Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania


jamani naomba huyu padri apigiwe tena simu aulizwe mambo zaidi, pengine tukagundua mengine, na vile vile huyu padri anaweza kuwa pia ni wa kuchonga. maana pesa iliyoliwa ni nyingi kiasi inaweza kufanya lolote lile,sintokaa niamini kifo hiki kamwe
 

kwani hata wewe unashindwa kuhongwa? usichezwe na nguvu ya pesa bana .kwani hata hapo ulipo wewe si unahangaikia mkate wako wako wa kila ?sasa ikitokea ukaupata kwa njia ya mkato zaidi utaukataa?
 
jamani naomba huyu padri apigiwe tena simu aulizwe mambo zaidi, pengine tukagundua mengine, na vile vile huyu padri anaweza kuwa pia ni wa kuchonga. maana pesa iliyoliwa ni nyingi kiasi inaweza kufanya lolote lile,sintokaa niamini kifo hiki kamwe

sawa major, mpigie basi simu huyo pa-adre !
 
Mkuu Kinepi,

Wewe unafaa kuwa mwandishi habari za uchunguzi.

Umeniacha hio na hio kazi ulioifanya...

Ndio hiki nichokisema kila siku, Tanzania hakuna press!

Gazeti limeongelea maongezi yao na Padri kana kwamba ishu hapa ni kuthibitisha kama Ballali alifanyiwa misa, au nani alimfanyia misa.

Ni mpaka Mkuu Kinepi alipopiga simu kuuliza swali husika: Je, umeuona mwili wa marehemu? Hiyo ndio ishu!

Ni investigation ya Kinepi ndio inatuambia padre anasema "mimi ndio niliombea nilichoambiwa kwamba ni maiti."

Ukisikiliza kwa makini kinachosemwa hapa, ni kwamba Padre anakubaliana na sisi, kwamba jamani eeeeh! God knows what was inside that big box! I may be a Priest, but I can't see thru wood, and I couldn't tell ya!

Ha ha ha aaaaaaaaa ........ This is just hilarious!

Again, hakuna Press Bongo! Kinepi, babu kubwa mtu wangu! LOL!
 

Mara ya kwanza kabisa niliposikia Ballali yuko Marekani, ilisemekana kuwa alikuwa amelazwa katika hospitali ya "New England Medical Center" - Boston.....
 
Msihofu Atafufuka Kama Yesu Wala Hawakucheza Pele Hapa
Prof Dr Ing Rev Tumaini Geofrey Temu
 
kwani hata wewe unashindwa kuhongwa? usichezwe na nguvu ya pesa bana .kwani hata hapo ulipo wewe si unahangaikia mkate wako wako wa kila ?sasa ikitokea ukaupata kwa njia ya mkato zaidi utaukataa?

Wanaohongwa ni masikini na mafukara wa akili, unaonekana kuwa ni mmoja wao, ila samahani sio mimi,

vipi wewe unahangaika kutafuta mkate wa kila siku? Kwa hiyo unafikiri ni kila mtu? Mbona una mawazo finyu sana mkuu ya kufikiria ndani ya box lako tu? Hapa JF tunakataa haya ya kufikiria ndani ya box lako tu na kudhani ni lazima uwe ukweli wa wote wengine that is pathetic thinking!, leave a lone kuisema mbele ya hadhara duh!
 
Ukisikiliza kwa makini kinachosemwa hapa, ni kwamba Padre anakubaliana na sisi, kwamba jamani eeeeh! God knows what was inside that big box! I may be a Priest, but I can't see thru wood, and I couldn't tell ya!

Nikisema niliongea na Padri na kwamba alisema ndani ya jeneza kulikuwa na mbuzi nitakuwa ninasema ukweli au uongo? Wakuu tafuteni hoja nzito za kusimamia hoja yenu kuwa Balali yupo lakini sio hizi nyepesi nyepesi, unless kuna mwenye tape aliyomrekodi huyo Padri, hii mimi siikubali lakini sina tatizo kukubali mengine yenye more proof zaidi kuliko niliongea naye!

Kwenye hili hata hawa waandishi wanakuwa wajinga wajinga tu!

haya later......!
 

Watu wengine bwana!!! Wakiweka wao "Dataz" humu basi wanataka kila mtu azikubali. Wakiweka wengine basi wataambiwa mpaka waweke video au sound recording ndio ziaminike.
 
