Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwanakijiji,
Then what?
FMES
Ubishe usibishe Mkuu jina lako liko juu hapa uwanjani,
tunatamani kusikia unasema nini, usisahau wewe ni msomi mzuri, msaada wako kwetu unahitajika, tuko tayari kulala chali ili mladi umesema, tuko tayari kwa lolote, na tuko tayari kuamini kile unachokisema Mkuu. Baba tunapopata mkanganiko wa kimawazo toka kwenu ninyi wakuu wetu hapa jamvini, hakika meli inaweza kuyumba,sasa sisi tushike wapi?
Invisible na wewe(FMES) ndiyo mlituaminisha kifo cha baba yetu, sasa mara mnarukaruka, kwa kuwa Invisible yeye kasafiri hayupo tutaendelea kumsubiri ili aje atujuze zaidi kuliko!!!
Mwanakijiji,
Unajua Utata tumeuzua sisi wenyewe hakuna chombo cha habari chochote kile ambacho kinaweza kuandika upupu kama huu wetu hapa.
1. Tumeambiwa Balali amefariki, tunataka ushihidi wakati sisi wenyewe hatuna ushahidi kuwa yu hai isipokuwa tunatafuta mchawi nje ya serikali inayohusika..hakuna mwingine isipokuwa Marehemu mwenyewe.
2. Katika picha zimetokelewakuna ile limo la kubeba maiti na wajuzi mnaweza kufahamu kwamba hilo gari hutoa maiti kule ilikohifanyiwa hadi kwenye mazishi na haiwezekani kabisa kuwepo na utaratibu huo kama hakuna kibali halali cha mfu, mahala gari hilo linapokwenda chukua maiti, kuishughulikia (make up) kwanza kabla ya kuilaza ktk jeneza na mengine mengi ambayo hayafanywi na familia ya marehemu iwe hata Mkewe.
Hivi kweli serikali ya Marekani wanaweza kuingia kanyaboya kama hili!
3. Kuna ndugu za marehemu wamekuja hapa na hasira kubwa ya kuwaeleza mchawi nani leo mnakuja wakatisha tamaa kuwa wao ndiuo waongo!.. sababu ati hawakuionyesha maiti kwa wananchi wote wakati mtu kafia ugenini. Kwa desturi, kama hizi ndio maana waislaam hawaonyeshi maiti kwa sababu ya watu kama hawa hapa. Kinachowapeleka msibani ni UDAKU.. kujua maiti imeharibika kiasi gani, marehemu alikonda kiasi gani wengine watasema Duh, hata nywele zilimnyonyoka na kadhalika lakini yote haya yanamsaidia nini marehemu ama familia ya mfiwa!... ZERO..
!4. Balozi wetu alikuwepo na wengine wengi ambao hakuna kati ya watu mnaowekea mashaka hamjajaribu kuonana nao na kuuliza maswala haya isipokuwa hapa kijiweni ambapo hakuna mtu aliyekwenda isipokuwa yule mmoja mnayemwekea mashaka pia. balozi hawezi ku report kwa rais wake false report huu ni ujinga mkubwa sisi kufikiria hivyo
5. Familia ya wazazi wa Marehemu walikuwepo na hadi sasa hivi wapo ktk majonzi leo bado mnawawekea pia mashaka wao kama ilivyokuwa kifo cha Chifupa.
6. Na mwisho, amefia state gani haiwezi kuwa sababu kama marehemu kazikwa DC na walihudhuria watu mazishi hayo wengi wao wakiwa wageni nje ya viongozi wa serikali yetu. Ujumbe toka Ofisi mbali mbali za kimataifa ziliwakilishwa iwe kweli ulikuwa uongo hawa watu wakubali kuacha kazi zao kuhudhulia kanyaboya la Mama Muganda..basi huyu mama ana nguvu za ajabu sana.
