Mwanakijiji,
Labda nami nitumie mtindo wenu pamoja na kwamba umechagua pale unapotaka kuongeza swali badala ya kujibu hoja zangu..
Well nianze hili:-
Mkandara.. utata hatukuuzua sisi; wameuzua wao wenyewe. Kama Taarifa iliyopelekwa Ikulu na BoT inasema kuwa Ballali amefia Boston, halafu nyumba ya mazishi wanasema amefia DC, si haki kutalaumu sisi kwa utata huo
Utata wenu ni wapi Balai amefia au ni Balali kafa kweli? maanake sioni report mbili hizo zilizotolewa zikisema amekufa na nyingine ikisema hakufa..Kama report imeenda Ikulu na kusema amefia Boston kwani huyo aliyeipeleka hawezi kufanya makosa na Familia ikarekebisha hilo. Swala ni Balali amekufa au hakufa au sio, mengine yote ni uzushi unaotokana na dhana yenu.
Mzee mantiki yako hapo ni nzuri sana, the only thing you are missing ni motive gani inaweza kuwepo kwa mtu kufake kifo. Je mtu mwenye fedha nyingi akitaka kuigiza kifo anaweza, and to what extent atafanya hivyo? Has it been done before?
.. bado wewe hujanipa motive katika maelezo yako. Mtu mwenye fedha nyingi sana yuko salama zaidi Marekani labda iwe anatafutwa na serikali ama vyombo vya kimataifa.. Balali hakuwa mmoja wa hao watu Kisha kama ni kukimbia Mafia bado ushihidi upo ktk mashirika ya usafiri, airport na pengine passport yake kutumika.
Kama serikali yetu inamhitaji basi ni wao wanaotakiwa kuweka mashaka ya kifo hiki kwa sababu kinawaweka ktk hali mbaya zaidi. Ushahidi wa Balali Upo TAKUKURU na kule Dodoma alikokwenda kujieleza.. sasa Balali wa nini kama aliweza kuondoka salama sehemu zote mbili. Mwenye fedha hakimbii starehe hata siku moja na kama imewahi kutokea basi ni kwa wale waliopewa maficho na serikali za majuu..
Nafasi ya serikali ya Marekani kwenye misiba ni nini?
Nafasi ya serikali ya Marekani nakuomba soma maelezo yangu hapo juu kuhusiana na kibao cha kifo ambacho ni lazima kiwepo kabla hujakubaliwa mazishi..Hii ikiwa ni pamoja na clearance toka hospital kuhusiana na kifo cha huyo mtu.
Point nzuri sana.. binafsi sioni kama hoja ya kuoneshwa mwili kwa public ni hoja yenye nguvu sana... lakini katika mazingira na wingu hili nadhani hoja ya an independent observer ambaye angesema ameona mwili wa Marehemu Ballali. Siku ya Jumanne familia ilipoenda kuview mwili pale DeVol funeral home nani ambaye hakuwa sehemu ya familia aliyepata nafasi ya kuona?
Wewe ulitaka nani awepo ambaye ungemwamini zaidi!... member wa JF wote sio wakazi wa DC na pengine hawana uhusiano na marehemu. Hata kama wangealika watu hasa toka JF mtu kama mimi nisingeenda bado mngeuliza mbona Mkandara hakwenda....kuna kitu hapa. Kama ni wewe wangezua jingine kuwa umelipwa fedha nyingi sana na Mama Muganda.
Mkandara, Ombeni Sefue kwa mara kadhaa huko nyuma na Ubalozi wake wameulizwa alipo Ballali na hawakujua; hata baada ya kifo uliza ni lini wao walipewa taarifa, na kama afisa yoyote wa Ubalozi alikuwepo siku ya Jumanne kwenye family viewing. Ombeni alitakiwa na serikali kwenda kwenye mazishi Ijumaa na familia walitoa mwaliko huo, lakini kama ni ushahidi basi ni shahidi wa Jeneza na ibada. Ombeni hajauona mwili wa Ballali.
