Naomba tutoe ufafanuzi kuhusu hii kampuni ya Meremeta. Barua ya Jeetu Patel ambayo imeletwa tena hapa inadai Ballali alikuwa na shares pamoja na Anna Muganda.
Rev. Kishoka,
Kulingana na madai ya Dr. Slaa, Anna Muganda hakuwa na share kwenye Meremeta bali alikuwa na shares kwenye kampuni inayoitwa Time Mining ambayo baadaye ilipewa kazi ya kuongoza Meremeta.
Haya makampuni ni mengi mno, rahisi kuchanganya. Yote yana kitu kimoja in common, ni kumwimbia Mtanzania maskini.
Source: Gazeti la Mwananchi
Wapinzani wamwanika Mzindakaya,Gavana Balali,mkewe
*Wadai amekiuka kanuni za Bunge
*Wamhusisha kashfa ya ubadhirifu
Na John Stephen
KAMBI ya Upinzania bungeni imesema Mbunge wa Kwela, Christant Mzindikaya amevunja kanuni za bunge kwa kuzungumzia suala ubadhirifu Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ambalo ana maslahi nalo wakati akijua wazi kuwa ni kuvunja taratibu za bunge.
Akiwasilisha hotuba ya kambi ya hiyo bungeni jana Msemaji Mkuu wa kambi hiyo, Dk Willibrod Slaa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Karatu, alisema kanuni za bunge hazimruhusu mbunge kuzumgumzia jambo lolote ambalo ana maslahi nalo isipokuwa baada ya kusema jinsi anavyohusika na jambo hilo.
Mbunge hatazungumzia jambo lolote ambalo yeye mwenyewe ana maslahi ya kifedha nalo, isipokuwa baada ya kutaja jinsi anavyohusika, na kiwango cha maslahi hayo?. Dk Slaa alinukuu kifungu cha kanuni za bunge na kuongeza kuwa; Mheshimiwa Mzindakaya hakutamka lolote kuhusu maslahi yake katika jambo hili,
Mbunge huyo alilieleza kuwa kutokana na utafiti walioufanya, walibaini kuwa Mzindikaya ana maslahi na jambo alilolizungumzia bungeni na kwamba mwaka 2004 alichukua mkopo kwa shughuli zake binafsi wa Sh9.7 billioni kutoka benki ya Standard Chartered kupitia kampuni ya SAAFI na kudhaminiwa na BOT.
Alisema kwamba SAAFI ilidhaminiwa na BOT huku mhusika mkuu katika tuhuma hizo akiwa ni Gavana wa benki hiyo na kwamba baada ya miaka 4 bila deni hilo kulipwa hadi sasa benki kuu Ikiwa mdhamini, iliwajibika kulilipa deni hilo kwa benki ya Standard Charter.
Dk Slaa alisema hivi sasa tena Mzindakaya ameomba adhaminiwe na BOT mkopo mwingine tena wa Sh billioni mbili na kwamba mkopo huo uko kwenye hatua ya kujadiliwa na BOT. Katika hotuba yake hiyo, Dk. Slaa alisema kauli ya Mzindikaya kwamba wabunge hawafanyi utafiti si sahihi na kwamba Ililenga kuwapotosha Watanzania.
Alisema pia kauli ya mbunge huyo wa Kwela kwamba kuna uwezekano wa baadhi ya Wabunge kutumika na wafanyabiashara wa nje ili kuwasemea mambo yao si jambo zuri na kwamba kauli hiyo Itawafanya Watanzania waamini kuwa wabunge hao wanatumiwa. "Hii ni kauli nzito sana kusemwa dhidi ya mbunge yeyote, wa upinzani au wa chama tawala, kwa sababu wote ni wabunge kama Mzindakaya, tumechaguliwa na Wananchi wetu kama yeye," alisema Mbunge huyo.
Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alisema kuwa kambi ya upinzania imestushwa na kiwango cha ubadhirifu wa fedha za umma na hujuma wa kiasi cha malipo ya fedha yenye utata wa Sh40 bilioni ambazo ziliripotiwa na gazeti moja la kila siku hapa nchini. Alisema Kampuni ya Kagoda Agricultural Ltd iliyosajiliwa Septemba 29, 2005 na baada ya wiki zisizozidi nane ilipewa zaidi ya Sh.30.8 billioni kupitia akaunti ya External Service Debt na benki Kuu ambapo Gavana ndio msimamizi mkuu.
Kuhusu matamshi ya Waziri wa Fedha, Zakia Megheji kuwa wapinzani wana upeo mdogo wa kuelewa mambo, Dk. Slaa alisema kuwa majibu ya waziri huyo hayakuridhisha akiwa mbunge na mwakilishi wa Wananchi katika kuisimamia serikali.
Akizungumzia tuhuma zinazomhusu Gavana wa Benki Kuu, alisema inamhusisha moja kwa moja Gavana huyo na kwamba alifanya uzembe katika upotevu au matumizi mabaya ya fedha za Serikali ndani ya Benki hiyo. Alisema taarifa ya mkaguzi mkuu inamtaja pia mkewe, Anna Muganda kuwa mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Time Mining, ambayo ndiyo iliyokuwa inaendesha kampuni ya Meremeta, na hatimaye imeuzwa kwa bei ya kutupa na baada ya BOT kulipa dhamana ya zaidi ya Dola za marekani 100,000, kabla ya kuuzwa kwa Rand Gold, ambako mama huyo pia anamiliki hisa. "Watanzania tunajiuliza hapa kuna nini? Serikali kila ikihojiwa Bungeni haitoi majibu kama alivyojibu waziri wa Fedha Bungeni juzi. Wakurugenzi wa Alex Stewart waliolipwa zaidi ya Dola za marekani 65 millioni nao walitoka Time Mining ambako Ana Muganda anahusika." alisema Dk. Slaa.
Dk Slaa aliomba Gavana Balali ajiuzulu kutokana na kashfa hizo zinazomkabili. Vile vile , Dk Slaa alisema kuanzia sasa kambi ya upinzani inatambulika kama kambi ya ushindani kwa vile wao ni washindani na sio wapinzani.