Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

1.
ii)Huwezi kukataa kwamba wewe ni miongoni mwa watu waliosababisha confusion na shaka kuhusu kufa kwa Balali. Mimi binafsi hii ilikuwa ni mara ya kwanza kuona umeleta dataz mbili tofauti ndani ya kipindi kifupi kabisa: moja ikikanusha habari za Invisible kuhusu kufa kwa Balali na ingine ikihibitisha kwamba Balali kafa! Hatujamzoea FMES wa namna hii. FMES tunayemjua hapa JF ni yule ambaye huzifanyia kazi dataz zake kwanza kabla ya kuzimiwaga na akishakuzimwaga huwa zinabaki hivyo na huthibitika hivyo. Sasa mkuu ulitaka kweli watu tusi-question incosistency ya posts zako mbili?

Mkuu Kitila,

You are too big for this lows, ninaletaje confusion wakati hoja zangu ziko clear kuwa ni kwa nini nimesema one au two, nilikataa kutokana na dataz nilizokuwa nazo, lakini nilipomaliza tu kusema hapa, dada yangu ambaye ni member pia hapa akanipigia simu na kunifahamisha kuwa amealikwa kwenye msiba na maziishi, na haya nimeyasema wazi sikuyaficha,

Nikafanya uchunguzi na nikasema wazi ni kwa nini nimefikia conclusion kuwa niaamini 100% kuwa amefariki, the matter of fact nilikuwa so sure na dataz za kufariki kwake mpaka nikawa mtu wa kwanza ku-despute tarehe ya kifo na mahali alipofia, na nikawa pia mtu wa kwanza kusema wazi kuwa hakufia kwenye nyumba yake zya Bethesda kama wengi walivyokuwa wakiamini kuwa alikuwa anaishi huko, ni kwa mara ya kwanza nimeleta habari kuwa alinunua nyumba mahali tofauti na Bethesda, alipikuwa anarudi bongo kuwa gavana na nikasmea mpaka location yake kuwa ni karibu na Watergate Hotel au Watergate Apartments, mahali panapoitwa Foggbottom niktaja mpaka majirani zake ni kina Condy Rice na Bob Dole,

I mean kweli kuna anything unclear kwenye hizi dataz kwamba mtu a conclude kwamba mimi ni part ya mduara fulani wa serikali wa kuuwa viongozi na kuwadanganya wanannchi on it?
 
1.


Sasa mkuu nilitegemea utakuwa mstaarabu na ku-apologise kwa kunisngizia maneno mazito ambayo huna ukweli kabisaa mkuu, ninasema hivi hizi accusations zako ni majungu na uongo, pia ni uzandiki na very irresponsible tena kwa mtu kama wewe, kuni-place kwenye kikundi fulani cha Conspiracy Thoeries za "kuua viongozi wa serikali ili kuficha uozo wake"[/B] unasema ni kutofautiana kimawazo? Ni kuwa na independent in thinking? Ni kuwa objective? Ni kutofikiri ndani ya box lako mkuu? Unasema this is not personal?


Mkuu ninasubiri utoe facts za kunihusisha na mduara wa watu wanaoua viongozi wetu, kama huna kubali na useme kuwa huna facts ila uliyajenga majungu, uzandiki, na uongo against me bila ya kuwa na ukweli hata mmoja, sidhani kama hili ni gumu kulifanya kwa mtu kama wewe!

Ahsante Mkuu! [/SIZE]


...Interesting. Mkuu, naona umeamua kuandika yako. Uzuri hapa JF record huwa zinatunzwa na kujitunza zenyewe. Ok, nionyeshe basi kwenye posts zangu ni wapi nilisema hayo maneno uliyosema hapo (bolded and highlighted in blue colour)?

Mkuu naona umeamua kuja na vitisho vya kutosha. Hata hivyo, ujue tu kwamba wengine tulishapita huko, hatutishwi tena! Narudia tena kuwa wewe ni miongoni mwa watu hapa JF waliochang'anya watu kuhusu habari za kifo cha Balali. Ulikanusha mara ya kwanza kuwa Balali hajafa na mara ya pili ukaja kuthibitisha kuwa amekufa, same person, same place here in JF. Upo kwenye mduara wa kutudanganya kuhusu ukweli wa kuugua na kufa kwa Balali. If you think saying this is criminal, as you said in your post, as a responsible citizen, you know what to do when a felllow citizen commits criminal offence.
 
Naanza kuamini maneno ya Jmushi kuwa wale tuliuokuwa tunawategemea kuwa wanaweza kutuongoza au vioo kwenye JF wamefika mahali sasa hatuna imani nao tena. There is something fishy going on here. Wana JF wake up
 
1.


I mean kweli kuna anything unclear kwenye hizi dataz kwamba mtu a conclude kwamba mimi ni part ya mduara fulani wa serikali wa kuuwa viongozi na kuwadanganya wanannchi on it?

FMES, huu mtindo unaotumia ulitumiwa sana enzi za kueneza ukomunisti ambapo viongozi wa serikali za kikomunisti walikuwa wanatumia propaganda kama hizi kuzima dissenting opinion. Watu walikuwa analishwa maneno ili waonekane wabaya mbele za macho ya wananchi wenzao. Hata hivyo, kwa sasa hivi propaganda kama hizi haziwezekani kwa sababu ya teknolojia. Sasa ni wapi mimi nimesema hayo maneno? Post yangu unayo-quote katika kujenga hoja zako inasema vingine lakini unaendelea kuhitimisha kwamba mimi nimesema hayo maneno niliya-quote hapo juu. Inabidi nikuulize, lengo lako hasa ni nini? Ni propaganda ua una zaidi?
 
Unasema balozi Sefue aliuona mwili, kweli una uhakika na hiyo statement? Kuna watu walihudhuria hayo mazishi na wanasema hakuna aliyeuona mwili hapo. Hata statements mbalimbali zilizotolewa zilisema hakutakuwa na kuuona/kuuaga mwili zaidi ya kuliaaga jeneza ambalo lilikuwa limefunikwa.

Now ninakusikia mkuu, kwanza ninaomba niseme hivi ninaamini kuwa wote mnaopinga kuwa hakufa hamtumwi na mtu yoyote ila ni mawazo yenu tu ambayo ni independent, ninategemea kuwa this should work equally kwetu members wote hapa JF, kwamba hatutumwi na mtu yoyote unless kuna ushahidi unaoonyesha kuwa kuna mtu anatumwa na wengine!

Pili nisingeweza kusema kuwa Balozi Sefue ameuona mwili, wakati sina uhakika, ambayo ninauhakika nayo on this ishu nimeyaesema wazi na pia ambayo sina uhakika nayo nimesema wazi, kuwa bado sina uhakika:-

1. Hospitali aliyowahi kulazwa marehemu akiwa hai, au ambayo ilitumika baada ya kifo chake au mahali popote ulipopelekwa mwili baada ya kifo kwa uchunguzi.

