Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

NOW I KNOW FOR SURE.... what I have been suspecting all along.

Let me start whistling again........ don't ask me why.
 
GENTLEMEN, IS IT GOD WHO POISONED DK BALALI IN DODOMA??? kwa nini tunamsingizia mungu kwa kazi aliyoifanya binadamu? Was Muungwana realist on this or not. I wonder kama ni kweli huo ni ukweli au ni political talk.
 
Mheshimiwa Raisi wa Tanzania -JK ameshasema kuwa kifo cha Balali ni kazi ya mungu. Je wewe unabishana na Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania?

Amefanya kipi kinachostahili aaminiwe na wananchi? Si alikuwa mstari wa mbele kusema tuhuma za wapinzani dhidi ya BoT zilikuwa ni uzushi tu!!!? ukweli sasa tunaujua. Alikuwa kimya kabisa muda wote huu kuzungumzia ufisadi mkubwa uliotokea BoT sasa mmoja wa wahusika kafariki, jamaa kapata nguvu ya kuongea. Hakuwepo hospitali, hakuona ripoti ya kifo kilisababishwa na nini, hivyo ni bora anyamaze tu awaachie familia ya Ballali wakitaka kuongea wataongea.
 
Huyu Jamaa naona akili yake iko likizo au labda iko UFISA.........................DINI. Naona yeye anaamini binadamu na sio MUNGU. JK akisema .....NDIO MZEE, EL akisema .....NDIO MZEE, CHENGE akisema .......NDIO MZEE. Hii ndio sababu kubwa iliyomfikisha BALALI alipo. Anaishia kuwa mtumwa wa MAFISADI baada ya kumtumia watakavyo kwa matakwa yao binafsi. Dawa ni kuondoa hiki CHAMA CHA MAFIA madarakani au kuweka watu ambao wako competent katika nafasi zao za kazi.

GAVANA wa benki kuu lazima U-QUESTION any move ambayo SERIKALI inachukua haswa maswala ya FEDHA na UCHUMI kwa ujumla. Sio unakurupuka na BILLION 25 kwa wananchi bila kumshiriksha MCHUMI yeyote eti tu upate ujiko wa MABILION YA JK. Matokeo yake ufisadi tu wa kutupwa usiokuwa na kipimo wala utu.

Kwa hiyo serikali isipike watu hapa kupitia tume ya kuchunguza EPA kuziba watu midomo na kuwatangazia UMMA eti BALALI KAFA. Huyo aliyefanya FACE-LIFT lazima amekuwa milionare kwa jasho la wananchi wa Tanzania.
 
Kwa kawaida sisi waTanzania tuna utaratibu wa kusafirisha mwili nyumbani iwapo atafariki nje ya nchi. Michangi huwa inafanyika kwa sababu hii..... Halafu pia hatuna tabia ya kuchoma mwili.......
Sasa maswali yangu kuhusu Ballali ni:
Kwanza: Kwanini waTanzania hatukuelezwa au kushirikishwa katika jambo hili....? (Niko Boston ndio maana nauliza swali hili).
Pili: Kwa nini mwili wake usirudishwe nyumbani....?
Tatu: Kwa nini mwili wake uchomwe....?
Nne: Ballali alikuwa mfanya kazi wa serikali. Kwa nini Serikali ilimtelekeza katika mauti yake....?
Siungi mkono ufisadi alioufanya Ballali....kwahiyo ningependa kuona picha yake kabla ya mazishi ili nihakikishe kama kweli amefariki dunia au walitafuta pacha wake na kumzika.....na Ballali akayesa.
 
Ila nimekubali mafisadi ni soo babake... duuuu! Yaani unaambiwa wamemfanyia plastic sugery Balali na kumshauri abaki Marekani maisha yake yote yaliyobaki , then wakaishauri familia yake zitangaze msiba na waseme watazika kulekule marekani... na hairuhusiwi mtu wa nje ya wanafamilia kuhudhuria kwa kuwa mtashtukia kwamba anayezikwa ni maiti iliyonunuliwa mortuary ya hukohuko majuu na kuvikwa sura ya balali. Then baada ya hapo wabongo mnaletewa picha za mazishi kama vile kafariki kweli..... loooo kama hamjashtukia hilo mmeliwa!!!! Poleni eeeee wabongo wenzangu kwa kulishwa mchanga wa macho!!!!!! MAfisadi Hureeeeeeeee! Mkapa, Chenge, Mgonja, Mramba, Kikwete, Lowasa, na wengine wote naona mna-toast glass za wine tu kushangilia dili kutimia... Mna akili fyetu nyie !!!!
 
Ila nimekubali mafisadi ni soo babake... duuuu! Yaani unaambiwa wamemfanyia plastic sugery Balali na kumshauri abaki Marekani maisha yake yote yaliyobaki , then wakaishauri familia yake zitangaze msiba na waseme watazika kulekule marekani... na hairuhusiwi mtu wa nje ya wanafamilia kuhudhuria kwa kuwa mtashtukia kwamba anayezikwa ni maiti iliyonunuliwa mortuary ya hukohuko majuu na kuvikwa sura ya balali. Then baada ya hapo wabongo mnaletewa picha za mazishi kama vile kafariki kweli..... loooo kama hamjashtukia hilo mmeliwa!!!! Poleni eeeee wabongo wenzangu kwa kulishwa mchanga wa macho!!!!!! MAfisadi Hureeeeeeeee! Mkapa, Chenge, Mgonja, Mramba, Kikwete, Lowasa, na wengine wote naona mna-toast glass za wine tu kushangilia dili kutimia... Mna akili fyetu nyie !!!!


