Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

KM,

Tatizo ni maslahi, jaji Warioba hapo anatetea pesa ambazo na yeye amefaidi kule Mwananchi Gold.

Si umeona hata Mzindakaya naye katusaliti baada ya kupewa bilioni tisa kule kwenye kiwanda fake cha nyma?

Warioba anamlaumu Mkapa, huku na yeye ameruhusu mafisadi kumchangia kwenye kampuni yake? Mkapa na yeye angemkatia kidogo kama alivyofanya Ballali, leo hii angelikuwa anamtetea.

Tanzania tumejaza mafisadi kila sehemu.

Mamaaa!

Nilikuwa najiuliza Warioba ana interest gani katika hii mi-statement anayoitoa toa?

Mzee nae ana soo zake? Duuh! Tumekwisha!

Jamani sasa tufanyeje? Mpaka Warioba?
 
Wait a minute, Utamlaumu vipi ikiwa kuna HISA kubwa ya serikali?

Utamlaumu vipi Chenge kuhusu Tangold ikiwa government inamilika hisa asilimia 100?

Mwananchi Gold haina tofauti na Meremeta, njia walizotumia kuchota pesa zinafanana.
 
Kwani hiyo Mwananchi ni mali ya Warioba, au alikuwa mwenyekiti tu! maanake naona ya Mzindakaya kilikuwa kiwanda chake..
 
Kwani hiyo Mwananchi ni mali ya Warioba, au alikuwa mwenyekiti tu! maanake naona ya Mzindakaya kilikuwa kiwanda chake..

Nimekuambia suala la Mzindakaya ili kuonyesha conflict of interest. Suala la Warioba linafanana sana na suala la Chenge. Wote sio wamiliki, walikuwa wanasema ni kampuni za serikali, kumbe ni kampuni za wizi wa mali za wananchi kupitia BOT. Mmoja alikuwa mwenyekiti wa kampuni mwingine ni mkurugenzi wa kampuni nyingine.

Mtu aliyefaidika na hizo pesa kama Warioba unataka amshambulie Ballali? Ndio maana wengine tunaamini kama una interest kwenye jambo ni bora kukaa kimya au kueleza wazi interests zako zikoje, vinginevyo ndio mwanzo wa conflict of interest.

Jiulize Warioba analipwa ngapi huko Mwananchi Gold? Kama alikuwa anajitolea bure, nitamwondoa kwenye list, lakini kama amefaidika na mapesa ya wananchi kuingizwa kwenye kampuni yao bila mpangilio na yeye ni mmoja wao, ndio maana sishangai akiwatetea wenzake.

Mahali popote hapa duniani hiyo ni conflict of interest.
 
...Mtu aliyefaidika na hizo pesa kama Warioba unataka amshambulie Ballali? Ndio maana wengine tunaamini kama una interest kwenye jambo ni bora kukaa kimya au kueleza wazi interests zako zikoje, vinginevyo ndio mwanzo wa conflict of interest.

M-TZ,

Hiyo concept ya conflict of interest Bongo ni ngeni.

Na sijui kwa nini. Kina Warioba wamekuwa exposed kwenye mambo ya Siasa na Serikali kabla mimi sijazaliwa. Kwa nini sisi ndio tuje tushtukie hivi vitu wao wanajifanya hawavijui? Kwa nini hawafuatilii hii misingi ya kwanza kabisa ya public ethics?
 
Kuhani Mkuu.. concept ya conflict of interests siyo ngeni kama inavyodhaniwa na wengi. Iliingizwa kwenye sheria ya Maadili ya Viongozi ya 1995. Sasa ugeni wake unatoka wapi? Nadhani ni sahihi zaidi kusema kuwa kuepuka conflict of interests ndiyo jambo ambalo viongozi hawaoni umuhimu wake.
 
Mtanzania,
Nipe somo kidogo hapa. Wakati Warioba ni mwenyekiti wa hiyo Mwananchi alikuwa na wadhifa (nafasi) gani serikalini?..
 
Kuhani Mkuu.. concept ya conflict of interests siyo ngeni kama inavyodhaniwa na wengi. Iliingizwa kwenye sheria ya Maadili ya Viongozi ya 1995. Sasa ugeni wake unatoka wapi? Nadhani ni sahihi zaidi kusema kuwa kuepuka conflict of interests ndiyo jambo ambalo viongozi hawaoni umuhimu wake.

Iliingizwa lakini haitekelezwi, then the question becomes who is responsible to enforce the law? and why has the organ with such responsibility failed miserably?
 
Is it Mwananchi Gold or Mwananchi Green which is alleged to be a subsidiary company of CCM?
 