2. Mwanakijiji, ambaye ninamuheshimu sana kwenye idara ya investigations na dataz, bado tunatofautiana kwenye tarehe au siku ya kifo,

Ninasema tena kuwa sasa hivi niko very close na kukamilisha hizi two ishus, ambazo tayari ninazo dataz zake, ila ninahitaji kuthibitisha tu kwa sources mbali mbali kitu ambacho sio rahisi kama inavyoonekana, na siwezi kuweka hapa bila kuwa 100% sure si unajua jinsi nitakavyoshambuliwa, otherwise ningekuwa nimeshaweka wazi hapa, lakini nitakapohakikisha nitaweka wazi,

Kuhusu Balozi Sefue na kuuona mwili bado ni too early kuweka hapa on how it happened, lakini nimektumia kwenye PM maana nisije nikaharibu source zangu za info, kuhusu Jasusi na nachosema sijui kabisaa mimi ninafanya uchunguzi wangu bila ya kumuhusisha yeye wala any member wa hapa, ila ninaamini kuwa yeye anajua 100% kilichotokea, na kwamba amekubali kuwa dataz zangu ziko 95% kweli, kwa hiyo I am still working kumalizia the other 5%,

Otherwise, tunaendelea kukata ishu kwa sababu tunaelimisha na kuelimishana pia in the process, kwa ndugu zangu wengine ninasema hivi kwenye maisha hatuwezi kuchagua au kuamua nini kitokee na nini kisitokee, lakini yakitokea ni lazima tupambane nayo, najua kuwa this thing is getting too tiring kwa some, lakini kwa the furture record ni lazima sisi wananchi wa sasa tuweke record straight kwa ajili ya the future generations.

Ahsante Wakuu!
 
ni wazi kwamba FMES alikuwa amesaulika katika ule mduara wa waliokuwa wanapika uongo kuhusu kuugua na kifo cha Balali.

Mkuu Kitila,

Haya ni maneno yako mwenyewe, au? Anyway sina mpango wa kulumbana na wewe on this! Kama kwa kujaribu kukuuuliza ukweli wako on this ni kuwa Communist na kuwa na makubwa zaidi, basi mkuu umeshinda ninakupa hiyo. Unajua kama ninavyosema siku zote watu ninaowaheshimu kama wewe huwa sina malumbano nao sana.
 

Mkuu Heshima mbele,

Sikujua kuwa ndani ya hii forum kuna viongozi, nilijua kuna wamiliki na sisi members wachangiaji ambao tuko huru kufikiri na kutoa maoni yetu kwa hoja,

Eti kumbe wewe ulikuwa unanittegemea mimi? ni wapi uliwahi kusema hayo? Eti huna imani na mimi kwa sababu ninaamini 100% kuwa Balali amefariki? Ila una imani na wale anaosema hakufariki?

Kwa hiyo ili uniamini na niwe kiongozi wako hapa JF ni lazima niseme siamini kuwa Balali amefariki? Ndiyo standards mnazotaka kuzianzisha hapa? JF i-Wake up on what? ni lini watu hapa walilazimishwa kukubali wasiyotaka? mkuu acha unafiki hapa tunatka objectiveness, na hoja kama watu hawana kuna walionazo na ni haki ya kila mtu hapa kuzi-dispute hoja anazoona hazina ukweli waka elimu kwa watu hapa, sasa nashangaa kwako wewe kuwaomba JF waamke una maana watu walikuwa wamelala hapa JF, samahani mimi sio part ya hao waliokuwa wamelala! Tatizo ni kuwa wewe na wenzako hamtaweza hata siku moja kuharibu jina langu iwe hapa au huko kwingne nje ya hapa kwa sababu mlichojaa ni unafiki na siasa za bongo hamzijui, ni hoja nzito tu zneye ukweli ndio zitaendela kusimama hapa, sio majungu, unafiki na uongo, na hapa JF hatuwezi kukubali tunachokikataa kutoka serikalini ambacho wewe na wenzako mnajaribu kukiweka hapa,

Kuna wananchi wengi sana wanaokuja kujifunza hapa mambo serioua ya siasa yetu na wengi wao mambo ya makazini mwao, na kila siku wanantutumia ujumbe kwa pembeni kuwa wanafajirika, sasa mnakuja kutokea watu wachache hapa wenye tamaa za umaarufu bila hoja amabcho ndio hsa uti wa mgongo wa Jf, ni hoja nzito na ukweli, sio majungu, uongo na unafiki kama huu wako mkuu! Wote mtalegea na kuharibikiwa, huku mimi nikiendele akuweka hoja na dataz hapa, naona toka niwatwange last week mnahangaika sana, na inasikitisha kwamba mmeanza hata kuwa-corrupt watu niliokuwa ninawaheshimu sana hapa, ninazo habari zote mkuu wewe unanionaje, ila kumbuka tu kuwa mnahangaika bure, commitment yangu ni kwa wananchi na taifa langu, ndio maana kama umegundua siku hizi niliacha kabisa kuongelea vyama vya siasa, taifa mebele na wananchi wenzangu, I hope mtafanikiwa na hizo sifa mnazo zitafuta kwa nguvu, lakini labda niwatahadharishe wasiowajua kuwa nyinyi ni watu wahatari sana tunawajua maana hata wake zenu wanalia sana!

Msimamo wangu kuhusu kifo cha Balali ni 100% kuwa amefariki, wako ni upi mkuu?
 
Tujikumbusheni tulikotoka!....I'm fed up na siasa.
Kwa wale mnaoishi DC kwa nini msiende ST. Stephen Martyr Church mkajaribu kufanya uchunguzi wenu kuhusiana na kuonyeshwa kwa mwili wa marehemu!.

