William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
Mushi sasa unaongea hoja ambazo ni muhimu kwa taifa, hapo tupo pamoja mkuu!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
You know the pendullum swings both ways, na kama kuna watu wanafikiria kuna mduara kama huo hapa JF na mimi nachelea kufikiria kuwa akina Yebo Yebo, Kitila Mkumbo, Mtanzania na Kuhani Mkuu nao wako kwenye mduara wa kuendeleza hizi conspiracy theories ili ionekane kuwa Balali aliziiba zile hela na sasa amefake kifo and out of reach na kuwakinga mafisadi halisi ili waendelee kupeta untouched kule bongo.Vipi na ninyi wana JF mmetumiwa na mafisadi, au?
Inaonekana kuna kundi limeshaamua kuwa kuna "mduara" wa kudanganya kuhusu ukweli wa kuugua na kufa kwa Balali. Fair enough.
JMushi14. Balali and his wife Anna Muganda, maintain foreign bank accounts, houses
and property along side Vimal Mehta, Jeetu Patel and Don Andy in
Switzerland, London, Dubai, and Mauritius.
Serengeti Breweries Ltd. Factory was bought with stolen tax payers VAT
money from 1994. Currently making claims of investing millions in Tanzania.
Source of funds is Bank of Tanzanias Foreign Debt Service Account
Sanjay Mehta& Ajay Mehta: Capo Bastones. Brothers of Vimal
Mehta who are all managing different businesses which have stolen estimated
funds of USD 285 million from Government of Tanzania since 2002 and USD 25
Million in 1992-1 995 period.
Bank M: Recently licensed by Bank of Tanzania without proper procedure. The
owners of the Bank are Jeetu Patel, Daudi Balali through an
offshore company, Vimal Mehta, Sanjeev Kumar, Bhasker Narayanan, Anna
Muganda. See section on Bank M for detail
Ni lazima nione, nihakikishe ndipo niamini. Hata wakionyesha picha za Dk. Ballali akiwa kwenye jeneza bado sitaamini kifo hiki, hata nikionyeshwa picha za mazishi yake akiingizwa kaburini kule Marekani sitaamini, mpaka pale nitakapoambiwa kwamba DNA imechukuliwa na kupimwa na kuhakikisha kwamba huo ni mwili wa Dk. Ballali. Katika hali hii, inawezekana wakatengeneza kitu tu na kukipachika picha ya Dk. Ballali, ili tuaamini kwamba amekufa, na maisha yakaendelea kama kawaida
Mtanzania,
Heshima mbele mkuu, muache Jasusi, tuendele sisi wengine mkuu sidhani kama it too much to ask, ninajua kuwa wewe ni mstaarabu badala yake nitwange mimi ikiwezekana, leave the man alone please!
Kitila Mkumbo,
Mkuu navyofahamu mimi wewe ni mwanasiasa na umesoma yaani una elimu ya darasa, hivyo ni mategemeo yangu utakuwa mbele zaidi ya watu kama hawa kia Karugendo maadam kasema yeye ni Padre hana jipya!..
Kwa lugha fupi mnaturidisha kule kule tulikotoka, na nadhani wanaojenga mduara ni kina nyie hapo ambao kwa kila hoja yenu swala la EPA limekuwa secondary kwenu isipokuwa Balali ambaye toka ameondoka mwaka jana hakuwa muhimu isipokuwa baada ya kifo chake, almost 1 year have passed.
Kwa maelezo kama ya huyu Padre:-
Sasa kama ukweli wenyewe unatakiwa kwa nguvu hizo kweli hii tutafika? Kama hamuamini kafa sasa DNA ya nini ikiwa mtu huyo ni mzima na nani anajua kuisoma hiyo DNA! kamba si bado zitaendelea? Na kuna sheria gani inayowalazimisha familia ya marehemu kutimiza hayo kuridhisha baadhi ya watu ambaop hawataki kuamini...
Hata hivyo ikisha bainika kweli ni yeye mtafanya nini? au akiwa sii yeye mtafanya nini maanake kila kitu ni hatua.. nini hatua yenu baada ya kuthibitisha..Oooh samahani kabla ya yote hayo mnataka nini kifanyike sasa hivi..Kuundwa kwa kamati nyingine ya kuchunguza kifo au sio?... swala la EPA ambalo report yake imetoka inakaribia mwaka sasa liwekwe kando kwanza!