Yote yanawezekana unayosema pia yawezekana ila jamaa alikuwa dhaifu kitambo kwa mujibu wa vipimo vya macho yangu some kind of progressive disease.

Katika yote yaliongelewa ktk maada zote kuhusu kifo chake kuwa ni fake au halisi nimeona hakuna pande inayoweza kusema kuwa kinyume cha wanavyoamini ni uwongo (and the vice verse is the truth).
Kwa kuwa mtu ana haki za kusimamia kuwa jamaa hajafa kama bado unamuona by your naked eyes kuwa yu mzima vinginevyo usibishe kuwa kafa ila labda uombe kudhibitishiwa kifo chake kwa njia ambayo ww utaamini.

Na pia mtu ana haki ya kusimamia kuwa it is the death fake kama ameona hilo likifanyika kwa macho yake vinginevyo asibishe akiambiwa kweli kafa kihalisi.
Mtu ana haki ya kusimamia kuwa kweli jamaa kafa kama na kama tu kaona hatua ya kufa ya anayesemwa kuwa kafa,mwili halisi wa mfu anayesemWa kufa.

Logic by connecting some facts its depents on what is fact to you and its reliability.Basi si matumizi ya faida na sanifu ya nishati ktk kongamano juu ya hili.
 
Kuhusu kulipua mabomu mbona mwanzisha maada naona kaweka kiulizo mimi sioni la wao kusema likawa kwenye mfumo wa bomu litakalo tikisa.
 
Ballali alikiona kifo

na Kulwa Karedia na Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MAELEKEZO ya kuzikwa Washington nchini Marekani kwa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), yalitolewa na yeye mwenyewe, siku kadhaa kabla hajafikwa na mauti, Ijumaa ya wiki iliyopita.

Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka kwa ndugu wa karibu wa Ballali aliyeko katika msiba huo Washington, zinaeleza kuwa, gavana huyo wa zamani wa BoT alifikia uamuzi wakati hali yake kiafya ilipokuwa ikizorota kutokana na kuumwa.

Mmoja wa wanafamilia ya Ballali aliyezungumza na Tanzania Daima jana, kutoka Washington, Marekani uliko msiba huo, alisema Ballali alitangaza uamuzi huo mbele ya jamaa zake, akiwamo mkewe Anna Muganda.

Kwa mujibu wa mwanafamilia huyo ambaye juzi alikuwa mmoja wa watu walioithibitishia Tanzania Daima kuhusu kifo hicho cha Ballali, hata kusababisha kuwa chombo pekee cha habari kilichoandika taarifa hizo jana, Ballali alifikia uamuzi huo kutokana na kufadhaishwa na namna jina lake lilivyokuwa likihusishwa na tuhuma nzito za ufisadi.

“Yeye mwenyewe ndiye aliyeamua azikwe huku Washington. Siku zote amekuwa akitueleza namna alivyokuwa akifadhaishwa sana kutokana na kuchafuliwa kwa jina lake, hata baada ya kuitumikia nchi yake kwa juhudi kubwa, moyo mkunjufu na kwa uadilifu wa hali ya juu.

“Alitueleza hapa kwamba hajapata kuiibia nchi yake hata senti moja. Hapo ndipo aliposema akifa angetaka azikwe huku huku Washington na si nyumbani, ambako alihusishwa na kila aina ya tuhuma,” alisema mwanafamilia huyo ambaye hakupenda kutajwa jina gazetini, akisema yeye hakuwa msemaji.

Mwanafamilia huyo alisema kwamba, katika mazishi yake, Ballali atazikwa bila ya kuwapo mama yake mzazi, aliyepo hapa nchini, ingawa atasindikizwa na dada zake wawili ambao walikwenda kumjulia hali huko Washington hivi karibuni.

“Inavyoonekana mama yake hataweza kuwahi mazishi. Hata hivyo dada zake wawili, Elizabeth na Margaret, wote tunao hapa msibani na hao ndio watakaoiwakilisha familia yake katika mazishi,” alisema mtoa habari wetu huyo.

Hata hivyo, taarifa nyingine kutoka kwa jamaa wa Ballali walio Dar es Salaam zinaeleza kuwa, ingawa dada zake hao wawili walikwenda kumjulia hali kaka yao, waliwasili Washington, Marekani wakiwa wamechelewa na kumkuta ameshafariki dunia.

Mtoa habari wetu kutoka Washington aliieleza Tanzania Daima kwamba, ndugu hao wawili wa Ballali walikuwa wakitarajia kurejea nchini wakati wowote kuanzia Jumatatu ijayo.

“Pengine msiniulize mimi hapa maswali mengi. Mpango uliopo hapa ni kwamba hawa dada zake wawili, Eliza na Maggy, wanatarajia kuitisha mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam na kutoa taarifa kamili kuhusu kifo cha kaka yao,” alisema ndugu huyo wa Ballali.