WAKUU wa Serikali na vigogo ndani ya Chama Cha Mapinduzi wanahaha kutokana na kashfa nzito ya wizi wa mabilioni Benki Kuu (BoT), na sasa wanafanya kila liwezekanalo ili kuwakinga baadhi ya watuhumiwa wa moja kwa moja wasianikwe hadharani, Raia Mwema imeambiwa.
Hali hiyo inatokana na ukweli kwamba kama yote yatakuwa yamesemwa na kuwekwa hadharani, kuhusu nani wamehusika, basi sura za vigogo kadhaa serikalini na ndani ya CCM zitakosa pa kujificha.
"Sasa kuna shinikizo kwamba watakaokwenda kuhojiwa na tume ya Rais wasitaje baadhi ya majina yaliyohusika katika kashfa hii, majina ambayo yanajitokeza mara kwa mara katika kushiriki wizi huu mkubwa ndani ya BoT," mmoja wa wanachama wakongwe wa CCM ameiambia Raia Mwema.
Lakini kwa mujibu wa ofisa huyo, suala hilo limeleta mgawanyiko mkubwa ndani ya chama chenyewe, huku baadhi wakisema wahusika wawajibike kwa madhambi yao kama yatadhihirika mbele ya vyombo vya sheria ili chama kisije kuathirika.
" Hilo ni suala ambalo linaendelea ndani ya CCM sasa, tena mpaka hata katika ngazi za juu kabisa za Kamati Kuu, ambako kuna wanaotaka mtu aliyehusika awajibike na wengine ambao wanataka mambo haya yazimwe," anaongeza ofisa huyo.
Raia Mwema imefahamishwa pia kwamba baadhi ya watu, watuhumiwa na wasio watuhumiwa katika wizi huo, wamekuwa wakitafadhalishwa wasitaje jina la kigogo mmoja ndani ya CCM ambaye kwa kupitia kampuni ya kughushi, alishiriki kikamilifu kuchota mabilioni ya fedha ambazo sasa inaaminika ziliingia katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2005.
"Hata kabla ya baadhi yao kuitwa mbele ya Kamati aliyoiunda Rais Jakaya Kikwete kuchunguza wizi huo wa BoT, wamekuwa wakipelekewa ujumbe mahsusi kwamba watakapokuwa mbele ya Kamati, wasitaje jina la kigogo huyo.
"Wameelezwa wataje majina ya wafanyabiashara wawili wenye asili ya Asia ili ionekane kwamba hawa ndio pekee waliochota fedha hizo. Na wanaambiwa kwamba wafanyabiashara hao kwa sasa wako tayari kuchukua mzigo huo badala ya kigogo huyo.
"Mmoja kati ya wafanyabiashara hao wanaotajwa kuchukua mzigo wa kigogo huyo ni Jeetu Patel, mwenye kumiliki kampuni tisa ambazo zimetajwa wazi katika wizi huo na ambaye tangu suala hili litangazwe na Serikali yuko nje ya nchi," anasema ofisa huyo akiongeza kwamba mwingine ni mfanyabiashara wa Dar es Salaam ambaye yuko karibu na CCM na ambaye mara kadha amejitosa kutaka kuwa mgombea ubunge.
Vyanzo mbalimbali vya habari vinaeleza kwamba wingu kubwa limetanda kuhusiana na utendaji wa Kamati ya Rais Kikwete inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu Johnson Mwanyika na kufanya baadhi ya watu wajiulize iwapo kweli ukweli wa kashafa hiyo utakuja kufahamika katika mazingira ambayo dola inashiriki kutaka kuficha ukweli kuhusu wahusika wakuu.
Baadhi ya wachunguzi wa masuala nyeti kama haya wameiambia Raia Mwema kwamba hakuna cho chote ambacho Serikali na CCM wanaweza kukiokoa kwa kuweka shinikizo ili baadhi ya wahusika wasitajwe katika uchunguzi.
"Wanachofanya ni kuahirisha tu tatizo. Kesi kubwa katika suala hili si wingi wa fedha hizi na wala si nani alihusika, bali tatizo ni kwamba hawa watu walighushi nyaraka. Kwa vyovyote vile kughushi nyaraka ni kosa zito na upelelezi ukifanyika sawasawa, hatimaye hao ambao wanataka kusafishwa sasa watajikuta wakitajwa na kusutwa na nyaraka.
"Kama kweli kuna utashi serikalini, kama ambavyo Rais Kikwete alijaribu kuonyesha wakati wa kutangazwa kwa hatua dhidi ya wizi ndani ya BoT, basi hakuna namna ila kuliacha suala hili liishe bila Serikali wala CCM kuingilia ili hatimaye wahusika wapatikane," anasema mtoa habari wetu.
Raia Mwema imeambiwa pia kwamba jitihada hizo zinazoendelea zimeigusa pia familia ya aliyekuwa gavana Dk. Daudi Ballali ambayo imepelekewa ujumbe kuwaomba wamwambie Dk. Ballali anyamaze.
"Wamekwenda mara mbili na mara zote wamefikisha ujumbe kwamba wanataka wawasiliane na ndugu yao (Dk. Ballali) Marekani ili afunge mdomo wake. Nimeambiwa kwamba familia imechanganyikiwa.
"Wao kama wanafamilia hoja sasa ni kaka yao apone, lakini mara wanapelekewa ujumbe kwamba dola haitaki azungumzie kokote suala hilo la BoT. Hawaelewi maana ya yote haya ni nini. Na tukumbuke kwamba hawa ni Watanzania tu wa kawaida, ujumbe kama huo lazima utawachanganya," anasema mtoa habari huyo.
Bado Dk. Ballali hajaweza kusema lolote, lakini taarifa za waliokuwa karibu naye zinasema kwa jinsi anavyohisi amechafuliwa, wakati ukifika atasema ili asafishe jina lake.
"Huko aliko anasononeka. Haohao ndio waliokuwa wakimshinikiza alipe yale mabilioni. Na hata alipojaribu kubisha ili taratibu za malipo zifuatwe aliambiwa alipe. Sasa wamekwisha kumtumia hata hawazungumzii afya yake ambayo si nzuri. Wanataka ikiwezekana anyamaze moja kwa moja," anasema mmoja wa watu wa karibu na Dk. Ballali ambaye, kutokana na sababu zinazoeleweka, ameomba asitajwe.
Kwa sasa Dk. Ballali anaelezwa kuwa nchini Marekani na bado ana nia ya kurudi Tanzania pamoja na kuwa siku hasa haijulikani hasa kwa kuwa Serikali ya Marekani imetangaza kumfutia viza yake.
Ubalozi wa Marekani nchini, wiki hii umetoa taarifa ukijivua kuwajibika kumrejesha nchini Dk. Ballali kwa maelezo kwamba jukumu hilo kwa sasa ni la Serikali ya Tanzania.
Lakini baada ya viongozi wote wa juu wa CCM kukanusha hadharani kuhusika kwa chama hicho tawala, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, amesema kwamba CCM haihusiki moja kwa moja katika sakata la BoT pamoja na kwamba upo uwezekano wa watu binafsi ndani ya CCM kuhusika.
Kutoka Dodoma inaelezwa kwamba Wabunge wameitaka serikali kuwasilisha bungeni ripoti kamili ya ukaguzi wa BoT, hiyo ikiwa baada ya Waziri wa Fedha, Zakia Meghji kuwasilisha bungeni taarifa ya kuelezea hatua za serikali kuhusu ukaguzi huo.
Hata hivyo Spika Sitta amewaeleza wabunge kwamba ofisi yake imekua na mawasiliano na serikali kuhusu suala hilo.
Wakati hayo yakiendelea, gazeti la The Citizen la Jumamosi, Januari 26, 2008 liliandika kuhusika kwa watu wazito ndani ya serikali na likieleza majina ya kampuni za Excellent Services Limited na Clyton Marketing Limited bila kutaja majina ya wakurugenzi wake.
Hata hivyo, vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na gazeti la serikali la Kiswahili la Habari Leo lilitaja wakurugenzi wa kampuni hizo na kuainisha jinsi zilivyosajiliwa na kupanda kwa mtaji wake.
Kwa mujibu wa habari hizo ambazo zimethibitishwa na Msajili wa Makampuni (BRELA), wakurugenzi wa Excellent Services yenye makao yake Sokoine Drive, Namba 11649, waliomo ni pamoja na Emmily Samanya, Peter Sabas, Levis Msiko, Elisifa Ngowi na Massimo Faneli, ilipoanzishwa 2004 kwa mtaji wa Sh 500,000/- kabla ya mtaji kuoanda hadi kufikia milioni 50 mwaka 2005.
Kumbukumbu za BRELA na magazeti zimewataja wakurugenzi wa Clyton Marketing Limited, iliyosajiliwa Juni 6, 2005 kuwa ni pamoja na Edwin Mtoi na Elisifa Ngowi. Anuani ya kampuni hiyo ni Plot Namba 707, Mkwepu Dar es Salaam.
"Mmoja kati ya wakurugenzi katika makampuni hayo mawili (anamtaja jina) anatajwa kuwa mkurugenzi mwandamizi na mwenye nguvu katika Idara ya Usalama wa Taifa na amekuwa humo kwa muda mrefu akiwa karibu sana na Mkurugenzi Mkuu aliyestaafu, Cornel Apson," anaeleza ofisa mwandamizi serikalini na kuendelea:
"...(anamtaja jina) amekua katika kitengo kinachofanya kazi ya kupambana na uhalifu ikiwamo ugaidi, rushwa, biashara ya fedha haramu na uhalifu mwingine wa kimataifa, jukumu linalomsogeza karibu zaidi na kamati iliyoundwa na Rais kuchunguza sakata la BoT."
Wakati hayo yakiendelea, kamati hiyo imekwisha kuanza kuwahoji kwa kina wamiliki wa makampuni 22 yanayotajwa katika sakata la BoT huku ikielezwa kwamba nyaraka zote za makampuni hayo zimechukuliwa kutoka BRELA.
Kwa mujibu wa habari hizo nyaraka hizo hasa baada ya kupatikana kwa makampuni yaliyodaiwa kutosajiliwa zimechukuliwa na kamati iliyoundwa na Rais na hakuna mwenye nafasi ya kusoma majalada hayo kwa sasa.
Makampuni ambayo nyaraka zake zilikosekana ni pamoja na G&T International Limited, ambayo imefahamika kumilikiwa na Octavio Timoth na Beredy Malegesi, ambaye anaelezwa kuwa shahidi muhimu katika sakata hilo na huenda "akazibwa mdomo," kwa mujibu wa vyanzo vya habari ndani ya serikali.
Kampuni nyingine ambayo nyaraka zake zimeonekana ni Changanyikeni Residential Complex Limited inayomilikiwa na Jose Vander Merwe, Samson Mapunda na Charles Mabina ikiwa na makao yake, Sinza, Kumekucha, Dar es Salaam.
Sakata la BoT, linaiweka CCM katika mtego mkubwa kutokana na kuhusishwa kwake moja kwa moja na matumizi ya fedha hizo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, lakini viongozi wake wamekanusha madai hayo.
Sasa inafahamika kwamba sehemu kubwa ya fedha ikiwamo zile zilizotokana na kampuni iliyoghushi nyaraka ya Kagoda Agricultural Limited (KAL) iliyochota Sh bilioni 40/- ziliingia katika uchaguzi huo kupitia wana CCM maarufu waliokua katika harakati za kampeni ya Jakaya Kikwete.
Fedha hizo na nyingine ziligawiwa kwa baadhi ya wabunge kwa viwango vilivyotofautiana, na nyingine zilipotea ama kuibwa kutokana na kutokuwapo utaratibu rasmi wa udhibiti na uhakiki wa fedha kitaalamu.
Kwa ujumla sakata zima limemuelemea Dk Ballali ambaye pamoja na kuhusika kwake, ana siri nzito inayoweza kuibua kashfa ya aina yake katika historia ya siasa za Tanzania kama si ya kimataifa.
Pamoja na maelezo kwamba Dk. Ballali alifanya malipo yenye utata kutokana na wakuu wake wa kisiasa kushinikiza, sakata hiyi nzima iliwahusisha watendaji wa BoT na wana CCM maarufu, bado hakuna kati yao anayetajwa wala kuitwa na kamati ya uchunguzi
 
