Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania


Je hii ripoti ya Mkaguzi Mkuu ni ya mwaka gani na inaweza kupatikana? Tukishajua hayo, tuiulize Serikali, je kwa nini haikufanyia kazi ripoti hii na kuchukua hatua za Kitendaji na Kisheria baada ya ripoti kutolewa? Je Ukurugenzi wa Anna Muganda ulithibitishwa na nani au mamlaka yapi? Je Mkaguzi Mkuu alikagua jarida la kampuni ya Time Mining pale Brela au kule Afrika Kusini ilikosajiliwa na kuona jina la Anna Muganda?

Kama hayo yote yalithibitishwa kuwa ni kweli, kwa nini Serikali ilipobaini mchezo mchafu haikumchukulia Ballali hatua za kinidhamu mara moja pamoja na za kisheria?

Ikiwa Gavana wa Benki Kuu alifanya uzembe ambao uliruhusu upotevu wa mamilioni ya pesa za Serikali, ni kwa nini mpaka leo Serikali imekaa kimya na kuanza uchunguzi wa tatu wa swala hilo hilo?
 
Okay wakuu kama nilivyoahidi, ninathibitisha dataz zifuatazo, na ninazitoa hapa kwa mara ya kwanza kwa taifa zima na sio JF tu:-

1. Marehemu Balali alikuwa amelazwa katika Hospitali ya George Washington University Hospital, na ndipo alipofanyiwa kila kitu mpaka kuleekea kuzikwa.

Hii Hospitali haiko mbali sana na nyumbani kwake, yaani kule Foggbottom, karibu na Watergate Hotel au Watergate Apartments.

2. Father aliyeendesha misa ya mazishi na mazishi yenyewe, anaitwa Father Sirianni wa kanisa la St. Stephen,

Ndugu zangu naomba sasa na wengine mchukue from here na kutafuta zaidi za mbele, kwa sasa nipumzike kidogo, maana this has been a very diffficult week, ni matumaini yangu kuwa nitakuwa nimewapunguzia mzigo mzito hasa ndugu yangu Mtanzania, ambaye ndiye hasa unayenisukuma kuutafuta ukweli na dataz,

Bado tunaendelea kuukaribia ukweli zaidi kwa manufaa ya taifa, JF mbele zaidi!
 
naam ! nitapenda kuona watu watakavyozungusha vichwa vyao humu ! lols... am really loving it.
 

The Meremeta Gold Company

The Governor is the custodian of this ill conceivedmining project.

He guaranteed this project from the Government for USD 100 million in 1999.

Anna Muganda was a major shareholder and partner who brought in Time Mining to manage and operate the Meremeta Mines on behalf of the Government of
Tanzania.


She went on to become the wife of Balali in 2004.

The Meremeta Mines was a classic example of Daudi Balali giving Guarantees to companies in which he had an interest, the company thereafter filed bankruptcy and the Bank of Tanzania paid the funds against the Guarantee.

Noting the strategic importance of having its own Gold Mine, Bank of Tanzania invested heavily into this mine while the South African partners raised the money
 
Kwa wale wanaodhani kuwa kifo cha Ballali kitatunyamazisha...Basi ni wale watakaoweza kuziita dola bilion 3 "vijisenti"

Uhusiano wa Mama Anna Muganda Ballali ulianza kabla hajawa Governor!
Na pia uhusiano wa Mama Anna Muganda Ballali na familia ya Mkapa pia haukuanza juzi!
Hivyo basi Ballali na yeye ana uhusiano na Mkapa..Hivyo hawezi kujitokeza!
Uhusiano wa Anna Muganda Ballali na Dr Ballali mwenyewe ulihanikizwa na fursa ya kupeana ushauri wa masuala ya kiuchumi kwenye serikali ya Mkapa...Ambapo basi inawezekana hapo ndipo walipoanza ku engineer THE WHOLE MAFIOSO DEAL!
Wanajua kila kitu!
Kama hii isssue ni kweli..Then hawa ni mafiosso na sielewi kwanini waachwe nje!

Hawa watu wanaweza kututafuta ili watuuwe!
Situation hapa si nzuri hata kidogo!

Halafu huko Italy nako nina wasiwasi sana!
Huko ndiko kulifungwa ndoa!

Washington ndiko mtandao mahali upo!
Labda mtu aliyewakutanisha Ballali na Mama Muganda ni Mkapa mwenyewe....Ama pia inawezekana ni Mama Anna Muganda Ballali aliyewakutanisha Mkapa na Ballali!

Usishangae kama walipanga the whole deal loong time!
Toka akiwa IMF akijuana na Mama Anna Muganda anayejuana na Mkapa....Mkapa aliyemtoa IMF na kumwajiri kama Governor...!


 
Again marehemu hakulazwa Georgetown Hospital kama ilivyokuwa ikifikiriwa, sababu kuna watu ambao tunawafahamu ambao wangekuwa wa kwanza kujua.

Ahsanteni Wakuu!
 