Alisema alikuwa na imani kwamba, katika mkutano wao huo na waandishi wa habari, unaotarajiwa kufanyika wakati wowote wiki ijayo, maswali yote kuhusu nini hasa kilimpata Ballali hata kufikwa na mauti hayo kitawekwa hadharani.

Habari nyingine kutoka Boston na Washington zinaeleza kwamba, kulikuwa na taarifa zilizokuwa zikisema kwamba, Ballali alikuwa akisumbuliwa na aina moja ya saratani kwa muda mrefu sasa.

Hata hivyo wakati kukiwa na taarifa hizo, baadhi ya ndugu, marafiki na jamaa zake wamekuwa wakieleza wasiwasi wao kwamba, Ballali alilishwa aina fulani ya sumu isiyojulikana, siku kadhaa kabla hajakimbizwa Marekani kwa matibabu.

Taarifa hizi za kulishwa sumu zimekuwa zikienea kwa haraka katika maeneo tofauti, mbali ya Tanzania Daima pekee kuligusia jambo hilo jana, likimkariri ndugu mmoja wa Ballali aliyekiri kuwapo kwa wasiwasi huo miongoni mwa wanafamilia.

Jamaa mwingine wa Ballali aliyeko huko huko Washington Marekani, aliieleza Tanzania Daima kwamba, familia ilikuwa ikijiandaa kuwasiliana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani ili kesho aweze kuhudhuria misa maalumu ya kumuombea marehemu itakayofanyika kabla ya mazishi yake yanayopangwa kufanyika kesho hiyo hiyo.

Ndugu huyo wa Ballali alisema, walikuwa na imani kuwa serikali ilikuwa na taarifa kamili, baada ya wao kuwasilisha Ofisi ya Rais Ikulu na baadaye kwa Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, juzi hiyo jioni.

Wakati Ballali akitarajiwa kuzikwa kesho, uongozi wa BoT jana alasiri ulitoa taarifa rasmi ya kukiri kupokea taarifa hizo za kifo cha Ballali na kusema unaungana na familia yake katika kipindi hiki kigumu.

Akitoa taarifa hiyo ya maandishi kwa waandishi wa habari jana, Ofisa Mwandamizi wa Kitengo cha Habari cha BoT, Emmanuel Mwero, alisema ofisi ya Gavana (Ndulu) ilipokea habari hizo kwa masikitiko makubwa.

“Ofisi ya Gavana imepokea habari za kusikitisha jana usiku (Jumanne) kuwa gavana wa zamani wa BoT, Daudi Ballali, amefarikia Ijumaa Mei 16, mwaka 2008 huko Boston, Marekani,” ilisema taarifa hiyo wakati ukweli ni kwamba Ballali alikuwa amefia Washington.

Katika taarifa hiyo, Ballali anaelezwa kuwa alijiunga na BoT kama gavana Julai 14, 1998, nafasi aliyodumu nayo hadi Januari 8 mwaka huu, uteuzi wake ulipotenguliwa na Rais Kikwete, baada ya kupokea taarifa za ukaguzi wa EPA, uliofanywa na Kampuni ya ukaguzi wa hesabu ya Enrst & Young.

Hata hivyo, si BoT wala serikali, ambayo ilikuwa mwajiri wa Ballali, iliyotoa taarifa ya ufafanuzi kuhusiana na mazishi ya Ballali, ambaye ni mmoja wa watu waliopata kushika nafasi nyeti za uongozi nchini.

“Ndugu waandishi habari hii imejitosheleza, hivyo tunawaomba mkaitumie na kama kutakuwa na jambo lolote, Gavana Beno Ndullu atawaita,” alisema Mwero.

Taarifa kutoka ndani ya benki hiyo zinasema kuwa, jana asubuhi wafanyakazi wote walisambaziwa kupitia anuani zao za e-maili, wakijulishwa kuhusu msiba huo.

Tanzania Daima ilipofika katika nyumba aliyokuwa akiishi wakati akiwa gavana, iliyoko Masaki Plot 387, jijini Dar es Salaam, hali ilikuwa ya utulivu, ingawa walikutwa walinzi wa Kampuni ya Ultimate Security.

“Ni kweli hapa ni nyumbani kwa Gavana, lakini tangu Ballali alipoondolewa, nyumba imebaki wazi, tupo sisi na mfanyakazi wa ndani tu,” alisema mmoja wa walinzi hao.

Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, jijini Dar es Salaam, Salvatory Rweyemamu, alipoulizwa kuhusu taarifa hizo za msiba alisema yeye hakuwa msemaji na akamwita Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Kassim Mpenda aliyekuwapo hapo.

Mpenda kwa upande wake alisema serikali imepanga utaratibu juu ya taarifa hizo na kwamba msemaji mkuu ni Gavana wa BoT, Ndullu.

“Ni kweli hata miye nimesikia kwamba Ballali amefariki dunia, sasa mimi siyo msemaji, kumbukeni serikali inafanya kazi kwa utaratibu, hivyo imemteua Dk. Ndullu kuwa msemaji mkuu wa suala hili, nawaomba mtafuteni,” alisema Mpenda.

Kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo, Ballali aliwahi kuwa mchumi wa BoT mwaka 1967-1976, kabla ya kufanya kazi katika Shirika la Fedha Duniani (IMF).

