unachojaribu kuniambia hapa ni nini? What my party political affiliaton has to do na msimamo wangu au my belief on this ishu? Unasema umaesikia kuwa mimi ni CCMkama vile ni siri au dhambi?

Ngoja nikuambie sasa kuwa mimi ni mwanachama wa CCM damu, now do you have a problem with that? Halafu haya maneno yenu yasiyokuwa na research on this ishu msiyaunganishe na credibility au state ya JF, JF has absolutely nothing to do misimamo ya wachangiaji wa hii topic, ila ifike mahali wananchi tujifunze kusimama tuhesabiwe, badala ooh FMES amesema, oooh MMJ amesema, No stand up na sema unachotaka kusema, Balali amekufa sbabau zangu one two three, au Balali hajafa sababu one two three, lakini haiwezekani ikawa ooh FMEs ooohhh MMJ,

Mkandara heshima mbele kwa kusimama na kuhesabiwa, bila matusi wala kejeli au viroja, hoja hujibiwa kwa hoja, na ninashukuru kuwa unasimama kwa unachoamini badala ya kufuata upepo tu!
 
Imani yangu imeongezeka maradufu...mpaka sasa bado:

1. Naamini Balali hajafa.

2. Naamini alikuwa raia wa USA.

3. Naamini siku moja tutakuja kujua ukweli...
 
Kwani tatizo ni kwamba amekufa au hajafa? Kwangu mimi hoja kuwa amekufa haina mashaka sana.. na hoja kuwa yawezekana hajafa haina msingi zaidi.

Mushi hii ni quote ya Mkulu MMJ, ni kipi usichoelewa hapa mkuu? Ujumbe wangu kwa viongozi wa Tanzania mnaohusika na hiki kifo na kufikiri kuwa sasa mmepona, labda tuwamegee tu kuhusu dataz kidogo, kutoka kwa dataz nzito tulizonazo,

The dataz ni kwamba pamoja na sehemu zote ambazo marehemu aliacha documents zinazowahusu, kuna ambazo ziko mikononi mwa wajumbe wa Congress ya USA, sasa the dataz ni kwamba wao wanasubiri itakapofikia Tanzania kupewa zile hela za Bush na ule mkopo maalum wa mamillioni ya dola ambao uliahidiwa kwa Mkulo majuzi, ndio mtakiona cha moto, wale wote mliohusika in one way or another,

Siwatishiii nyau, ila ninaamini mnazo akili za kutosha kujua the seriousness ya hizi dataz, maana hamuwezi kufanya uhuni wenu mpaka US, kama mlifikiri kuwa mna akili sana kama za kumwagia waandishi tindikali sasa subirini the fallout,

ndugu yangu Muuungwana sikia hiyo mwanangu kutoka kwangu FMES!
 
sasa na wewe tuambie umefanya nini zaidi tu ya kuweka logic
Need I say the least that logic is the base of reasoning and unless you're illogic you'll never use incredible sources to testify Ballali's death? Sources Sources Sources; you came here testifying Ballali died in DC, does your sources more credible than JKs' who said Ballali died in Boston when sending condolences to Ballali's family? Do you want me to give benefit of doubts!
maana unaona Mtanzania, anaweka hoja kwa nini haamini kuwa Balali hajafa
You mean this?
Mtanzania said:
Ukifuatilia kwa karibu utagundua sources za Invisible, Tanzania Daima, Mbowe, Jasusi, FMES zinatoka sehemu moja, juu kabisa ya mti amekaa mke wa Ballali.
By the way, since I register (Aug. 2007) I've never change my membership nor register another name, only JS. The problem is you think all members will accept what you say and whenever one disagree you jump to a conclusion that is the one disagree previous. My brother/sister, no one is after your credibility and no one even know who you are! We are all trying to contribute despite of whether will converge to same point on not. If we do not converge then someone has to admit instead of calling other opinions NONSENSE!
 
Back
Top Bottom