Siko peke yangu karibu na Ukweli!....

Mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, Jaji Joseph Warioba akizungumzia kifo hicho cha Dk. Ballali wiki hii, ameiambia Raia Mwema kwamba anaona unafiki wa hali ya juu katika matamshi na matendo ya wanasiasa.
"Huu ni unafiki mkubwa. Muacheni Ballali apumzike kwa amani. Kwanza walimwita ni fisadi, sasa wanasema shahidi muhimu amekufa. Katoka kuwa fisadi wakati wa uhai kuwa shahidi katika mauti," alisema Warioba katika mahojiano ya simu mwanzoni mwa wiki hii.
Aliongeza Warioba: "Amekuwa kafara. Taarifa ya Serikali kuhusu fedha za EPA ilionyesha wazi Ballali amechukuliwa hatua katika utaratibu wa kawaida wa kuwajibika. Haikumtuhumu kwamba alikuwa ameiba fedha. Fedha zile bilioni 133 ni jumla ya fedha zote zilizochukuliwa na kampuni 22 zilizotajwa katika taarifa ya Serikali.
"Ballali hakutajwa katika orodha ya kampuni hizo. Hilo Serikali inajua, viongozi wa siasa wanajua na vyombo vya habari vinajua. Lakini wote hao, kwa kipindi chote alichokuwa hai walimhukumu kama mtu aliyekuwa ameiba fedha. Lakini waliochukua fedha zile wanafahamika.
"Kwa muda wa miezi mitano Kamati (ya uchunguzi wa kashafa ya EPA) imekuwa ikiwaambia wananchi inakusanya fedha hizo kutoka kwa watu wanaoitwa. Ilipoulizwa kuhusu Ballali ilisema haimuhitaji. Maana yake hakuwamo katika orodha ya waliochukua fedha zile. Lakini sasa amefariki wimbo umebadilika. Wanasiasa na vyombo vya habari vinamwita si fisadi tena, bali shahidi muhimu wa wizi wa EPA.
"Huu ni unafiki mkubwa. Kuna visingizio kwamba ugonjwa wa Ballali haujulikani, lakini Serikali inajua kwani alikuwa analipiwa matibabu na Benki Kuu. Alikuwa Boston, Marekani, ile nchi iko wazi mtu angetaka kujua angejua. Lakini sasa wanasiasa na vyombo vya habari vinalalamika kwamba ugonjwa wake ulifanywa siri. Kumbe ni uzembe wao.
" Sasa tumeanza kutafuta mchawi huku. Na hapa ikisha kutamkwa neno fisadi tu, basi hata kama mtu hana ushahidi unakuwa fisadi. Lakini yote haya hakuna anayekuambia Ballali aliiba kiasi gani. Wamuache apumzike kwa amani, siku moja ukweli utafahamika."
 
Mkuu FMES,

Inabidi niseme wazi kwamba nakuamini kwa data nyingi na pia kwamba hata kwenye suala hili la Ballali umenisaidia kuelewa mengi. Aidha ni kwamba tunaelewana vizuri kwenye 99% ya mambo yanayotokea hapa JF.

Kwenye hili la Ballali naamini tofauti na source zangu zingine zimeweza kunisaidia kujua
kwamba baadhi ya data ulizotoa sio sahihi.

Siamini yafuatayo:

1. Siamini Ballali kafa, ushahidi wote uliopo hautoshi kunifanya niamini kafa.
2. Siamini tunajua Ballali alilazwa hospitali gani na mji upi.
3. Sio kweli kwamba balozi Sefue alionyeshwa mwili wa Ballali alipoenda kuhudhuria
mazishi. Isingeliwezekana yeye aonyeshwe wakati watu wengine waliokuwepo
wasione.
4. Sijui Ballali alikufa lini na wapi kama kweli amekufa.
5. Siamini Ballali alilishwa sumu, naamini ilikuwa sababu tu ya kutoroka TZ.


Baadhi ya mambo hapo juu ni rahisi mno kupata majibu yake lakini naamini hatuwezi kupata majibu kwasababu hayo majibu kama ni ya kweli yatatufanya tugundue huu udanganyifu mkubwa dhidi ya Watanzania.

Labda hapa ni kukubali kutofautiana. Kwasisi ambao hatuamini, basi tuendelee kuchunguza na kutafuta ukweli mpaka tutakapojiridhisha kama kweli kafa au tunadanganywa. Kama data zaidi zitapatikana kuonyesha Ballali kafa, basi nitakuwa wa kwanza kubadilika ila kwa sasa naona sababu za kuamini hajafa ni nyingi zaidi.
 