Mkuu twendeni kwenye issue za muhimu, marehemu alikwisha hojiwa na hao TAKUKURU nushahidi wake sio lazima awepo yeye maanake inafahamika kuwa tayari kisha toa ushihidi wake. Kama kweli wangemtaka kisheria basi kesi nzima ingefunguliwa wakati akiwa nchini na ushahidi wake kusomwa lakini ni baada ya ushahidi wake aliiitwa Dodoma kuhusiana na ushahidi huo. From that day hakuwa salama kama alivyokuwa Amina Chifupa!..
Mkuu, kumbuka watu walifikiria mzaha ulipozungumzia hali yake, wachawi wakatafutwa... mara alikuwa na Ukimwi, wengine wakadai mwili wake wauone kuthibitisha kilichomuua. Tukaondoa kabisa dhana na machafu na dhulma ya serikali yetu..msiba huo ulipita kama ndoto, leo hatunaye na bado tumeshindwa kuwaweka wazi Mafisadi pamoja na kwamba list ipo mikononi mwa rais mwenyewe!..
How dump can we one be!... sisi kuendelea kutafuta wachawi nje ya circle inayohusiana na mabalaa yote haya!
Conclusion moja tu.. NDIVYO TULIVYO.
Nilikuwa na maana hospital alikokuwa amelazwa, kisha tukaambiwa karudi nyumbani hali yake iliendelea vizuri na baadaye atarudi TZ kutoa ushahidi.. yote haya hamkuyawekea mashaka isipokuwa leo mliposikia amekufa!..
Yaani mnadai kujua zaidi kuhusu maiti kuliko alipokuwa hai as if kutabalisha kitu.. sasa kama hii sio NDIVYO TULIVYO nini hasa!
Utata wenu ni wapi Balai amefia au ni Balali kafa kweli? maanake sioni report mbili hizo zilizotolewa zikisema amekufa na nyingine ikisema hakufa..Kama report imeenda Ikulu na kusema amefia Boston kwani huyo aliyeipeleka hawezi kufanya makosa na Familia ikarekebisha hilo. Swala ni Balali amekufa au hakufa au sio, mengine yote ni uzushi unaotokana na dhana yenu.Mkandara.. utata hatukuuzua sisi; wameuzua wao wenyewe. Kama Taarifa iliyopelekwa Ikulu na BoT inasema kuwa Ballali amefia Boston, halafu nyumba ya mazishi wanasema amefia DC, si haki kutalaumu sisi kwa utata huo
.. bado wewe hujanipa motive katika maelezo yako. Mtu mwenye fedha nyingi sana yuko salama zaidi Marekani labda iwe anatafutwa na serikali ama vyombo vya kimataifa.. Balali hakuwa mmoja wa hao watu Kisha kama ni kukimbia Mafia bado ushihidi upo ktk mashirika ya usafiri, airport na pengine passport yake kutumika.Mzee mantiki yako hapo ni nzuri sana, the only thing you are missing ni motive gani inaweza kuwepo kwa mtu kufake kifo. Je mtu mwenye fedha nyingi akitaka kuigiza kifo anaweza, and to what extent atafanya hivyo? Has it been done before?
Nafasi ya serikali ya Marekani nakuomba soma maelezo yangu hapo juu kuhusiana na kibao cha kifo ambacho ni lazima kiwepo kabla hujakubaliwa mazishi..Hii ikiwa ni pamoja na clearance toka hospital kuhusiana na kifo cha huyo mtu.Nafasi ya serikali ya Marekani kwenye misiba ni nini?
Wewe ulitaka nani awepo ambaye ungemwamini zaidi!... member wa JF wote sio wakazi wa DC na pengine hawana uhusiano na marehemu. Hata kama wangealika watu hasa toka JF mtu kama mimi nisingeenda bado mngeuliza mbona Mkandara hakwenda....kuna kitu hapa. Kama ni wewe wangezua jingine kuwa umelipwa fedha nyingi sana na Mama Muganda.Point nzuri sana.. binafsi sioni kama hoja ya kuoneshwa mwili kwa public ni hoja yenye nguvu sana... lakini katika mazingira na wingu hili nadhani hoja ya an independent observer ambaye angesema ameona mwili wa Marehemu Ballali. Siku ya Jumanne familia ilipoenda kuview mwili pale DeVol funeral home nani ambaye hakuwa sehemu ya familia aliyepata nafasi ya kuona?
