Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Rev. Kishoka,
Kulingana na madai ya Dr. Slaa, Anna Muganda hakuwa na share kwenye Meremeta bali alikuwa na shares kwenye kampuni inayoitwa Time Mining ambayo baadaye ilipewa kazi ya kuongoza Meremeta.
Haya makampuni ni mengi mno, rahisi kuchanganya. Yote yana kitu kimoja in common, ni kumwimbia Mtanzania maskini.
Source: Gazeti la Mwananchi
Akizungumzia tuhuma zinazomhusu Gavana wa Benki Kuu, alisema inamhusisha moja kwa moja Gavana huyo na kwamba alifanya uzembe katika upotevu au matumizi mabaya ya fedha za Serikali ndani ya Benki hiyo. Alisema taarifa ya mkaguzi mkuu inamtaja pia mkewe, Anna Muganda kuwa mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Time Mining, ambayo ndiyo iliyokuwa inaendesha kampuni ya Meremeta, na hatimaye imeuzwa kwa bei ya kutupa na baada ya BOT kulipa dhamana ya zaidi ya Dola za marekani 100,000, kabla ya kuuzwa kwa Rand Gold, ambako mama huyo pia anamiliki hisa. "Watanzania tunajiuliza hapa kuna nini? Serikali kila ikihojiwa Bungeni haitoi majibu kama alivyojibu waziri wa Fedha Bungeni juzi. Wakurugenzi wa Alex Stewart waliolipwa zaidi ya Dola za marekani 65 millioni nao walitoka Time Mining ambako Ana Muganda anahusika." alisema Dk. Slaa.
Dk Slaa aliomba Gavana Balali ajiuzulu kutokana na kashfa hizo zinazomkabili. Vile vile , Dk Slaa alisema kuanzia sasa kambi ya upinzani inatambulika kama kambi ya ushindani kwa vile wao ni washindani na sio wapinzani.
Je hii ripoti ya Mkaguzi Mkuu ni ya mwaka gani na inaweza kupatikana? Tukishajua hayo, tuiulize Serikali, je kwa nini haikufanyia kazi ripoti hii na kuchukua hatua za Kitendaji na Kisheria baada ya ripoti kutolewa? Je Ukurugenzi wa Anna Muganda ulithibitishwa na nani au mamlaka yapi? Je Mkaguzi Mkuu alikagua jarida la kampuni ya Time Mining pale Brela au kule Afrika Kusini ilikosajiliwa na kuona jina la Anna Muganda?
Kama hayo yote yalithibitishwa kuwa ni kweli, kwa nini Serikali ilipobaini mchezo mchafu haikumchukulia Ballali hatua za kinidhamu mara moja pamoja na za kisheria?
Ikiwa Gavana wa Benki Kuu alifanya uzembe ambao uliruhusu upotevu wa mamilioni ya pesa za Serikali, ni kwa nini mpaka leo Serikali imekaa kimya na kuanza uchunguzi wa tatu wa swala hilo hilo?