Unajua Kikwete kisha wajulia sana na kawapateni anapotaka... mtaundiwa kamati, majibu yatakuja kwake kwanza na baada ya hapo yatalala kwa miezi sita kwisha yaende bungeni ambako Sitta atakataa kuyazungumzia na kadhalika.
Hivi kwa kuuliza kwenu hamuoni kama mnawajengea CCM kibanda cha kuficha mengine yote!..Na jinsi navyoiona picha hata swala la EPA bungeni limepata nafasi ya kuulizwa wabunge kuwa Balali hayupo sasa hili swala tutalimaliza vipi bila shahidi muhimu kuwepo!..wao wataendelea kudai hawajui aliko wala hawakupata nafasi ya kuona maiti, wakati hao hao walitueleza mwanzo kuwa amekufa nasi hatukukubali. Hivyo interest za wananchi zinatangulia kwanza.
Mkuu jengeni hoja zenu kwenye issue ya EPA kama ilivyo wakilishwa na kama ikibidi muufikishe ujumbe kwa wananchi kuwa serikali imekataa katakata kuwachukulia hatua mafisadi (Wahujumu) basi na iwe kwa maandamano makubwa kila mkoa!...msicheze mchezo wa CCM hata kidogo never intertain that crap!
Bila woga kwa mara ya kwanza watajeni majina wahusika wote... liwe na liwe tuone kama watawafungulia mashtaka mahakamani, hapo mtawaita wakaguzi wa Ernst and Young kutoa ushahidi..Sijui nao watawaficha ama kuwaua...
Mkandara,
Unajua kwamba kwenye haya ya Ballali, Jaji Warioba ni katika wale ambao wangeumbuliwa kwenye Meremeta? Ana kila haki ya kusema tumwache apumike salama. Wako wengi kwenye hilo kundi.
Mtanzania,
Angalia habari vizuri....Jaji Warioba hahusiki, hajawahi kuhusika wala kuhusishwa na Meremeta....naamini amejisemea kama private citizen na sio kama mtu mwe masilahi binafsi na kifo cha marehemu Balali!
Mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, Jaji Joseph Warioba akizungumzia kifo hicho cha Dk. Ballali wiki hii, ameiambia Raia Mwema kwamba anaona unafiki wa hali ya juu katika matamshi na matendo ya wanasiasa.
Huu ni unafiki mkubwa. Muacheni Ballali apumzike kwa amani. Kwanza walimwita ni fisadi, sasa wanasema shahidi muhimu amekufa. Katoka kuwa fisadi wakati wa uhai kuwa shahidi katika mauti, alisema Warioba katika mahojiano ya simu mwanzoni mwa wiki hii.
Aliongeza Warioba: Amekuwa kafara. Taarifa ya Serikali kuhusu fedha za EPA ilionyesha wazi Ballali amechukuliwa hatua katika utaratibu wa kawaida wa kuwajibika. Haikumtuhumu kwamba alikuwa ameiba fedha. Fedha zile bilioni 133 ni jumla ya fedha zote zilizochukuliwa na kampuni 22 zilizotajwa katika taarifa ya Serikali.
Ballali hakutajwa katika orodha ya kampuni hizo. Hilo Serikali inajua, viongozi wa siasa wanajua na vyombo vya habari vinajua. Lakini wote hao, kwa kipindi chote alichokuwa hai walimhukumu kama mtu aliyekuwa ameiba fedha. Lakini waliochukua fedha zile wanafahamika.
Kwa muda wa miezi mitano Kamati (ya uchunguzi wa kashafa ya EPA) imekuwa ikiwaambia wananchi inakusanya fedha hizo kutoka kwa watu wanaoitwa. Ilipoulizwa kuhusu Ballali ilisema haimuhitaji. Maana yake hakuwamo katika orodha ya waliochukua fedha zile. Lakini sasa amefariki wimbo umebadilika. Wanasiasa na vyombo vya habari vinamwita si fisadi tena, bali shahidi muhimu wa wizi wa EPA.