Ndugu wa karibu wa Ballali alisema wanatarajia kufanya misa ya mazishi ya Ballali na kumualika Balozi wa Tanzania nchini Marekani, katika shughuli za mazishi zitakazofanyika kesho jijini Washington, Marekani.


Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 22 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
ningependa maiti ya huyu mheshimiwa iletwe nchini ili tuwe na uhakika kuwa ni kweli amefariki kwa sababu naona kuna zengwe, angalia namna viongozi wetu wanavyolikwepa na kutupiana mzigo juu ya taarifa hiyo.

na juma magogo - 22.05.08 @ 08:18 | #12509

Wanadamu mwisho wao mavumbi,fedha na mali ni za Mungu;Mafisadi jifunzeni kuwa mambo haya yana mwisho,ingawa hatuna hakika kuwa balali alikuwa fisadi,chenye uhakika ni kwamba alisaidia kufilisi nchi na kusaidia wengine kula nchi;Fisadi tunaye humu nchini "Mzee wa Vijisent"aukumbuke mwisho wa Balali arudishe fedha zetu Akamrudie Mungu.

na kibeberu, tanzania, - 22.05.08 @ 08:19 | #12510

Yaani hapa naona ni changa la macho BOT wanasema amefia BOSTON ila ndugu zake wanadai amefia Washington kweli kuna ukweli hapa mm naona yupo visiwa vya Malta anakula maisha taratibu huku ss tukipigwa changa la macho wadanganyika wenzangu.

na Mkula, Namanga, - 22.05.08 @ 08:27 | #12512

kama ni ukeli Dk.Ballali kafariki, Mungu amlaze mahali pema peponi.Kifo, kwa wakati wowote sio jambo la kushabikia hata kama mtu aliye aga dunia alikuwa muovy kiasi gani.Japo Dk.Ballali alishtumiwa kwa visanga vingi vya ufisadi si vyema kuaanza kusheherekea kifo chake.La msingi ni serikali ifanye mpango wa kuusafirisha mwili mpaka tanzania na kufanya mipango ya mazishi ili kuwahakikishia watanzania wote ni kweli amefariki.

na deco, kenya, - 22.05.08 @ 08:45 | #12517

Jamani tusianze kumkumu marehemu.
Kwanza ailikuwa hajahojiwa ili apate kutoa utetezi wake, bahati mbaya kifo imemkuta.
Kwa kuwa suala la EPA lina watu wengi, na Balali alikuwa na wasaidizi wengi , kwa mawazo yangu naona bado mengi yatafahamika hata bila kuwepo huyu mzee.
Mungu amlaze pema peponi- ndiyo maisha yana mwanzo na mwisho.

na john, mwanza, - 22.05.08 @ 08:46 | #12518

Nimepokea kwa maskitiko makubwa taarifa ya kifo cha Dr Daudi Balali,kwa sababu kuu mbili kama sio tatu 1 amefariki wakati ambao taifa linamhitaji kuliko wakati uwao wote 2 Balali amekufa wakati ambao watanzania walikuwa wanamsubili kwa hamu kubwa iliaweze kuwajibia maswali mengi yanyo husu pesa zao 3 ni dhahili kuwa mheshimiwa Raisi sasa atapumua vizuri sasa pamoja na wale wote wanao husika na upotevu wa pesa zetu katika account ya madeni ya nje [epa] Ndio watapumua kwa sababu Balali ndiye aliye kuwa anajua nani amechukua nini na kupeleka wapi na tarehe gani,kwa upande mwingine ni kwamba Balali ndiye aliye kuwa ameshikilia hatima ya pesa za watanzania na kuweza kuwafichua wote walio husika ktk wizi wa pesa zetu.Sasa kwa kifo hiki tutegemee nini kipya juu ya Taifa hili iliyo baki ni kuendelea kumwomba Mungu atuhurumie juu ya Viongozi wetu wasio na huruma na watu wengine.

na Mch:Ibrahim Mwandandila, Mbeya/Tanzania, - 22.05.08 @ 08:49 | #12520

Mjomba kaa chonjo mchanga sasa wanamwaga kwa kutumia malori machoni , iweje tu gazeti la tanzania daima ndio liseme la kwanza haya magazeti mengine yalipata kigugumizi gani kusema au makampuni mengine yako karibu na mafisadi , au serikali imeona atasema mengi ikaamua kukata umeme kwenye gridi ?

na msemakweli, Dar -Tanzania , - 22.05.08 @ 08:56 | #12522

MIMI NAULIZA SWALI NI KWELI KWAMBA SERIKALI HAIKUONA UMUHIMU WA KUMLETA MAREHEMU NYUMBANI TANZANIA?NA FAMILIA YAKE MNAFIKIRI INAJISIKIAJE KUMZIKA MPENDWA WAO HUKO WASHNGTON MAREKANI?ANY WAY MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMEN.

na HILDER MMBANDO, TANZANIA, - 22.05.08 @ 08:57 | #12524

Balali anazikwa Washington!!!!!! Je Serikali imelipokeaje hilo? (Huyu mtu alikuwa na siri kubwa sana na Serikali). Hata kama atazikwa huko au Tanzania,Naomba angalizo juu ya ugonjwa wake na tuhuma dhidi yake (ufisadi). Je inawezekana alipoona anakabiliwa na tuhuma aliamua kunywa sumu yeye mwenyewe? Je ni kwanini alikimbilia huko? Je Tayari alikuwa na himaya yake huko tangu akiwa gavana na ndio maana ameweza kupata hata kibali cha kuzikwa nje ya nchi yake mtu mwenye wadhifa na uwezo wa kurudishwa nyumbani kutunza heshima ya familia na serikali?