Below is The Anna Muganda Ballali-Malegesi-Johnson Lukaza-Makubo questionable connection....

Pia masikitiko makubwa kwa namna walivyozichezea pesa za masikini wa Tanzania wanaokufa kwa njaa na magonjwa kwa matumizi yao ya kifahari,kianasa na kimafiosso....!

 
Hawa watu Daudi vs Anna walikuwa wana chumbiana kuanzia kabla ya mwaka 1995!
Akiwa hajaletwa na Mkapa kutoka huko IMF!

Halafu wamekuja kufunga ndoa muda mfupi tu kabla siri haijagundulika na kabla hajafa na mara baada ya scandal yao inyowezekana ilipangwa zaidi ya miaka ishirini iliyopita!
Kuoana kwao na kuja Marekani wakati wa hicho kifo chake kinachoonekana kilipangwa kikianza kukaribia...Inaonyesha ni mpango maalum ili siri iweze kufichwa na huyo ambaye sasa ni MKE ambaye hapa Marekani kisheria ana haki nyingi sana juu ya siri za Ballali!
Na hawezi kuzitoa siri hizo kama na yeye asipojumuishwa kwenye uchunguzi huu kama mtuhumiwa!

Yani wakati wengine tukiwa watoto wadogo..Wao walikuwa wana MASTER PLAN ya kulitoka taifa Dolla billioni 3!

Hii NI KUFURU KUBWA NA HAIWEZI KUFUMBIWA MACHO!
Na ndio maana Serikali haitaki mgombea binafsi!

Maana bila mgombea binafsi hakuna kitakachochunguzwa naweza kusema nimegundua!

Ballali anaweza akawa amefichwa/kuuwawa na watu ambao hawawezi kuchunguzwa na serikali ama wale ambao wana affiliations nyingi pamoja na wale ambao wanahusika moja kwa moja na umafia huu!

Serikali inajua kila kitu na imeshindwa kuwa responsible kwa wananchi lili kulinda maslahi ya CCM!

Lakini mpango mzima ni deal iliyopangwa zamani na ilitengenezwa ili kuwatega hata wale ambao wanaweza kujifanya vimbelembele!
 
Kuna anayejua Ballali ali divorce lini?
Maana sijui ni kwanini alipewa madaraka mtu aliyekuwa hana familia!
Mke wake wa kwanza waliachana lini?
Walikutana vipi na Anna Muganda?
Walioana mwaka 2004...Na hapo ni baada ya wizi kwishatokea ili wawe kama Bonnie & Clyde...Tatizo ni kwamba hawajafa wote!
Kwasababu Mama amekataa kutoa ushirikiano na ni wazi kwamba hawakufa pamoja...Sasa then ni wazi kuwa hata yeye anaweza akawa alipenda Ballali afe ili ajinusuru!
Yeye na serikali ya CCM wana manufaa na kifo ama kutoweka kwa Ballali!
This is their chance to come clean!
 


Mushi,
You are a piece of shit. We are supposed to be talking about issues and not personalities Di8vorce ya mtu na ndoa ya mtu inahusiana vipi na nini?
You are a piece of shit. FMES samahani mkuu, nilisema sitarudi tena lakini siwezi kuvumilia upumbavu kama huu!
 

Can someone help me please...who owns Mwananchi newspaper?
 

Issue hapa sasa ni mtu aliyekuwa karibu vya kutosha na mtuhumiwa wa kwanza!

Na tukianza kudig info za scandal ya watu wazito kama hao..Ni lazima sasa tuingie kwenye mjadala wa mahusiano yao hayo ambayo yalishuhudia scandals zote hizi zikitokea chini ya uangalizi wake Ballali kwa kushirikiana na mpenziwe aliyekuja kuwa mke mnamo mwaka 2004!

Sasa kama wengine wakigoma kuzungumzia kuhusu mke wake huyo aliyekuwa naye kipindi hicho billioni 3 za kimarekani zikipotea...Then unataka tumzungumzie yule wa kwanza amabaye hakuusika?
Mjadala si utakufa?
Tusipojadili uhusikaji wa Anna Muganda Ballali...Basi na mjadala huu si utakufa pia?

Mtu ambaye na yeye pia ni mtuhumiwa!
Sasa kama wana connection ya ki Bonnie and Clyde watatenganishwa vipi?

Si ni yeye huyo Anna Muganda Ballali amekataa kutoa ushirikiano kwa watanzania kwa vigezo vya siri ya familia?

Yani kwamba watanzania hawahusiki na upotevu wa zaidi ya dolla billion 3 za kimarekani ambazo yeye na mumewe huyo aliyetutangazia kuwa ni marehemu walihusika kwa namna moja ama nyingine kuzifuja pesa za masikini!?

Mwanamama aliyekuwa na uhusiano na pia aliyeoana na Ballali kabla ya scandal kujulikana aachwe nje ya mjadala kwa vigezo vipi hivyo?

Halafu kuwa naye kipindi chote hadi kifo kilipotangazwa asitajwe kwenye huu mjadala?
Narudia tena...Kama mama hatotoa ushirikiano basi acha iwe mbaya!
 