Naomba tutoe ufafanuzi kuhusu hii kampuni ya Meremeta. Barua ya Jeetu Patel ambayo imeletwa tena hapa inadai Ballali alikuwa na shares pamoja na Anna Muganda.

Lakini makaratasi mengi na hata mahojiano Bungeni yanaonyesha kuwa Meremeta ilikuwa Mradi wa Jeshi kuchimba dhahabu kwa kushirikiana na kampuni ya Trinexx ya Afrika Kusini ambao wao ndio walitoa initial Capital in condition kuwa Watarudishiwa Capital na Interest na hawakuwa na nia au haja ya kupata mavuno ya dhahabu.

"Jeshi" liliposhindwa kuendeleza mradi, Serikali ikalibeba hilo jukumu na kuwalipa hawa Trinnex. Hivyo Serikali ya URT ndiyo mmiliki wa Meremeta na waliotajwa kama Wakurugenzi, kuanzia Gavana, Makatibu wakuu Hazina, Madini na Mwanasheria Mkuu wamepewa Ukurugenzi kwa nafasi zao za kazi na si binafsi.

Lakini yawezekana kutokana na udhaifu wa vyombo vyetu vya Sheria na Serikali, basi umiliki huu wa Shirika hili la Serikali umehamia mikononi mwa hawa ndugu kwa nafasi zao binafsi na si kwa nafasi zao za kazi.

Naomba niweke nukuu ya thread niliyoanzisha On Meremeta na nukuu kutoka East African na This Day.

http://www.nationaudio.com/News/EastAfrican/21042003/Regional/Regional2104200315.html

http://www.afdevinfo.com/htmlreports/org/org_60044.html

http://allafrica.com/stories/200804181038.html

http://www.thisday.co.tz/News/4076.html

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=5865
 
Rev. Kishoka,
Mkuu hii nzito sana yaani naona kwa nini watu wanakwepa swala la EPA! I mean hapa ndipo penye usiri mkubwa. Meremeta inatisha kama wimbo wa harusi!..
 
Mtanzania,
Nipe somo kidogo hapa. Wakati Warioba ni mwenyekiti wa hiyo Mwananchi alikuwa na wadhifa (nafasi) gani serikalini?..

Mkandara,

Nafikiri una maana ya hiyo conflict of interest siyo? Tulichomaanisha sisi ni kwamba hiyo
kampuni yao ilichotewa mapesa na BOT ya Ballali, kumtetea Ballali bila ya yeye kusema na wao walifaidika na mapesa ya Ballali kunaweza kuleta conflict of interest.

Hatuongelei hapo yeye Warioba kuwa serikalini. Ni sawa na Mzindakaya, alimtetea Ballali bungeni bila kutaja kufaidika kwa kampuni yake na hiyo BOT. Ilibidi Dr. Slaa ndiye aliambie bunge jinsi Mzindakaya naye alivyofaidika na mapesa ya Ballali.

Kama ambavyo wengi wameandika mara nyingi, EPA ni mtoto tu wa ufisadi, matatizo makubwa zaidi yako kwenye hizi kampuni zingine mbalimbali kama Meremeta, Tangold, Mwananchi Gold nk.
 
Naomba tutoe ufafanuzi kuhusu hii kampuni ya Meremeta. Barua ya Jeetu Patel ambayo imeletwa tena hapa inadai Ballali alikuwa na shares pamoja na Anna Muganda.

Rev. Kishoka,

Kulingana na madai ya Dr. Slaa, Anna Muganda hakuwa na share kwenye Meremeta bali alikuwa na shares kwenye kampuni inayoitwa Time Mining ambayo baadaye ilipewa kazi ya kuongoza Meremeta.

Haya makampuni ni mengi mno, rahisi kuchanganya. Yote yana kitu kimoja in common, ni kumwimbia Mtanzania maskini.

Source: Gazeti la Mwananchi

Wapinzani wamwanika Mzindakaya,Gavana Balali,mkewe

*Wadai amekiuka kanuni za Bunge
*Wamhusisha kashfa ya ubadhirifu

Na John Stephen

KAMBI ya Upinzania bungeni imesema Mbunge wa Kwela, Christant Mzindikaya amevunja kanuni za bunge kwa kuzungumzia suala ubadhirifu Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ambalo ana maslahi nalo wakati akijua wazi kuwa ni kuvunja taratibu za bunge.