Siko peke yangu karibu na Ukweli!....

Mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, Jaji Joseph Warioba akizungumzia kifo hicho cha Dk. Ballali wiki hii, ameiambia Raia Mwema kwamba anaona unafiki wa hali ya juu katika matamshi na matendo ya wanasiasa.
“Huu ni unafiki mkubwa. Muacheni Ballali apumzike kwa amani. Kwanza walimwita ni fisadi, sasa wanasema shahidi muhimu amekufa. Katoka kuwa fisadi wakati wa uhai kuwa shahidi katika mauti,” alisema Warioba katika mahojiano ya simu mwanzoni mwa wiki hii.
Aliongeza Warioba: “Amekuwa kafara. Taarifa ya Serikali kuhusu fedha za EPA ilionyesha wazi Ballali amechukuliwa hatua katika utaratibu wa kawaida wa kuwajibika. Haikumtuhumu kwamba alikuwa ameiba fedha. Fedha zile bilioni 133 ni jumla ya fedha zote zilizochukuliwa na kampuni 22 zilizotajwa katika taarifa ya Serikali.
“Ballali hakutajwa katika orodha ya kampuni hizo. Hilo Serikali inajua, viongozi wa siasa wanajua na vyombo vya habari vinajua. Lakini wote hao, kwa kipindi chote alichokuwa hai walimhukumu kama mtu aliyekuwa ameiba fedha. Lakini waliochukua fedha zile wanafahamika.
“Kwa muda wa miezi mitano Kamati (ya uchunguzi wa kashafa ya EPA) imekuwa ikiwaambia wananchi inakusanya fedha hizo kutoka kwa watu wanaoitwa. Ilipoulizwa kuhusu Ballali ilisema haimuhitaji. Maana yake hakuwamo katika orodha ya waliochukua fedha zile. Lakini sasa amefariki wimbo umebadilika. Wanasiasa na vyombo vya habari vinamwita si fisadi tena, bali shahidi muhimu wa wizi wa EPA.
“Huu ni unafiki mkubwa. Kuna visingizio kwamba ugonjwa wa Ballali haujulikani, lakini Serikali inajua kwani alikuwa analipiwa matibabu na Benki Kuu. Alikuwa Boston, Marekani, ile nchi iko wazi mtu angetaka kujua angejua. Lakini sasa wanasiasa na vyombo vya habari vinalalamika kwamba ugonjwa wake ulifanywa siri. Kumbe ni uzembe wao.
“ Sasa tumeanza kutafuta mchawi huku. Na hapa ikisha kutamkwa neno fisadi tu, basi hata kama mtu hana ushahidi unakuwa fisadi. Lakini yote haya hakuna anayekuambia Ballali aliiba kiasi gani. Wamuache apumzike kwa amani, siku moja ukweli utafahamika.”

Mkandara,

Unajua kwamba kwenye haya ya Ballali, Jaji Warioba ni katika wale ambao wangeumbuliwa kwenye Meremeta? Ana kila haki ya kusema tumwache apumike salama. Wako wengi kwenye hilo kundi.
 
Tujikumbusheni tulikotoka!....I'm fed up na siasa.
Kwa wale mnaoishi DC kwa nini msiende ST. Stephen Martyr Church mkajaribu kufanya uchunguzi wenu kuhusiana na kuonyeshwa kwa mwili wa marehemu!.

Mkandara,

Wala watu hawahitaji kwenda sasa, walikuwepo kwenye tukio. Labda walitupiwa changa la macho lililowafanya wasione wakati eti akina Sefue na maboss wa IMF wanaona.
 
Wakuu FMES, Kitila, Mkandara na wengine,

Tunatofautiana kwenye hili jambo lakini naomba isigeuke kuwa personal.

Kuna watu wengi sana hapa wana imani kubwa na nyie wakongwe wa JF na hoja zenu nyingi zinasomwa kama njia ya kupata ukweli.

Tuendeleze kukata ishu kwa kuandika tunayoyaamini bila kushambuliana. Lazima tujifunze kwamba kutofautiana kwa hoja sio uadui.

Baadhi ya maandiko niliyoyasoma hapo juu yamenisikitisha sana. Tafadhali acheni hizo hasira na turudi kukata ishu na kutafuta ushahidi juu ya hili jambo lililo mbele yetu.

Asanteni.
 
1
. 1. Siamini Ballali kafa, ushahidi wote uliopo hautoshi kunifanya niamini kafa.

Kwenye hili tuko ukurasa mmoja mkuu kuwa wewe huamini na mimi ninaamini 100% kuwa amefariki.

2.
2. Siamini tunajua Ballali alilazwa hospitali gani na mji upi.

Kwenye hili nimesema kuwa nina raw dataz bado sijazisafisha na kuzithibitisha, lakini uko right.

3.
. Sio kweli kwamba balozi Sefue alionyeshwa mwili wa Ballali alipoenda kuhudhuria mazishi. Isingeliwezekana yeye aonyeshwe wakati watu wengine waliokuwepo wasione.

Hili siwezi kuligusa sana, zaidi ya kusema kuwa walikuwepo watu karibu 100 kwenye kanisa na mazishi, kulikuwa na utata mkubwa wa balozi na maofisa kukubaliwa kwenda kwenye msiba, lakini dakika ya mwisho wakakubaliwa na sababu nzito ya msingi ilikuwa Balozi kwenda kuhakikisha kwa kuuona mwili, walioruhusiwa ni watoto wa marehemu, wakuu wa IMF, na Balozi Sefue,

Ambaye hata kabla hajaondoka pale you could tell kuwa alikuwa anapeleka ujumbe wa simu mahali kwa haraka sana baada tu ya kuuona, lakini sina mpango wa kukulazimisha on this, na siwezi kama nilivyokuambia kusema nimezipataje hizi maana nita-compromise source.

4.

4. Sijui Ballali alikufa lini na wapi kama kweli amekufa.

Kwenye hili mimi nimesema kuwa amefariki nyumbani kwake hilo nina uhakika 100%, lakini tatizo lipo kwenye siku mimi ninaamini kuwa alifariki Jumapili, lakini ninakuelewa kuwa huamini ni sawa kabisa mkuu!

5
. 5. Siamini Ballali alilishwa sumu, naamini ilikuwa sababu tu ya kutoroka TZ.

Mimi ninaamini hili kwa sababu hata kabla haijasemwa wazi nilishaongea na viongozi wa mwisho kuwa naye Dodoma, ambao walimuona akilalamika kuhusu maumivu ya tumbo kwa mbali, niliwakatila kata kata kuwa wanosema ni uongo, juzi wameniuliza vipi? nikawambia niko speechless!

lakini ninaheshimu pia mawazo yako ya kutokubali!
 