Huu ni unafiki mkubwa. Kuna visingizio kwamba ugonjwa wa Ballali haujulikani, lakini Serikali inajua kwani alikuwa analipiwa matibabu na Benki Kuu. Alikuwa Boston, Marekani, ile nchi iko wazi mtu angetaka kujua angejua. Lakini sasa wanasiasa na vyombo vya habari vinalalamika kwamba ugonjwa wake ulifanywa siri. Kumbe ni uzembe wao.
Sasa tumeanza kutafuta mchawi huku. Na hapa ikisha kutamkwa neno fisadi tu, basi hata kama mtu hana ushahidi unakuwa fisadi. Lakini yote haya hakuna anayekuambia Ballali aliiba kiasi gani. Wamuache apumzike kwa amani, siku moja ukweli utafahamika.
Kitila Mkumbo,
Mkuu navyofahamu mimi wewe ni mwanasiasa na umesoma yaani una elimu ya darasa, hivyo ni mategemeo yangu utakuwa mbele zaidi ya watu kama hawa kia Karugendo maadam kasema yeye ni Padre hana jipya!..
Kwa lugha fupi mnaturidisha kule kule tulikotoka, na nadhani wanaojenga mduara ni kina nyie hapo ambao kwa kila hoja yenu swala la EPA limekuwa secondary kwenu isipokuwa Balali ambaye toka ameondoka mwaka jana hakuwa muhimu isipokuwa baada ya kifo chake, almost 1 year have passed.
Kwa maelezo kama ya huyu Padre:-
Sasa kama ukweli wenyewe unatakiwa kwa nguvu hizo kweli hii tutafika? Kama hamuamini kafa sasa DNA ya nini ikiwa mtu huyo ni mzima na nani anajua kuisoma hiyo DNA! kamba si bado zitaendelea? Na kuna sheria gani inayowalazimisha familia ya marehemu kutimiza hayo kuridhisha baadhi ya watu ambaop hawataki kuamini...
Hata hivyo ikisha bainika kweli ni yeye mtafanya nini? au akiwa sii yeye mtafanya nini maanake kila kitu ni hatua.. nini hatua yenu baada ya kuthibitisha..Oooh samahani kabla ya yote hayo mnataka nini kifanyike sasa hivi..Kuundwa kwa kamati nyingine ya kuchunguza kifo au sio?... swala la EPA ambalo report yake imetoka inakaribia mwaka sasa liwekwe kando kwanza!
Unajua Kikwete kisha wajulia sana na kawapateni anapotaka... mtaundiwa kamati, majibu yatakuja kwake kwanza na baada ya hapo yatalala kwa miezi sita kwisha yaende bungeni ambako Sitta atakataa kuyazungumzia na kadhalika.
Hivi kwa kuuliza kwenu hamuoni kama mnawajengea CCM kibanda cha kuficha mengine yote!..Na jinsi navyoiona picha hata swala la EPA bungeni limepata nafasi ya kuulizwa wabunge kuwa Balali hayupo sasa hili swala tutalimaliza vipi bila shahidi muhimu kuwepo!..wao wataendelea kudai hawajui aliko wala hawakupata nafasi ya kuona maiti, wakati hao hao walitueleza mwanzo kuwa amekufa nasi hatukukubali. Hivyo interest za wananchi zinatangulia kwanza.
Mkuu jengeni hoja zenu kwenye issue ya EPA kama ilivyo wakilishwa na kama ikibidi muufikishe ujumbe kwa wananchi kuwa serikali imekataa katakata kuwachukulia hatua mafisadi (Wahujumu) basi na iwe kwa maandamano makubwa kila mkoa!...msicheze mchezo wa CCM hata kidogo never intertain that crap!
Bila woga kwa mara ya kwanza watajeni majina wahusika wote... liwe na liwe tuone kama watawafungulia mashtaka mahakamani, hapo mtawaita wakaguzi wa Ernst and Young kutoa ushahidi..Sijui nao watawaficha ama kuwaua...
Mheshimiwa Warioba, sikiliza Mzee!
Marekani ni nchi ya wazi, ni kweli, lakini mtu baki yeyote huwezi kuambiwa habari zozote za mgonjwa. Ndo maana hakuna aliyejua afya ya mgombea John McCain mpaka wiki iliyopita alipotoa health report yake. Vinginevyo daktari hawezi kusimama jukwaani akasema 'mgonjwa wangu Ballali ana Ukimwi ...amelazwa hospitalini kwangu chumba namba tisa!" Hapo umechemsha!