na Mamboleo - 22.05.08 @ 09:07 | #12527

HIVI KUMBE SIKU HIZI ZOTE ILIKUWA INAJULIKANA WAPI BALALI YUPO!! DU AMA KWELI MFICHA MARADHI KIFO HUMUUMBUA! LEO HATA NYUMBA YAKE INAJULIKANA ILIKUWA WASHINGTON NA HATA DADA ZAKE JUZI WALIONDOKA KWENDA MJULIA HALI! WALIPITA VIPI HAPA US EMBASSY? KUNA MCHEZO UNACHEZWA HAPA, KAENI CHONJO, HUYO HAJAFA, ILA LIMEULIWA JINA TU, ILI APATIWE JINA JIPYA NA URAIA MPYA AWE MWINGINE KABISA! KALAGABAHO!!

na Mtanzania, Tz, - 22.05.08 @ 09:08 | #12528

muda huu hatutakiwi kuserehekea kifo cha balali kwa sababu kila mmoja atakufa,lakini nadhani hawa ndugu zake wahajaribu kumtetea tu,ukwli ni kwamba kamati ilioundwa kuchunguza kashfa ya epz imebakisha mwezi mmoja tu kuweka kila kitu hadharani,na hii huenda ikawa sababu iliomfanya balali afariki,maaana hata ndugu ake wanasema alisema azikwe huko huko,inamaana alikuwa na wasiwasi mkubwa na alijuwa mwisho wake,mimi bado naimani kuwa itakapotoka taarifa ya epz kutafichuka ma´*** mengine mengi tu,hivi muheshimiwa mkapa yuko wapi,balali alikuwa mtu wake wa karibu sana,kikazi na kifamilia,kwa nini ananyamaza kimya,huu si uungwana,na kama andhani akinyamaza kimya ndo watu watamsahau anajidanganya,hii serikali ya sasa inamvumilia kwa ajili inataka iingie tena madarakani 2010,na inahitaji watu wa mkapa wawape kura,lakini baada ya 2010 watamdhalilisha mkapa,msishangae akipandishwa mahakani,ni bora ajitokeze atueleze watanzania serikali yake ilivyofanya madudu kama hakuhusika.

na john mzalendo - 22.05.08 @ 09:08 | #12529

Kifo cha ndg balali kinatukumbusha wajibu wetu kwa Muumba.mambo yote ya duniani ni ya muda mfupi na yakupita.Ni vema watu tuliokabidhiwa dhamana kuwa waadilifu.Kifo hutukumbusha na kutuasa kuwa wongofu katika maisha yetu.Kila mtu ni lazima kijihukumu mwenyewe kabla ya kuwahukumu wengine.Ufisadi si kwa viongozi tu,bali hata kwa watu wa kawaida.Hatuwezi jua haki ya balali machoni pa Bwana.Tumuombee mwenzetu alietangulia mbele za haki kwani siku ya mwisho kila mmoja wetu anawezajikuta nae yufisadi.Mungu amsamehe na kumrehemu mpendwa wetu Balali.amen

na PETER B KADILIKANSIMBA, TANZANIA/mbeya, - 22.05.08 @ 09:09 | #12530

Hapa nazidi pata wasiwasi juu yakifo cha mheshimiwa huyu.kwan taarifa za kifo chake zinachanganya,Wengine boston(serikali)wengine washington(wanafamilia).Muda wa siku tatu.Kweli serikali ilishindwa kupata taharifa sahihi na kwa haraka!utandawazi kama huu?LAKINI IPO SIKU AMBAYO UKWELI UTAJITENGA NA UONGO.

na alfredy fabian, tanzania, - 22.05.08 @ 09:16 | #12533

Kwanza natoa pole sana kwa ndugu na jamaa wa marehemu Dr. Daud Balali pili naomba serikali ishiriki kikamilifu katika mazishi ya marehemu maana aliifanyia kazi kwa muda mrefu, na baadaye waendelee na uchunguzi wa upotevu wa fedha zetu. Hili linawezekana maana kama gavana ni lazima wasaidizi wake wanajua kilichokuwa kinaendelea kuhusu akaunti ya epa. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi

na amos, Arusha, - 22.05.08 @ 09:18 | #12536

itakuwa vyema zaidi kama Balali atazikwa nchini Tanzania ambako ndiko alikozaliwa, na kulitumikia taifa hili. kwani kwa yote yaliyotokea ni mengi na watanzania tumsamehe, tumuombee kwa Mola apate kupumzika vema peponi. pia mafisadi wengine jifunzeni sana kuhusu nchi hii

na Mrs Kissia, Kahama, - 22.05.08 @ 09:21 | #12537

Balali huko ulikoenda kaa chonjo kujibu tuhuma ulizofanya kuhusiana na nchi hii. binadamu ni mavumbi na mavumbini umerudi hela zote umeziacha wapi?