Mkuu Mtanzania,
Mwenye kuwekea shaka ni wewe na wanasiasa wengine, hivyo nadhani mahala pa kuanzia ni hapo kanisani. Unaweza kupiga simu ukajifanya kachero ama sehemu ya kuorodhesha vifo toka Tanzania ukitaka uhakika wa kifo cha Balali na pengine kuulizia Mchungaji aliyeendesha misa hiyo ili akupe confirmation ya mwili wa Balali. Pia kuna mahala nakumbuka niliona picha ya limo likiuchukua mwili wa Marehehmu hiyo pia wachungujzi wenyeji wa DC wanaweza kufahamu hilo gari lilikuwa limeegeshwa wapi mkafuatilia. Halafu, pia mnaweza kulitazama kwa makini mkajua ni kampuni gani iliyotumika kukodishwa ikafuatiliwa pia kujua wao waliuchukua mwili huo toka wapi kwenda wapi?..Ndio spy game zenyewe mnakuja na ushahidi wenu labda mnaweza kutubadilisha na sisi wengine tuliokuwa kizani. Sina haja ya kukuhakikishia kitu maadam naamini hakuna maiti inayozikwa Marekani bila kibali cha kifo..
Usitegemee serikali yetu kufanya lolote wakati toka mwanzo hili swala lilikuwa gumu kwao.
Mkuu Warioba hata kama amehusika na hiyo Meremeta kasema ukweli kwamba majina ya kampuni zinazokisiwa yanajulikana na kama yumo basi anakubali kuwepo ktk kundi lakini haihusiani na kifo cha Balali.. jina la Meremeta bado lipo kama washtakiwa. Serikali ilikana kuwa Balali hahusiki wala hakuna kampuni hata moja inayomhusisha yeye.
Kumbuka tena mwanzo wa hoja hii ya EPA wengi wenu humu mlisema Balali ni FISADI, sisi wengine tulisha pima kutokana na habari zilizotangulia kuwa Balali ni shahidi mkubwa wa wananchi. Nakumbuka mada hiyoi ilikuwa ndefu sana na kundi kubwa lilikuwa Balali ni Fisadi tu, Kafa sasa mnaanza kugawanyika wengine fisadi wengine mnakubali ni shahidi na hasa serikali inayojaribu kuonyesha kwamba hakuna kitu kitakachowezekana kuendelea bila Balali kuwepo. Iwe ni deal la serikali kupotosha wananchi kwa kumficha ama kweli wamemuua lakini ukweli utabakia kuwa kesi ya EPA bado ipo na sasa hivi imechukua sura nzito zaidi. Ushahidi upo, uchunguzi wa Ernst & Young upo, mahojiano ya Balali na TAKUKURU yapo, sasa hicho kifo cha Balali tunakihitaji cha nini?..
Nionavyo mimi humu kuna wana siasa wengine ambao sasa badala ya kuhoji swala la EPA wanajiingiza ktk mkenge wa serikali kuhusiana na kifo cha Balali.. amefichwa hakufichwa won't help us anything kwa sababu Balali ni raia tu kama sisi kesha vuliwa Uheshimiwa wake pale JK alipoondoa visa yake. Na kama kweli hawa wanasiasa wangekuwa na uchungu kama wanaouonyesha leo hii bila shaka wangefuatilia utata huu tuliokuwa nao leo kwa karibu zaidi kuhakikisha shahidi huyu haingii mitini.
Na hata baada ya yote hayo bado mnayo nafasi kama wanasiasa kutafuta ukweli zaidi kwa njia zenu ikiwa mnaona Balali ndiye haswa anayehitajika.
Mkuu nimesoma mada aliyoanzisha Lunyungu inayohusu Balali kuumbua viongozi! hapo ndipo nilipotoa kipande hiki cha Warioba, na kuna mwanasheria kazungumza mengi kuhusiana na waraka aliouacha marehemu Balali - Tazama , lakini nimeona mtazamo wa wengi humu kuwa hamkuchangia kitu... maneno yaliyosemwa humo ni mazito sana na yenye kutupa picha zaidi lakini kwa udanganyifu wenu mnataka tu tuongeleee kifo cha Balali!...Hata wakuu wangu kina Dr.Slaa wamezamia ktk hoja inayohusiana na kifo wakati the real deal EPA inahalalishwa kifo kuliko Balali mwenyewe.
Why, hadi sasa hivi nakuna kichwa!
 
Mkuu Bob,

Wabunge wengi wanasema in private kuwa kuwepo au kutokuwepo kwa Balali, hakupunguzi wala kuongeza anyhthing, wanasema kuwa ushahidi upo wa kutosha on EPA na waliohusika, na wanashangaa kwa nini imekuwa a big deal wakati siku zote wao wanajua kuwa kila kitu kipo, why Balali?

Kwa maoni yangu ni kwamba inaonekana kuwa kuna viongozi fulani wenye tatizo na kuwepo kwa Balali, nina dataz za yote yaliyofanyika usiku wa kuamkia siku ya kupigwa kwa Lowassa bungeni, mbinu walizozitumia kina Lowassa, Almeir, Makamba, na Chenge, kuacha badhi ya wabunge waliowarubuni pia, siwezi kuwa-rule out on anything,

Lakini hili la EPA halikwepeki, wabunge wanayo majina yote ya mawaziri na viongozi walishiriki sasa either wawapige wazi au waogope, lakini kusingizia Balalai ni unafiki wa viongozi wetu, halafu pia bado hatujui kama Balalai anahusika na maovu au hapana, lakini ninasema hivi serikali ya bongo kama kweli haiwezi kuficha forever mambo yaliyofanyika US, kama walishindwa kuzuia ya Richmonduli itakuwa haya!
 
Mkuu Mtanzania,
Mwenye kuwekea shaka ni wewe na wanasiasa wengine, hivyo nadhani mahala pa kuanzia ni hapo kanisani. Unaweza kupiga simu ukajifanya kachero ama sehemu ya kuorodhesha vifo toka Tanzania ukitaka uhakika wa kifo cha Balali na pengine kuulizia Mchungaji aliyeendesha misa hiyo ili akupe confirmation ya mwili wa Balali. Pia kuna mahala nakumbuka niliona picha ya limo likiuchukua mwili wa Marehehmu hiyo pia wachungujzi wenyeji wa DC wanaweza kufahamu hilo gari lilikuwa limeegeshwa wapi mkafuatilia. Halafu, pia mnaweza kulitazama kwa makini mkajua ni kampuni gani iliyotumika kukodishwa ikafuatiliwa pia kujua wao waliuchukua mwili huo toka wapi kwenda wapi?..Ndio spy game zenyewe mnakuja na ushahidi wenu labda mnaweza kutubadilisha na sisi wengine tuliokuwa kizani. Sina haja ya kukuhakikishia kitu maadam naamini hakuna maiti inayozikwa Marekani bila kibali cha kifo..
Usitegemee serikali yetu kufanya lolote wakati toka mwanzo hili swala lilikuwa gumu kwao.
Mkuu Warioba hata kama amehusika na hiyo Meremeta kasema ukweli kwamba majina ya kampuni zinazokisiwa yanajulikana na kama yumo basi anakubali kuwepo ktk kundi lakini haihusiani na kifo cha Balali.. jina la Meremeta bado lipo kama washtakiwa. Serikali ilikana kuwa Balali hahusiki wala hakuna kampuni hata moja inayomhusisha yeye.
Kumbuka tena mwanzo wa hoja hii ya EPA wengi wenu humu mlisema Balali ni FISADI, sisi wengine tulisha pima kutokana na habari zilizotangulia kuwa Balali ni shahidi mkubwa wa wananchi. Nakumbuka mada hiyoi ilikuwa ndefu sana na kundi kubwa lilikuwa Balali ni Fisadi tu, Kafa sasa mnaanza kugawanyika wengine fisadi wengine mnakubali ni shahidi na hasa serikali inayojaribu kuonyesha kwamba hakuna kitu kitakachowezekana kuendelea bila Balali kuwepo. Iwe ni deal la serikali kupotosha wananchi kwa kumficha ama kweli wamemuua lakini ukweli utabakia kuwa kesi ya EPA bado ipo na sasa hivi imechukua sura nzito zaidi. Ushahidi upo, uchunguzi wa Ernst & Young upo, mahojiano ya Balali na TAKUKURU yapo, sasa hicho kifo cha Balali tunakihitaji cha nini?..
Nionavyo mimi humu kuna wana siasa wengine ambao sasa badala ya kuhoji swala la EPA wanajiingiza ktk mkenge wa serikali kuhusiana na kifo cha Balali.. amefichwa hakufichwa won't help us anything kwa sababu Balali ni raia tu kama sisi kesha vuliwa Uheshimiwa wake pale JK alipoondoa visa yake. Na kama kweli hawa wanasiasa wangekuwa na uchungu kama wanaouonyesha leo hii bila shaka wangefuatilia utata huu tuliokuwa nao leo kwa karibu zaidi kuhakikisha shahidi huyu haingii mitini.
Na hata baada ya yote hayo bado mnayo nafasi kama wanasiasa kutafuta ukweli zaidi kwa njia zenu ikiwa mnaona Balali ndiye haswa anayehitajika.
Mkuu nimesoma mada aliyoanzisha Lunyungu inayohusu Balali kuumbua viongozi! hapo ndipo nilipotoa kipande hiki cha Warioba, na kuna mwanasheria kazungumza mengi kuhusiana na waraka aliouacha marehemu Balali - Tazama , lakini nimeona mtazamo wa wengi humu kuwa hamkuchangia kitu... maneno yaliyosemwa humo ni mazito sana na yenye kutupa picha zaidi lakini kwa udanganyifu wenu mnataka tu tuongeleee kifo cha Balali!...Hata wakuu wangu kina Dr.Slaa wamezamia ktk hoja inayohusiana na kifo wakati the real deal EPA inahalalishwa kifo kuliko Balali mwenyewe.
Why, hadi sasa hivi nakuna kichwa!
You're speaking the language! Go on Mkandara or else this should be closed, frankly!
 