Akiwasilisha hotuba ya kambi ya hiyo bungeni jana Msemaji Mkuu wa kambi hiyo, Dk Willibrod Slaa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Karatu, alisema kanuni za bunge hazimruhusu mbunge kuzumgumzia jambo lolote ambalo ana maslahi nalo isipokuwa baada ya kusema jinsi anavyohusika na jambo hilo.

Mbunge hatazungumzia jambo lolote ambalo yeye mwenyewe ana maslahi ya kifedha nalo, isipokuwa baada ya kutaja jinsi anavyohusika, na kiwango cha maslahi hayo?. Dk Slaa alinukuu kifungu cha kanuni za bunge na kuongeza kuwa; Mheshimiwa Mzindakaya hakutamka lolote kuhusu maslahi yake katika jambo hili,

Mbunge huyo alilieleza kuwa kutokana na utafiti walioufanya, walibaini kuwa Mzindikaya ana maslahi na jambo alilolizungumzia bungeni na kwamba mwaka 2004 alichukua mkopo kwa shughuli zake binafsi wa Sh9.7 billioni kutoka benki ya Standard Chartered kupitia kampuni ya SAAFI na kudhaminiwa na BOT.

Alisema kwamba SAAFI ilidhaminiwa na BOT huku mhusika mkuu katika tuhuma hizo akiwa ni Gavana wa benki hiyo na kwamba baada ya miaka 4 bila deni hilo kulipwa hadi sasa benki kuu Ikiwa mdhamini, iliwajibika kulilipa deni hilo kwa benki ya Standard Charter.

Dk Slaa alisema hivi sasa tena Mzindakaya ameomba adhaminiwe na BOT mkopo mwingine tena wa Sh billioni mbili na kwamba mkopo huo uko kwenye hatua ya kujadiliwa na BOT. Katika hotuba yake hiyo, Dk. Slaa alisema kauli ya Mzindikaya kwamba wabunge hawafanyi utafiti si sahihi na kwamba Ililenga kuwapotosha Watanzania.

Alisema pia kauli ya mbunge huyo wa Kwela kwamba kuna uwezekano wa baadhi ya Wabunge kutumika na wafanyabiashara wa nje ili kuwasemea mambo yao si jambo zuri na kwamba kauli hiyo Itawafanya Watanzania waamini kuwa wabunge hao wanatumiwa. "Hii ni kauli nzito sana kusemwa dhidi ya mbunge yeyote, wa upinzani au wa chama tawala, kwa sababu wote ni wabunge kama Mzindakaya, tumechaguliwa na Wananchi wetu kama yeye," alisema Mbunge huyo.

Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alisema kuwa kambi ya upinzania imestushwa na kiwango cha ubadhirifu wa fedha za umma na hujuma wa kiasi cha malipo ya fedha yenye utata wa Sh40 bilioni ambazo ziliripotiwa na gazeti moja la kila siku hapa nchini. Alisema Kampuni ya Kagoda Agricultural Ltd iliyosajiliwa Septemba 29, 2005 na baada ya wiki zisizozidi nane ilipewa zaidi ya Sh.30.8 billioni kupitia akaunti ya External Service Debt na benki Kuu ambapo Gavana ndio msimamizi mkuu.

Kuhusu matamshi ya Waziri wa Fedha, Zakia Megheji kuwa wapinzani wana upeo mdogo wa kuelewa mambo, Dk. Slaa alisema kuwa majibu ya waziri huyo hayakuridhisha akiwa mbunge na mwakilishi wa Wananchi katika kuisimamia serikali.

Akizungumzia tuhuma zinazomhusu Gavana wa Benki Kuu, alisema inamhusisha moja kwa moja Gavana huyo na kwamba alifanya uzembe katika upotevu au matumizi mabaya ya fedha za Serikali ndani ya Benki hiyo. Alisema taarifa ya mkaguzi mkuu inamtaja pia mkewe, Anna Muganda kuwa mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Time Mining, ambayo ndiyo iliyokuwa inaendesha kampuni ya Meremeta, na hatimaye imeuzwa kwa bei ya kutupa na baada ya BOT kulipa dhamana ya zaidi ya Dola za marekani 100,000, kabla ya kuuzwa kwa Rand Gold, ambako mama huyo pia anamiliki hisa. "Watanzania tunajiuliza hapa kuna nini? Serikali kila ikihojiwa Bungeni haitoi majibu kama alivyojibu waziri wa Fedha Bungeni juzi. Wakurugenzi wa Alex Stewart waliolipwa zaidi ya Dola za marekani 65 millioni nao walitoka Time Mining ambako Ana Muganda anahusika." alisema Dk. Slaa.