na Meryciana Joram, Kahama, - 22.05.08 @ 09:24 | #12538

hapo hakuna kifo wanataka macavel style .huyo balali aliogopa nini hata kuzikwa hapa bongo wakati yeye ni safi?hivyo huyo mtu alipanga kutokanyaga tz milele mpaka akatae pia kuzikwa hap?watu kama hawa wanpewaje nyazifa nyeti wakati si wazalendo?pia kumbe waweza kuwa kibuli kwa gvnmt.sas ukweli ni kwamba yupo la azikwe hapa ili kuwe na udhibitisho,na ikishindikana twende watnzania wakutosha kudhibitisha hilo na si ndugu wanatuzingua


na big mo, tanzania, - 22.05.08 @ 09:32 | #12539

Nakumbuka serikali ilisema haimuhitaji Balali kwa sasa,sijui inatuambia nini kwani ndiye mtuhumiwa namba moja katika uwizi wa fedha za EPA.

na robi, arusha, - 22.05.08 @ 09:38 | #12543

Kifo sio kitu kizuri kwa yeyote;tusikitike pamoja na wafiwa.Historia itasema kama Balali alikuwa mkosa au la; lakini Mungu ndiye hakimu wa HAKI.

na john, Tanzania-Dsm, - 22.05.08 @ 09:43 | #12546

Waafrika kukubali kifo cha kawaida huwa si rahisi. Ndio maana hata mzee mwingine akifa akiwa na miaka 80 baadhi ya makabila ya Afrika huenda kupiga bao kujua kwa nini amekufa.
Bahati nzuri Balali amefia kwenye hospitali zenye uwezo mkubwa kiteknolojia. Badala ya waandishi wa hapa bongoland kupepeta pumba eti kapewa sumu wapate ukweli huu kutoka kwa waganga waliomshughulikia huko Marekani.

na Maarufu - 22.05.08 @ 09:43 | #12547

maswaiba wawekwe kiti moto hapo kuna kitu.che brother tunakuomba mwenyewe utoe mali zako na unifuate kabla ya kuukumiwa na wanadam hapa dunian.sas jamaa anakwenda maakama kuu huko hakuna wakili mguu wala kidole kwani haki ya watz haiwezi kwenda bila kuwjibishwa na kufilisiwa mali..kama atzikwa huko basi aliyempa kibarua aliyajua hayo kama si kummaliza ushaidi usiwe na ukweli wa kutosha.sas hakuna kuogopa K KAZA BUTI 2010 tunakupa wewe hao wanopanga kugombea hata maoni hawavuki na wakati huo watakuwa watuhumiwa hawagombei tena
.mwisho mauti yanawakuta na tuhuma nzaito ujafaidi visent zaidi ya posho zetu tu.

na mwenyenia, tanganyika, - 22.05.08 @ 09:47 | #12552

MH, UMAFIA UNA MAMBO. HAPA HUYU KAFA ILI WAANZILISHI WA DILI HILI WAWEZE KUFANIKISHA UONGO WAO. Bila shaka MR. Clean atashanglia sana maana huyu jamaa angekuja kumropokea siku moja. Hongera waliofanikisha kifo chake maana mwosha huoshwa. Lakinio, bado JK ana kazi: Balali alimfukuza.. je mwanzilishi wa dili hili atatajwa?
MJOMBA, BADO MIAKA MIWILI UNATAKIWA UTWAMBIE ULICHOTUAHIDI MWAKA 2005 WAKATI WA KAMPENI KIMEFIKIA WAPI. Maana mpaka sasa naona kama umeduwaa , hujui wapi tunatoka na kuelekea.....hizo ni salamu tu

na nyumbu, Arusha, - 22.05.08 @ 10:08 | #12557

Mwe maswali ya wadanganyika atajibu nani kama balaaa hili limeshachukuliwa na mwenyezi mungu lakini bora mungu kamchukua maana wabongo wangeweza kujichukulia sheria mkononi wakamchoma moto kama kibaka wa tandale bila hata kumsikiliza. eee baba muweke mahala pema peponi balaa hili!

na mjimwema,KIGOMA
 
Kama ni kweli Balali alihuzunishwa na kitendo cha kudhalilishwa hapa nchini akiwa bado mzima kwa nini hakusema lolote. Kama hakuiba hata senti tano kwa nini alikaa kimya? Ndugu zake wakaribu watueleze.
 
Kuna mtu amefikiria kwamba Balali labda kafa ukimwi maana ndiyo ugonjwa bila tiba. kama alipewa sumu basi alichomwa damu ya ukimwi.
 
Ansbert Ngurumo



NILIWAHI kudokeza mambo mawili kwenye safu hii kuhusu aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), hayati Daudi Ballali.

Kwanza nilihoji kama ugonjwa wake ulitokana na kulishwa sumu. Sikujibiwa. Pili, nilisema kwamba taarifa za watu wanaojua mambo yanayoendelea serikalini zilieleza kuwa Ballali asingerejea Tanzania.

Yote mawili yamekuwa. Ballali hakurejea. Sasa taarifa mpya zinasema kwamba kabla hajafa alimtaja mtu aliyemlisha sumu iliyosababisha ‘ugonjwa' wake, hadi akakimbizwa nje ya nchi kutibiwa.

Watu wake wa karibu wamemnukuu hayati Ballali akimtaja mtu aliyemlisha sumu. Yawezekana hii ni kauli mojawapo ambayo wanafamilia walitaka kuiweka hadharani katika mkutano na wanahabari. Tuwape muda.