Mkuu Kitila,

Haya ni maneno yako mwenyewe, au? Anyway sina mpango wa kulumbana na wewe on this! Kama kwa kujaribu kukuuuliza ukweli wako on this ni kuwa Communist na kuwa na makubwa zaidi, basi mkuu umeshinda ninakupa hiyo. Unajua kama ninavyosema siku zote watu ninaowaheshimu kama wewe huwa sina malumbano nao sana.


These are your words FMES, not mine:

"Mkuu ninasubiri utoe facts za kunihusisha na mduara wa watu wanaoua viongozi wetu", kama huna kubali na useme kuwa huna facts ila uliyajenga majungu, uzandiki, na uongo against me bila ya kuwa na ukweli hata mmoja, sidhani kama hili ni gumu kulifanya kwa mtu kama wewe!

Ahsante Mkuu! [/size

Sawa kabisa mimi nilisema kwamba wewe ulikuwa kwenye mduara wa kudanganya kuhusu kuugua na kufa kwa Balali. Lakini tazama sasa wewe ulivyokuja kugeuza maneno hapo juu. Je, kusema kwamba wewe ulikuwa kwenye mduara wa kupika uongo kuhusu kuugua na kufa kwa Balali ni sawa na kusema "mduara wa watu wanaoua viongozi wetu"? Hizo ndizo naziita siasa za kikomunisti.

Well, hata mimi sipendi kabisa kulumbana na wewe kwa sababu tangu nijiunge na hii forum nimejifunza mengi sana kutoka kwako. Huwa nakukosoa pale inapobidi na ninapoona kwamba ni lazima. My only humbe advice is that you should stop thinking that you are infallible bacause you are not. As binadamu, sisi sote hukosea na tunakosoleka ukiwemo wewe. Haya mkuu tuendelee na issues zingine; wewe mwenyewe umeshasema hapa kwamba taifa letu lipo njia panda. Sasa na sisi tusiende pembeni, tukaacha njia!
 
Ndugu wana jf...Naona niseme jambo moja ambalo nadhani kuna baadhi halitawafurahisha..Lakini once again ni mawazo tu ili tujadili.
Kwanza kabisa nianzie na issue ya mama Anna Muganda Ballali.
Yeye kwa taarifa nilizonazo ni kwamba ni mtuhumiwa muhimu wa hizi kashfa za ufisadi.

Amekuwa akihusishwa sana na Kashfa za BOT mara baada ya kuoana na Ballali huko Florence Italy mwaka 2004.

Tunajua kuhusu ndoa lakini hatujui kuhusu swali kwamba ni lini walikuwa na uhusiano na ni kwa muda gani kabla hawajaamua kuoana.

Mama Anna Muganda Ballali nasikia rumours pia kuwa ana uhusiano wa karibu sana tu na Mkapas

Sasa taarifa kamili za kila kitu kinachohusiana na kifo cha Daudi T S Ballali anazo mama Anna Muganda Ballali...Ameamua kuzificha!

Ushauri wangu kwake ni huu....
Tunaomba atoe ushirikiano kwasababu kama ni kweli watuhumiwa wengine wa ufisadi hawakutaka Ballali aishi, na yeye mwenyewe kuwa ni mmojawapo wa watuhumiwa hao basi mashaka yanaweza kuongezeka as ni nani haswa aliyemuua ama kumficha Ballali kati yake yeye na serikali.

Narudia tena...Wananchi wanaweza kufikiri kuwa...Adui mkubwa wa Ballali ni wale waliokuwa karibu naye kwa kiasi kikubwa...Wale waliokuwa karibu yake ambao pia walikuwa wameguswa na kashfa hizo za ufisadi!

Ni muhimu mama Anna Muganda Ballali atoe ushirikiano kabla wananchi hawajaanza kumfikiria vingine kwa kuficha kila kitu chenye kuhusu ugonjwa na hicho kinachodaiwa kuwa kifo kinachotakiwa kuwa siri ya Mama Muganda Ballali peke yake.
 
Hii Arubaini ya mwaka huu ni kali, yangu macho na masikio. Ngoja na mimi niwe mkorofi maana nishatuhumiwa kuwa "najua" ukweli!

Scenario A.

Ballali, hajafa! Inasemekana kabadilisha sura na jina sasa kahamia Fiji na si Malta kama Mbunge Slaa alivyodai. Inasemekana kuwa mkewe Ballali Mama Anna Muganda na ndugu za Ballali wameamua kuwapiga kanyaboya Watanzania na kumpeleka mpendwa wao mafichoni na kutuzuga Watanzania. Yote haya kuhusu kuugua, kulazwa, mashine ya kusaidia uhai, Boston, DC, Close Casket, makachero, RO kumtembelea, Dada za Ballali kutaka kusema mbovu na kuaswa wakae kimya yote ni Mazingaombwe.

Ballali ni mzima wa afya na akili na sasa yupo mafichoni, kazuga kifo ili kuagana na ndugu zake. Wanaojua kuwa bado yupo hai ni jamaa wachache sana ambao tumepewa nyeti. Ila haijulikani ni kwa nini ameamua kujificha. Swali ni jee anakimbia kwa kuwa alihujumu au anajificha kwa kuwa waliomtumia kuhujumu wanamtafuta wammalize ili uchunguzi na kesi dhidhi ya watu na makampuni yanayotuhumiwa kuhujumu BOT (CCM ikiwepo) ukose ushahidi na hivyo uchunguzi kusitishwa na kupunguza uwezekano wa kesi kufikishwa mahakamani.