Dk Slaa aliomba Gavana Balali ajiuzulu kutokana na kashfa hizo zinazomkabili. Vile vile , Dk Slaa alisema kuanzia sasa kambi ya upinzani inatambulika kama kambi ya ushindani kwa vile wao ni washindani na sio wapinzani.
 
"Binadamu wazima na fahamu zao, huishi kama wanyama wa mwituni, ambao uhai wa kila mmoja wao hutegemea ujanja wake wa porini, ukali wa meno yake na urefu wa makucha yake. Upebari ni unyama" - Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.


Sijui huko aliko anasema nini Mwalimu Nyerere?
 
Kuhani Mkuu.. concept ya conflict of interests siyo ngeni kama inavyodhaniwa na wengi. Iliingizwa kwenye sheria ya Maadili ya Viongozi ya 1995. Sasa ugeni wake unatoka wapi? Nadhani ni sahihi zaidi kusema kuwa kuepuka conflict of interests ndiyo jambo ambalo viongozi hawaoni umuhimu wake.

Mwnkjj,

Uko sawa 100%, to the extent that sheria za 'conflict of interest' zipo. Lakini naomba nikujibu ni nini kigeni hapa kuhusu 'conflict of interest.'

Sheria haisemi ueleze ulivyonufaika na uhusiano wako na mtu kabla hujamtetea hadharani, kitu ambacho wengine tunakosoa kwamba Warioba hajakifanya hapa. Alichokivunja Warioba hapa, jambo ambalo ni concept ngeni kwetu, ni ile "roho" ya ile sheria, japo si maandishi ya sheria ya msingi (text).

Sheria inasema hivi:

The Public Leadership Code of Ethics Act, 1995-13
Section 6(e)
in relation to public interest… public leaders shall so arrange their affairs as will prevent real, potential or apparent conflicts of interest...


Kwanza, Warioba sio kiongozi sasa hivi. Sheria hii haikumhusu Warioba jana wakati anamtetea Ballali. Pili, hata kama angekuwa kiongozi, bado hajavunja sheria eti tu kwa kutoa matamko yanayo vutia ngozi kwake. Ili kuivunja, ilibidi awe anafanya shughuli ya umma yenye maslahi yanayopingana, mengine ya kumnufaisha yeye, mengine manufaa ya umma. Kumtetea mtu bila kuweka bayana uhusiano wako nae hakutoshi kuvunja hii sheria.

Sasa, "roho" ya sheria ambayo Warioba hajaiheshimu -concept ambayo ndio ngeni kwetu - ni kwamba ukimuongelea au kutetea mtu ambae uliwahi kuwa na mahusiano nae yenye manufaa kwako, kwanza tuambie historia ya uhusiano wako na unaemtetea, ili huo uwazi utupe imani kwamba wakati ule unafanya kazi ya umma ulikuwa hautumikii mabwana wawili wakati mmoja.

Uelewa huo wa ‘roho' ya sheria (concept of the spirit of the law) ndio wa kigeni. Kwamba unafuata, sio tu sheria yenyewe ya msinig, bali hata ile ‘roho' ya sheria. Kwamba unaende kilomita moja zaidi ya ile unayotakiwa kwenda. Huko ndiko hatujafika. Huko ndiko kugeni.
 
Hii kama kweli ni masikitiko makubwa sana!

The Alex Stewarts Auditor Saga
Don Balali hired this firm to audit the gold exports from Tanzania
by mining companies. This company was based in Washington and before
Tanzania, has never audited a single mining company. Coincidentally, most
of the Alex Stewarts expatriate staff were the same individuals that were
working for Time Mining, a company that operated and managed Meremeta Gold
Company and then left with USD 100 million of Tanzanias funds. The
shareholders and beneficiaries of Time Mining are Anna Muganda and other
close associates of Don Balali. This type of audit agreement was the first
in the history of Africa, with a company that has never done this type of
auditing, and was paid a commission of 1.9 % from the total gold royalty
the Government of Tanzania collected of 3.9%. This amounted to USD 1.5
Million per month, USD 18 Million per year and USD 72 million over the
period of three years this company has had a contract with BOT. Sources
within the company noted that the operating cost per month including the
audit work done by 3 expatriates and 3 local staff in total does not exceed
USD 50,000. Therefore, Don Balali was paying the auditing company closely
associated with his wife 30 times its operating cost per month. Even with a
profit margin of 100%, this company should never have been paid more than
USD 100,000 per month by BOT. Taking the USD 100,000 per month figure as an
acceptable rate which may have been charged by any larger auditing firm,
the loss to Tanzania would be USD 17 million per year and USD 68 million
over the 4 year period. Information recently obtained note that the
Governor intends to extend the contract for a period of 3 years and again
this June 2007. The Alex Stewarts CEO and Don Andy have been have been
doing the rounds, visiting several Ministers to extend this contract with
BOT. Alex Stewarts now boasts of doing gold auditing in several countries
in Africa
 
Hii kama kweli ni masikitiko makubwa sana!