Pili, unasema hela za EPA zote zililipwa kwa makampuni ambayo siyo ya Ballali, na kwa mtaji huo, Ballali hakuwa fisadi. Wewe ulikuwa Mwanasheria wetu mkuu, na leo ni Jaji wa Kimataifa, utajifanye hujui kitu kinachoitwa "kickback"? Ballali analipa fedha za EPA kwa kampuni X, inayomilikiwa na ndugu Y, halafu Y anakuja kumpoza Ballali pembeni bila kuacha fingerprints kwenye makaratasi. Mzee Warioba hiyo concept huijui, au unataka kufanya wenzio wajinga kwa sababu umepata bullhorn ya Raia Mwema unakozungumza bila kuswalishwa?
Tatu, unasema Ballali aachwe apumzike kwa amani, halafu hapo hapo unasema siku moja ukweli utajulikana. Ukweli utashuka wenyewe kama mvua za masika kutoka mbinguni? Si ndo maana watu wanachunguza? Na kuna ubaya gani unapofanya uchunguzi ukamhusisha aliyekuwa anatunza ufunguo sehemu ujambazi ulipotokea bila kufuli kuvunjwa? Ndio hivyo ulivyo kuwa unaendesha Wizara ya Sheria? Warioba hata wewe unachemsha hivi?
Nne, unadai Serikali inajua ugonjwa kwa sababu walilipia gharama. Hilo tunalijua, ni Kisukari tuliambiwa. Mbona husemi kuhusu Hospitali? Au Ballali alipewa hela taslimu akaambiwa kajitibie kokote, zitakazobaki turudishie chenji? Na zikipungua tuma ki-memo tukuongezee? Hospitali haitumi bili? Si ndio ufisadi huo tunaoungelea. Na wewe si hivi karibuni umekuwa ukikemea ufisadi, sasa tukueleweje we Mzee unapoongea kutoka pande zote mbili za mdomo wako? Ni hospitali gani hiyo waliyo ilipa lakini hawaijui, kama sio ya Profesa Maji Marefu?
Credentials za huyu Mzee Warioba ni za Mwanasheria Mkuu, na Jaji wa Kimataifa, na Waziri Mkuu, na Waziri wa Sheria, na Makamu wa Rais wa Jamhuri. Na bado anachemsha hivi. Unadhani kuna matumaini Tanzania?
Kigoma,
Fuatilia hili na unaweza kutafuta hata hapa JF maana tulishajadili hili jambo.
Jaji Warioba ni katika wahusika wa Meremeta, ndio maana wengine tungetaka uchunguzi huu uwe mkubwa zaidi na uchunguze pesa zote zilizochotwa BOT na kupewa wanasiasa. Wapo wengi kwenye kundi.
Nakushauri fuatilia, ukishindwa nijulishe, nitakusaidia.
Soma hii link: http://www.klhnews.com/index2.php?option=com_docman&task=doc_view&gid=10&Itemid=85
Wait a minute, Utamlaumu vipi ikiwa kuna HISA kubwa ya serikali?'The government owns 35 per cent of the 80 per cent owned by Tanzanians, while the rest belongs to a consortium of Tanzanian companies under the umbrella of Mwananchi Trust'
Meremeta na Mwananchi.....ni kampuni tofauti......
Mwananchi Gold....ni kampuni ya kusafisha dhahabu na kuiongezea thamani....kabla haijauzwa....Jaji Warioba ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi....usijaribu kuwapotosha wana JF...
http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2005/12/02/55188.html
http://www.bot-tz.org/Publications/FinancialReports/FinancialStatements/2004/NOTES.pdf
'The government owns 35 per cent of the 80 per cent owned by Tanzanians, while the rest belongs to a consortium of Tanzanian companies under the umbrella of Mwananchi Trust'
Unaweza kumhukumu Jaji Warioba kwa kukubali...kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa hii kampuni....LAKINI sio kwa yeye binafsi kujihusisha na ufisadi...huyu jamaa sio fisadi, hajawahi kuwa fisadi na sidhani kama ataanza leo wala kesho!