Kwa sababu zinazoeleweka, hatutamtaja ‘muuaji' huyo hapa kwa sasa. Lakini kadiri siku zinavyokwenda, iwapo na sisi hatutalishwa sumu, kama hatajitaja, tutamtaja siku moja, katika kuweka vema historia ya mapambano dhidi ya ufisadi.

Siku mambo yote yatakapokuwa yamewekwa vizuri, Watanzania watakaokuwa hai wakati huo watapata fursa ya kutambua jinsi ufisadi ulivyowahi kuwa sehemu nyeti ya utawala wa nchi hii.

Kitu kimoja hakitawashangaza. Nacho ni sura na majina yanayozungumzwa na kuhusishwa na ufisadi katika serikali za awamu ya tatu na ya nne.

Hata katika hili la sasa, mtu yule yule aliyetajwa na hayati Ballali, kwamba ‘ndiye alinilisha sumu,' ni kigogo yule yule ambaye amekuwa anahusishwa katika mazingira na matukio mengi ya ufisadi wa kupindukia.

Yumo katika orodha ya mafisadi 11 walioanikwa hadharani na Dk. Willibrod Slaa, Septemba 15, 2007 katika mkutano wa hadhara wa Temeke Mwembe Yanga, Dar es Salaam.

Yumo miongoni mwa waasisi wa kaulimbiu ya ‘Maisha bora kwa kila Mtanzania.' Ni mmoja wa watu ambao kwa sasa wanaangaliwa kwa macho ya chuki, kwa kuwasababishia Watanzania maisha duni.

Ni mmoja wa vinara waliofadhili na kutangaza kwa nguvu zote dhana ya ‘Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya' ambayo imekuwa ikifupishwa kwa kuitwa ANGUKA; na kuwa kiini cha anguko la Tanzania.

Ni muasisi wa dhana iliyoangusha uchumi wa nchi na kudunisha maisha ya Watanzania, huku akiasisi dhana nyingine ya kimya kimya ya ‘Maisha bora kwa kila fisadi.' Mtu huyu huyu aliyetajwa na hayati Ballali kwamba ndiye alimlisha sumu, yumo miongoni mwa vigogo wanaotuhumiwa kulihujumu taifa kwa kuunda mitego ya uchotaji wa pesa za wananchi kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu (EPA).

Ndiye anayetajwa kuwa mmoja wa vigogo walionufaika na pesa za Richmond; mtu ambaye inasemekana alikula njama kuchomoa mafaili ya Richmond katika kumbukumbu za msajili wa makampuni ili ‘kuiingiza mjini' Kamati ya Bunge iliyokuwa inachunguza tuhuma dhidi ya kampuni hiyo.

Ni kigogo huyo huyo ambaye kwa wakati fulani alidhaniwa kuwa na hisa katika urais wa Jakaya Kikwete, hata ikawalazimu wanahabari kumhoji rais moja kwa moja kuhusu suala hilo.

Ni mtu huyo huyo ambaye miezi michache iliyopita, kabla ya masuala ya ufisadi kupamba moto, alikuwa akidhaniwa kuwa mfadhili na mkombozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM); na ambaye baadhi ya watu wanaojua jinsi awamu hii inavyofanya kazi, waliwahi kudokeza kwamba ‘ndiye rais' wa Tanzania asiyeishi Ikulu, anayeendesha nchi atakavyo kupitia kwa rais aliyechaguliwa, anayeishi Ikulu.

Lakini kikubwa kinachomgusa na kumfadhaisha kigogo huyu ni taarifa kwamba ndiye ameshiriki kwa kiasi kikubwa kuchota mabilioni ya EPA kutoka BoT na kuyazungusha kwenye miradi yake, huku akiingiza mengine kwenye kazi za CCM, zikiwamo harakati za kampeni za uchaguzi mkuu.

Kutokana na ukaribu wake na walio madarakani, serikali imeshindwa hata kuchukua hatua madhubuti dhidi ya walioiba pesa za EPA; ikasema haiwajui, lakini ikakiri kwamba wanarudisha pesa taratibu! Serikali hii hii ikashindwa kuiweka hadharani ripoti kamili ya uchunguzi wa wizi wa EPA kama ilivyoandaliwa na wataalamu wa Ernst & Young.

Serikali ikamficha mtu wake kwa jinsi ile ile ilivyokuwa inaficha ugonjwa wa Ballali, nchi aliko na hospitali alikolazwa, huku baadhi ya maofisa wa serikali wakisemekana kumtembelea mgonjwa wao kushuhudia kama bado yuko hai.

Usiri wa serikali katika suala la Ballali umeiaibisha yenyewe, na umeondoa kabisa imani ya wananchi kwa serikali hii. Umeonyesha unyonge na udhaifu mkubwa wa watawala wa sasa, na kudhihirisha wasiwasi ambao tumekuwa nao siku zote, kwamba nchi hii sasa inaendeshwa na mafisadi.

Lakini huu umekuwa usiri uliokithiri, kiasi cha serikali kudiriki kuficha hata kifo chake, hadi gazeti hili lilipoibua taarifa hizo, na kulazimisha serikali kukiri.