The Alex Stewarts Auditor Saga
Don Balali hired this firm to audit the gold exports from Tanzania by mining companies. This company was based in Washington and before Tanzania, has never audited a single mining company.

Coincidentally, most of the Alex Stewarts expatriate staff were the same individuals that were working for Time Mining, a company that operated and managed Meremeta Gold Company and then left with USD 100 million of Tanzanias funds.

The shareholders and beneficiaries of Time Mining are Anna Muganda and other close associates of Don Balali.

This type of audit agreement was the first in the history of Africa, with a company that has never done this type of auditing, and was paid a commission of 1.9 % from the total gold royalty the Government of Tanzania collected of 3.9%.

This amounted to USD 1.5 Million per month, USD 18 Million per year and USD 72 million over the period of three years this company has had a contract with BOT.

Sources within the company noted that the operating cost per month including the audit work done by 3 expatriates and 3 local staff in total does not exceed
USD 50,000.

Therefore, Don Balali was paying the auditing company closely associated with his wife 30 times its operating cost per month. Even with a profit margin of 100%, this company should never have been paid more than
USD 100,000 per month by BOT.

Taking the USD 100,000 per month figure as an
acceptable rate which may have been charged by anylarger auditing firm, the loss to Tanzania would be USD 17 million per year and USD 68 million over the 4 year period. Information recently obtained note that the
Governor intends to extend the contract for a period of 3 years and again this June 2007.

The Alex Stewarts CEO and Don Andy have been have been doing the rounds, visiting several Ministers to extend this contract with BOT.

Alex Stewarts now boasts of doing gold auditing in several countries
in Africa

Hayo hapo juu kama kweli basi shughuli itakuwa ndio kwanza imeanza maana naona mpango mzima ulikuwa ni wa kimafia!

Yani kampuni ya ku audit ya Alex Stewarts ILIYOLETWA NA Ballali kufanya kazi iliyokuwa ya ku audit mauzo ya nje ya dhahabu yenye kufanywa na kampuni za Tanzania ilikuwa ni kutoka huko washington alikofia Ballali....Ikiwa na uhusiano na mkewe...Mkewe aliye na uhusiano na Mkapa na Malegesi na Lukaza!

Na uhusiano wake na Mkapa nafikiri bado ni madhubuti!

Hapo ilikuwa ni dili la kimafia lenye kujidai kufanya uchunguzi wa kujichunguza wenyewe ili kuweza kuficha ukweli mbele za wananchi.

Halafu ikiwa kampuni hiyo ya Alex Sterwart ya ukaguzi wa mahesabu ina uhusiano pamoja na kuwa na wafanyakazi wengine waliokuwa wakifanya kazi kwenye kampuni ya Anna Muganda Ballali ya "Time mining" ambayo ilikuwa iki isimamia MEREMETA GOLD...

Then malipo waliyokuwa wakipeana na upotevu wa mabilioni ya dola halafu kuna watu wanasema kuna mipaka hapa kweli?
Hizo pesa ni nyingi sana jamani!

Hivi mnajua zingeweza kuwafanyia nini wabongo?
 
Mushi,

Hiyo barua ya Jeetu Patel pamoja na kuwa inasisimua lakini haina credibility kwa kuwa iliandikwa kuvuruga kiini na chimbuko la uhalifu.

Ukiangalia walichosema kuhusu Meremeta na ukweli unaozungumziwa kuhusu Meremera inabidi ujiulize kama hii ililetwa mapema kuzuga wananchi ili kuvuruga taratibu nzima za uchunguzi.

At this minute baada ya kuona aliyosema Slaa na uchunguzi mbali mbali kuhusu EPA, Meremeta na Tangold, it is safe to say kuwa labda Serikali was right ilipotaka kujua ni nani alianzisha hii barua ambayo inaonekana wazi ilitumwa kwa makusudi na jumuia ambayo inapingana na ile iliyokwisha jipatia "riziki" au kulikuwa na ugomvi.

Hii Time Mining inayosemwa ni ya Anna Muganda ni kampuni ya Afrika Kusini, sasa tutafute ndugu walioko SA watutafutie date of incorporation na listed onwers and directors.

http://www.timemining.co.za/default.htm
 
Back
Top Bottom