Mkuu mbona unazungusha hapa! linmi ubalozi wamepewa taarifa haiwezi kabisa kuingiliana na mashaka ya kifo. Mara ngapi watu wamekufa na Ubalozi wamepewa habari mwisho mwisho, na kuna wengine hata Ubalozi hawakufahamishwa...Ni lini Balozi alitakiwa kuuona mwili ili kuhakikisha kifo kimetokea. Je, unataka kusema kuwa hata Sefue ameingizwa mjini?.. mbona yeye ndiye mwenye ukaribu sana na familia ya inayokisiwa? au ndio Sefue pia yupo kundi moja na Balali, Mkapa na wengineo kukimbia upepo. Maanake sielewi wanamkimbiza mafichoni kwa kitu gani haswa ikiwa Mkpa mwenyewe tumesha ambiwa tumwache mzee wa watu. My point ni kwamba ku view maiti sio big deal at all na binafsi nimewahi kufanya hivyo sii zaidi ya mara tatu maisha yangu yote..haipunguzi imani ama ukweli wa kifo. Basi nadhani hata Ditopile yawezekana yuu hai ulipata kuuona mwili wake.Mkandara, Ombeni Sefue kwa mara kadhaa huko nyuma na Ubalozi wake wameulizwa alipo Ballali na hawakujua; hata baada ya kifo uliza ni lini wao walipewa taarifa, na kama afisa yoyote wa Ubalozi alikuwepo siku ya Jumanne kwenye family viewing. Ombeni alitakiwa na serikali kwenda kwenye mazishi Ijumaa na familia walitoa mwaliko huo, lakini kama ni ushahidi basi ni shahidi wa Jeneza na ibada. Ombeni hajauona mwili wa Ballali.
Mkuu waliohudhulia mazishi yale sii Wabongo tu huyu mama hawezi kuwafunga kamba watu wote kwa fedha gani?... Nguvu gani aliyokuwa nayo kuweza kuwapanga watu hadi makaburini ili kuficha ukweli wa kifo cha mmewe.. come now mkuu vipi hata familia ya wazazi wa marehemu wanunuliwe kwa kitu gani hasa!..Only if you knew what you actually said.
Mkuu wanaojua habari za Balali wanafahamu aliumwa toka alipotoka Dodoma na swala la sumu lilijuilikana mapema sana isipokuwa halikuzungumzwa kama vile Amina Chifupa..Una maana gani "from that day hakuwa salama"?
Sijakuelewa hapo! Binadamu wenye akili timamu hutafuta criminal baada ya crime kutokea, sasa kama kifo cha Balali ni crime as it is hapo mnaweza kwenda kokote. Hao viongozi unaowasema pamoja na kutishiwa bado nyie macho yenu yapo kwa Balali sio viongozi yaani focus yote mnajaribu kuiondoa toka kwa viongozi the real suspects na kuipeleka kwa maiti.. Ushahidi upo Takukuru, viongozi waliokuwepo Dodoma na baadhi ya watu ambao wameomba muda kuhakikisha haki inapata nafasi yake. Kote huko kuna ushahidi tosha ambao umekaliwa kuficha ukweli. Msiyaone yote haya ila mnatafuta mchawi hapa kuficha ubaya wa serikali yetu. Awe amekufa ama hakufa, hili swala bado liko wazi kabisaaa! Balali sio evidence anaweza kuwa shahidi kama tutaweza fungua mashtaka.. hadi leo nani kafungua?... hakuna wakati report tunazo mikononi.Mkandara hakuna watu wenye uwezo wa kufanya lolote, to go to unimaginable lenght to cover a crime. Wanadamu ndivyo walivyo. Na hakuna watu ambao wana hatari ya kufanya lolote kama walio madarakani au wenye nafasi nyeti ambazo zinatishiwa na ukweli. They are capable of wiping out whole communities if need be.