Nawaonea huruma watumishi wa serikali hii wasio mafisadi, lakini wanaofunzwa kutunza siri za mafisadi.

Tabia hii ya serikali ndiyo imewafanya wananchi wengine kudhani kwamba hata Ballali mwenyewe hajafa; kwamba ni njama za mafisadi kumficha kabisa ili kuua ushahidi katika suala la EPA.

Lakini hata wale wanaoamini kwamba amefariki dunia, wanajenga hoja hiyo hiyo; kwamba wamemuua ili kuficha siri yao.

Kwa kifo cha Ballali lipo jambo ambalo hatutalijua kamwe kuhusu wizi wa EPA. Maana kabla hajafa, Ballali mwenyewe alisema hakula hela za EPA, bali anawajua waliozichota, na kwamba asingekufa peke yake.

Sasa wamemtanguliza wakidhani atakufa peke yake. Lakini sisi wengine tunasema kwamba hao hao waliomtanguliza, watamfuata.

Hatuwezi kujua mapenzi ya Mungu, na si vema kumsingizia Mungu. Lakini akili timamu inatueleza kuwa kama tungekuwa na serikali makini, kifo cha Ballali kingeahirishwa.

Huyu ndiye alipaswa kulindwa na serikali ili aweze kutoa ushahidi ambao ungeiwezesha serikali kuchukua hatua za kujisafisha, na kudhibiti ufisadi mwingine.

Lakini kwa kuwa si serikali makini, na kwa kuwa haina nia ya kujisafisha; na kwa kuwa inawajua na kuwalinda waliohusika na wizi wa EPA; na kwa kuwa wanaohusishwa na kifo cha Ballali ni wale wale walioshiriki kuiumba serikali hii; Watanzania hawatakuwa na makosa wakiibeza na hata kuituhumu kwa kumuua Ballali.

Ndiyo maana, ingawa kwenye misiba hatutarajii watu wamkejeli marehemu, Watanzania wameshindwa kuzuia hisia zao. Kwa kujitahidi sana, wamezielekeza zaidi kwa serikali badala ya marehemu.

Mojawapo ya kauli zilizozagaa mitaani sasa ni kwamba ‘kafa Ballali, bado wengine kumi.' Hawa wanaosema hivi wanarejea orodha ya ‘mafisadi' iliyotajwa na Dk. Slaa, ambayo huko nyuma niliwahi kuiita ‘JK Eleven.' Lakini kikubwa ni kwamba huyo anayesemekana kumlisha sumu Ballali ni mmojawapo wa hao kumi waliobaki.

Hili linakomaza dhana nyingine kwamba watu hawa sasa wameamua kumalizana wakigombea maisha bora walioyowanyima wananchi.

Tunachojua tulio wengi ni kwamba Ballali si wa kwanza. Na hawezi kuwa wa mwisho. Lakini mwisho wao wote ni mmoja.

Yawezekana bado kumi au zaidi ya kumi. Lakini ukweli ni kwamba Ballali ametangulia, ushahidi wa EPA umekufa, na imani ya watu kwa serikali imekufa!

+447853850425
ansbertn@yahoo.com
www.ngurumo.blogspot.com

source: http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/5/25/makala2.php

Kama RA vile
 
Damn it! Why not mention him we dare talk openly.
 
Siamini kama kufa kwa Balali ndio kufutika kwa ushahidi wote kuhusu EPA. Siamini kama Balali alikuwa akifanya mambo yote haya ndani ya BOT bila kumhusisha mtu mwingine. Ukweli ni kwamba Balali alikuwa ni shahidi mkuu, lakini naamini wapo watu wengine wengi ndani ya BOT, ndani ya Wizara ya Fedha na ndani ya serikali kwa ujumla wenye ushahidi kuhusu ufisadi wa EPA. Cha msingi ni kuwalinda wasinyweshwe "sumu" kama ilivyotokea kwa Balali.
 
Damn it! Why not mention him we dare talk openly.

No hatuwezi kumtaja kwa kuunganisha hisia za mtu kwani hitaharibu kijiwe chetu, kumbukeni wanatafuta sababu ya msingi kuakikisha hiki kijiwe kinafungwa huu ndo wakati wa kuwa makini zaidi ili tuendelee kumkoma nyani gradi, kama kuna ushaidi wa kutosha tafadhari mtaje kama unaushaidi wa mazingira then please do not do that.
 
Siamini kama kufa kwa Balali ndio kufutika kwa ushahidi wote kuhusu EPA. Siamini kama Balali alikuwa akifanya mambo yote haya ndani ya BOT bila kumhusisha mtu mwingine. Ukweli ni kwamba Balali alikuwa ni shahidi mkuu, lakini naamini wapo watu wengine wengi ndani ya BOT, ndani ya Wizara ya Fedha na ndani ya serikali kwa ujumla wenye ushahidi kuhusu ufisadi wa EPA. Cha msingi ni kuwalinda wasinyweshwe "sumu" kama ilivyotokea kwa Balali.

Itakuwa vipi kamati ya EPA itakapoleta taarifa ambayo kila jambo anatakiwa athibitishe Ballali kama vile nani alimwndikia vimemo vya akasaini.
Au walete taarifa kuwa yale ni makampuni ya Ballali na Ditto na kwa sababu wameshakufa no Mo MONEY
 
Back
Top Bottom