Angalieni Thisday walivyoandika:

Ballali, who was recently reported to have died in the US, was sacked from his job in January this year by president Jakaya Kikwete after being implicated in the EPA scandal by the Ernst & Young audit report.

Ina maana hata wao hawana uhakika na kifo cha Ballali.

Hapo mkuu ES una kazi ngumu kweli!
 
samahani maelezo ya mahojiano na Padri yamechelewa kidogo.
Bali Padri kwa kinywa chake amekiri hakuona mwili wa Balali.
Simu ya kanisa ni : 202 785 0982.

Dah hii sasa kali...Mkuu Kinepi naomba usife moyo ukweli utajulikana tu kama walizika jeneza tupu tutajua tu.Endelea na kazi nzuri.
 
Katika historia ya nchi yetu na uafrika kwa ujumla. mazishi ya balali yametia fora kwa kufichwa fichwa. Alikufa wakakaa kimya mpaka waliposukumwa. Hakukuwa na maombolezo yoyote nyumbani kwake Tanzania. Mwali haukuwekwa wazi. Watu hawakuruhusiwa kushiriki mazishi. Kuna watu wamefuatilia majina ya watu waliofariki katika ile county balali alipofialakini hakukuwa na jina lolote la balali.

Kwa nini lakini watanzania tunafanywa mandondocha kiasi hiki na sisi tunakubali tu. Hata kama serikali ilikubaliana na balali aseme ukweli ili asichukuliwe hatua kitendo cha "kumpoteza" walichofanya ni cha kijinga kabisa. lakini wajue ukweli utajulikana tu, sooner than later.
 
Jamani naomba kuuliza. Hivi ndugu na jamaa zake wamefanya msiba hapo bongo??? Kweli hii haingii akilini hata kidogo. Naanza kuamini li-jamaa halijafa................ Linatanua somewhere na mapesa yetu. Nafikiri mama yake anaukweli wote na hawezi kuficha!!!!
 

Jamani mi napenda kujua kitu kimoja:

Mzee ES ana interest gani na kuf/kutokufa kwa Balali mpaka watu wote mnang'ang'ania yeye tu?Yeye alileta ripoti kuwa Balali kafa kutoka kwa vyanzo vya kuaminika toka kwake,hata huyu Kinepi naye kaleta speculation tu (kwani hakuna uthibitishop mpaka sasa) kuwa Balali hajafa,ajabu mnamuunga mkono yeye kwa haraka zaidi bila kumtaka alete ushahidi au hamumng'ang'anii kama Mzee ES.Kilichobaki sasa ni kila mtu aamini chake kama Mwafrika wa Kike,Mtanzania walivyoamua.Kitu kimoja kiko wazi:Balali hatarudi milele Tanzania,cha muhimu kwetu ni kupambana ili tuweze kurecover kiasi kilichoibwa na kuzuia mambo haya yasijirudie tena.

Muda tunaotumia kubishana Balali kafa au hajafa ingekuwa ni busara zaidi kujiuliza kama tunaweza kurecover pesa zetu za EPA na kudili na issues nyingine za ufisadi.

By the way Mzee ES nawa mikono tu kwenye issue hii.
 

Mkuu maswali mazito haya, inaelekea huyu ni padre kutoka nchi za magharibi mwa Afrika...419.
 
Asante sana kinepi.
Tangu thread ya kwanza kuwa Ballali amekufa, niliandika kuwa hii ni scientific msukule au political ndondocha. Kwa faida yetu- msukule ni pale mtu halisi anafichwa na linazikwa jitu tu, labda gogo au mgomba. Ndondocha ni kama hivyo hivyo. Wanaozika wanaaminishwa kuwa wanazika mtu kumbe la.
Hii ndiyo imefanyika kwa Ballali. Ili afichwe kabisa, hospitalini yawezekana alifanyiwa plastick surgery na kubadilishwa sura. Ebu mkumbukeni Michael Jackson kabla na baada ya plastick surgery - waweza kumtambua?
Pia wana JF, ebu tukumbuke thread ya Mwafrika wa kike. Katika maelezo yake aliandika kuwa alihudhuria mazishi yale, lakini kwa asilimia 95 anaamini Ballali hajafa.
K
Mwafrika wa kike tulikuuliza maswali ya jeneza kufunguliwa hukujibu ila uliahidi kufuatilia hati ya kifo -je umekwama wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…