Kama Ballali is a victim of such people or if he perceived the gravity of the threat posed to him.. ana haki na sababu ya kufanya lolote lile kukwepa mikono ya watu hao. Na njia pekee ni ya kifo.
Mzee kilichotokea BoT si jambo dogo, ni sisi tunaliona dogo lakini kama lingetoka Federal Reserve ya US, au Benki Kuu nyingine yoyote leo hii ingekuwa mshike mshike wa ajabu. Hivyo, Ballali siyo tu ni mtu muhimu lakini naffasi yake katika sakata zima imechanganyika mno kiasi kwamba siyo tu a player but also a victim. Na naamini at the end he discover he was more the later than the former.
Kwani tatizo ni kwamba amekufa au hajafa? Kwangu mimi hoja kuwa amekufa haina mashaka sana.. na hoja kuwa yawezekana hajafa haina msingi zaidi. Lakini zote mbili zina implication yake na kwangu ndio hasa kiini cha mjadala huu.
Jmushi... mimi sijabadili mawazo yangu kuhusu lolote kwani sikuwahi kutoa mawazo yangu kuhusu jambo hili.
MKJJ mawazo yako yanajulikana toka mwanzo kuwa Ballali apewe kinga..Na msimamo wako wewe mwenyewe baada ya wewe mwenyewe kutangaza kifo chake ni kuwa Ballali alitakiwa kupewa kinga.
Naomba tusiingize siasa na tuwe honest...Maana hizo kauli zako hapo juu zinapingana na nyingine ulizopost previously...Ambazo umeonekana uki question baadhi ya legitimacy ya issue zinazodai kuwa Ballali kafa.
Angalia MWK alivyopata support kubwa ya wana jf baada a kuweka wazi kuwa yuko upande wa wananchi..Upande uliogubikwa na mashaka kutokana na mazingira halisi ya kifo hicho pamoja na kesi nzima ya EPA!
Kitendo chako cha kusema hujabadilisha mawazo kimenishtua kidogo.
Field Marshall nasikia wewe ni CCM na hivyo ndio maana naona pia unashindwa kujua ni upande upi ni sahihi..Licha ya kwamba unaelekea kubase kwenye kauli zako za 100% belief on Ballali's death.
Kwani tatizo ni kwamba amekufa au hajafa? Kwangu mimi hoja kuwa amekufa haina mashaka sana.. na hoja kuwa yawezekana hajafa haina msingi zaidi.
Need I say the least that logic is the base of reasoning and unless you're illogic you'll never use incredible sources to testify Ballali's death? Sources Sources Sources; you came here testifying Ballali died in DC, does your sources more credible than JKs' who said Ballali died in Boston when sending condolences to Ballali's family? Do you want me to give benefit of doubts!sasa na wewe tuambie umefanya nini zaidi tu ya kuweka logic
You mean this?maana unaona Mtanzania, anaweka hoja kwa nini haamini kuwa Balali hajafa
By the way, since I register (Aug. 2007) I've never change my membership nor register another name, only JS. The problem is you think all members will accept what you say and whenever one disagree you jump to a conclusion that is the one disagree previous. My brother/sister, no one is after your credibility and no one even know who you are! We are all trying to contribute despite of whether will converge to same point on not. If we do not converge then someone has to admit instead of calling other opinions NONSENSE!Mtanzania said:Ukifuatilia kwa karibu utagundua sources za Invisible, Tanzania Daima, Mbowe, Jasusi, FMES zinatoka sehemu moja, juu kabisa ya mti amekaa mke wa Ballali.