Scenario B

Ballali amekufa! Baada ya kuugua kwa muda mrefu kwa ugonjwa usiojulikana ambapo inasemekana alilishwa sumu kama ilivyosadikiwa kuwa Rutihinda, Kibona na Kolimba walikufa kwa sumu kali. Ballali alilishwa sumu hii baada ya vuguvugu la kuanza kuhoji pesa za mfuko wa Madeni EPA zianze na hata akaitwa Dodoma Bungeni kutoa maelezo.

Ballali na familia yake walijaribu sana kuokoa maisha ya marehemu, na wakatumia njia nyingi kuficha ukweli wa mahali alipolazwa ili wale waliokuwa wakitaka uhai wake ufikie tamati wasimpate. Hali yake ilidhoofika sana na kiasi cha kutoweza kujulikana kutokana na athari za sumu. Mwili wake ulikuwa umeharibika sana, Mungu amlaze mahali pema peponi.

Scenario C

Ballali amekufa. Inasemekana alichokuwa akiugua ni lile gonjwa la kisasa ambalo yeye na yule Mzee wa Perma Sharp Liyumba walikuwa ni wataalam katika masuala nyeti. Hili la sumu ni kuzuga watu, jamaa kakanyaga waya, moto chini safari imetoka. Tunamsubiri Liyumba.

Scenario D

Ballali shahidi muhimu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusiana na kashfa ya Uhujumu wa pesa za mfuko wa madeni Benki Kuu EPA, inasemekana haijulikani kama bado yupo hai au amekufa. Haijulikani mahali alipo baada ya kuondoka Tanzania kwenda kwa matibabu USA. Kumekuwa na Utata kuhusiana na ama Ballali yupo hai au amefariki kutokana na ugumu na utata ambao ulitokea tangu alipoondoka Tanzania kwenda kwa Matibabu USA baada ya kutoa maelezo Bungeni kuhusiana na tuhuma za uzembe uliosababisha hujuma kubwa Benki Kuu ya pesa za EPA, Minara ya Benki, Meremeta na Tangold.

Utata huu unatokana na kwamba inasemekana Uchunguzi wa EPA unaonyesha kuhusika kwa viongozi wakuu wa Serikali katika kupanga hujuma hii ambayo walionufaika na pesa hizi walikuwa ni Wagombe wa CCM wa Uchaguzi 2005 wa Kiti cha Urais wa Muungano na Bunge la Muungano(wengi wamenufaika kwa kupata ushindi bila kujua kuwa pesa za kuwasaidia washinde Uraisi na Ubunge zilikuwa za hujuma), CCM, Viongozi kadhaa wa Serikali kwa nafasi zao binafsi na watu binafsi wengi wakiwa ni wafanya biashara.

Ballali inasemekana aliidhinisha malipo yote haya ya Meremeta, Tangold na EPA kwa kupokea Maagizo na Amri kutoka kwa waajiri wake (Waziri wa Fedha na Ikulu). Ingawa Serikali imetamka rasmi kuwa Ballali si Shahidi au Mtuhumiwa, mazingira mazima na hata uchunguzi wa suala la hujuma Benki Kuu unamfanya Ballali aonekane kuwa ni kiungo kikubwa ambacho kitaleta ufafanuzi wa kina wa kilichotokea BOT. Sambamba na Ballali, Katibu Mkuu wa Hazina Gray Mgonja na wote waliokuwa Mawaziri wa Fedha wakati wa hujuma hizi, ni watu muhimu sana katika uchunguzi.

Aidha, uongozi wa Taifa na hasa Raisi na Ofisi yake ambao walikuwa na dhamana kubwa kuidhinisha malipo makubwa kama hayo, yanawekwa katika darubini kujua ni vipi Benki Kuu iliweza kuidhinisha malipo makubwa kama hayo katika kipindi cha miaka 5 bila Hazina au Ikulu kujua na kutaka taarifa kamili za ukaguzi wa mahesabu.

Scenario E

Ballali amekufa, inasemekana ameuwawa kwa sumu kali ambayo alinyweshwa au kulishwa alipokwenda Dodoma kujibu maswali Bungeni kuhusiana na sakata la hujuma za pesa za mfuko wa madeni. Inasemekana walimuua Ballali ni vigogo kadhaa wa kisiasa, serikali na jumuiya za wafanyabiashara ambao walihusika ama moja kwa moja au kupitia wapambe wao katika mipango na hata kuidhinishwa kwa malipo hewa ya EPA, Tangold na Meremeta.

Vigogo hawa ama inasemekana walimlisha au kumnywesha sumu Ballali mapema kabla ya hujuma hizi kuanza kutangazwa hadharani kupitia barua ya Jeetu Patel na ile listi maarufu ya JK 11 iliyotolewa na Mbunge wa Karatu Dk. Slaa ambazo zilitoa mwangaza na kubainisha kuwa kuna hujuma BOT kwa kuwa walikuwa wamekwisha kupata walichokitaka na hivyo Ballali hakuwa na faida kwao mithili ya Roberto Calvi ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Vatican Bank Ambrosiano ambaye alikutwa amejinyonga/amenyongwa kwenye daraja moja huko ulaya baada ya kashfa ya hujuma na Benki hiyo ya Ambrosiano ambayo inamilikiwa na Kanisa Katoliki kuhusiana kibiashara na lile genge la kihalifu nchini Italia maarufu kwa jina la Mafia.

Hivyo basi wakati tuko kwenye Matanga au Arubaini na kutafuta mchawi, najiuliza Ballali awe hai au amekufa kama jamii ilivyogawanyika, je Serikali itakuwa wazi na wakweli kuchunguza na kufikisha kwenye mkondo wa Sheria wale wote waliohusika na uhujumu wa fedha BOT kupitia Tangold, Meremeta na EPA?

Ikiwa Serikali ilishasema haimtafuti Ballali kwa sababu yeyote ile, je madai kuwa Serikali ya CCM ndiyo mnufaika mkubwa wa hujuma hizi ni kweli? je ni kwa nini Serikali ya CCM inakuwa na kigugumizi na kuonekana kufanya uchunguzi kuhusiana na tuhuma za ufisadi na uhujumu kwa mashaka na kwa uzembe wa hali ya juu?

Ni kwa nini Serikali ilianza majadiliano na "watuhumiwa" badala ya kwanza kuwakamata na kuwashitaki wote wanaosemekana wamehusika na hujuma hii?

Je kufa au kuwepo hai kwa Ballali kuna maanisha kesi imekwisha, ushahidi ni mgumu au ni kuwa Serikali ya awamu ya nne, ina kazi ngumu kuchukua hatua kwa kuwa iliingia madarakani kwa kutumia fedha hizi za hujuma?

Is Ballali the only person to get us answers and deliver the whole saga to conclusion? What about Mgonja, Mramba, Yona, Sumaye, Shein, Lumbanga, Chenge and Mkapa? what about Deputy Governor and head of department that handled EPA money at BOT?

Is someone trying to tell us that Ballali single handedly enginereed and structured the whole fiasco at BOT from Meremeta, Tangold and EPA? who was responsible to audit BOT and Ballali all those years?

Does paper trail starts and ends with Ballali alone?

Nasubiri siku ya kuinua jamvi tumalize matanga.
 
Back
Top Bottom