Mkuu mbona unazungusha hapa! linmi ubalozi wamepewa taarifa haiwezi kabisa kuingiliana na mashaka ya kifo. Mara ngapi watu wamekufa na Ubalozi wamepewa habari mwisho mwisho, na kuna wengine hata Ubalozi hawakufahamishwa...Ni lini Balozi alitakiwa kuuona mwili ili kuhakikisha kifo kimetokea. Je, unataka kusema kuwa hata Sefue ameingizwa mjini?.. mbona yeye ndiye mwenye ukaribu sana na familia ya inayokisiwa? au ndio Sefue pia yupo kundi moja na Balali, Mkapa na wengineo kukimbia upepo. Maanake sielewi wanamkimbiza mafichoni kwa kitu gani haswa ikiwa Mkpa mwenyewe tumesha ambiwa tumwache mzee wa watu. My point ni kwamba ku view maiti sio big deal at all na binafsi nimewahi kufanya hivyo sii zaidi ya mara tatu maisha yangu yote..haipunguzi imani ama ukweli wa kifo. Basi nadhani hata Ditopile yawezekana yuu hai ulipata kuuona mwili wake.
Only if you knew what you actually said.
Mkuu waliohudhulia mazishi yale sii Wabongo tu huyu mama hawezi kuwafunga kamba watu wote kwa fedha gani?... Nguvu gani aliyokuwa nayo kuweza kuwapanga watu hadi makaburini ili kuficha ukweli wa kifo cha mmewe.. come now mkuu vipi hata familia ya wazazi wa marehemu wanunuliwe kwa kitu gani hasa!..
Ebu nambie wewe unafikiri Balali kajichimbia akikimbia kitu gani hasa!..hao wachunguzi waliokwenda Marekani? kuna uhakika gani kama hawa walikuwa wametumwa na serikali licha ya hapo sio mara ya kwanza wao kwenda US.
Una maana gani "from that day hakuwa salama"?
Mkuu wanaojua habari za Balali wanafahamu aliumwa toka alipotoka Dodoma na swala la sumu lilijuilikana mapema sana isipokuwa halikuzungumzwa kama vile Amina Chifupa..
Mkandara hakuna watu wenye uwezo wa kufanya lolote, to go to unimaginable lenght to cover a crime. Wanadamu ndivyo walivyo. Na hakuna watu ambao wana hatari ya kufanya lolote kama walio madarakani au wenye nafasi nyeti ambazo zinatishiwa na ukweli. They are capable of wiping out whole communities if need be.
Kama Ballali is a victim of such people or if he perceived the gravity of the threat posed to him.. ana haki na sababu ya kufanya lolote lile kukwepa mikono ya watu hao. Na njia pekee ni ya kifo.
Sijakuelewa hapo! Binadamu wenye akili timamu hutafuta criminal baada ya crime kutokea, sasa kama kifo cha Balali ni crime as it is hapo mnaweza kwenda kokote. Hao viongozi unaowasema pamoja na kutishiwa bado nyie macho yenu yapo kwa Balali sio viongozi yaani focus yote mnajaribu kuiondoa toka kwa viongozi the real suspects na kuipeleka kwa maiti.. Ushahidi upo Takukuru, viongozi waliokuwepo Dodoma na baadhi ya watu ambao wameomba muda kuhakikisha haki inapata nafasi yake. Kote huko kuna ushahidi tosha ambao umekaliwa kuficha ukweli. Msiyaone yote haya ila mnatafuta mchawi hapa kuficha ubaya wa serikali yetu. Awe amekufa ama hakufa, hili swala bado liko wazi kabisaaa! Balali sio evidence anaweza kuwa shahidi kama tutaweza fungua mashtaka.. hadi leo nani kafungua?... hakuna wakati report tunazo mikononi.
Mzee kilichotokea BoT si jambo dogo, ni sisi tunaliona dogo lakini kama lingetoka Federal Reserve ya US, au Benki Kuu nyingine yoyote leo hii ingekuwa mshike mshike wa ajabu. Hivyo, Ballali siyo tu ni mtu muhimu lakini naffasi yake katika sakata zima imechanganyika mno kiasi kwamba siyo tu a player but also a victim. Na naamini at the end he discover he was more the later than the former.
Mkuu kwa mtaji huu swala la BoT linaonekana dogo sana isipokuwa Balali ndiye swala..siku zote crime hutazamwa kilichotokea act na sio mtu aliyetenda kwanza hilo ni swala la baadaye mahakamani.. Up to this moment hakuna mashtaka yoyote hivyo wapuuza ni sisi wenyewe. Yaonyesha wazi kuwa fedha zile ziliondoka benki kuu kihalali isipokuwa walishindwa kurudisha mikopo hiyo!... nani aliyekuwa akiidhinisha mikopo hatujui nini hatua za kwanza kupata mikopo iole hajtujui..leo hii Balali ni mkisiwa baada ya kufa tena basi sio mhusika mkuu isipokuwa shahidi na wapo wengi pale BoT wanaweza kutoa ushahidi kama wa Balali nani kawatafuta!