As far as I know personal relationships are untouchable in JF. Stick to the issues you moron!
 
hapana naona tunakoenda sijui kukoje... basi jmushi tafuta majibu badala ya kuuliza maswali tu..!
 
As far as I know personal relationships are untouchable in JF. Stick to the issues you moron!

Mtusi yako hayatanitisha hata iweje!
Kama mnataka nifungieni!
Mpambano nitau hamishia kwingine!
Na hii ni mara ya mwisho...Sitavumilia matusi!
Nitajibu mapigo!
Hapa si tulishaambiwa ni kijiweni?
Sasa nini unaanza jazba?
Hizi kashfa zilikuwa personal before lakini siyo sasa!
 
hapana naona tunakoenda sijui kukoje... basi jmushi tafuta majibu badala ya kuuliza maswali tu..!

Majibu na maswali vyote vyote vinafaa!
Kuna baadhi ya majibu ya namna Anna Muganda Ballali alivyohusika na kashfa!
Halafu hapo naona ndio penyewe maana naona mizuka inaanza kupanda!
There is no any other way possible other than THE TRUTH Na hizi kauli zenu za kutumbia sisi wananchi tusiulize maswali bali tuje na majibu ni kauli mbovu mbovu ambazo zinaonyesha utata!

Mjadala ukitoka nje ya mada watu wanasema ni kijiwe...Nikiuleta panapotakiwa...inageuka na kuwa issue personal!

Kuna issue ngapi ama thread ngapi hapa za personal tena za Muungwana mwenyewe na wazito wengine ndiyo ije kuwa Anna Muganda Ballali?

Mi nakwambia haendi mtu mahali hapa labda tuuwane!

Na hivyo maisha yangu kwa hatarini ni Jambo ambalo sasa nitakuwa nalo aware kwasana kutokana na ukweli kuwa dola bilioni 3 zinatisha!
 

Anko vipi tena....this is out of your character....
 
Wakuu,

Kweli naona tuko kama wale watu waliochorewa mlango ukutani halafu wakawa wanang'ang'a nia kutoka nje kupitia kwenye mchoro huo badala ya mlango wa kweli. Kati ya malumbano yaliyoendelea, Mchungaji Kishoka aliuliza kama tutapata usuluhishi wa EPA ikiwa mama Ballali ataongea na Mkuu JMushi1 akasema tutapata kujua undani wa suala hili.

Kwa kweli nilipenda swali la Mchungaji kwani naona kwamba tumemsimamia rohoni mama wa watu ambaye kwa sasa angependa amalizie msiba wake na kuendelea maisha. Hivi kama mama Ballali akiamua kusema (kama inavyosemekana aliamua kutojihusisha na serikali baada ya kumfanya mumewe adui wa umma) "I will not dignify any of your nonsense by answering any question or taking any part on this", tutafaidika vipi? Wahenga walisema, unaweza kumleta punda mtoni kwa lazima lakini huwezi kumlazimisha anywe maji (sikusudii kumfananisha mama Ballali na punda bali ni kuelezea pointi yangu).

Mkuu Mushi nae alimjibu mchungaji jawabu zuri sana (na kwa hili nakubaliana naye) kuwa tunataka tujue undani wa EPA. Nafikiri hii ndio fundamental desire of every JF member...kujua ilikuwaje. Lakini kwa bahati mbaya naona tumeingia kiza na kumshupalia Ballali as if yeye ndio mtuhumiwa. Kama ni shahidi nyota wa serikali, kwanini wengine hatujawashupalia, kina Mramba, Mgonja, Rostam, Chenge na wengineo wengi?

Inasikitisha kuona kuwa tunatoka nje ya mstari na kuanza kufuatilia jinsi Ballali alivyofunga ndoa na mkewe au wake wa zamani...how is this relevant? Najua kuna watu watataka kusema kuwa Ballali na mkewe walishirikiana, lakini kabla ya kusema hivi, waelewe kwamba, Ballali hakuwahi kushtakiwa wala kutajwa kama mtuhumiwa hivyo mambo ya familia yake yalikuwa ni ya kwake na sio ya taifa.

Ningependa kupendekeza kuwa huyu mama mwacheni apumzike, keshateseka sana kuuguza na hahitaji maneno kuchangamsha siku yake. Kwa wale ambao wanaamini kuwa Ballali amefariki, vema, endelea na imani yako kwa amani. Vivyo hivyo kwa wale ambao hawaamini kuwa Ballali amefariki, vema, endelea na imani yako kwa amani. Kwa wengine kama mimi, well, tuiweke serikali kitimoto ili tujue ni nani walihusika na hatima yao ni ipi? Na kwanini wengine waliondolewa nyadhifa zao serikalini wakati wengine bado wanaendelea kupeta. Je tutegemee fedha nyingine zaidi zichotwe wakati tunakaribia uchaguzi ujao? Nafikiri haya ndio maswali tunapaswa kudeal nayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…